Mjumbe Kamati Kuu CHADEMA ahamia CCM, Nape asema Zitto ameogopa kwenda Igunga

Hiyo si siasa bali ni tamaa ya uchumia tumbo kwa maslahi binafsi, mwanasiasa makini mwenye ufahamu nini maana ya kuwaongoza
na kuwatetea wananchi awezi kujidhalilisha kwa kununuliwa na pesa zillizopatikana kiufisadi, kwa maana hiyo yuko kinyume na wananchi
na hafai kuwa kiongozi mbele yao.

CHADEMA kuhusu huyo mjumbe wa kamati kuu aliyenunuliwa mchukulie ni mzigo wa takataka mlioutupa jalalani, kwani alikuwa ameficha makucha yake na sasa kuyatoa na kuonyesha kama yeye si muadilifu na kujiondolea sifa za uongozi.

Ni bora alivyoondoka kuliko kukitia doa chama cha CDM. Kama ni ufisadi, rushwa na kutumia mabavu kuwakandamiza na kuwaibia
wananchi hayo yote akayafanye akiwa Ccm. CDM ibakie safi daima.

Amelipwa Tshs ngapi huyo? Watajichuja wenyewe mpaka wabaki watu makini, CHADEMA mapambano mbele kwa mbele, mafisadi, wasaliti, wanafiki wataondoka tuu!

Salaam,

NILITAKA KUJADILI HILI LAKINI NIKASHANGAA KUONA KILICHO KWENYE THREAD NA KILICHOKO KWENYE TEXT ILIYOANDIKWA NA NKOROMO HAVIFANANI, NADHANI SINA HAJA YA KULIJADILI HILI.

LAKINI TULIYOCHANGIA MPAKA SASA HEBU TUJIULIZE KWENYE TEXT KUNA MAHALI IGUNGA IMETAJWA? HAYO YA KUSEMA NAPE KASEMA ZITTO HAENDI IGUNGA YAMETOKA WAPI?

UKIZOEA KUDANGANYA IPO SIKU UTAJIDANGANYA HATA JINA LAKO, HIVI KAMA UNAWEZA WEKA STORI YOTE NA BADO UKATUNGA MANENO YAKO HII AIBU KUBWA.

NDO MAANA NASEMA TUNACHOKIFANYA JF KITAKUWA HAKIAMINIKI KWA KURUHUSU MAMBO KAMA HAYA, POST ZINGINE HAZIRUHUSIWI TUKIAMINI KUNA UTHIBITI MKUBWA MENGINE COZ YANA MASILAHI, FLANI BASI YATAPITA TU HATA KAMA YANA MAPUNGUFU YA WAZI KABISA...

KWENYE STORI WAPI PAMESEMWA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CHADEMA? Haya twendeni ni forum yetu
Usijali mdau huyo kachomeka tuu, ila ilikuwaje huyo Mkt wa CDM achomokee CCM???????? Kweli kabisa katumia busara sio njaa kali, na nyie mkampa ulaji atangaze kutimka?????????

Kuna watanzania wanashabikia mambo ya kijinga. Yaani nchi hii haiwezi kuendelea daima, tutanyonywa na wachache milele kwa ushabiki wa kijinga na kutanguliza maslahi binafsi mbele !

Dah, kumbe source gazeti la uhuru??????????????? Jamani mda wangu ningesoma mambo mengi sana!craaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap!ujinga wenu pelekeni huko!!!!!!!!!!!!!!!!!

Siasa za kizamani sana.

Siasa za viongozi hatuzitaki na ndio maana tuliisifia CDM kuweza kufukuza uanachama madiwani watano wa Arusha. Huyu kibaraka mmoja ni punje ndogo sanaaaaaa. siasa za viongozi kwa kweli ni za CCM yupo sahihi aende tu huko.

Tuna hitaji siasa na sera ambazo zipo mikononi mwa Umma si watu wachache, na hii ndio hasa sababu iliyoperekea watu wengi kuikataa CCM.

Watawanunua mpaka lini? wao watashabikia kwa muda fedha zao zikiisha watakuja tena upande wa nuru

Mambo mawili muhimu kuhusu jambo hili:

i) Huyu hajawahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA. Alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Singida Mjini. Akasimamishwa uenyekiti baada ya kubainika kwamba alikihujumu chama katika uchaguzi wa 2010 kwa kusababisha madiwani wa CCM wapite bila kupingwa na yeye mwenyewe kuficha mihuri ya chama baada ya kuhongwa. Mapema mwaka huu Baraza la Uongozi wa Mkoa likamfukuza rasmi uongozi wa chama. Tatizo la viongozi wa CCM hawafanyi utafiti wanapokea kanyaboya wao wanafikiri wamepata wala hawashtuki.

ii) Hii ni mara ya pili Nakamia anatangaza kuhama CHADEMA. Mara ya kwanza alitangaza siku aliyekuwa Mwenyekiti wa Iramba alipohama huko Shelui. Nashangaa mwandishi anaripoti kama vile hili ni jambo jipya. By the way, hawa bwana ni mtu na mdogo wake.

CCM inawapasa kutambua kuwa, baada ya udanganyifu wa muda mrefu, wananchi wameamka na hawapo tayari kupokea propaganda za kijinga kama hizi wanazofanya Nape na rafiki yake Mwigulu. Hata hivyo, tunawashukuru Mwigulu na Nape kwa kazi nzuri wanayofanya ya kumalizia pumzi ya mwisho ya CCM.

Nina taarifa kwamba na wewe uko kwenye payroll ya ccm ni kweli?

Huyo gamba njaa kali bora arudi where he belongs, amekuta chama makini hakina mambo ya ufisadi so kumemshinda.
Du, kumbe CCM inamuogopa Zitto kiasi hicho! kama mimi ningekuwa Nape nisingeonyesha uwoga wangu to that extent, ningefunga tu mdomo. Sasa Zitto atakapoenda kupiga kampaign Igunga sijui Nape atakuja na sera gani tena.

NA BASHIR NKOROMO, SINGIDA

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ameshushia kilio tena kwa CHADEMA baada ya Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Singida Mjini, Nakamia John kuhamia CCM.

Nakamia ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu na Kamati Kuu ya Taifa ya CHADEMA, alitangaza kuhamia CCM na kukabidhi kadi yake ya CHADEMA kwa Nape katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za udiwani za CCM, Kata ya Urughu, jimbo la Iramba Magharibi mkoani hapa.

"Kama unakumbuka Mheshimiwa Nape, mimi ndiye nilikuvalisha gwanda la CHADEMA ulipokuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wetu mkuu kule Dar es Salaam, leo hii nimeamua niwe nawe katika chama makini CHama Cha Mapinduzi", alisema Nakamia na kuongeza.

"Ukiwa nje ya CHADEMA unaweza kudhani ni chama makini sana, lakini ni chama cha udikteta ukiokithiri, kisicho na utaratibu unaoeleweka, chenye viongozi wa ngazi za juu ambao wanapenda kila wanalotaka liwe hata kama haliwezekani".

Aliwataka Watanzania ambao bado wanadhani CHADEMA kina manufaa kuachana nacho haraka wasiendelee kugeuzwa mtaji wa maandamano ambayo alisema viongozi wa chama hicho huyapanga kwa lengo la kukusanya fedha kwa manufaa yao.

"Ninyi mnadanganywa kila siku eti nguvu ya umma, kumbe mnapumbazwa na kuacha kufanya kazi za maendeleo badala yake wanawapanga katika maanadamano, wanawapiga picha za video kisha wanapeleka kwa wafadhili kuombea fedha za kula wao ninyi mkiendelea kufa njaa", alisema Nakamia.

Akimpokea, Nape alimpongeza na kuwataka Watanzania wengine kuiga alivyofanya Nakamia akisema kwamba kila anayekiunga mkono CHADEMA asidhani kuwa atapata manufaa yoyote kimaendeleo.Akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Urughu, Simon Tyosela, Nape aliwataka wakazi wa Kata hiyo kuhakikisha wanampigia kura mgombea huyo wa CCM ili aweze kusimamia miradi yote iliyopangwa kutekelezwa katika eneo lao.

Nape alionya wananchi kutofanya makosa, akisema endapo wataacha kumchagua mgombea wa CCM wakampigia wa CHADEMA watambue kwamba wamekataa maendeleo kwa kuwa yale yote yaliyopangwa kutekelezwa yapo ndani ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi kinachotawala.Uchaguzi mdogo unafanyika kwa lengo la kukidhi taratibu na sheria tu za nchi, lakini kimsingi hakuna kinachoweza kubadilishwa katika mipango ya maendeleo."Baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana, wananchi walichagua ilani ya kijani (ya CCM) kwamba ndiyo itekelezwe kwa miaka mitano hadi uchaguzi mkuu mwingine, kwa vyovyote vile anayefaa kupewa kujumu kusimamia lazima awe wa CCM", alisema Nape.

"Wewe unatambua kuwa sera zinazotekelezwa kwa sasa hadi miaka mitano ni za CCM na mipango yote iliyopo inatekelezwa chini ya ilani hiyo, unachagua mgombea mwenye ilani nyingine ambayo haina kazi, unataka kusimamisa au kuendeleza maendeleo kweli?" alihoji Nape.Alisema anao uhakika kwamba mgombea wa CCM taibuka na ushindi na alichokuwa akifanya juzi, si kuzindua tu kampeni bali kuandaa sherehe za mgombea huyo kutawazwa kuwa diwani wa kata hiyo.

"CHADEMA walishashindwa hata kabla ya uchaguzi kufika, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe alishaliona hilo mapema ndiyo maana hakuweza kuja kuzindua kampeni za chama hicho hapa kama alivyokuwa amewaahidi." alisema Nape na kuongeza."Zitto aliposikia tu kuwa mimi nitakuja hapa akaona basi biashara imeingia ruba, akaamua kuingia mitini, kwa hiyo kwa kuwa hakuja hapa sitafanya kampeni maana imeshakwisha".

Aliwataka wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Tyosera na pia kuhakikisha wanazilinda kura hizo.Nape aliwataka Umoja wa Vijana wa CCM kuunganisha nguvu zao kuhakikisha siku ya uchaguzi kina mama na wazee wanakwenda kupiga kura bila kutishwa na yeyote hasa CHADEMA ambao alisema wana tabaia ya kukodi watu kutoka nje ya jimbo kuzuia wazee na wanawake kwenda kupiga kura.

Uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Urughu unafanyika kufuatia Tyosera ambaye alikuwa diwani wa CHADEMA kujiuzulu na kuhamia CCM, na baada ya kuhamia CCM amegombea katika kura za maoni na kuongoza kwa kura nyingi.Akizungumza Tyosera alisema aliamua kuhama kujiuzulu na kuhamia CCM kwa sababu wakati akiwa diwani kwa tiketi ya CHADEMA kila akiwa katika baraza la Halmashauri alijiona kama kunguru ndani ya yangeyange.

-- Regards;-Bashir Nkoromo

Senior Photo/Journalist

Uhuru Publications Ltd,Publishers of Uhuru, Mzalendo and Burudani tabloids

Cell; +255 498008, +255 789 498008

P O Box 9221, Dar es Salaam.Tanzania

email: nkoromo@gmail.com, bnkoromo@yahoo.com.

-------------------------------------------------------Blog:Chachandu Daily Nkoromo Daily Blog

Shitambala wa mbeya yuko wapi?

Mwache aende.

Mambo mawili muhimu kuhusu jambo hili:

i) Huyu hajawahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA. Alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Singida Mjini. Akasimamishwa uenyekiti baada ya kubainika kwamba alikihujumu chama katika uchaguzi wa 2010 kwa kusababisha madiwani wa CCM wapite bila kupingwa na yeye mwenyewe kuficha mihuri ya chama baada ya kuhongwa. Mapema mwaka huu Baraza la Uongozi wa Mkoa likamfukuza rasmi uongozi wa chama. Tatizo la viongozi wa CCM hawafanyi utafiti wanapokea kanyaboya wao wanafikiri wamepata wala hawashtuki.

ii) Hii ni mara ya pili Nakamia anatangaza kuhama CHADEMA. Mara ya kwanza alitangaza siku aliyekuwa Mwenyekiti wa Iramba alipohama huko Shelui. Nashangaa mwandishi anaripoti kama vile hili ni jambo jipya. By the way, hawa bwana ni mtu na mdogo wake.

CCM inawapasa kutambua kuwa, baada ya udanganyifu wa muda mrefu, wananchi wameamka na hawapo tayari kupokea propaganda za kijinga kama hizi wanazofanya Nape na rafiki yake Mwigulu. Hata hivyo, tunawashukuru Mwigulu na Nape kwa kazi nzuri wanayofanya ya kumalizia pumzi ya mwisho ya CCM.
thanks Mkuu,
nimetafuta sana confirmation hii, kwa kuwa akili yangu ilikataa kabisa kukubali kuwa huyu jamaa aliwahi kuwa kwenye kamati kuu ya CDM.
kwangu mimi kamati kuu ni kubwa sana kwa mtu kama huyu, hawezi kuwepo kwa zaidi ya mwezi kwenye kamati kuu makini kama ya CDM na akaendelea kufikiria na kutumikia tumbo. watu kama hawa IQ yao huwa ndogo sana na DOA analoliacha kwenye kizazi chake ni la milele .
Nawaomba Mods wawe wanaedit au kuweka kanusho chini ya thread kama hizi, huu ni UZUSHI na UWONGO kwa nini unaachwa??? CDM ni chama kikubwa ambacho watz wanakitegemea huwezi ukaacha upotoshaji kama huu kuendelea!! pls Mods do the needful, I am watching you!

Huyu hajawahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA. Alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Singida Mjini..

Asante kwa maelezo yaliyonyooka, nadhani Magwanda wenzako sasa watapumua, naomba unielimishe kido hivi kamati kuu ya CHADEMA ina comprise watu gani hasa (vyeo)?

Nina taarifa kwamba na wewe uko kwenye payroll ya ccm ni kweli?

Kama na Kitila Mkumbo yuko kwenye payroll ya CCM basi ni msaada mkubwa sana! kwa malipo hayo KM anaibadilisha TZ kwa kuwafanya watu wabadilike na wajitambue.....akishazalisha akina KM laki moja ambao hawako kwenye payroll ya ccm na wakaendelea kujimultiply kwa kuconvice wengine then nchi itapata UKOMBOZI tu. kuna watu hawaelewi au hawajui chain ya mabadiliko, leo hii hata Dk Slaa akitangaza kurudi ccm(Mungu epushia mbali) bado watu tutaendeleza mapambano ni kwamba ataweza kutupunguzia kasi kwa muda tu ila hatatuzuia kuendelea kutafuta tunachokitaka. walikuwepo akina Wassira huku upinzani leo wako wapi? nani anawathamini? kama sio uchakachuzi hata huo Ubunge asingepata.
Kama ungebahatika kupata speech hata moja tu ya kwenye mikutano ya CDM ya Bwana Kitila Mkumbo usingeamini kirahisi kuwa yuko kwenye payroll ya ccm kama ambavyo mimi siwezi kuamini hivyo kwa sbb najua anachokifanya kwenye chama.

Ukombozi limekaa ki-jumuia zaidi? chimbuko la ukombozi huu mnaoutafuta ni kutokana crusade au?

Nape mtoto mdogo sana Zito hawezi kukuogopa kamwe anakazi za maana sana kwa ajili ya watanzania na si kwa ajili ya wakubwa fulani kama wewe Nape ufanyavyo.

Back
Top Bottom