“Mjumbe” agusia kilichojiri wakati wa Uteuzi wa Wagombea uongozi CCM 2012

Mzalendo JR

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,193
515
WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikimaliza vikao vyake vya juu mjini Dodoma, siri nzito zimeanza kufichuka, namna ambavyo baadhi ya wajumbe walivyokuwa wakihangaika kutaka wapambe wao wapitishwe kwa kila namna.

Vikao hivyo ni pamoja na Kamati ya Maadili, Mkutano Mkuu na Halmashauri Kuu ya Taifa.

Habari za kuaminika zilizopatikana jana, zinasema mvutano huo uliibuka baada ya wajumbe kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, kung’ang’ania kwa nguvu zote kuhakikisha wapambe wao wanapitishwa.

“Ndugu yangu vita ilikuwa kubwa mno, kuna mmoja wa wajumbe ambaye ni waziri katika Serikali yetu (jina tunalo), alipambana mpaka jasho likamtoka, akitaka safu yake iingie kwa nguvu,…wapambe wake hawa ni wabunge ambao wanajiita wapambanaji wa ufisadi, unajua huwezi amini, lakini wameangukia pua, mwenyekiti wetu alitumia busara za hali ya juu, …pamoja na njama zote hizi, nakwambia chama kimetenda haki ya kuwachagua wagombea ambao wana sifa zote.

“Mmoja wa wajumbe, waliokuwa mstari wa mbele kuongoza mashambulizi hayo, ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye alikuwa akitetea jina la Mbunge wa Kahama, James Lembeli ili lipitishwe.

“Chama kimetenda haki, kimeniokoa mimi binafsi na wengine waliokuwa wamelengwa kuangamizwa, tunashukuru chama na busara zilizotumika kuvunja ngome za maangamizi zilizokuwa zimepangwa.

“Mfano baadhi ya majina, yalipendekezwa mikoani, lakini muhtasari wa taarifa za majina hayo ulipofikishwa Dodoma, ulikuwa umechakachuliwa, …baadhi ya wajumbe walisimama kidete kutetea muhtasari huo uchukuliwe kama ulivyo.

“Hali ilikuwa mbaya, kwani ilifikia hatua John Chiligati kuzomewa na wajumbe, baada ya kupinga jina la Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja ambaye alikuwa anapambana na Lembeli,” alisema mjumbe huyo.

Alipoulizwa na MTANZANIA, Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta alisema, yeye hakuchangia jambo lolote, zaidi ya kunyoosha mkono na kushusha.

“Sikuchangia jambo lolote, sikuwa na kundi lolote ndani ya kikao, sikuwa na kampeni, kama ni kampeni ningezifanya kwa mke wangu, lakini hakuwa na misukosuko yoyote kuanzia Tabora hadi Dodoma, …kitendo cha kusema nilikuwa na kundi, wanajua Lembeli ni rafiki yangu… hayo ni maneno ya kupanga baada ya kuona jina la Lembeli halikurudi, hata mimi nilishawahi kupata misukosuko kama hii, nawaomba watu watulie,” alisema.

via MTANZANIA

Source: wavuti.com - wavuti
 
Busara aliyoitumia mwenyekiti ni kuipitisha familia yake manake asingefanya hivyo pangechimbika Ikulu
 
Back
Top Bottom