Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
WILISONI, KATUPE MBALI HIYO RIPOTI KABLA HAIJAANGAMIZA ZAIDI CCM NA TAIFA KWA UJUMLA MAANA HATA KIDOGO HAIKUA ZAO LA LILE JINA LA UBATIZO LA 'SCIENTIFIC RESEARCH' ULIOIPA LA SIVYO CCM MTAJIKUTA MKITOA TIBA YA GOTI KWA UGONJWA WA KICHWA!!!
Mr Archimedes & the Scientific Research
Mr Ndiamukama & the Scientific Research
Ama kweli la kuvunda halina ubani. Inakuaje Wilson NdiaOmukama na timu mpya ya CCM ianze safari ya kujivua gamba kwa hatua ya kuzua maswali kiasi hiki??
Willisoni NdiaOmukama kaanza kazi CCM kwa guu baya tena la hatari LA KUBUNI, KUANDIKA NA KUPELEKA MBELE YA KAMATI KUU NA HALMASHAURI KUU ya chama chake uongo takatifu juu ya Jamii Forums na WAMILIKI WA KUCHONGA kukiingizwa humo CHADEMA shauri ya kupendwa na vijana wengi wenye umri wa DOTI KOMU nchini.
Hakikakwa wale watu wanaojua kitu 'SCIENTIFIC RESEARCH' inavyopashwa iwe basi mpaka sasa hivi watapendekeza bila ajizi Mzee NdiaOmukama akajipeleke mwenyewe jela Ukonga kwa kuidhalilisha fani ya watafiti na wasomi nchini. Ni Scientifi Reseach gani hiyo isiweza kuhimili Test of Time wakati hata mwezi haujaisha tangu watangaze matokeo yake???
Mzee Achemidis, mwanasayasi aliyebobea duniani, siku alipoona ameruka na kupiga mbizi ndani ya kijibwawa chake cha kuogelea nyumba kuja kuibuka na kuanza kujipangusa pangusa maji usoni ili aweze kuona vizuri mandhari yanayozunguka bwawa lake huku akiendelea kufurahia maisha ndani ya bwawa hilo, ghafla alishangaza kila aliyekwepo (wanafamilia) maeneo hayo hapo pale alipochomoka toka ndani ya bwawa huku akipiga kelele kwa kujishangilia kwamba 'LEO HII NIMEGUNDUA UKWELI, JAMANI LEO NIMEVUMBUA JAMBO ZITO LITAKALOCHANGIA KUBADILISHA KABISA SURA YA ULIMWENGU NA JINSI TUNAVYOENENDA'.
Mara mama Archemidis naye akachomoka jikoni na mwiko mkononi kwa shauku ya kutaka kufahamu kitu gani kimemsibu mumewe ndani ya bwawa lao la kifahari. Kule kuingia tu sebuleni mara anamkuta baba huyu yuko kifua wazi, kalamu na karatasi mkononi huku mwili mzima ukichuruzika maji na akili kama imeruka vile kiasi cha kutoweza kutambua uwepo wa mkewe pemeni mwaka.
Mara mama akaona Mzee Archemidis akipima uzito mdoli kwenye mzani mara akitubukiza huo mdoli kwe maji aliyoyaleta sebuleni kwenye karai karibia kujaa pomoni lakini kwa kuacha japo kanafasi kwa juu. Katika kutumbukiza kule huo mdoli mara maji yakamwagika chini pale sebuleni na hata kumfanya mama akasirike dalili za kuhitajika kurudia kupiga deki.
Ghafla tena Mzee wa watu akalipuka kwa sauti kuu akisema 'Hakika leo Nimefanya Uvumbuzi wa miaka nenda rudi dumu daima' itakayochangia kuboresha hadhi na ubora wa maisha ya binadamu. Mara kaanza kuangusha maandishi micharazo kibao mfululuzi hata maji yote mwilini yakakauka kau!!
Ni tangu siku hii ndipo kitu KANUNI ZA MZEE ARHEMIDIS (Mgiriki huyu) zilipozaliwa zikisema kwamba mwili na au kitufe chochote kikizamishwa kwenye karai iliyojaa maji siku zote husababisha kipimo cha maji yale kwenye karai kumwagika kwa kadiri sawasawa kwa ulinganifu wa uzito wa mwili au kitufe husika!!!
Na kwa wale wadadisi wa mambo mnajua kwamba kwa msaada wa Kanuni za mzee huyu leo hii tunaona chombo kikubwa zaidi ya Meli Duka-la-Vitabu-laDunia MV Dulos likitia nanga hapo Magogoni Dar es Salaam na watu kibao kumiminika ndani kujinunulia vyakusoma LAKINI BILA CHOMBO HICHO KUZAMA - ajabu ilioje hiyo; ni ule 'ukichaa' na nusu kurukwa akili kwa yule Bahari Mgiriki Mzee Archemidis kwenye raha zake tu pale nyumbani.
Ninachosema hapa ni kwamba ugunduzi ule ulikua ni zao la kile kinachoitwa SCIENTIFIC RESEARCH: UTMOST CURIOSITY & INQUISITIVENESS ambayo hadi leo imechangia kweli kufanya sura ya ulimwengu kubadilika, mifumo na ubora wa maisha ya binadamu kuwa nzuri zaidi.
Jambo hili lasadikiwa kutokea zaidi ya miaka 2000 iliyopita lakini Uvumbuzi huo bado unabeba ukweli usiopingika hata leo - THE FACTS OF THE MATTER HAS SINCE STOOD GROUNDS THE TEST OF TIME.
Sasa je huu utafiti wa Mzee Wilsoni NdiaOmukama na Profesa Mmoja wa Dodoma naomba sana watu mnijulishe kama kweli ulikua SCIENTIFIC RESEARCH kweli au majungu ya mfamaji baada ya kuona Watanzania tunakikataa CCM en masse??
Kama Jamii Forums huenda ilitajwa visivyo kwenye ripoti ile ambayo hivi sasa inatumika kama a Working Document ya CCM na serikali yake je kuna mtu yeyote atakayeendelea kuamini chochote kingine kilichoandikwa mle kuwa na ya haki na haki mtupu na kwamba gamba la CCM kuvuliwa ni zao lake na wala si matokeo ya shinikizo toka CHADEMA???
Mzee NdiaOmukama hebu kaa chini na huyo li-Nape lako mkatafakari juu ya huo Waraka wa Magamba kabla hamjaadhirika zaidi kwenye kuendelea kunadi hicho kinachodhihirika hivi sasa kuwa ni Uozo na Majungu ya watu waliojimulia kukaa chini ya mti mahala na kujiandikia kifurahishacho roho na mitazamo binafsi na hatimaye kulibatiza jina SCIENTIFIC RESEARCH iliyoshindwa kuhimili mikikimikiki ya nyakati hata kabla ya mwezi kwisha.
Hebu kajifunzeni kwanza kutoka huyo Mgiriki hapo juu ili CCM ije na mkakati mwingine maana huu wa Magamba na kusingizia JF ndio hiyo tayari wengine tunaisoma KULE KUDODA hata kabla ya utekelezaji wake.