Mkakati wa Kumuhujumu JK na Lowassa

MVUA GAMBA

Senior Member
Apr 13, 2011
102
63
Wana JF,

Baada ya kikao cha NEC dodoma Mh MEMBE alimwaaita wajumbe wa NEC wafuatao na Kufanya NAO kikao Nyumbani kwake wajumbe hao ni

NAPE NNAUYE
Capt CHILIGATI
LUSINDE maarufu kwa Jina kibajaji
Makongoro Nyerere
Mzee Samweli sita ambae alifatwa nyumbani kwake akiwa amejipumzisha
Ndg Wilson Mukama

Wajumbe hawa walikutana nyumbani kwa MEMBE baada ya kikao cha nec mzee sita aliwahi kutoka kwenda kupumzika baada ya SUMAYE kuongea.

Katika kikao hicho ukaandaliwa mpango madhubuti wa kupambana na kikwete kwakua hawa jamaa wanaamini Kikwete amewatosa na kuamua kujiunga na Lowasam

Makubaliano.

(1) Kutoa siri za kikwete na hapa hasa mali alizonazo Nje ya Nchi na hapa atakae fanya hii kazi ni Bwana Membe.

(2) Kutumia urafiki uliopo kati ya Membe na baadhi ya watu ndani ya idara ya usalama kufanikisha Mpango huu.

(3) Mzee Samweli Sitta aanzishe mazungumzo na CHADEMA ama CUF ili kuandaa mpango wa kujiunga na chama kimojawapo kati ya hivo viwili kwakuwa Sitta ameona kuwa hakuna njia ya kumzuia Lowassa kushinda ndani ya CCM.

(4) Kutokana IMANI na matumaini ambayo NAPE aliyokuwa nayo baada ya mkutano wa JK na wabunge wa CCM Dodoma, NAPE alimfata Bwana Mwigulu akiwa na Chiligati, Nape amedaiwa kumwambia Mwigulu "Bwana MKUBWA (JK) ameishaingia line ameelekea KIBLA tusaidie kesho tummalize huyu Lowassa, mzee anataka sisi katika kamati kuu tuanzishe, kaka usituangushe"

Baada ya hili kutotokea NAPE amedai atahakikisha analipiza kisasi kwa kuanika SMS walizo-chat na JK, kuonyesha JK alikuwa anamtuma.

Mpango wao unalenga kwanza kuonyesha JK haaminiki, Pia wanadai kwakuwa amewasaliti watamuanika.

PIA Mbunge Ismail Aden RAGE akiwa uwanja wa Ndege wa Tabora Juzi katika VIP akiwa amefatana na Mbunge wa Bukene Selemani Zedi alinukuliwa akisema, "Nimeongea na Mzee Sitta amesema njia pekee ya kupambana na Lowassa na Kikwete ni Nje ya CCM, mimi najiandaa kuondoka" haya ni maneno ya sita ambayo Rage aliyanukuu kwa Selemeni Zedi na Rage akasema Nadhani mzee Sitta yupo Sahihi acha aende JK na Lowassa wote ni Mafisadi.

Wana JF, chanzo cha habari hizi ni mtu aliyekuwa katika vikao hivo vya Dodoma na Membe na Nape walikutana Protea wakiwa na Jack Gotham na Balozi wa heshima wa Comoro. Walikutana kuendelea kupanga mikakati, kumekuwa na Vikao vingi sana ambavyo vimeanza kufanyika, na Membe sasa na yeye anjipanga kuanza kutumia makanisa; hivi karibuni na yeye atakua na Harambee ktk kanisa Katoliki Magomeni.

Kwahiyo mnyukano CCM ndo umeanza sasa waliokuwa watu wa Kikwete sasa wanaanza mipango ya kumhujumu na kuanza kutoa siri za mali zake zilizopo Uarabuni.

Nawasilisha
 
Sooooooooooooon and very Soooooooooon ukilea kidonda tegemea nini?
 
Kikwete kajihujumu mwenyewe kwa kushindwa kutenda kazi zake kama kiongozi wa nchi. Angeweza hata kukamilisha 60% to 70% ya ahadi zake katika kampeni za 2005 basi Watanzania wengi tungemfagilia sana lakini hadi sasa hajaweza kutimiza hata 1% ya ahadi zile. Anatafuta mchawi kumbe mchawi ni yeye mwenyewe. URAIS si lelemama.
 
Nashauri tu memba wenzetu wengine kama wana uwezo mkubwa wa kutunga hadithi kama hizi ni kwa nini basi wasiandike vitabu vya hadithi ili wauze waingize pesa?
 
Nashauri tu memba wenzetu wengine kama wana uwezo mkubwa wa kutunga hadithi kama hizi ni kwa nini basi wasiandike vitabu vya hadithi ili wauze waingize pesa?

Mkuu kama ni hadithi basi jamaa anajua kutunga manake wahusika wote wanauvaa uhusika hasa kuanzia uwanja wa ndege Tabora hadi Dodoma!! Kwangu mimi sishangai kwa hali ilivyo ndani ya CCM kwa sasa. Nadhani mpasuko ni dhahiri ila sasa watakaopasuka ndio bado hawajajulikana. Ila kwa hadithi hii nimeanza kuona mwanga.
 
Wa-Tz mnacheza na TB JOSHUA?? NGOJA MUONE SASA

Yaani wewe mpaka kesho unaamini manabii wa uongo? Miujiza iliisha yesu alipoondoka duniani kama hujui hawa wote wanaojiita manabii wanamtumikia shetani hawana tofauti na sangoma.Ukienda kwa mganga hukosi la kuambiwa. Kama kweli atakuwa raisi Joshua alitakiwa amwambie hayo maono siyo yeye kuuliza eti nikigombea uraisi 2015 nitashinda? jibu ndiyo kwa joshua sianafanya biashara watu wanalipia huduma yake ulitaka amwambiaje. Nenda na wewe kamwambia huyo joshua miaka mitano ijao utakuwa hai au la uonejibu utakalopewa.

"Wapenzi, msiiamini kila roho, bali ZIJARIBUNI HIZO ROHO, kwamba zimetokana na Mungu kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani" (1Yohana 4:1).

"Angalieni, mtu asiwadanganye, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao WATAWADANGANYA WENGI ... Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki. Kwa maana watatokea MAKRISTO WA UONGO … nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate KUWAPOTEZA, kama yamkini hata walio wateule, Tazama, nimekwisha KUWAONYA MBELE" (Mathayo 24:5, 23-25).
 
Back
Top Bottom