CV ya Prof. Ibrahim Lipumba, msomi, mtumishi aliyetukuka na mwanasiasa mvumilivu

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Haya JF,

Maneno mengi huku tunawaweka nyuma na kuwakebehi wasomi wetu Prof Ibrahim Haruna Lipumba kwa sasa yupo USA kama mtaalamu wa uchumi Duniani,unaweza kumsikia BBC Swahili akihojiwa na kuuliza maswali juu ya mstakabari wa uchumi Duniani na Afrika kwa ujumla.

Hapa bongo tunamwona hafai,tupo radhi kumtukana na kumkebei lakini wenzetu wanaotumia akili zao vyema wanamtumia kweli kwenye maji mengi wanao kufa kwa njaa ni wale wajinga.

Maisha ya awali ya Prof Ibrahim Haruna Lipumba ni safara yenye kusisimua na kujitutusa kizalendo huku tukiweka kando roho zetu za eda, Lipumba mwenyeji wa ubwa, mhafidhina wa kizalendo, mwenye tabasamu la kati, mwenye busara ya nera na asiyeishiwa hekima, ni simulizi la kujivunia utaifa wetu na Utanganyika wetu kila umuelezapo binadamu huyu aliyebeba alama ya usomi wa Kitanzania.

Prof Ibrahim Haruna Lipumba alizaliwa tar. 6 Juni Mwaka 1952, katika kiji cha Ilolangulu Wilaya ya Tabora Mkoani Tabora Tanzania. Ameanza elimu ya msingi 1959 - 1962 katika shule ya msingi ya Swedish Free Mission Primary School, Sikonge 1962 - 1966 : L.A Upper Primary School, Sikonge

Baadae kuendelea masomo na Elimu ya Sekondari 1967 hadi1970 Tabora Boys Secondary School 1971 hadi 1972 Pugu Secondary School Kisha Elimu ya Chuo Kikuu 1973 hadi 1977 University of Dar es Salaam 1978 hadi 1983 Stanford University. Akapata Shahada BA (Hon.Economics) University of Dar es Salaam 1976 MA (Economics) University of Dar es Salaam 1977 MA (Economics) Stanford University 1979 Phd (Economics) Stanford University1983

Uzoefu wa Uongozi

Aliwahi kuwa mweka hazina wa Umoja wa Vijana Tabora Boys Secondary School toka mwaka 1969 hadi 1970 pia akawahi kuwa Katibu mkuu wa wa Kikundi cha Majadiliano cha Tabora Boys Secondary School toka mwaka 1969 hadi 1970, baadae akaja kuwa Mjumbe wa kamati ya Umoja wa Vijana katika shule ya pugu Secondary School hiyo ilikuwa mwaka 1970 hadi 1971, baadae akaja kuwa tena Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam toka mwaka 1975 hadi 1976. na pia ndiye Mwanzilishi na Rais wa Kwanza wa Stanford African Students Association (SASA), Stanford University; Stanford, California USA hiyo ilikuwa mwaka 1978.

Kazi
◾1976 hadi 1977 Mkufunzi Msaidizi (T.A)
◾1977 hadi 1983 Mhadhiri Msaidizi
◾1983 hadi 1986 Mhadhiri
◾1986 hadi 1989 Mhadhiri Mwandamizi
◾1989 hadi 1993 Profesa Mshiriki
◾1991 hadi 1993 Msaidizi wa Rais Mambo ya Uchumi
◾1993 hadi 1995 Fulbright Visiting Professor, Williams College, Massachussets, United States of America
◾1996 hadi 1998 Senior Research Fellow, United Nations University, World Institute of

Economic Research, Helsinki Finland.

Heshima za Kitaaluma

◾1993 hadi 1995 Fulbright Visiting Professorship
◾1986 hadi 1989 Kellogg International Fellow in Food Systems
◾1977 hadi 1983 Rockefeller Foundation Fellowship
◾1976 Zawadi ya Mwanafunzi Bora, Best Student

Award, Faculty of Arts and Social Sciences,University of Dar es Salaam.

