Mkakati wa kulifunga MwanaHalisi, Kumziba Mengi na kumfukuza Sitta Waanza

Nyumbu-

JF-Expert Member
May 26, 2009
988
349
Katika hali ya kutapatapa na kuhakikisha mafisadi hawaguswi, juhudi za maksudi zimeanza kuchagiza kuzibwa midomo watu wote wanaojaribu kuongea ukweli.

Jitihada hizo zimeanza na gazeti la Rai, toleo la jana.

Katika gazeti hilo, mwandishi amelituhumu mwanahalisi kwamba ni jukwaa linalotumiwa na wabaya wa JK ili kuiangusha serikali.

Wanadai Mwanahalisi limejiandaa kuuhadaa umma kuwa JK hafai kwa kumhusisha JK na ufisadi wa nci hii na kusema yeye ni sehemu ya ufisadi au ni mfadhili wa uozo huo.

Wanalinukuu gazeti la Mwanahalisi la Jumatano hii kwa kujaribu kuonyesha uhusiano wa Manji, Rostam na Kagoda.

Pia wamechukizwa na makala inayosema "JK, jisafishe Kwanza mwenyewe kabla ya kusafisha CCM" nk. Wakati huo huo, Gazeti la mwanahalisi limeripoti kwamba toleo lao la wiki iliyopita lilihujumiwa kwa baadi ya vizito kununua nakala nyingi kwenye mikoa ya Mbeya ili watu wakose kusoma habari za Dowans nk ilki kuzia wananchi kupata welewa wa nini kilijiri katika mkataba huo wa kinyonyaji.

Kwa upande wa Mengi, anatuhumiwa kwamba ni mwanasiasa popo, kwani yuko CCM lakini ndiye kinara wa kutumia magazeti ya Mwanahalisi kumzunguka Kikwete.

Isitoshe ,Sitta anatuhumiwa kwamba anatumia uwepo wake kwenye CCM na Kamati kuu ili kumdoofisha JK, kwa kutoa siri za ndani ambazo Mwandishi anasema ni za kupikwa.

Katika makala hiyo, hakuachwa kuhusishwa Slaa na maandamano ya vyuo vikuu, na pia sehemu zinginezo. Wakimkandia Mengi, wamesema ni mfanyabiashara anayejifanya mzalendo na mwenye huruma wakati ni kinyume chake!

Wanahitimisha kwa kutaka vyombo vya usalama kuwadhibiti akina Mwanahalisi, Sitta na wenzake, na watu kama Mengi, kwani ni hatari kwa usalama wa taifa 'lililozoea amani na utulivu". Wanazidi kumpaka mafuta JK kwa kusema ndiye raisi pekee ambaye ameonyesha wazi kuchukia rushwa na kwamba amechukua hatua ya kuipa meno TAKUKURU na kwamba kesi kadhaa za ufisadi zimepelekwa mahakamani.

KAZI NDO IMEANZA........
 
Watu wamefunguka macho siku hizi, hiyo mikakati haitasaidia kitu... Ishu zitawafikia tu wananchi hata wakiamua kufunga viwanda vyote vya uchapishaji!!!!!
 
Siku zote penye ukweli uongo hujitenga, acha wapige kelele kwenye magazeti yao... Lakini mwisho wa siku dhaifu atajulikana sababu maisha ya mwananchi wa kawaida yanazidi kuwa magumu wakati viongozi na wanaccm wachache wanazidi kuwa matajiri.... Siku wananchi wakichoka na wameshaanza kuchoka hutowatuliza kwa makala za kipuuzi kwenye magazeti uchwara!!!:coffee:
 
Ukisikia paa uje imekukosa, aliyerenga hana shabaa. Ndio kama hizo njama za kitoto zilizoandikwa. Binafsi nahisi hiyo nakala imeandikwa na either Lowasa au Rostam halafu akampa mwandishi huyo atoke nayo. Ingawa huwa sisomi Rai na sina mpango wa kuitafuta hiyo habari lakini inaonyesha mwandishi ni mtu wa karibu mno na JK na anajua udhaifu wa JK wa kupenda kusifiwa na kusikiliza hoja za kitoto kama za huyu anataka kuwachanganisha, huyu anataka nchi isitawalike nk. Kwa kuwa Slaa anamnyima usingizi JK jamaa wameamua kumfariji mkwere kwa kudai Slaa anachochea migomo vyuoni wakati wanafunzi wameishasema wazi nini madai yao. Ushauri wangu kwa mwandishi, JK mwenyewe ndo anataka nchi isitawalike kwa kutuzidishia mgao wa umeme hadi hapo Mungu atakapotuhurumia, nchi itatawalikaje gizani jamani?? Kila kitu bei juu kwa sasa, hadi chumvi, sukari, mafuta ya kupikia, vitunguu, nyanya... Je hapo nchi itatawalika?? Na ole wenu muilipe Dowans....
 
Tatizo la hawa watu nguvu zote wanamalizia kwenye mikakati ya kijinga badala ya kutatua matatizo ya wananchi, mapimbi kweli yani hayajui hata kula na kipofu
 
Shaka ondoa, watanzania wameamka. Ikumbukwe Tunisia na Misri sababu kubwa ya mwanzo wa maandamano haikuwa kuagusha serikali bali zilikuwa ni kadai uhuru wa kupata habari na ugumu wa maisha.

Wakifuata ushauri wa huyo mwandishi wajue wanaweza wakawa wanawaelekeza watanzania chakufanya!
 
