Mjumbe Hauawi: Please Soma Huu Ujumbe!

Status
Not open for further replies.
Apr 27, 2006
26,588
10,374
"Ewe Mchagga unaombwa kufika Rombo Bar katika Harambee ya kumchangia Mramba kupata dhamana. Tatizo hili la Mramba si la Warombo peke yao ila ni la sisi Wachagga wote wa Machame, Kibosho, Uru, Old Moshi, Marangu, Kilema, Kirua, Sanya juu nakadhalika. Tusaidiane kwenye hili tatizo kwa kuwa ni letu sote wana wa Kichagga. Ndesamburo, Mxxxxxx , Mareale, Shirima wa Precision Air, na Alex Masawe wote wameshafika.

Au ndugu Mchagga weee, tafadhali tuma mchango wako kwenye Account maalum tuliyoifungua kwa ajili ya hili tatizo letu, kwenye:-

A/C No. 01421145081, NBC ARUSHA BRANCH."

Mungu awe nanyi, tafadhali Wachagga wote hima tumsadiei ndugu yetu Mramba.

Mods Iki-expire Ipelekwe Inakotakiwa.
 
Kama wangetushirikisha kwenye mgao wakati zikimiminika, then tungeshiriki kwa sasa.....Lakini NG'O ASILANI......
 
Divisive tribalism, kama kuna haja ya mchango kwa nini wasiseme watanzania? Au watu wa Rombo? Ina maana wakazi wa Rombo ambao huyu ni mbunge wao, ambao si wachaga wajisikiaje wakipata ujumbe huu?
 
Mimi ni mchaga lakini hii mambo ya kusema hili ni tatizo la Wachagga sikubaliani nalo kabisa. Wrong cause!
 
Lighten up bro! it's a joke, it's circulating everywhere. Wanakutana wapi?Kibo palace?
 
kama sio "joke" basini ile wanigeria wanaita 419.
kuna mtu anataka "kutajirika na mramba" naamini
mnanipata
 
ES...inawezakna yote 2 makuu!!!

1. Wanarombo au Wachaga wanataka kumsaidia Mramba. pamoja na Wizi aloufanya Mramba kwa nchi, lkn amefanya mambo "Mema" huko Uchagani...Barabara, wafadhili kujenga shule...na mengineyo ambayo wengine wanaweza kusema.

2. Hata Kama rombo wapo wasio wachaga, lkn Hawawezi kuwa na Uchungu kama walivyo wazawa wa Rombo...so organizers wamelijua hilo mapema...as kuwaita wengine ktk Kikao hicho kunaweza haribu "Michango Endelevu"

3. Pia Ujumbe wa Kafara hapo Juu unaweza pia ukawa kweli...Maana ktk dhiki kama hizi wajanja wengine wanaweza tumia fursa hio kujipatia pesa!!!
 
Kama hii message ni ya kweli, basi tuna kazi ngumu ya kupambana na mafisadi tanzania. Sasa mkishamtoa Mramba, na wale wachaga wengine walioko keko na segerea nani atakayewatoa ??? Huyu fisadi acha aonje joto ya jiwe ili liwe fundisho kwa viongozi tuliowapa dhamana.
 
Mimi ni mchaga lakini hii mambo ya kusema hili ni tatizo la Wachagga sikubaliani nalo kabisa. Wrong cause!

There you go my friend!!! That is why I love Tanzanians whether you're from rombo mashati, namabengo or kasulu. Thanks a lot.
 
ES...inawezakna yote 2 makuu!!!

1. Wanarombo au Wachaga wanataka kumsaidia Mramba. pamoja na Wizi aloufanya Mramba kwa nchi, lkn amefanya mambo "Mema" huko Uchagani...Barabara, wafadhili kujenga shule...na mengineyo ambayo wengine wanaweza kusema.

