Mkaguzi na mdhibiti mkuu (cag) apewa rungu: Pinda akubali liwalo na liwe

BabuK

JF-Expert Member
Jul 30, 2008
1,845
329
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amempa ‘rungu’, Mdhibiti na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu Hesabu za Serikali (CAG) la kuwafikisha moja kwa moja kwenye vyombo vya Dola, viongozi wa Serikali wanaoiba au kufuja fedha za umma.

Kutokana na rungu hilo, sasa utaratibu wa awali wa CAG kusubiri kuwasilisha kwa Kamati za Bunge majina ya viongozi wa taasisi za Serikali zinazobainika kufuja au kuiba fedha za umma, ili kuwasilishwa bungeni umefutwa rasmi.

Hii inaweza kuwa habari mbaya kwa viongozi wengi wa taasisi za umma, ambao wamekuwa wakitajwa bungeni, kwamba taasisi zao zimefanya manunuzi au kutumia fedha kinyume
na taratibu, kwa vile kwa agizo hilo la Pinda, CAG atakuwa akiwafikisha kwenye vyombo vya Dola moja kwa moja.

“Nachukua nafasi hii kumwagiza rasmi CAG, kwamba kwa zile taasisi ambazo atabaini kuwapo ubadhirifu wa fedha za umma, awafikishe moja kwa moja kwenye vyombo vya Dola wahusika wa ubadhirifu huo na si kusubiri kuwasilisha taarifa bungeni,” alisema Pinda.

Katika majumuisho ya hotuba yake ya Makadirio ya Matumizi kwa mwaka huu wa fedha, bungeni juzi jioni, Pinda pia alisema Serikali haitakuwa na huruma kwa viongozi wa halmashauri ambao watabainika kufuja au kuiba fedha za umma.

Alisema kutokana na mpango huo wa Serikali, kitengo cha ukaguzi wa ndani ambacho awali kilikuwa chini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, kimeondolewa katika ofisi hiyo na kuwa kitengo kinachojitegemea.

Alisema kwa kuwa huru, kitengo hicho kitafanya ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma zilizoelekezwa kwenye halmashauri husika bila kuwapo kwa mwingilio au ushawishi kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na maofisa wake.

Alisema tofauti na ilivyokuwa awali, sasa viongozi wa halmashauri watakaobainika kufuja
fedha au kukosa maadili ya kazi, hawatahamishwa kutoka wilaya au halmashauri moja kwenda nyingine na badala yake watafukuzwa kazi na kufikishwa mahakamanimara moja.

Aliwataka viongozi wa halmashauri na idara nyingine za Serikali kuanzia sasa kuweka
hesabu zao sawa kila mara ili CAG anapofika akute hesabu hizo zipo tayari kwa kukaguliwa tofauti na ilivyo sasa ambapo CAG anapofika kwenye ofisi hizo ndipo viongozi wake wanaanza kuhaha kutafuta vielelezo vya hesabu za fedha.
CHANZO: HabariLeo

 
Big up Pinda, Big up Kikwete.

Haya ndio magamba yanayovuliwa, walifikiri magamba kuwa ni watu, magwanda wanachekesha kweli.
 
Hapo mwana wa mkulima amenena. Na hao wakaguzi wawache tabia zao za kuhakiki vitabu pekee wanavyo agizia kupelekewa gesti.
 
Hivi Waziri Mkuu ana mamlaka ya kuinyang'ang'anya Bunge majukumu na kutangua kazi za kamati za Bunge?

CAG anatumwa na kipengele cha 30 ( 1 ) cha Public Finance Act, 6/2001, 2004 amendment, na ibara ya 143 ya Katiba, 2000 amendments, sio Pinda. Kila anachofanya CAG kiko spelled out na provisions za sheria, Pinda anawezaje kujiamkia asubuhi kubadilisha majukumu ya Mkaguzi Mkuu?
 
Mkuu Taso, umezungumza point muhimu sana! Naona tena Waziri Mkuu kaongea bila kufanya utafiti. Hivi hapo bungeni hakuna washauri wa sheria?
 
Hivi Waziri Mkuu ana mamlaka ya kuinyang'ang'anya Bunge majukumu na kutangua kazi za kamati za Bunge? CAG anatumwa na kipengele cha 30 ( 1 ) cha Public Finance Act, 6/2001, 2004 amendment, na ibara ya 143 ya Katiba, 2000 amendments, sio Pinda. Kila anachofanya CAG kiko spelled out na provisions za sheria, Pinda anawezaje kujiamkia asubuhi kubadilisha majukumu ya Mkaguzi Mkuu?[/QUOTE hapa umenena ukweli, Pinda kwa hili hizo ni kelele tuu! Kama ni vyombo vya dola mbona huwa anapeleka PCCB kwa uchunguzi zaidi?, hili litakua kama lile agizo la waziri wa fedha kipindi hiicho Zakiah Meghji kuwa malipo ya kutumia dola yasifanyike nchini lakini ndio yameshamili! CAG ATAPELEKA WATU MAHAKAMANI KWA MANDATE IPI? Hapo amedanganya umma tena
 
Kama kawaida Peter Pinda Kayanza amekurupuka!

PM Hana Mamlaka ya kumpa Mamlaka CAG mamlaka ya ku-Audit na ku-peleka wezi katika mahakama!
 
politics mkuu takemyword..kama tulivyodanganywa na mkulo mafuta yatapungua kuanziajuzi same mhezo uliochezeka hapo
 
hakuna kitu hapo.....hamjui huu gao huwa unarudi kule juu ulikotoka........hakuna kitu...hakuna kitu bla..bla..bla.....
 
Nimeongea watu wenye taaluma ya ugaguzi wa mahesabu, hakuna mkaguzi duniani kote kwenye uwezo wa kumpeleka mtu mahakamani, yeye anaweza kuwa shahidi tu, ..... Sasa hapo yawezeka cag alimshauri vibaya pinda, kwani nae si mkaguzi,hiyo fani alivamia tu
 
Mnao lalama kwa hili hamna mantiki, Waziri Mkuu kisha sema, kama hakuna sheria basi zitungwe.
 
Mimi nilivyoelewa ni kwamba:
CAG akishafanya Ukaguzi wake, then akabaini frauds, anachopaswa kufanya kulingana na Maagizo haya ya PM ni kuwaripoti hawa wabadhirifu katika Vyombo vya Dola moja kwa moja. Vyombo vya Dola hapa ni PCCB, Polisi, n.k
 
Back
Top Bottom