mkakati wa serikali ya tano kiuchumi

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,658
2,804
Kumekuwa na malalamiko mengi sana huko uraiani kuhusu ugumu wa maisha na hali kuwa ngumu kuliko kawaida tokea kuanza kazi ka Serikali hii ya awamu ya tano inayosimamiwa na Mhe Dk John Joseph Pombe Magufuli.

Wengi wetu tumekuwa tukilia ugumu wa maisha huku tukijaribu kuoanisha mambo yalivyo sasa na mwaka wa mwisho au miaka ya mwisho ya Rais wa awamu ya Nne Dk Kikwete,wengi tunasema hela haipatikani,hela ngumu na vitu kama hivyo.

Kwa kukusaidia tu ,hali kama hii ni vyema ukatambua kuwa ipo karibu miaka yote ya maraisi wapya na hujitokeza kati ya mwaka wa kwanza na wa pili wa serikali mpya hii ni kutokana na kuwa katika kipindi hiki chote Serikali huwa inajipanga katika kujijenga upya kuanzia kimikakati na hata kiutendaji ukitia ndani na mikakati iliyoachwa na serikali iliyokwisha.

Katika kipindi hiki cha mwanzani hali za maisha ya watu huwa ngumu kuliko kawida kutokana na pesa nyingi kushikiliwa na serikali kwa ajili ya kuimarisha idara za serikali kwa ajili ya serikali mpya kwa miaka mitano hadi kumi ijayo hali ambayo inachangia ugumu wa maisha.

Ukivuta kumbukumbu utakubaliana nami kuwa hata katika miaka miwili ya mwanzao ya JK watu walikuwa wanamponda sana na kusema hayo maisha mapya kwa kila mtanzania yako wapi,miaka kumi imepita leo hii watu wanadai walikuwa wanaishi maisha bora yenye uchumi nafuu kwa kila mtu huku pesa ikipatikana ,hii ni kutokana na Serikali ya awamu ya nne kutumia miaka miwili yake ya mwanzo katika kuijenga sera hiyo ambayo iliyaongoza maisha ya watu kwa kipindi chote.

Sera ya hapa kazi tu ya Mhe Magufuli ni vigumu leo hii kuanza kuina matunda yake hasa ikizingatiwa ndio kwanza inaaanza kufanya kazi ,kupitia sera hii kutakuwa na sera ndogo ndogo zitakazoanzishwa ili kuhakikisha lengo linatimia,kwa mutadha huo huenda hali ngumu ya maisha ikawa juu kwa kipindi hiki cha miaka miwili ya mwanzo ya utawala a JPM .

Hivo wanandugu ni vyea tukawa na subra katika kuangalia utendaji kazi wa Serikali hii ,na lawama juu ya serikali hii tuanweza kuziweka hadharani katika mwisho wa meaka wa tatu na nne ya utawala wa JPM kwani kwa kipindi hiko tayari kutakuwa na picha halisi ya sera hii ya HAPA KAZI TU
 
Back
Top Bottom