2. Hata Kama rombo wapo wasio wachaga, lkn Hawawezi kuwa na Uchungu kama walivyo wazawa wa Rombo...so organizers wamelijua hilo mapema...as kuwaita wengine ktk Kikao hicho kunaweza haribu "Michango Endelevu"

3. Pia Ujumbe wa Kafara hapo Juu unaweza pia ukawa kweli...Maana ktk dhiki kama hizi wajanja wengine wanaweza tumia fursa hio kujipatia pesa!!!

Namba 2 ni shameless attitude ya kikabila.Kwa hiyo prerequisite ya kuwa na uchungu na mbunge ni ukabila? Kwamba mtu asiye mchagga hawezi kuwa na uchungu na Mramba kuliko mchagga?

What blatant generalization and shameful oversimplification.
 
Watu walikwisha onya siku nyingi kuwa huu ufisadi uliokithiri unaweza kutuletea matatizo makubwa ambayo hatukuyatemea kama taifa. Sasa hizi hila za kutafuta tribal sympathy zinaweza kufuatiwa na mgawanyiko wa kikabila, kidini, na kirangi; tukifika hapo ufisadi utakuwa umetupiga mwereka mkuba kabisa! Muhalifu ni muhalifu awe mweupe, msukuma, muisalamu au mkristu haijalishi kamwe!! Lazima sheria ichukuwe mkondo wake bila ya kumuonea mtu.
 
Kama hii message ni ya kweli, basi tuna kazi ngumu ya kupambana na mafisadi tanzania. Sasa mkishamtoa Mramba, na wale wachaga wengine walioko keko na segerea nani atakayewatoa ??? Huyu fisadi acha aonje joto ya jiwe ili liwe fundisho kwa viongozi tuliowapa dhamana.

Nadhani sio kweli,
Inawezekana kukawa na kikao cha jamaa na marafiki wa Mramba lakini sio kikao cha wachagga. Wachaga wanatofauti zao kubwa na nachelea kuona nguvu stahili kama ujumbe huu ulivyoandikwa. Lakini tusubiri na wenye japo visimu vyao watuwekee picha za kikao hicho!
 
Huu mzaha,sio rahisi kiasi hicho.....kama meseji hiyo inaukweli basi inawalenga ndugu na jamaa zake waliofaidika naye.......
Kwa upande mwingine..kufa kufaana in action..
 
"Ewe Mchagga unaombwa kufika Rombo Bar katika Harambee ya kumchangia Mramba kupata dhamana. Tatizo hili la Mramba si la Warombo peke yao ila ni la sisi Wachagga wote wa Machame, Kibosho, Uru, Old Moshi, Marangu, Kilema, Kirua, Sanya juu nakadhalika. Tusaidiane kwenye hili tatizo kwa kuwa ni letu sote wana wa Kichagga. Ndesamburo, Mxxxxxx , Mareale, Shirima wa Precision Air, na Alex Masawe wote wameshafika.

Au ndugu Mchagga weee, tafadhali tuma mchango wako kwenye Account maalum tuliyoifungua kwa ajili ya hili tatizo letu, kwenye:-

A/C No. 01421145081, NBC ARUSHA BRANCH."

Mungu awe nanyi, tafadhali Wachagga wote hima tumsadiei ndugu yetu Mramba.

Mods Iki-expire Ipelekwe Inakotakiwa.

Kufa kufaana.

Attention sasa inaamishiwa kwenye Ukabila..washindwe na walegee. Hiyo meseji ilitakiwa isomeke vingine na si wachagga...wachagga wamewekwa hapo kama kisusio...
 
I hope si kweli lakini kama ni kweli pia sitashangaa nikikumbuka ya EL umasaini bila kusahau ya vijisenti usukumani. Kazi nzito.

Kweli bwana, wale jamaa (wamasai na wanyantuzu) si waliwatukuza hao jamaa (EL na Vijisenti)????. Kwa mramba yawezekana ni marudio tu ya ujinga huo ambao pengine ni uozo ulio ktk bongo za waTZ wengi!!!!

Yasemekana Mramba alisaidia sana warombo wenzake kifedha!!!! Pengine wanajaribu kulia juani baada ya kuvuna kivulini pamoja!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom