Mkanda wa jeshi (Herpes zoster/ shingles) fahamu kuhusu dalili na tiba yake

Ponda majani ya mkaratusi/msandarusi (gum /eucalyptus) na uweke kiasi kidogo kwenye maji yanayochemka,chemsha kwa dakika 15 kisha ipua sufuria na uache mchanganyiko upoe, chovya kitambaa kisafi kwenye mchanganyiko na ukamue maji yaliyozidi, kukunje kitambaa na ukiweke sehemu yenye malengelenge, rudia kuweka kitambaa kila baada ya saa 2.

2.unaweza kutumia majani ya gerania (geranium) au mrujuani (lavender) kama hakuna msandarusi /mkaratusi (gum /eucalyptus)

3.Ponda kidonge kimoja cha aspirin na uchangaye na vijiko viwili vya vaseline kisha upake kwenye malengelenge, unaweza kurudia mara 3 kwa siku (zingatia panadol, paracetamol hazifai kwa mkanda wa jeshi)

Kama hakuna unafuu Ndani ya wiki 2 (au kama malengelenge yamepata uambukizo) tafadhali nenda hospital. Nasubiri mrejesho!
 
mi nakushauri uende hospital utapata sindano na dawa ya kupaka
 
Unakula kitunguu saumu kizima kabisa au punje mzizi mkavu? Je unakitafuna au ni kama hiyo njia ulioleza mwanzo?
Unakula kitunguu saumu kizima kam nilivyoeleza hapo mara ya pili kwa muda wa siku 7 au siku 14 kila siku asubuhi kabla ya kula kitu mugloka
 
Last edited by a moderator:
please,nisaidieni majina hamuwezi amini siyajui hata baada ya kumaliza form four katika shule ya kata,walimu wa kata,madarasa ya kata pamoja na matokeo yangu ya kata.
 
please,nisaidieni majina hamuwezi amini siyajui hata baada ya kumaliza form four katika shule ya kata,walimu wa kata,madarasa ya kata pamoja na matokeo yangu ya kata.

Wewe unaumwa!! Eti kata! Kata! Nani alikudanganya sekondari ni vyuo vya tiba?!!
 
kuna dogo ana blister kama miezi 3 mgongoni na kwenye mkono kwenye maungio je inaweza kuwa mkanda wa jeshi@mzizi mkavu
 
Wakuu Habari zenu?
Mke wangu ambaye ni mjamzito alipata vipele msongamano mwilini juu ya kiuno kuanzia uti wa mgongo kuja upande wa tumboni. Pia iliambatana na maumivu makali Sana.

Alienda Zahanati akapimwa damu na mkojo akaonekana Hana shida. Dokta kamuandikia atumie Detol, Entezema na Erithromycin ili kutibu alichokiona kuwa ni skin rashes.

Baada ya kuangalia magonjwa mbalimbali kwa mtandao niliona picha inayofanana na hali ya mke wangu, kuwa ni Herpes zoster. Na hata dalili kadhaa nilipomuuliza zilifanana na zilizoelezwa pale.

Sasa wakuu Naona hataiweza Erithromycin kwa sababu ameitumia mwezi wa tatu na mwezi wa nane kwa shida nyinginezo alizokuwa nazo. Na pia kwa hali yake ya sasa kuwa ni mjamzito, ningeomba dawa mbadala.

Updates:
Jana nilitoka nyumbani na kumuacha wife akiwa ameanza dozi ya erithromycin. Pia nilikuwa nimrudishe hospitali lakini mvua kubwa ikanyesha. Hata hivyo mvua ilipotulia, aliwasiliana na docta wa Arusha Dispensary bwana Joshua ambaye Mara kwa Mara hututibia. Dokta huyo alimuita na kumcheki kisha kukomfirm kuwa ni herpes hao walikuwa wakimshambulia.

Anaeleza kuwa alidungwa sindano makalioni, mikononi na mapajani kwa ajili ya kukausha vipele. Pia alishauriwa aendelee na erithromycin ila aache Mara Moja matumizi ya ile Entezma na badala yake atumie Acyclovir Kama inavoonyeshwa na mkuu MziziMkavu kwenye bandiko lake hapo chini.

Ntamaholo Fanya jambo nipate kurasa kazaa za Salamu kutoka kuzimu ili nijifariji. Maana natekeleza andiko lisemalo "labda kwa ugonjwa au kwa sala"

Update new:
Baada ya kumaliza dozi ya Acyclovir tembe na cream na pia Erithromycin, sasa mapele tamekauka. Kuna vijigamba gamba vinaendelea kudondoka na Ana nafuu Sana. Bado anaendelea na Indomethacin. Inatia faraja Sana.

Kirchhoff,
Arusha.
 
Last edited:
Mkuuu nadhani kuna haja ya kurud tena kwa daktari umueleze kwamba yale maelekezo ya mwanzo hayajafua dafu. Ili akupe altenaive nyengine.

Pole mkuuu, pole kwa mkeo pia
 
Back
Top Bottom