Mzalendo wa ukweli
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 559
- 149
Ndugu wanajamvi wenzangu naomba tudiscuss hii kitu,jana kupitia vyombo mbalimbali vya habari madaktari takribani 200 ambao walikuwa katika mafunzo ya vitendo/Interns waliamua kuomba msamaha kwa serikali na watanzania kwa ujumla kwa kitendo chao cha mgomo ambao ulileta madhara ya baadhi ya wagonjwa kufariki kwa kukosa matibabu nk. Binafsi nimeshindwa kuwaelewa kilichowatuma kuja kuomba msamaha ni njaa kutokana na wengi wao kufutiwa vyeti vya usajili kama professional doctors ambayo ingewapelekea kukosa sifa za kuajiriwa au ni kujutia athari zilizosababishwa na mgomo wao ikiwemo vifo vya watanzania ambo ni innocent? Je ni kweli kwamba sababu za wao kugoma hazikuwa na mashiko yoyote na ndio maana wakaamua kuomba msamaha au yale yaliyowafanya kugoma yote yametekelezwa kwa kiwango cha kuridhisha?
Je ni sawa kwa wao kuomba msamaha serikali na watanzania kwa sasa au ni kama wamepotea hawajui what to do and what will come next?
Nawasilisha hoja.
Source:media (tv's and news papers)
Je ni sawa kwa wao kuomba msamaha serikali na watanzania kwa sasa au ni kama wamepotea hawajui what to do and what will come next?
Nawasilisha hoja.
Source:media (tv's and news papers)