Mshauri wa Uchumi

◾The World Bank
◾UNDP
◾Global Coalition for Africa
◾Preferential Trade Area for Eastern and Southern Africa ( COMESA )
◾Swedish International Development Agency ( SIDA )
◾NORAD
◾DANIDA
◾Ministry of Foreign Affairs Finland
◾Bank of Tanzania
◾Macroeconomic and Financial Management Institute of Eastern and Southern Africa (MEFMI)
◾African Capacity Building Foundation.

Shughuli za Kimataifa

Utafiti kuhusu kushiriki kwa nchi za kusini katika mfumo wa biashara wa kimataifa, Uruguay Round Multilateral trade negotiations kuanzia mwaka 1986 ha 1990.

Utafiti kuhusu sera za kilimo za nchi zinazoendelea.

Kuwasilisha maelezo (Testmony) kuhusu matatizo ya madeni ya Afrika kwenye kamati ya Bunge la Marekani - House Sub Committee on International Development, Finance, Trade and Monetary Policy - Februari 1994.

Kuwasilisha, maelezo (Testmony) kuhusu shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na uhusiano wake na nchi masikini kwenye kamati ya Bunge la Marekani House - Sub Committee on International Development, Finance, Trade and Monetary Policy - Aprili 1994

Kutayarisha "Report of Group of Independent Advisers on Development Cooperation issues between Tanzania and Aid Donors". Juni 1995

Kuteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya sera ya maendeleo (member of the United Nations Committee for Development Policy (1995 hadi 1999.)

Kutayarisha vigezo vya kuainisha nchi masikini sana duniani. (The list of Least Developed Countries (1997 na 2000)

Kutayarisha na kuratibu utafiti na kupendekeza sera za viwango vya kubadilishana sarafu (exchange rate policy) na sera za kulegeza masharti ya mfumo wa fedha (financial liberalization) Kampala, Uganda (1997).

Kutoa taarifa katika Kamati ya Umoja wa Mataifa ya mambo ya uchumi na maendeleo (ECOSOC) kuhusu mgogoro wa kimataifa wa fedha katika nchi za Asia, NewYork (1998).

Kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha muundo na sera za fedha, Wizara ya Fedha, Windhoek, Namibia (1998).

Kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha muundo na sera za fedha, Wizara ya Fedha, Mbabane, Swaziland (1998).

Kutathmini maendeleo ya ‘The Macroeconomic And Financial Management Institute Of Eastern And Southern Africa', (MEFMI) ili kuwasaidia wahisani kufanya maamuzi juu ya kuendelea kuisaidia taasisi hiyo,1998.

Shughuli za Kitaifa

◾Mjumbe - Kamati ya kurekebisha mashirika ya umma, 1992 - 1993

◾Mwenyekiti - Tume ya kuchunguza matatizo ya chama cha ushirika cha mkoa wa Shinyanga (SHIRECU), 1992

◾Mwenyekiti - Tume ya Waziri wa Fedha ya kuchunguza matatizo ya Shirika la Bima (NIC) 1993

Baadhi ya Tafiti za Uchumi na Maandishi Muhimu

◾Stabilization Policies in Tanzania, University of Dar es Salaam, 1984

◾African Unity, Some Practical Guidelines, MAWAZO Vol. 1. No. 2, Mei 1983. Published by Stanford African Students Association.

◾Problems and Prospects of African Economic Integration , MAWAZO Vol. 1. No. 1, Aprili 1982

KATIKA SIASA,

Lipumba katika siasa ameanza kuhudumu tangu mfumo wa vyama vingi ulipoingia nchini 1992, na yeye Lipumba ni muumini wa siasa za kiliberali, anaamini katika usawa, haki kwa wote na uhuru wa kutoa maoni,

Katika uwanda huu wa siasa Lipumba hajafanikiwa vyakutosha, chama chake hakijawa sehemu ya tishio kubwa kwa chama tawala kwa siasa za kitaifa kwa ujumla, hii inatokana na madhaifu machache ya Prof Lipumba katika uga huu wa siasa za kisasa,

Siasa za kisasa zinahitaji mageuzi, zinahitaji kusafiri na nyakati pia siasa zinahitaji fikra mpya kulingana na mapokeo mapya ya kidunia hasa katika ukuaji wa fikra za kibinadamu. Hayo Lipumba ameyakosa ama hana kabisa, CUF hayo imeyakosa ili kuiishi dunia mpya ya fikra chanya.

