Mkama: CCM yashikilia urais kutopingwa mahakamani

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49
Wakati Tanzania ikiendelea kutoa maoni kuhusiana na kuandikwa kwa Katiba mpya, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinaendeleza utamaduni wa matokeo ya urais kutopingwa mahakamani.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mkama baada ya Tume ya Uchaguzi ya nchini Malawi kutembelea chama hicho kwa lengo la kujifunza jinsi chaguzi za Tanzania zinavyoendeshwa.

Maelezo hayo yamekuja kufuatia swali lililoulizwa na mmoja wa wajumbe wa tume hiyo kutoka Malawi, Mchungaji Maxwell Banda, ambaye alitaka kujua kama CCM kimeridhika na utaratibu wa sasa wa kutopinga matokeo hayo mahakamani.

Mkama alisema kupinga matokeo ya urais mahakamani ni kuifanya nchi kukaa muda mrefu bila Rais wakati ikisubiri hukumu itolewe. Aliongeza kuwa, maamuzi ya kesi kama hiyo huchukua miezi sita au zaidi.

Alitaja moja ya changamoto zilizopo kwenye chaguzi hapa nchini kuwa ni vyama vya upinzani kutoridhika na matokeo pindi yanapotangazwa. “Katika siasa siku zote mshindi huwa haulizi matokeo lakini uzoefu unaonyesha vyama pinzani vimekuwa havikubali matokeo yanayotangazwa,” alisema.

Kuhusu mgombea binafsi, Mkama alisema nchi ambayo haijakomaa kidemokrasia kama Tanzania ni vigumu kwa mgombea huyo kumudu gharama za uchaguzi.

Alisema mfumo wa vyama ni mzuri ikilinganishwa na mgombea binafsi kwa sababu maambuzi hufanywa na watu wengi wakati mtu binafsi hutumia misimamo yake.

Naye Banda alisema mtazamo wa wamalawi kuhusu mgombea binafsi wao huamini kuwa huleta changamoto kwenye vyama vya siasa kutokana na jinsi wanavyoendesha kampeni na kukuza demokrasia.

“Malawi wameruhusu mgombea binafsi kutokana na ukosefu wa demokrasia kwenye vyama na kwa sasa wana wabunge 39 kati ya 193 ambao wanatokana na wagombea binafsi,” alisema Banda.

Mjumbe mwinginewa tume hiyo ya Malawi, Gloria Chingota kwa upande wake alisema wamejifunza mambo mengi kupitia chaguzi za hapa nchini ambazo zitawaongoza kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2014.

Aliongeza kuwa, wataishauri serikali yao kuwa na viti maalum katika bunge lao kama ilivyo hapa Tanzania kwa lengo la kuwajengea uwezo wanawake wao. Pia alisema Tanzania inaweza kujifunza kutoka Malawi jinsi ya kuimarisha demokrasia.

Aidha alisema nchi yake ipo makini katika uchaguzi ambapo mpiga kura anaweza kupiga kura bila ya kuwa na kitambulisho kwa sababu wasimamizi huwatambua kwa picha na majina kupitia vituo vya kupigia kura.

Tume hiyo hapa nchini imetembelea Tume ya Uchaguzi nchini (NEC), mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na vyama vya siasa kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF).

CHANZO: NIPASHE

Kwa nini viongozi wengi wa nchi hii huwa wanatoa majibu mepesi mepesi katika hoja nzito? Hata Mukama naye kumbe ni wale wale? Kazi tunayo.
 
CCM iangalie kauli hiyo isiwatokee puani kama KANU ya Kenya did the same na kukataa kubadilisha katiba kwa sababu wakati huo walikuwa chama tawala.Haikupita muda wakashindwa na kuwaomba walioshinda wabadilishe katiba lakini walikataa na kuwaambia acha na sisi tufaidi.Hivyo 2015 au 2020 sio mbali chama chochote cha upinzani kinaweza kushinda kwani Watanzania wanabadilika sana .Mimi watoto wangu wakianza kupiga kura hawatakuwa wanajua kuhusu CCM au Nyerere kiivyo!na kwa ilivyo kwa CCM kutorecruit Vijana na hata kuwapa fursa za uongozi .So angalieni kauli zenu zitawatafuna soon
 
Mkama kachanganyikiwa na matokeo ya igunga jela imemkosakosa kwa matamko yake, sasa hivi anaweweseka
 
Hofu ya kushindwa uchaguzi na kuchakachua matokeo ndiyo kunakowafanya waendelee kuwa na misimamo iliyopitwa na wakati kama hii ya urais kutopingwa mahakamani.
 
