Elections 2010 Mkakati: Nimeamua na wewe amua leo, Say no to CCM

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Katika hotuba aliyoitoa Rais Kikwete wakati akizungumza na wazee wa CCM Dar Es Salaam alisema hajali kama Wafananyakazi Zaidi ya 300,000 wa Serikali wakimnyima Kura, hata wasipompigia kura atashinda tu.
Baada ya Kuitafakari sana ile kauli yake mimi na Familia yangu tumeamua Kumnyima kura JK katika uchaguzi wa 2010.
Naomba na wewe na Familia yako muamue leo, you all say no to JK and his party in 2010 general election
Kuna wafanyakazi 350,000 hawa wana watoto, dada, mama, kaka n.k lets say nyuma ya kila mfanyakazi kuna watu sita
Jumla ya Kura dhahiri ambazo JK amezikataa zitakuwa ( Mfanyakazi + 6) * 350,000 = 2,450,000
 
Kama wafanyakazi wakiweza kuhamasika hivi basi si haba sauti zao zitasikilizwa next tyme
 
kwa upande wangu pia, nafikiri kuna umuhimu wa kubadilisha aina ya msosi, kwa wataalam wa afya, haishauriwi kula chakula cha aina moja tuuu kila siku, unatakiwa kuchanganya kidogo ili virutubisho vikichangamana upata lishe timilifu ukiw aunakula ugali tuu kila siku hautajua utamu wa aina zingine za vyakula, na unaweza ukajengeka kichwani kuamini kuwa chakula ni ugali tu hamna kingine. nafikiri kuna umuhimu wa kuibadili ccm na chama kingine ili tuone watu wengine hao watafanya nini ambacho ccm haijafanya. tukiendelea kukaa na ccm maisha yote, tunaweza kuajenga jamii inayoamini kuwa bila ccm hakuna Tanzania. nchi zingine ambazo wamebadili system, huwa kunakuwa na maendeleo na accountability nzuri sana ya viongozi, na kiongozi atafanya juu chini akijua kuwa akifanya mchezo tu itakuwa hasara kwa chama chake na pia wananchi watamwondoa madarakani..kwa hapa kwetu, ccm imekuwa kama mfalme, hata kuwaweka accountable tu kwenye mambo fulani hatuna uwezo huo, hivyo wao watatuongoza kokote kule na vyovyote vile watakavyopenda. huu ni ushauri wangu kwa wapiga kura.
 
Katika hotuba aliyoitoa Rais Kikwete wakati akizungumza na wazee wa CCM Dar Es Salaam alisema hajali kama Wafananyakazi Zaidi ya 300,000 wa Serikali wakimnyima Kura, hata wasipompigia kura atashinda tu.
Baada ya Kuitafakari sana ile kauli yake mimi na Familia yangu tumeamua Kumnyima kura JK katika uchaguzi wa 2010.
Naomba na wewe na Familia yako muamue leo, you all say no to JK and his party in 2010 general election
Kuna wafanyakazi 350,000 hawa wana watoto, dada, mama, kaka n.k lets say nyuma ya kila mfanyakazi kuna watu sita
Jumla ya Kura dhahiri ambazo JK amezikataa zitakuwa ( Mfanyakazi + 6) * 350,000 = 2,450,000

Niko pamoja nawe ila naomba tusonge mbele zaidi kwamba kila mfanyakazi ajitahidi kushawishi watu 50 tu watakoinyima kura CCM na JK, kwa mana hiyo JK na CCM watakosa kura zaidi ya milion 15 kumbuka waliojiandikisha ni watu milioni 21+,

Itakuwa heshima kwa watanzania wote walioteseka kwa miaka zaidi ya 40 katika mateso.

Tuamue kwa dhati
 
I am sorry to say that huo uamuzi nilifanya hata kabla ya hotuba yake ya mbayuwayu!!!
 
Niko pamoja nawe ila naomba tusonge mbele zaidi kwamba kila mfanyakazi ajitahidi kushawishi watu 50 tu watakoinyima kura CCM na JK, kwa mana hiyo JK na CCM watakosa kura zaidi ya milion 15 kumbuka waliojiandikisha ni watu milioni 21+,

Itakuwa heshima kwa watanzania wote walioteseka kwa miaka zaidi ya 40 katika mateso.

Tuamue kwa dhati

Inawezekana Mkuu, the good thing ni kwamba hakuna hata Mfanyakazi mmoja asiyejua Machungu ya Maisha!