Tatizo kubwa lipo kwenye muundo wa Chama na falsafa yake ikiwemo itikadi, CUF kiliundwa kwa mtazamo wa harakati za wanyonge waliokosa vyote katika nchi inayojengwa na wanyonge wenye moyo na kuliwa na wajanja wenye meno (ccm). Muundo huu ulibeba taswira hasi hasa baada ya makutano hawa kukosa vyote kabisa na kikubwa ikawa ni elimu, na wezo wa kushawishi makundi ya wasomi kujiunga nao.

Hili lilikuwa pigo kuu, kwakuwa ili chama kiweze kuishi na kutembea katika kila hatua ya mageuzi ni lazima kiwezeshwe na wasomi na wenye fikra chanya (mawazo mapya), Chama kikajijenga mwambao mwa nchi, kikapata ufuasi mkubwa katika matabaka ya wanyonge tena wanyonge hasaaaa yani wasioweza kulinda kura zao hata kwa masaa 12 tu, hili lilikuwa pigo hasa ukipambana na ccm inayosafiri na kuishi kwa mbeleko ya Usalama wa Taifa na vyombo vingine vya dola.

Msomi Lipumba pekee yake asingeweza kuleta mageuzi mapya ndani ya CUF bali alihitaji na anahitaji nguvu kubwa ya fikra za wasomi kila pembe ya nchi ili kusafiri kisiasa, Itikadi ya CUF imeweza kushamiri Zanzibar kwasababu ya slogan yake imara hasa ile ya uhuru wa Zabzibar, lakini Uhuru ukipatikana CUF itakosa itikadi kabisa yenye kuishi kisiasa, itakosa kama ilivyo ccm leo huko visiwani.

Muungao wa vyama ndugu wa UKAWA umeileta CUF katika uso wa dunia mpya, umemleta Prof Lipumba yule wa 2001, sasa sauti kuu ya siasa za nera imezaliwa upya, mwana wa unyamwezi amerejea katika uga wake.

Kama UKAWA watampitisha Prof Ibrahim Haruna Lipumba kugombea urais, basi sarafu halisi itakuwa imetua mahali stahiki kati ya hazina walizo nazo UKAWA.
 
Lipumba namkubali.

ebu tuache ushabiki mtanzania mwenzangu,Hivi ni kwa nini hatumtumii huyu bwana tatizo lipo wapi,maana inasemekana alishawahi kuwa mshauri wa uchumi wa Raisi Uganda,kwanini hapa bongo hatumtumii huyu Prof?
 
Hatumtumii au hajitumii mwenyewe? si aliacha kazi ya kufundisha UDSM? Akiomba kazi chuo chochote hapa Tanzania na Africa nani atamkataa? au anachagua kazi? Hehehe ile ya Magogoni haiwezi yuko biased bana...!
 
hivi wewe bado umelele? wangapi wametolewa UDSM kwa ushabiki wa siasa unataka tuwataje kwa majina? wangapi wamenyimwa mikataba kwa mambo ya kisiasa?

nadhani hatutaki kumtuia tu,lakini Raisi mwinyi alimtumia kama mshauri wake wa uchumi sasa sielewi kwanini sasa?

ebu sikilza bbc sasa usikie jamaa anavyo jibu maswali toka kwa watu tofauti wenye maono tofauti,nadhani umefika wakati kuweka siasa pembeni na kuwatumia wanataalamu wetu

angalia zambia ya sasa,raisi kachukua hata wale wataalamu waliopo nje ya chama chake

vipi bongo? tunaangalia mtaalamu anatumiwa na watu wa nje?
 
ebu tuache ushabiki mtanzania mwenzangu,Hivi ni kwa nini hatumtumii huyu bwana tatizo lipo wapi,maana inasemekana alishawahi kuwa mshauri wa uchumi wa Raisi Uganda,kwanini hapa bongo hatumtumii huyu Prof?

CCm hawahitaji wasomi.
 
Wabongo bwana kwenda USA na kuhojiwa BBC ndo imekuwa nongwa; kuna kujua nadharia za uchumi na kunakujua namna ya kufix uchumi. Prof Haruna ni mzuri kwenye nadharia za uchumi. Lakini sio mweledi wa kutengeneza uchumi. Hawezi kwenda Ugiriki akatengeneza uchumi wa nchi ile kwasababu hataweza. Ulishawahi kuona Prof amekuja na kabrasha linaloeleza namna ya kukwamua uchumi wa nchi hii? zaidi ya kuwa picky kwenye baddhi ya maeneo fulani fulani. Lakini sijawahi kuona mkakti wake mbadala wa kukwamua uchumi- usiniambie habari ya ilani ya uchaguzi
 
ccm mbwiga sana,huyu prof angetusaidia,walau kidogo,ona sasa,hizo positions wanawapa mademu zao waliopata ziro form4!
 
ccm wanazingua sana,huyu prof angetusaidia,walau kidogo,ona sasa,hizo positions wanawapa mademu zao waliopata ziro form4!
 
Prof Wa pumba huyu

Vitabu vingapi ameandika? Theory ngapi amezianisha kwa jina lake, ningependa soma mahali Lipumba theory on microeconomics
Mkuu Lipumba Ameandika maandiko mengi. Kwakua mie sio mchumi sifahamu eneo aliloliandikia ila nilibahatika kuona a kabati lenye maandiko yake kwenye Library ya chuo kimoja chenye sifa duniani. Nilijisikia vizuri sana ughaibuni kule nilikokuwepo.
 
Wabongo bwana kwenda USA na kuhojiwa BBC ndo imekuwa nongwa; kuna kujua nadharia za uchumi na kunakujua namna ya kufix uchumi. Prof Haruna ni mzuri kwenye nadharia za uchumi. Lakini sio mweledi wa kutengeneza uchumi. Hawezi kwenda Ugiriki akatengeneza uchumi wa nchi ile kwasababu hataweza. Ulishawahi kuona Prof amekuja na kabrasha linaloeleza namna ya kukwamua uchumi wa nchi hii? zaidi ya kuwa picky kwenye baddhi ya maeneo fulani fulani. Lakini sijawahi kuona mkakti wake mbadala wa kukwamua uchumi- usiniambie habari ya ilani ya uchaguzi
Nakubaliana na wewe kabisa tatizo sisi watanzania tukisikia fulani ni mtaalamu wa Uchumi basi au mtu kafanya kazi World Bank tunakuwa tunafikiria kuwa hawa ndio watu wanajua jinsi ya kuubadili uchumi wa nchi husika mfano mdogo tu ni akina Balali na sasa huyu Benno Ndulu ambaye alikuwa anafanya kazi kama Lead Sector Specialist with the Macroeconomic Division ya World Bank lakini still ukiangalia hakuna chochote cha maana alichobadilisha kwenye uchumi wa nchi zaidi ya shilingi kushuka kila siku na wanatoa figures and analysis ambazo haziko sawa
 
Mkuu Lipumba Ameandika maandiko mengi. Kwakua mie sio mchumi sifahamu eneo aliloliandikia ila nilibahatika kuona a kabati lenye maandiko yake kwenye Library ya chuo kimoja chenye sifa duniani. Nilijisikia vizuri sana ughaibuni kule nilikokuwepo.

Toa reference mkuu! Niko kwenye mtandao prof wa Pumba huyo he never nominated into any international award
 
hapo ndipo watu ndani ya jf wanaponifurahisha.wakiambiwa Chama cha mashoga/magamba hawafai kuongoza nchi wanabisha.mtu wao akishikwa pabaya wanalalamika.sasa angalia wote wanaolalamika ni wadini haohao na ni magamba haohao.
 
Thank you!
 
Nakubaliana na wewe kabisa tatizo sisi watanzania tukisikia fulani ni mtaalamu wa Uchumi basi au mtu kafanya kazi World Bank tunakuwa tunafikiria kuwa hawa ndio watu wanajua jinsi ya kuubadili uchumi wa nchi husika mfano mdogo tu ni akina Balali na sasa huyu Benno Ndulu ambaye alikuwa anafanya kazi kama Lead Sector Specialist with the Macroeconomic Division ya World Bank lakini still ukiangalia hakuna chochote cha maana alichobadilisha kwenye uchumi wa nchi zaidi ya shilingi kushuka kila siku na wanatoa figures and analysis ambazo haziko sawa

mkuu

nashukuru kwa kuisemea nafsi yangu, micro economy in Tz is dead
 
Back
Top Bottom