Mkakati wa kina Ponda waanza kukwama Dar

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
Ule mkakati unaoratibiwa na Sheikh Ponda Issa Ponda wa kushawishi waislam wasishiriki zoezi la sensa lililoanza leo linaelekea kutopata mafanikio baada ya waislam walioweka mabango majumbani kwao ya kutokuhesabiwa kukubali wenyewe kuhesabiwa bila kikwazo.

Shuhuda wa habari hizi ambaye ni mimi mwenyewe nimeshuhudia makumi ya waislam wakihesabiwa kuanzia ubungo jirani na mitambo ya umeme ya Aggreco hadi mabibo ambapo waliohesabiwa walisema wanahesabiwa kwakuwa hawataki 'maneno' na serikali.

Walidai kuwa wanaunga mkono hoja za wenzao za kutokuhesabiwa lakini wakasema serikali ikiamua jambo haishindwi hivyo wanaepuka kitakachofuata baada ya huo mgomo.

Maeneo ya Mburahati, kigogo nq Luhanga mwitikio wa kuhesabiwa umekuwa mzuri, ingawa wapo wachache waliogoma lakini zimesikika lawama kutoka kwa baadhi ya Maustaadh wakilalamika KUSALITIWA na wenzao ambapo wamelia na WOGA wa waislam kwenye mambo aliyoyaita ya msingi.

Karani wa Sensa aliyekuwepo Mabibo -Sahara na Mabibo Muleba hadi jirani na Mabibo External wamesema hadi muda huu zoezi liko vizuri na wachache waliogoma watashughulikiwa.

Wamesema jukumu lao ni kuandikisha na kaya itakayogoma itapelekwa kwa mwenyekiti wa serikal za mtaa ambaye naye atawahesabu, wakimgomea huyovndipovwatakapochukuliwa na polisi kwenda kuhesabiwa kinguvu rumande wakati huo wakisubiri vifungo.

Afisa mtendaji wa kata ya Mabibo amesema kama waislam wataendelea na mchezo huu wa kijinga watakuwepo wengi watakaopoteza ajira maana serikali imejipanga kuwafunga wote watakaogoma kuhesabiwa

551633_279319032169526_1913081750_n.jpg
 
Ni vema diplomasia ikatumika katika suala hili kuliko vitisho vya "kufungana".
 
Hekima kidogo tu inahitajika na kubaki na amani kwa kila familia.

Waache wakuhesabu waende zao na ubaki na maisha yako bila kuvurugwa au kuvurugana na kujipotezea muda wa kufanya mambo yako.
 
unatudanganya kutuambia kuwa kuwa watafungwa watu kwa kutohesabiwa.
Hakuna kitu kama hicho.
Kama ni hivyo wangeanza kumkamata ponda na wenzake na serekali ingekuwa haiwaombi waliogoma kushiriki badala yake ingewaambia ni lazima na ambaye atagoma atashtakiwa.
Haujasikia hotubo ya raisi jana?
Alikuwa anaomba na sio kuagiza.
Mi nawapongeza wote walio hesabiwa na wale ambao hawakukubali nao nawapongeza kwani kila mtu ana uhuru wa kufanya anacho amini kuwa ni sahihi zaidi.
 
Mbona wafuasi wa CHADEMA na MAKANISA mnaendekeza propaganda? Kama mtu hataki muacheni?
 
Mi niko home nawangoja hao wanaojidai eti wakristo wanatakwimu wakati hawajawahi kuhesabu waislamu ni mwapuuzi
 
Ule mkakati unaoratibiwa na Sheikh Ponda Issa Ponda wa kushawishi waislam wasishiriki zoezi la sensa lililoanza leo linaelekea kutopata mafanikio baada ya waislam walioweka mabango majumbani kwao ya kutokuhesabiwa kukubali wenyewe kuhesabiwa bila kikwazo.

Shuhuda wa habari hizi ambaye ni mimi mwenyewe nimeshuhudia makumi ya waislam wakihesabiwa kuanzia ubungo jirani na mitambo ya umeme ya Aggreco hadi mabibo ambapo waliohesabiwa walisema wanahesabiwa kwakuwa hawataki 'maneno' na serikali.

Walidai kuwa wanaunga mkono hoja za wenzao za kutokuhesabiwa lakini wakasema serikali ikiamua jambo haishindwi hivyo wanaepuka kitakachofuata baada ya huo mgomo.

Maeneo ya Mburahati, kigogo nq Luhanga mwitikio wa kuhesabiwa umekuwa mzuri, ingawa wapo wachache waliogoma lakini zimesikika lawama kutoka kwa baadhi ya Maustaadh wakilalamika KUSALITIWA na wenzao ambapo wamelia na WOGA wa waislam kwenye mambo aliyoyaita ya msingi.

