Mkakati wa kuwavua ubunge wabunge wa CHADEMA wafichuliwa

Walichofanya ccm kwa kweli ni mbaya sanaaaaa.... Tokea wamvue Lema ubungu nimekuwa usiku silali, uzingizi hauji kabisa, naona ni bora kufa kulikoni kuendelea kuishi na haya majitu yanayoitwa ccm. Wanaroho mbaya sana kila kitu wanafikiria kwa matumbo yao!!!
 
MUNGU akazidi kuufanya moyo wa Farao mgumu mbele ya Musa ili apate kujitukuza!!!
Tuyaache yajifanye vichwa ngumu tu,, yanafikiri wa tz ni mambumbumbu kama yalivyozoea. Kwa mwendo huu 2015 mbona ni mbali sana?? Tusubiri kupiga kura za nini wakati tukipiga kura wanavuliwa baada ya muda? hakuna haja ya kusubiri tena kura kwa sababu uamuzi wetu unadharauliwa na wachache.
 
Heri ya Pasaka wana JF,
Kuna mkakati maalumu wa kuwavua ubunge wabunge wengine wanne wa CDM, lengo ni moja tu kupunguza nguvu ya chama.
Ni wazi kuwa kesi zote za wabunge wa CDM wamepewa majaji ambao sio waozefu na ndio wameteuliwa juzijuzi, kwa hyo wana maagizo maalumu kutoka ikulu.
Wabunge wanaotajwa kuvuliwa kwa vyovyote vile ni Lissu ambaye pamoja na mashahidi wa upande wa wadai kushindwa kuthibisha madai bado Jaji anashinikiza kesi iendelee.
Mwingine ni Mnyika ambae Jaji Upendo Msuya ameonyesha kuwa tayar ana yake kichwani kwa sababu yy na mdai ni marafiki sana na pia hata wakili wa upande wa wadai wamewahi kufanya kazi pamoja na Jaji. Lingine kubwa ni kuwa Jaji huyo ni kilaza sana kwenye kesi za uchaguzi na hana hukumu hata moja ya mambo hayo.
Opulikwa wa meatu na Mbasa wa Biharamulo pia wanatajwa kuwa wanavuliwa Ubunge.
Lengo: Lissu, Mnyika na Lema hawatakiwi kuwepo Bungeni wakati wa katiba mpya kutokana na misimamo yao
Source: watu waaminifu kwenye system

uvumilivu una kikomo chake, watambue kuwa watanzania si wajinga kihivyo. Wanatujaza hasira sana 2015 tutapiga kura za hasira, kisasi, kizalendo na kimaamuzi=magamba out! Wataficha wapi nyuso zao? Haya wee
 
HAWAWEZI KUENENDA BILA BUSARA KIASI HICHO!
kwani watajipunguzia heshima kwa jamii na hiyo itawaondoa magogoni 2015.kama kweli wana nia hiyo basi utakuwa ni ushauri mbaya kuwahi kutokea na kutekelezwa.
 
tunategemea kupata haki mahakamani na sio dhuluma. Vinginevyo watu wa mwanza, arusha, mbeya na musoma wajiandae.
 
Jmani, Mzaha mzaha ..... nyote mwajua hutunga usaha!!! Lema ilikuwa hivi hivi mzaha.. mzaha.. mzaha.. leo hayupo tena Bungeni! tukiishia kuongea hapa tuaishia kuwapoteaza hao wengine. Nila lazima mikakati ya dhati iwekwe kupambana na ujinga huu TUMECHOKA!!!!!!!!!
 
tusisahau kuomba Mungu.....wakati mwingine akili zetu huchoka sana tunapoacha kumtegemea Mungu na tunaweza fanya vibaya bila Mungu.....TUMEANZA NA MUNGU NA TUTAMALIZA NA MUNGU
 
Nyerere alisema huwezi kuwa kiongozi halafu unaishi kihunihuni tu, kama unataka kufanya uhuni kafanye barabarani.

Case ya Lema ni fundisho kwa wote wanaotumia majukwaa ya siasa kufanya uhuni wao. Kwa hao wengine I hope walishinda kihalali na kama ni hivyo basi wasiwe na mashaka kwakuwa sheria itafuata mkondo wake.
 
Hii itakuwa mbinu mbaya zaidi kwa ye yote anayepanga kuitumia, maana kama uchaguzi ukirudiwa washinde au cha chao kishinde itakuwa aibu ya mwaka.
 
Duu kama ndiyo utakuwa ndiyo mkakati wajue kuwa nchi hii wataeletea vurugu kubwa sana na watakuja potea kabisa katika ramani ya siasa ya nchi hii, vyama vya upinzani vingi vitapata nguvu kutoka kwa umma, na CCM itakuwa imekufa kifo cha Uzee
 
Wapime moto kwa KIDOLE cha mtoto mchanga waone.....wamefulia hakika. Yule Jamaa kijani na njano aliyetoa matusi kwa MBUNGE wetu VICENT NYERERE tunamuapia akifika MUSOMA tutamfanyizia sana tu. Ni muhuni na limbukeni wa kisiasa. Wathubutu kumgusa NYERERE katika mkakati wao waoneeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Saizi naanza kubeba kisu mfukoni. Huu ni upuuzi kabisa. Likitokea mbele yangu naona ni kumaliza kabisa.
 
:nod: Nakubaliana nawe mkuu...
kuna siku haya yote yatakwisha, yatakuwa kama Malawi..
Wote wanaoshiriki kuzingua wananchi, CDM ikiingia Magogoni
Ni kufukuza kazi, kamata weka lupango!
 
Back
Top Bottom