Mkanganyiko katika Gharama za Vocha za Simu

nyie wauzaji ndo mlitakiwa mtoe angalizo kwa hayo makampuni ya simu.....ukinipa vocha imeandikwa 1000 sikupi zaidi ya hiyo ..........habari ndo hiyo...mnataka kuuza 1100 print vouchers with that amount on it(tusaidieni kufikisha ujumbe kwa maboss wenu)
Jana nilienda kwa hawa Simbatelecom nikakuta bei iko juu. Nikawauliza swali, sasa mnataka sisi tuuze shilingi ngapi? wakaniambia utajua wewe.

mnataka kuuza 1100 print vouchers with that amount on it
Jamani mbona wakati mnanunua vocha ya sh. 1000 halafu unapata 1300 mbona hamkusema tunataka 1300 printed voucher?
ASANTE KWA TAARIFA TUTAENDA KUNUNU HUKO HUKO MNAKONUNUA. inawezekana kwa ufahamu wenu mnaenda kununua kwa wauzaji wa reja reja badala ya JUMLA, asante kwa TAARIFA, nitakuwa nanunua za wiki 3 kupunguza garama za kusafiri mpaka kwenye huduma
Hapo itakuwa vizuri zaidi, maana mtakuwa mmetupunguzia mzigo
ukinipa vocha imeandikwa 1000 sikupi zaidi ya hiyo
Wengi wamefanya hivyo lakini baada ya kuzungukazunguka huku na huko na kukuta bei ni hiyo hiyo wao wenyewe walirudi wenyewe kuchukua vocha kwa bei mpya.
hapo ni kazi ya mteja kusuka au kunyoa.
 
Tugomee huduma mwezi mmoja hadi waprint new vouchers otherwise old stock haiwezi uzwa kwa new price. It is unfair and this phucken govt haioni hili pia?
 
Tugomee huduma mwezi mmoja hadi waprint new vouchers otherwise old stock haiwezi uzwa kwa new price. It is unfair and this phucken govt haioni hili pia?

Je utakaa mwezi mzima bila mawasiliano yoyote ya simu kwa dunia hii ya sayansi na teke linalokujia?
 
Wakuu nami ni muhanga wa hili maana nilituma kijana aninunulie vocha ya 2000 nikaambiwa 2200.

Kazi kwelikweli wakuu
 
Na watanzania asilimia kubwa huishia hivi...

Unanyong'onyea kisha unaondoka hahahahahaha!

Tanzania inaweza kuongozeka kirahisi nimeamini...

Ni kweli mkuu,
Tanzania inaongozeka kirahisi mno. Mfano wa namna hii mwingie nilikutana nao kwenye daladala kipindi kile zinapandisha nauli kiholela. Nikaingia kwenye daladala konda akaja anakusanya pesa nikampa 200 akadai nauli ni 300 nikamwambia wewe ndo unaamua tu kujipandishia? Maana hata tiketi ilikuwa imeandikwa 200. Acha abiria wanigeukie, kwa nini nagoma kulipa 300. Konda akaniambia ngoja nikusanye pesa nikurudie, hakurudi tena kunidai. Baada ya kama wiki moja wiki wakarudi kutoza 200 kama kawaida.
 
Kwanini ulipie hela zaidi kwa vocha ambayo tayari imeandikwa thamani yake? Sidhani hii inaweza kusimama hata mbele ya sheria....

WIZI MTUPU!
ungejua sheria sio HAKI usingeyasema haya...hata soda zimepanda kwa taarifa yako....TZS500 per soda. tatizo ni serikali wamepandisha kodi ya products hizi.. producers wanauza TZS339.58 per soda na wauzaji wa rejareja wanashauriwa wauze 400 per soda?faida TZS 60.42 ambayo ni kidogo sana kwa kuwa hata bei ya mabanda imepanda percent fulani......Vocha,makampuni ya simu yanauza 490 kwa vocha ya 500 na 980 kwa vocha ya 1000...sasa wadau muuzaji wa rejareja huyu akiuza kwa hizo recommended price atafika kweli?walikuwa wanauza 460 kwa 940 kwa vocha za 500 na 1000 respectively sasa wamepandisha ila wanataka warejareja wabaki palepale itawezekanaje? MAISHA NDO YANAPANDA HIVYO.!!!!!!
 
-Arrrrg mnalalamika lalamika nini na nyie??

Kumbu kumbu zangu zinaonyesha kuwa hakuna huduma iliyowahi kususiwa baada ya kupandishwa bei zaidi ya kinywaji cha CHIBUKU…..nakumbuka wanywaji waliisusia na ikapunguzwa bei…

Mnasubiri nini na nyie?? Wasusieni for one week muone kama hawatashusha…..otherwise mkiendelea kulalama mods pls futa post zao….
 
huu ni wizi jamani, toka lini muda wa maongezi wa sh 1000 ukauzwa 1100 je huu ni uungwana?
 
huu ni wizi jamani, toka lini muda wa maongezi wa sh 1000 ukauzwa 1100 je huu ni uungwana?