Unajua mambo inayoandika mwana Halisi kama yangekuwa ya uongo gazeti lingefungiwa milele kutokana na kuchochea vurugu na kuchonganisha serikali na wananchi na Kubenea asingetakiwa aanzishe gazeti lingine lolote zu kufanya kazi ya uhariri popote pale. Lakini ni ukweli mtupu pale mwana Halisi ni mdomo wa watu wanaitakia nji mazuri kuikosoa serikali kwa data za ukweli kabisa!
Siyo rahisi kabisa Kubenea kupata data za ndani kiasi kile bila be trail kutoka serikali ya JK.
 
Rai ni gazeti lililonunuliwa na Rostam Aziz kwa madhumuni binafsi hivyo sishangai kuona tahariri ya namna hii
 
Labda wanunue magazeti yoooooote ndio tutakosa habari. Hapa kwetu tuna utaratibu tukikosa gazeti, mwenye nalo anatoa copy anatugawia. Hukumu ya icc inasomwa kama hadithi kila mtu anataka kuifahamu.
 
RAI=Rostam Azizi Incharge,jamani bado mnasoma hili gazeti la RAi lilipotosea mwelekeo km chama cha ccm?badilika kaka hilo gazeti wanasoma mafisadi wanaodhani kila mtu analipenda
 
mkuu hadi leo huwa unasoma gazeti la RAI?hebu badilika ndugu yangu

Njia pekee ya kumjua adui yako ni kujifanya mjinga na umsikilize. Baada ya hapo unatwanga kirahisi.
"The art of an assassin is to draw the victim closer; it makes stabing easier"
So ni vizuri tuwasome, ili tuwajue wanachopanga......au vipi Mkuu?
 
Hivi bado watu wanasoma Rai ?.

Mkuu ni vizuri kulisoma. Ndani yake pia kuna makala ya kupigia chapuo malipo ya Dowans, huku wakimponda Sitta kwamba ndiye aliyesababisha maumivu kwa serikali kwa kuishauri ivunje mkataba na Dowans.......kuna makala uchwara za udini na Slaa.....I advice you to get a copy and read the crap!
 
Niko tayari kulisoma Rai online ili kujuwa upuuzi wao, lakini siko tayari kutoa shillingi miatano yangu kununuwa hilo gazeti, kwani kulinunuwa hilo gazeti tafsiri yake ni wewe kuendelea kumuongezea utajili fisadi Rostam Aziz & co.
 
Katika hali ya kutapatapa na kuhakikisha mafisadi hawaguswi, juhudi za maksudi zimeanza kuchagiza kuzibwa midomo watu wote wanaojaribu kuongea ukweli.
Jitihada hizo zimeanza na gazeti la Rai, toleo la jana.
Katika gazeti hilo, mwandishi amelituhumu mwanahalisi kwamba ni jukwaa linalotumiwa na wabaya wa JK ili kuiangusha serikali.
Wanadai Mwanahalisi limejiandaa kuuhadaa umma kuwa JK hafai kwa kumhusisha JK na ufisadi wa nci hii na kusema yeye ni sehemu ya ufisadi au ni mfadhili wa uozo huo.
Wanalinukuu gazeti la Mwanahalisi la Jumatano hii kwa kujaribu kuonyesha uhusiano wa Manji, Rostam na Kagoda.
Pia wamechukizwa na makala inayosema "JK, jisafishe Kwanza mwenyewe kabla ya kusafisha CCM" nk. Wakati huo huo, Gazeti la mwanahalisi limeripoti kwamba toleo lao la wiki iliyopita lilihujumiwa kwa baadi ya vizito kununua nakala nyingi kwenye mikoa ya Mbeya ili watu wakose kusoma habari za Dowans nk ilki kuzia wananchi kupata welewa wa nini kilijiri katika mkataba huo wa kinyonyaji.
Kwa upande wa Mengi, anatuhumiwa kwamba ni mwanasiasa popo, kwani yuko CCM lakini ndiye kinara wa kutumia magazeti ya Mwanahalisi kumzunguka Kikwete.
Isitoshe ,Sitta anatuhumiwa kwamba anatumia uwepo wake kwenye CCM na Kamati kuu ili kumdoofisha JK, kwa kutoa siri za ndani ambazo Mwandishi anasema ni za kupikwa.
Katika makala hiyo, hakuachwa kuhusishwa Slaa na maandamano ya vyuo vikuu, na pia sehemu zinginezo. Wakimkandia Mengi, wamesema ni mfanyabiashara anayejifanya mzalendo na mwenye huruma wakati ni kinyume chake!
Wanahitimisha kwa kutaka vyombo vya usalama kuwadhibiti akina Mwanahalisi, Sitta na wenzake, na watu kama Mengi, kwani ni hatari kwa usalama wa taifa 'lililozoea amani na utulivu". Wanazidi kumpaka mafuta JK kwa kusema ndiye raisi pekee ambaye ameonyesha wazi kuchukia rushwa na kwamba amechukua hatua ya kuipa meno TAKUKURU na kwamba kesi kadhaa za ufisadi zimepelekwa mahakamani.

KAZI NDO IMEANZA........

RELAX Bro watanzania wa leo wana akili za kutosha, Hawawezi vumilia uozo huo TANZANIA YENYE NEEMA YAJA, Watumie rai, mtanzania, uhuru, mzalendo, tbc(japo ni jasho letu), kifo chao kimefika hawawezi toka!!!!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom