Mjumbe Kamati Kuu CHADEMA ahamia CCM, Nape asema Zitto ameogopa kwenda Igunga

Kumbe wanapiga picha za maandamanio ili wakaombee pesa kwa wafadhili!! Halafu wanawaacha watu wamepigwa na jua la maandamano wako hoi bin taabani na kesho wanaamka na shida zao! Peopleeeeeeeeeee.............powerrrrrrrrrrrrrrrr. ama kweli wajinga ndo waliwao

Mambo mawili muhimu kuhusu jambo hili:

i) Huyu hajawahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA. Alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Singida Mjini. Akasimamishwa uenyekiti baada ya kubainika kwamba alikihujumu chama katika uchaguzi wa 2010 kwa kusababisha madiwani wa CCM wapite bila kupingwa na yeye mwenyewe kuficha mihuri ya chama baada ya kuhongwa. Mapema mwaka huu Baraza la Uongozi wa Mkoa likamfukuza rasmi uongozi wa chama. Tatizo la viongozi wa CCM hawafanyi utafiti wanapokea kanyaboya wao wanafikiri wamepata wala hawashtuki.

ii) Hii ni mara ya pili Nakamia anatangaza kuhama CHADEMA. Mara ya kwanza alitangaza siku aliyekuwa Mwenyekiti wa Iramba alipohama huko Shelui. Nashangaa mwandishi anaripoti kama vile hili ni jambo jipya. By the way, hawa bwana ni mtu na mdogo wake.

CCM inawapasa kutambua kuwa, baada ya udanganyifu wa muda mrefu, wananchi wameamka na hawapo tayari kupokea propaganda za kijinga kama hizi wanazofanya Nape na rafiki yake Mwigulu. Hata hivyo, tunawashukuru Mwigulu na Nape kwa kazi nzuri wanayofanya ya kumalizia pumzi ya mwisho ya CCM.
Watu wengine mnatia hurima kwelikweli!! Weeee unasumbuka bure tu ndugu yangu,, ningekuwa wewe ningetunza pesa, muda na energy yangu. Mwigulu hutakaa umuweze pale Iramba. Tafuta jimbo lingine. Ni ushauri tu

Mbowe kiboko sana, yaani jamaa anapiga picha za video halafu anaenda kuombea misaada Ujerumani? Kweli mchaga ni mchaga tu. Lakini hongera Mbowe kwa ubunifu wa hali ya juu.

NAUYE ACHA KUPIGA MAYOWE KWANI NI JUU YETU WANA JF KUJISEMEA
WENYEWE JUU YA KUAMINIKA KWA JUKWAA AU LAA

Mtoto acha kupiga mayowe; tafadhali ni juu yao wana-Igunga kujisemea wenyewe. Wewe tunakuelewa kwa zaidi ya mara 200 kwamba unasukumia wazo gani kila unapofungua mdomo wako.

Kwa maoni yangu, JF hailazimiki kuaminika kwa CCM wala kuwadi wake yeyote yule hata tone kwa misingi ya ukweli kwamba Chama Chenyewe cha CCM hakiaminiki wala viongozi wake sasa kuna uhalali gani kutafuta kitu kisichofahamika kwao miaka yote kitokee JF??????????

Mtoto nasema acha kulia ovyo hapa jukwaani, acha wanajamvi tukazungumze wenyewe juu ya uaminifu wa JF au ukosefu wake. Invisible, hebu kaza kamba hapo mkuu kwani saa ya ukombozi ndio huu hapa.

Salaam,

NILITAKA KUJADILI HILI LAKINI NIKASHANGAA KUONA KILICHO KWENYE THREAD NA KILICHOKO KWENYE TEXT ILIYOANDIKWA NA NKOROMO HAVIFANANI, NADHANI SINA HAJA YA KULIJADILI HILI.

