Mzee Msemakweli
Senior Member
- Oct 12, 2010
- 159
- 34
Sio kweli, kama Mkapa amekataa kuzindua kampeni, hizo tarehe zitakuwa zimeingiliana tuu na ratiba zake kwa sababu ndani ya CCM rushwa is the order of the day!. CCM sio tuu inanuka rushwa bali ni imeoza kwa rushwa mpaka inatoa uvundo na la kuvunda siku zote halina ubani!. Kama kawaida wanaousikia huo uvundo wa rushwa, ni wale walioko nje ya CCM tuu!, kwa wana CCM wenyewe, pua zao zimeisha zoea hiyo harufu na hawaisikii kama unavyopita maeneo ya Feri, unapokelewa na harufu ila ukikaa kidogo tuu pua zinaizoea na huisikii tena!. Wenyewe wa Feri, hawaisikii kabisa!.
Ila pamoja na uoza wote huu wa rushwa huko CCM, matokeo ya uchaguzi huo ni mashindano kati ya udhalimu na uadilifu, uchafu wa rushwa vs usafi wa dhamira, ufalme vs ya demokrasia ya kweli, ukoloni wa kutawaliwa kifkra vs ya ukombozi wa kweli!. Nawahakikishia udhalimu, uchafu wa rushwa, ufalme, ukoloni wa kutawaliwa ki fikta ndio utashinda!. Naisubiri April 2 kuwathibitishia hili!.
Amini nawaambieni Udhalimu, Rushwa, Ufalme, Ukoloni wa Kifikra, Ufisadi, Udini, Ukabila na Utaifishaji wa Mali za Umma ni matokeo ya Ombwe la Uongozi hasa Rais; Kamwe havitadumu milele kwani mwisho wake umefika.
Je hamzioni dalili za mwisho wake? Maandamano kila kona ya nchi, Migomo kila pembe ya nchi na Wananchi kutokuwa na imani na Serikali yao. Amini nawaambieni mwisho wa hayo yote upo karibu sana. Uhuru dhidi ya uonevu ma watu wachache kuhodhi maliasili ya nchi unakuja kesho. Freedom is Comming Tomorrow guyz.