Hivi wewe Lugaon ukinunua bidhaa fulani kwa bei ya jumla ya sh. 1000 au 980 unategemea kuiuza kwa shilingi ngapi?
Jibu utakalopata ndio maana yake.
 
ungejua sheria sio HAKI usingeyasema haya...hata soda zimepanda kwa taarifa yako....TZS500 per soda. tatizo ni serikali wamepandisha kodi ya products hizi.. producers wanauza TZS339.58 per soda na wauzaji wa rejareja wanashauriwa wauze 400 per soda?faida TZS 60.42 ambayo ni kidogo sana kwa kuwa hata bei ya mabanda imepanda percent fulani......Vocha,makampuni ya simu yanauza 490 kwa vocha ya 500 na 980 kwa vocha ya 1000...sasa wadau muuzaji wa rejareja huyu akiuza kwa hizo recommended price atafika kweli?walikuwa wanauza 460 kwa 940 kwa vocha za 500 na 1000 respectively sasa wamepandisha ila wanataka warejareja wabaki palepale itawezekanaje? MAISHA NDO YANAPANDA HIVYO.!!!!!!

Alichosema huyu Vakwavwe ni kweli kabisa.
 
Haya mambo hayafanani kabisa na ya nchi yenye demokrasia, ukisoma hotuba ya mbunge mahiri Dr. Slaa ukaona gharama za chai maofisini na takrima vilivyopewa umuhimu kwa kutengewa fungu kubwa la fedha utashindwa kuelewa ni wapi nchi inapelekwa.

Wasomi wa nchi hii tuna "responibility" kubwa sana ya kuhakikisha watanzania wote wanaelewa haya mambo, else we can expect no changes in the near future. Uchaguzi mdogo wa Busanda ni mfano na ushaidi mkubwa wa jinsi ambavyo wananchi wengi hawaelewi Chama Cha Mafisadi kilivyo jaa ubabe!
 
mhh.. naona zote zimepanda!

ungejua sheria sio HAKI usingeyasema haya...hata soda zimepanda kwa taarifa yako....TZS500 per soda. tatizo ni serikali wamepandisha kodi ya products hizi.. producers wanauza TZS339.58 per soda na wauzaji wa rejareja wanashauriwa wauze 400 per soda?faida TZS 60.42 ambayo ni kidogo sana kwa kuwa hata bei ya mabanda imepanda percent fulani......Vocha,makampuni ya simu yanauza 490 kwa vocha ya 500 na 980 kwa vocha ya 1000...sasa wadau muuzaji wa rejareja huyu akiuza kwa hizo recommended price atafika kweli?walikuwa wanauza 460 kwa 940 kwa vocha za 500 na 1000 respectively sasa wamepandisha ila wanataka warejareja wabaki palepale itawezekanaje? MAISHA NDO YANAPANDA HIVYO.!!!!!!

Mkuu kama zote zimepanda, nadhani wataalamu wanaweza kusema hapo hizo kampuni zimekubaliana. Hata ukisema tax imepanda, ma-managers wa hizi kampuni za simu hawawezi kuja na solution moja ya kupandisha vocha kwa asilimia sawa. Kuna njia nyingine nyingi ambazo wangeweza kuchukua...kwa mfano, kupunguza muda wa kuongea na hiyo 1000. Bei ile ile, unapata muda kidogo. Hiyo isingeshtua watu sana kama kuuza ghali muda wa 1000 kwa 1100. Kinachonishangaza zaidi ni wote wamekuja na solution moja ya kupandisha bei ya muda kutoka 1000 kwenda 1100. Hii nadhani ni collusion fulani ivi. Sema ndo bongo yetu...sheria zimelala. Kitu kama hichi kingetakiwa kuchunguzwa sana.
Hivi ziko kampuni ngapi za simu? Sio tatu?
 
vema kama wamepandisha wabadilishe na chapisho badala ya 1000 waweke hiyo 1100 tujue moja, kiti kimeandikwa 1000 iweje utakiwe kulipia 1100, nini kinafichwa hapa, kama ni vigumu kubadilisha vocha kwa kuaw zimeishatolewa basi watafute jinsi ya kufidia katika gharama za upigaji wakati wanasubiri vocha zilizoandikwa bei mpya kuchapishwa!
 
Kwani tatizo la kuchapishwa 1000 ni nini? Wateja tunajua kuwa tunapata credit ya 1000, tunajua kuwa bei ni 1100. Sio kwamba tunanunua na matumaini ya kukuta credit ya 1100. Yaani hatujadanganywa kuzinunua tunafanya maamuzi wenyewe, na tunatoe hela huku tukijua tunachopata.

Sio rahisi wakakubali kuingia hasara ya mabilioni ya shiling huku wakisubiri vocha mpya.
 
serikali imetoa tamko kuwa haijapandisha bei za vocha na hao wafanya biashara wanaopandisha wanawahujumu wateja. bei ni kama ilivyochapishwa kwenye vocha yenyewe. ukichajiwa zaidi peleka huyo mhujumu kituo cha polisi
 
Back
Top Bottom