Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wazazi CCM DSM anarejesha kadi ya CCM na kujiunga na Upinzani!!!!

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,890
382
Bw MICAL ELIFURAHA MRINDOKO(0754 285538,0715295538) amerejesha kadi ya CCM na kujiunga na TLP.

Bw Mlindoko ambaye ni msomi wa MBA -DSM na mumiliki wa Vituo vya mafuta Engen Ubungo,Bp Tank Bovu na MOGAS kIBAHA AMESEMA hajisikii amani kukaa ndani ya CCM,kwani chama hicho kwa sasa ni Bomu linalowezakulipuka wakati wowote tangia sasa!!
Amesema tangia mchakato wa kura za Maoni 2010, Mchakato wa Kumupata mgombea wa Arumeru na huu wa Ubunge East Afrika umetawaliwa na Mfumo wa Kifalme ambapo watoto wa vigogo, wamekuwa wanapendelewa huku walioko madarakana wakiwa hawako tayari kutoka na kutoka na kununua madaraka kwa nguvu ya pesa
Amesema ndani ya CCM hakuna haki na unapotafuta haki unaweza kumwaga damu kamailivyo watokea Wabunge wa Chadema Mwanza na Mbeya.
Amesema amekihama CCM ilikutafuta haki nje ya CCM na kujiunga na Wapiganaji wa kweli kwani huwezi ukawa mpinzani wakati bado upo CCM!!!!
"HUWEZI KUSUKUMA GARI UKIWA NDANI YA GARI HAPO UTAKUWA MNAFIKI , NI LAZIMA UTOKE NDIPO ULISUKUME VIZURI'

'NAWASHAULI WANA CCM WOTE WANAO NUNG'UNIKA NDANI YA CHAMA WAHAME MARA MOJA NA KUJINGA NA UPINZANI ILI KULIKOMBOA TAIFA NA UFISADI"

Source: TLP Makao makuu
 
Anatafuta maendeleo kwenye vyama?!, siasa?!. Huyu anataka vya rahisirahisi.
 
Anatafuta maendeleo kwenye vyama?!, siasa?!. Huyu anataka vya rahisirahisi.
Huwa wanaongea hivyo hivyo baadae wanarudi. Hongeara zake, ametoka ligi kuu amejiunga ligi ya mchangani mpira wa vitambaa.
 
Back
Top Bottom