Mnyika anasema hayo ni maneno ya uchizi chizi
wanadhani bado nchi ni chama kimoja kushika hatamu
wamefunga macho na masikio kutokubali watanzania wameamka sasa
naona viongozi wa magamba wamekengeuka
 
Mimi naona kama Mzee Mukama ana point hapa. Kwa hulka ya kiafrika ya kutoridhika, ubinafsi, na kupenda madaraka sana, ni makosa matokeo ya urais kuruhusiwa kuhojiwa mahakamani. Kwa vyovyote vile ukipitisha sheria hii, kwamba urais uhojiwe mahakamani, itatokea kama alivyosema Mukama. Mrema angepinga urais wa Mkapa 1995 na nchi ingekaa na ombwe la uongozi kwa miezi sita na zaidi, Lipumba angepinga urais wa Mkapa 2000, Lipumba angepinga urais wa Kikwete 2005, Dr. Slaa angepinga urais wa Kikwete 2010.......na kwa hali ilivyo, 2015 Chadema wanachukua nchi, na kama sheria hii itaruhusiwa basi CCM watapinga urais wa Chadema mahakamani.
 
I dont understand Mukama anamaanisha nini anaposema 'wapinzania hawaridhiki na matokeo pindi yanapotangazwa? Where does that leave the Tume ya uchaguzi kama watu wanayakataa matokeo?
 
Wakati Tanzania ikiendelea kutoa maoni kuhusiana na kuandikwa kwa Katiba mpya, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinaendeleza utamaduni wa matokeo ya urais kutopingwa mahakamani.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mkama baada ya Tume ya Uchaguzi ya nchini Malawi kutembelea chama hicho kwa lengo la kujifunza jinsi chaguzi za Tanzania zinavyoendeshwa.

Maelezo hayo yamekuja kufuatia swali lililoulizwa na mmoja wa wajumbe wa tume hiyo kutoka Malawi, Mchungaji Maxwell Banda, ambaye alitaka kujua kama CCM kimeridhika na utaratibu wa sasa wa kutopinga matokeo hayo mahakamani.

Mkama alisema kupinga matokeo ya urais mahakamani ni kuifanya nchi kukaa muda mrefu bila Rais wakati ikisubiri hukumu itolewe. Aliongeza kuwa, maamuzi ya kesi kama hiyo huchukua miezi sita au zaidi.

Alitaja moja ya changamoto zilizopo kwenye chaguzi hapa nchini kuwa ni vyama vya upinzani kutoridhika na matokeo pindi yanapotangazwa. “Katika siasa siku zote mshindi huwa haulizi matokeo lakini uzoefu unaonyesha vyama pinzani vimekuwa havikubali matokeo yanayotangazwa,” alisema.

Kuhusu mgombea binafsi, Mkama alisema nchi ambayo haijakomaa kidemokrasia kama Tanzania ni vigumu kwa mgombea huyo kumudu gharama za uchaguzi.

Alisema mfumo wa vyama ni mzuri ikilinganishwa na mgombea binafsi kwa sababu maambuzi hufanywa na watu wengi wakati mtu binafsi hutumia misimamo yake.

Naye Banda alisema mtazamo wa wamalawi kuhusu mgombea binafsi wao huamini kuwa huleta changamoto kwenye vyama vya siasa kutokana na jinsi wanavyoendesha kampeni na kukuza demokrasia.

“Malawi wameruhusu mgombea binafsi kutokana na ukosefu wa demokrasia kwenye vyama na kwa sasa wana wabunge 39 kati ya 193 ambao wanatokana na wagombea binafsi,” alisema Banda.