Karani wa Sensa aliyekuwepo Mabibo -Sahara na Mabibo Muleba hadi jirani na Mabibo External wamesema hadi muda huu zoezi liko vizuri na wachache waliogoma watashughulikiwa.

Wamesema jukumu lao ni kuandikisha na kaya itakayogoma itapelekwa kwa mwenyekiti wa serikal za mtaa ambaye naye atawahesabu, wakimgomea huyovndipovwatakapochukuliwa na polisi kwenda kuhesabiwa kinguvu rumande wakati huo wakisubiri vifungo.

Afisa mtendaji wa kata ya Mabibo amesema kama waislam wataendelea na mchezo huu wa kijinga watakuwepo wengi watakaopoteza ajira maana serikali imejipanga kuwafunga wote watakaogoma kuhesabiwa

Duh, hii safi sana.
Serikali yetu tukufu na sikivu ni halali na ipo kisheria.
Mtu anayepingana nayo huyo ana nia ya ku-disrupt maisha ya mtz ambaye hana hili wala lile ambao wengi wao ni maskini wa kutupa. Next mi nashauri wote waliotutumia SMS za kipuzi watafutwe na kupelekwa mbele ya pilato, ifike mahali serikali ioneshe mabavu yake, maana lele zimezidi.
 
Afisa mtendaji wa kata ya Mabibo amesema kama waislam wataendelea na mchezo huu wa kijinga watakuwepo wengi watakaopoteza ajira maana serikali imejipanga kuwafunga wote watakaogoma kuhesabiwa
Kuwafunga nadhani ni mkwara tu. Ila kwa muislam yeyote mwenye ajira inayoeleweka na mstakabali wa maisha yake na familia yake unategemea ajira hiyo, hawezi kufanya upumbavu wa kugoma sensa halafu ahatarishe kibarua chake kwa kufunguliwa jalada polisi na usumbufu mwingine.
Watakaogoma ni wale 'kenge' ambao hata wakifunguliwa mashtaka au kuwekwa ndani hawatakuwa na kitu cha kupoteza. Watu kama shehe ponda and co ambao wana uhakika kupata chochote kutoka kwa wafadhili wao hata wakiingia kwenye misukosuko na dola.
 
Sensa kwa maendeleo ya Taifa...

Ila ukiangalia kwa makini watu wenye msimamo wa kugomea sensa humu JF na huku mitaani kwetu wana historia ya kuwa wafuasi wa Chama Cha Wananchi, CUF, wakiongozwa na Mkigoma. I am not pointing fingers to CUF, its just curiosity.
 
Nipo moro kama kawa hatuhesabiwi washapita kwetu hawajaambulia kitu.
Na itv wanajifanya kupitapita huku wakichaguwa watu wa kuwahoji. Hizi ni propaganda
 
hongereni kwa kutimiza masharti ya serikali na poleni kwa imani yenu kama mmekwazika lakini sisi tunasema ya kaisari mwachie kaisari, naimani zoezi hili litaisha salama na wadanganyika tutaendelea kushirikiana kama kawaida ili tuikomboe nchi yetu na umaskini uliotuzunguka bila kuangalia itikadi zetu za kidini
poeni sana kiimani na tusamehehane kwa majibu yoyote tulio toa wakati wa kujadili swala hili niwe mimi binafsi au wengine waliochangia.
 
Kina yakhe mkihesabiwa mnapungukiwa nn?ubishi mwingine haufai,ubishi kila kitu kwenye elimu,afya.sasa hata hili,mtakuwa wa mwisho mpaka siku ya mwisho shauri yenu.
 
Kwa maoni yangu serikali itakuwa imepoteza step endapo zoezi ili halitafanikiwa. Ilikuwa rahisi sana serikali kukubali kuweka hicho kipengele cha dini ili waislamu wakubali kushiriki lakini kwenye data capturing kipengele hicho kikatupwa na hivyo final results zisingeonyesha wangapi ni waislamu na wangapi ni wakristo!!! Lakini hatuwezi kujipa moyo hapa kwamba waislamu wamebadirisha msimamo na hivyo kukubali kuhesabiwa. Hizi propaganda kama zitasaidia basi, zitasaidia kidogo sana kuubadilisha ukweli!!!

Ni maoni yangu tu!!!!!

Tiba
 
Mimi ni karani wa sensa huku tandika kaya nyingi za waislamu nmezhesabu na zilizogoma ni kaya 5 nmesharipoti na hizo kaya zmekuwa noted kwa hatua kali zaidi
 
Back
Top Bottom