Mshahara : 100,000
Kodi ya Nyumba: 40,000 kwa Mwezi kwa Chumba ( Watu wanalipa gharama za Ufisadi bila kujijua: Rejea makala ya Lula
Ada kwa wanafunzi:
Usafiri at least 1000 kwa siku kwa mtu mmoja:
Umeme:
Maji:
Chakula:
Mavazi:

Vyote hivyo vilipwe na laki moja kwa Mwezi can you imagine mkuu? Hapo utawalaumu walimu wakiuza Visheti Shuleni?
 
Kila mtu angependa iwe hivyo lakini je tuna chama mbadala?kukosa alternative ya uongozi ndiko kutakakofanya CCM ipate ushindi wa kishindo.
 
Kila mtu angependa iwe hivyo lakini je tuna chama mbadala?kukosa alternative ya uongozi ndiko kutakakofanya CCM ipate ushindi wa kishindo.

If we change from that way of thinking ndipo mabadiliko ya kweli yatakapoanza ila Tukiendelea kufikiri hivyo siku zote majamaa yatatutawala milele
 
If we change from that way of thinking ndipo mabadiliko ya kweli yatakapoanza ila Tukiendelea kufikiri hivyo siku zote majamaa yatatutawala milele

Na kweli kama vyama vya upinzani havitasimama na kuonyesha uongozi CCM itaendelea kutawala kwa muda mrefu sana, wananchi wa tanzania sio wajinga ila ni waoga sana kuitoa nchi rehani, wapinzani bila kuwa na uongozi bora na wenye kuaminika hawataweza kushinda.
 
Na iwe hivyo

Very serious..Ni lazima asiyetaka kukosa ugali..kwa kuwa ugali wanaokula unatokana na kura za CHADEMA,hivyo kama hawataki kula basi wasiipigie kura CHADEMA au wahame kwangu..Ha ha ha!mwendo mdundo wote nimeshawaambia mapema kabisa...Wamenielewa sana..
 
Na kweli kama vyama vya upinzani havitasimama na kuonyesha uongozi CCM itaendelea kutawala kwa muda mrefu sana, wananchi wa tanzania sio wajinga ila ni waoga sana kuitoa nchi rehani, wapinzani bila kuwa na uongozi bora na wenye kuaminika hawataweza kushinda.
Si bora kama huwezi kuamini chama kingine upigie kivuli kama tulivyokuwa tunafanya zamani?
Walinifurahisha sana wapemba wale kwa kupiga kura kwenye kivuli. Ilionyesha ni kiasi gani hawakubaliani na sisi m. Mwisho wake leo si unaona wanabembelezwa na Karume?
Hivyo basi hiyo isikuumize, ukiona hakuna kinachokufaa pigia kivuli basi maana yaelekea wewe hakuna unayemwamini mkuu. Yaani hata wewe hujiamini. Maana nilitegemea wewe ugombee. Au umekosa hata chama cha kugombea?
 
Kila mtu angependa iwe hivyo lakini je tuna chama mbadala?kukosa alternative ya uongozi ndiko kutakakofanya CCM ipate ushindi wa kishindo.

Nadhani wakati umefika wa kuweka chama mbadala katika utawala. Kama CCM wakikaa bench kwa miaka mitano tu, itakuwa fundisho kwao kwa makosa wanayofanya ya kuwa mbali na mwananchi wa kawaida.
 
Maskini wengi wa familia yangu ambao 2005 walikuwa chini ya umri 18... juzi walishindwa kujiandikisha... Basi tena...
 
if there is enough people out there to do just that ! then we can have a second 'hung parliament ' in TZ he will be presdaa but wont manage to form a government.
 
"If we change from that way of thinking ndipo mabadiliko ya kweli yatakapoanza ila Tukiendelea kufikiri hivyo siku zote majamaa yatatutawala milele"
Kweli Ndege ya uchumi wakati wa mabadilliko ni sasa na tuwe tayari kutoa elimu ya uraia kwa watu wa karibu yetu nadhani tukianza kuelimishana na hao tunao waelimisha wakaelimisha wengine hesabu itapanda.

"IT CAN BE DONE LETS PLAY OUR PART"
 
kungekuwa kunatendeka haki kwenye uchaguzi ndugu zangu hlo lingewezekana tena bila shda yeyote

but......... mh!
 
Back
Top Bottom