Mjumbe mwinginewa tume hiyo ya Malawi, Gloria Chingota kwa upande wake alisema wamejifunza mambo mengi kupitia chaguzi za hapa nchini ambazo zitawaongoza kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2014.

Aliongeza kuwa, wataishauri serikali yao kuwa na viti maalum katika bunge lao kama ilivyo hapa Tanzania kwa lengo la kuwajengea uwezo wanawake wao. Pia alisema Tanzania inaweza kujifunza kutoka Malawi jinsi ya kuimarisha demokrasia.

Aidha alisema nchi yake ipo makini katika uchaguzi ambapo mpiga kura anaweza kupiga kura bila ya kuwa na kitambulisho kwa sababu wasimamizi huwatambua kwa picha na majina kupitia vituo vya kupigia kura.

Tume hiyo hapa nchini imetembelea Tume ya Uchaguzi nchini (NEC), mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na vyama vya siasa kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF).

CHANZO: NIPASHE

Hakika majibu yaliyotolewa na mkama yameonyesha kiwango halisi cha ukilaza katika madani za siasa za wakati huu. Sasa naanza kuamini kuwa mzee amefikia mwisho wa kufikiri, ubogo na moyo wake kama jiwe kama Dr Slaa alivyosema majuzi na pia akili zake sasa zaweza kufananishwa na akili za maiti

Kama hajatambua, maelezo yaliyotolewa na wajumbe wa tume ya uchaguzi Malawi matusi kwake, lakini kwa jinsi akili yake ilivyoganda halioni hilo.
 
Mimi naona kama Mzee Mukama ana point hapa. Kwa hulka ya kiafrika ya kutoridhika, ubinafsi, na kupenda madaraka sana, ni makosa matokeo ya urais kuruhusiwa kuhojiwa mahakamani. Kwa vyovyote vile ukipitisha sheria hii, kwamba urais uhojiwe mahakamani, itatokea kama alivyosema Mukama. Mrema angepinga urais wa Mkapa 1995 na nchi ingekaa na ombwe la uongozi kwa miezi sita na zaidi, Lipumba angepinga urais wa Mkapa 2000, Lipumba angepinga urais wa Kikwete 2005, Dr. Slaa angepinga urais wa Kikwete 2010.......na kwa hali ilivyo, 2015 Chadema wanachukua nchi, na kama sheria hii itaruhusiwa basi CCM watapinga urais wa Chadema mahakamani.....

Demokrasia ina gharama zake na kwakuwa tumeamua kufuata mfumo wa demokrasia lazima tuzikubali gharama zake.

Ni kweli katika nchi nyingi za kiafrika wapinzani wamekuwa wakipinga matokeo mara wanaposhindwa uchaguzi lakini usisahau kuwa hata vyama tawala vimekuwa vikifanya hivyo hivyo inapotokea vimeshindwa.

Pia ukumbuke kuwa madai ya upinzani juu ya ukiukaji wa sheria na taratibu za uchaguzi yamekuwa yakithibitishwa kuwa na ukweli na ndiyo maana hata vyama tawala vimekuwa vikikubali serikali za mseto.Nakushauri uvute kumbukumbu kwa yaliyotokea Kenya, Zimbabwe, Malawi n.k.
 
Mimi naona kama Mzee Mukama ana point hapa. Kwa hulka ya kiafrika ya kutoridhika, ubinafsi, na kupenda madaraka sana, ni makosa matokeo ya urais kuruhusiwa kuhojiwa mahakamani. Kwa vyovyote vile ukipitisha sheria hii, kwamba urais uhojiwe mahakamani, itatokea kama alivyosema Mukama. Mrema angepinga urais wa Mkapa 1995 na nchi ingekaa na ombwe la uongozi kwa miezi sita na zaidi, Lipumba angepinga urais wa Mkapa 2000, Lipumba angepinga urais wa Kikwete 2005, Dr. Slaa angepinga urais wa Kikwete 2010.......na kwa hali ilivyo, 2015 Chadema wanachukua nchi, na kama sheria hii itaruhusiwa basi CCM watapinga urais wa Chadema mahakamani.
zimmerman tokea pendekezo nini kifanyike ili sisi wapiga kura au wapigiwa kura tusiwe na shaka na matokeo yanayotangazwa na tume ya uchaguzi. Kwa nini nchi nyingine hata kabla ya kumalizika zoezi la kutangaza matokeo ya vituo vyote mgombea anayehisi kushindwa anampongeza anahisiwa kushinda?
 
Last edited by a moderator:
SIKU hizi CCM kila mtu anatoa mawazo yake na kusema ni ya Chama. Japo Mukama ni mtendaji mkuu wa CCM, sifikiri kama walikaa kama chama na haya asemayo ni maziomio ya kikao au ameshauriwa na mkewe kaja kututangazia! lazima uamuzi wa igunga umemtingisha huyu baba! Bora angesema haya ni mawazo yake, maana anarusiwa kutoa maoni yak.
 
Hakika majibu yaliyotolewa na mkama yameonyesha kiwango halisi cha ukilaza katika madani za siasa za wakati huu. Sasa naanza kuamini kuwa mzee amefikia mwisho wa kufikiri, ubogo na moyo wake kama jiwe kama Dr Slaa alivyosema majuzi na pia akili zake sasa zaweza kufananishwa na akili za maiti

Kama hajatambua, maelezo yaliyotolewa na wajumbe wa tume ya uchaguzi Malawi matusi kwake, lakini kwa jinsi akili yake ilivyoganda halioni hilo.
bado wanafikiria kama kwamba nchi itabakia kuwa mikononi mwa CCM na udanganyifu utaendelea milele kadri watakavyotawala mililele kama alivyosema katibu mwenezi wake.
Hawajui kwamba hii itawasidia wao pia na itaongeza hofu wa wadanganyifu
 
zimmerman tokea pendekezo nini kifanyike ili sisi wapiga kura au wapigiwa kura tusiwe na shaka na matokeo yanayotangazwa na tume ya uchaguzi. Kwa nini nchi nyingine hata kabla ya kumalizika zoezi la kutangaza matokeo ya vituo vyote mgombea anayehisi kushindwa anampongeza anahisiwa kushinda?

Napendekeza hivi, kwenye katiba mpya, ili kuondoa kutoaminiana kwenye ngazi ya urais, kwa kuhofia uwezekano wa mshindwa kumpinga rais mahakamani basi nafasi ya urais ifutwe. Chama chenye wabunge wengi kitoe Waziri mkuu atakayekuwa na madaraka ya kuongoza serikali kama zilivyo Uingereza na Israel.

Napendekeza pia matumizi ya teknolojia katika kuhesabu kura. Mambo ya kukusanya matokeo kutoka kwenye kituo kimoja kimoja, kuyakusanya jimboni, jimboni wilayani, wilayani mkoani, mkoani hadi kwenye tume ya uchaguzi taifani ndiyo yanayoleta kutoaminiana. Yanatoa mwanya kwa mwenye mpini kujiamulia kujitangazia madaraka hata kama ameshindwa.

Halafu haya mambo ya kupinga matokeo kwa vigezo vya technicalities za kisheria, mara Godbless Lema aliwaambia wapiga kura wasimchague yule maana ni al qaeda...etc. ni upuuzi unaotafuna hela zetu wavuja damu.

Hata hivyo sheria yetu ya sasa ya uchaguzi pamoja na madhaifu yake ilikuwa na common sense kidogo. Iliruhusu ubunge upingwe mahakamani lakini kwa ngazi ya urais iliona madhara. Majimbo ya Arusha, Sumbawanga, na sasa Igunga yamekaa bila wabunge lakini mambo yanaenda, utafanya hivyo kwa Amiri jeshi mkuu?

Ni nani atakayepinga Waziri Mkuu mahakamani nafasi inayopatikana kutokana na idadi ya wabunge wa chama chako?
 
"Sisi CCM hatuhofii hili la mgombea binafsi, kwanza likikubalika wapinzani ndio watakaoumia.. Unadhani kama kungekuwa na mgombea binafsi nani angehamia upinzani?" Nape alisema na kuhoji .

contradictions never cease in ccm.
 