LAKINI TULIYOCHANGIA MPAKA SASA HEBU TUJIULIZE KWENYE TEXT KUNA MAHALI IGUNGA IMETAJWA? HAYO YA KUSEMA NAPE KASEMA ZITTO HAENDI IGUNGA YAMETOKA WAPI?

UKIZOEA KUDANGANYA IPO SIKU UTAJIDANGANYA HATA JINA LAKO, HIVI KAMA UNAWEZA WEKA STORI YOTE NA BADO UKATUNGA MANENO YAKO HII AIBU KUBWA.

NDO MAANA NASEMA TUNACHOKIFANYA JF KITAKUWA HAKIAMINIKI KWA KURUHUSU MAMBO KAMA HAYA, POST ZINGINE HAZIRUHUSIWI TUKIAMINI KUNA UTHIBITI MKUBWA MENGINE COZ YANA MASILAHI, FLANI BASI YATAPITA TU HATA KAMA YANA MAPUNGUFU YA WAZI KABISA...

KWENYE STORI WAPI PAMESEMWA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CHADEMA? Haya twendeni ni forum yetu

Wacha hilo zezeta liende hatuna haja naye huyo msaliti sisi tunao penda haki nyuma mwiko

Habari hii inaboa kama habari ya TBC kupongezwa kwa kucover maafa znz na kama wale vijana wa Igunga maskini wanaorukaruka kwenye kampeni

Kumbe wanapiga picha za maandamanio ili wakaombee pesa kwa wafadhili!! Halafu wanawaacha watu wamepigwa na jua la maandamano wako hoi bin taabani na kesho wanaamka na shida zao! Peopleeeeeeeeeee.............powerrrrrrrrrrrrrrrr. ama kweli wajinga ndo waliwao

Bora ufadhili upatikane kuliko marijali wa Igunga kugombea pilau...nikiona mtu mzima anaipenda CCM napata kiungulia

Unaumia wewe mwenyewe bana sisi tunaongelea ukweli. Sasa hivi CCM wanaumia mno kuliko wakati mwingine wowote na watapeleka listi yao yote Igunga wanayoiamini na ndio mwisho wao. Chadema ikiamua nani atasimama?

si mpaka muamue...... amueni basi muone kitakachofanyika.. wenzio watakimbilia ujerumani wewe utakwenda wapi....?

Hata Yesu alipokuja Duniani walimkataa kuwa ndiye mkombozi, vivyo hivyo CDM wanaikataa kuwa ndo mkombozi wa watz lakini amini nawambieni sisi tunaamini ndo atakuwa mkombozi wetu tanzania. Mabadiliko hayaji kirahisi na hata Libya Gadaff hakupenda kuachia nchi kirahisi, Ivory coast, nk ndo ilivyo nasi tusikate tamaa mpaka kieleweke.

yaani unailinganisha Chadema na Yesu? watu mnaandaa maandamano halafu mnawapiga video na picha mnapeleka kwa mabwana zenu wawape misaada... kumbe nd' ninyi mliosababisha yule balozi arudishwe kwao?...

Wee kweli topical,hujitambui. Kama Slaa atakuwa mlafi atarudi,but it will never happen.
Unashangaa slaa kurudi ccm? muulize zitto kinachomfanya asiende igunga, kilichomfanya zitto atangaze kugombea urais mwaka 2015. CDM msijifanye hamjui. zitto kapewa hongo na barrick katulia tuliii. wote wachumia tumbo. mtashtuka nyumba haina mtu.

Kweli zitto amekwisha amefikia mpaka hatua ya kumuogopa Nepi kweli jamaa amepotea kabisa ,

NA BASHIR NKOROMO, SINGIDA

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ameshushia kilio tena kwa CHADEMA baada ya Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Singida Mjini, Nakamia John kuhamia CCM.

Nakamia ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu na Kamati Kuu ya Taifa ya CHADEMA, alitangaza kuhamia CCM na kukabidhi kadi yake ya CHADEMA kwa Nape katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za udiwani za CCM, Kata ya Urughu, jimbo la Iramba Magharibi mkoani hapa.

"Kama unakumbuka Mheshimiwa Nape, mimi ndiye nilikuvalisha gwanda la CHADEMA ulipokuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wetu mkuu kule Dar es Salaam, leo hii nimeamua niwe nawe katika chama makini CHama Cha Mapinduzi", alisema Nakamia na kuongeza.

"Ukiwa nje ya CHADEMA unaweza kudhani ni chama makini sana, lakini ni chama cha udikteta ukiokithiri, kisicho na utaratibu unaoeleweka, chenye viongozi wa ngazi za juu ambao wanapenda kila wanalotaka liwe hata kama haliwezekani".

Aliwataka Watanzania ambao bado wanadhani CHADEMA kina manufaa kuachana nacho haraka wasiendelee kugeuzwa mtaji wa maandamano ambayo alisema viongozi wa chama hicho huyapanga kwa lengo la kukusanya fedha kwa manufaa yao.

"Ninyi mnadanganywa kila siku eti nguvu ya umma, kumbe mnapumbazwa na kuacha kufanya kazi za maendeleo badala yake wanawapanga katika maanadamano, wanawapiga picha za video kisha wanapeleka kwa wafadhili kuombea fedha za kula wao ninyi mkiendelea kufa njaa", alisema Nakamia.

Akimpokea, Nape alimpongeza na kuwataka Watanzania wengine kuiga alivyofanya Nakamia akisema kwamba kila anayekiunga mkono CHADEMA asidhani kuwa atapata manufaa yoyote kimaendeleo.Akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Urughu, Simon Tyosela, Nape aliwataka wakazi wa Kata hiyo kuhakikisha wanampigia kura mgombea huyo wa CCM ili aweze kusimamia miradi yote iliyopangwa kutekelezwa katika eneo lao.

Nape alionya wananchi kutofanya makosa, akisema endapo wataacha kumchagua mgombea wa CCM wakampigia wa CHADEMA watambue kwamba wamekataa maendeleo kwa kuwa yale yote yaliyopangwa kutekelezwa yapo ndani ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi kinachotawala.Uchaguzi mdogo unafanyika kwa lengo la kukidhi taratibu na sheria tu za nchi, lakini kimsingi hakuna kinachoweza kubadilishwa katika mipango ya maendeleo."Baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana, wananchi walichagua ilani ya kijani (ya CCM) kwamba ndiyo itekelezwe kwa miaka mitano hadi uchaguzi mkuu mwingine, kwa vyovyote vile anayefaa kupewa kujumu kusimamia lazima awe wa CCM", alisema Nape.

"Wewe unatambua kuwa sera zinazotekelezwa kwa sasa hadi miaka mitano ni za CCM na mipango yote iliyopo inatekelezwa chini ya ilani hiyo, unachagua mgombea mwenye ilani nyingine ambayo haina kazi, unataka kusimamisa au kuendeleza maendeleo kweli?" alihoji Nape.Alisema anao uhakika kwamba mgombea wa CCM taibuka na ushindi na alichokuwa akifanya juzi, si kuzindua tu kampeni bali kuandaa sherehe za mgombea huyo kutawazwa kuwa diwani wa kata hiyo.

"CHADEMA walishashindwa hata kabla ya uchaguzi kufika, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe alishaliona hilo mapema ndiyo maana hakuweza kuja kuzindua kampeni za chama hicho hapa kama alivyokuwa amewaahidi." alisema Nape na kuongeza."Zitto aliposikia tu kuwa mimi nitakuja hapa akaona basi biashara imeingia ruba, akaamua kuingia mitini, kwa hiyo kwa kuwa hakuja hapa sitafanya kampeni maana imeshakwisha".

Aliwataka wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Tyosera na pia kuhakikisha wanazilinda kura hizo.Nape aliwataka Umoja wa Vijana wa CCM kuunganisha nguvu zao kuhakikisha siku ya uchaguzi kina mama na wazee wanakwenda kupiga kura bila kutishwa na yeyote hasa CHADEMA ambao alisema wana tabaia ya kukodi watu kutoka nje ya jimbo kuzuia wazee na wanawake kwenda kupiga kura.

Uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Urughu unafanyika kufuatia Tyosera ambaye alikuwa diwani wa CHADEMA kujiuzulu na kuhamia CCM, na baada ya kuhamia CCM amegombea katika kura za maoni na kuongoza kwa kura nyingi.Akizungumza Tyosera alisema aliamua kuhama kujiuzulu na kuhamia CCM kwa sababu wakati akiwa diwani kwa tiketi ya CHADEMA kila akiwa katika baraza la Halmashauri alijiona kama kunguru ndani ya yangeyange.

-- Regards;-Bashir Nkoromo

Senior Photo/Journalist

Uhuru Publications Ltd,Publishers of Uhuru, Mzalendo and Burudani tabloids

Cell; +255 498008, +255 789 498008

P O Box 9221, Dar es Salaam.Tanzania

email: nkoromo@gmail.com, bnkoromo@yahoo.com.

-------------------------------------------------------Blog:Chachandu Daily Nkoromo Daily Blog

****** yake

siasa uchwara na usanii za CCM zinatia kichefuchefu huyo bwana kutangaza hatua yake kwanini iwe Igunga kwanini hakukufuata Nape Ofisini kwako.Kwanini wewe binafsi hukuhudhuria ufunguzi wa kampeni Igunga?Wewe kujilinganisha na Zitto ni kichekesho! Yakowapi magamba uliyotuhahidi kuyavua?Tulikua tunafikiri ya kua haupo tena katika ulingo wa siasa baada ya kuonywa kuhusu kuropoka kwako.Ulikua umepigwa marufuku kukanyaga Igunga kwenye kampeni na maboss wako kwani katika mazingira ya Igunga kuwepo kwako ni kichefuchefu kwa wana Igunga.Sasa umekuja kiaina kwa kumnunua huyo ndugu CCM inaweza kumnunua mtu mmoja mmoja Lakini haiwezi kuwanunua watanzania wote .MUNGU IBARIKI TANZANIA

Kama CCM wanataka kuharakisha safari yao kuelekea kaburini basi waendekeze huu mchezo wa kununua watu! Uchaguzi ulipita walinunua sana lakini wameingia magogoni kwa msaada wa wataalam wa 'uchakachuaji'. How can they be sure kwamba huyo mjumbe wa CHADEMA ni kweli kahama? kwa sababu tu kawapa card ya chama A na kupokea card ya chama B? Hivi kinachofanya watu wachukie CCM ni kitu gani hasa?

Wapinzani walioko Singida wana matatizo yao AIDHA hawaelewi lengo lao kuwa wapinzani nadhani hii ndiyo maana hata kimaendeleo mkoa ni wa mwisho mwisho

Hata Yesu alipokuja Duniani walimkataa kuwa ndiye mkombozi, vivyo hivyo CDM wanaikataa kuwa ndo mkombozi wa watz lakini amini nawambieni sisi tunaamini ndo atakuwa mkombozi wetu tanzania. Mabadiliko hayaji kirahisi na hata Libya Gadaff hakupenda kuachia nchi kirahisi, Ivory coast, nk ndo ilivyo nasi tusikate tamaa mpaka kieleweke.
watu wenye upeo nusu utawajua tu kwa comment zao yan we unafurahia yaliyotokea Libya?watu wamekufa,wamepoteza mali zao na kila aina ya mambo yasiyotarajiwa leo we unashabikia!! Hee we unaonekana huna uzalendo wa nchi unapenda ukorofi tu,usiombee hayo yanayotokea Libya.

Back
Top Bottom