Napendekeza hivi, kwenye katiba mpya, ili kuondoa kutoaminiana kwenye ngazi ya urais, kwa kuhofia uwezekano wa mshindwa kumpinga rais mahakamani basi nafasi ya urais ifutwe. Chama chenye wabunge wengi kitoe Waziri mkuu atakayekuwa na madaraka ya kuongoza serikali kama zilivyo Uingereza na Israel.

Napendekeza pia matumizi ya teknolojia katika kuhesabu kura. Mambo ya kukusanya matokeo kutoka kwenye kituo kimoja kimoja, kuyakusanya jimboni, jimboni wilayani, wilayani mkoani, mkoani hadi kwenye tume ya uchaguzi taifani ndiyo yanayoleta kutoaminiana. Yanatoa mwanya kwa mwenye mpini kujiamulia kujitangazia madaraka hata kama ameshindwa.

Halafu haya mambo ya kupinga matokeo kwa vigezo vya technicalities za kisheria, mara Godbless Lema aliwaambia wapiga kura wasimchague yule maana ni al qaeda...etc. ni upuuzi unaotafuna hela zetu wavuja damu.

Hata hivyo sheria yetu ya sasa ya uchaguzi pamoja na madhaifu yake ilikuwa na common sense kidogo. Iliruhusu ubunge upingwe mahakamani lakini kwa ngazi ya urais iliona madhara. Majimbo ya Arusha, Sumbawanga, na sasa Igunga yamekaa bila wabunge lakini mambo yanaenda, utafanya hivyo kwa Amiri jeshi mkuu?

Ni nani atakayepinga Waziri Mkuu mahakamani nafasi inayopatikana kutokana na idadi ya wabunge wa chama chako?
SIMmerman huyo Waziri Mkuu atapatikanaje ndani ya chama chenye wabunge wengi? Uingereza wanaotazamiwa kuwa waziri mkuu huongoza kampeni za vyama vyao ili vipate wawakilishi wengi kama ilivyo kwa mgombea raisi hapa kwetu.
 
SIMmerman huyo Waziri Mkuu atapatikanaje ndani ya chama chenye wabunge wengi? Uingereza wanaotazamiwa kuwa waziri mkuu huongoza kampeni za vyama vyao ili vipate wawakilishi wengi kama ilivyo kwa mgombea raisi hapa kwetu.....

Ndio, vyama vya siasa vitahusika kuchagua watu watakao spearhead campaign za wawakilishi ili wao wapate nafasi ya uwaziri mkuu iwapo vyama vyao vitakubalika na wananchi kwa kuzingatia nafasi za uwakilishi walizopata bungeni.

Hata hapa kwetu kuna dalili kwamba inawezekana. Chachu kuu iliyosaidia CHADEMA kupata uwakilishi walionao sasa bungeni ni Dr. Slaa.

Kukubalika kwa Dr. Slaa, kulipelekea kukubalika kwa wagombea ubunge kupitia CHADEMA. Na kimsingi kama wangekuwa wengi na wa kutosha kuwa majority bungeni, na kama katiba inaruhusu hivyo, basi Dr. Slaa angequalify automatically kuwa Waziri Mkuu wa JMT ambaye pia ni Mkuu wa serikali.

Hata hivyo mi sio mwanasiasa na wala sijui sana mambo ya siasa. Sijui kwanini, kwa mfano, Nyerere aliabolish mfumo wa Kiingereza na kuweka mambo ya urais.

Mimi naona kama urais nchini kwetu ni mfumo fulani wa ufalme: madaraka yote anayahodhi mtu mmoja na kwa mfumo huu kuhoji ufalme mahakamani na nchi ikakaa bila mtu mwenye hayo madaraka ni hatari.
 
Dawa ya tatizo hili ni kurudisha kipengere cha mshindi kupata asilimia zaidi ya hamsini ya kura zote. Kipengere hicho kilienguliwa na mkapa kwenye "white paper" yake na kuweka cha "simple majority".
 
Back
Top Bottom