Elections 2010 Mjue mgombea mwenza wa CHADEMA

1.ni vema kiongozi wa nchi na makamu wake, wakawa na elimu ya kutosha.
2.makamu hushika nchi rais asipokuwepo.
3.mleta mada hajasema ni wapi, lini na muda gani dr silaa alikiri kuwa mgombea mwenza wake ni darasa la saba.
 
Darasa la Saba? Impossible... Una maana STD 7!?

Yaani Dr Slaa kashinda urais na akashindwa kuendelea na urais kwa sababu yoyote kavile ugonjwa hinvyo makamu wa rais anachukua madaraka na kuwa rais, yaani katika karne hii tuongozwe na mtu wa darasa la saba atatuletea nini, ni bora awe hajui kingereza kabisa kuliko darasa la saba.
Shame on you Chadema,
 
Bill Gates aliondoka chuoni akiwa Mwaka wa Pili (College Sophomore), leo ni MULTI-BILLIONAIRE!

Sometimes, suala la elimu halina msingi wala halihusiki na uwezo wa mtu kuwa kiongozi. Unaweza kuwa na PhD lakini usiwe na sifa ya kuwa kiongozi. Uongozi ni kipaji na si elimu! Kama una uwezo wa kuchambua masuala nyeti, kwa kuweza kusoma miswada ya sheria - inayoandikwa kwa Kiingereza - si lazima uwe na Bachelors, Masters au PhD degree.

Binafsi, simuoni Profesa Lipumba (ambaye ana PhD) kuwa PRESIDENTIAL MATERIAL. Ni mchumi, tena mchumi mzuri, lakini HAWEZI KUWA KIONGOZI!

Jamani, jifunzeni kwanza SIFA za UONGOZI. Si elimu peke yake. Mbona Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa hajahitimu Chuo Kikuu alipoanza uongozi wa Tanganyika? Mmesahau hili?

Tuongee mambo muhimu zaidi, si hizi trivial pursuits! Hazijengi!
 
Bill Gates aliondoka chuoni akiwa Mwaka wa Pili (College Sophomore), leo ni MULTI-BILLIONAIRE!
Hapa unataka kusema nini?

Uongozi wa 'vipaji' ni kitu kimoja tu ktk requirements nyingi zinazohitajika ktk kukabili changamoto za sayari ya leo. Dunia ya leo inahusu KNOWLEDGE, ndio maana wenye busara zao wanasema KNOWLEDGE IS POWER, kwa maana kwamba unaweza ku-control mustakabali wake vyema zaidi. Leo watu wanazungumzia mambo ya kukutanika pamoja kama kijiji, kwenye kuuza na kununua, kuimarisha na kujenga miundombinu ya kisasa, kuinua sayansi na teknolojia...binafsi nisingependa wala hata kutaka kusikia ati mtu wa STD7 ashike hata ukatibu kata..this is an insult to us all. Karne hii STD7?? who are we? somekind of zombies?? HELL NO!
Binafsi, simuoni Profesa Lipumba (ambaye ana PhD) kuwa PRESIDENTIAL MATERIAL. Ni mchumi, tena mchumi mzuri, lakini HAWEZI KUWA KIONGOZI!
Sasa mbona ni kiongozi wa CUF?
Jamani, jifunzeni kwanza SIFA za UONGOZI. Si elimu peke yake. Mbona Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa hajahitimu Chuo Kikuu alipoanza uongozi wa Tanganyika? Mmesahau hili?
Nyerere alifit scenarios na challenges za karne ile hata hivyo hakuwa successful kivile..na wengine wanasema hata ALIFELI..sasa huwezi kumchukulia Nyerere kama mfano watu wakakuchukulia serious, kwene hii kadhia.
Tuongee mambo muhimu zaidi, si hizi trivial pursuits! Hazijengi!
This is VERY IMPORTANT TO US, even if some of us fail to recognize the importance kwa ujinga au kwa blind love.
 
Kama Kikwete ameweza kuwa rais na kuitawala Tz kwa miaka mitano.. nakuhakikishia hata mbwa ataweza!!!!
 
Chadema chama cha vihiyo;

M/Kiti Mbowe, kihiyo

Katibu Canoon law

Naibu M/kiti Sd7

Kweli tuwaachie nchi hawa vihiyo ????
Unajua huyo makamba(katibu wa CCM) ambaye akikwambia kula matapishi yangu, utakula ana elimu gani?
Unaweza ukawa huna elimu lakini una good constructive ideas. Hicho ndo tunachotaka.
Most of CCM leaders including some of the members like you hawana constructive ideas za kutufanya tuondokane na umasikini.
 
Hizi posts za kutetea std 7 awe VP zanifanya nianze kuhisi wenye matatizo ni sisi wananchi na sio viongozi.Na kama mko serious kabisa na mnaamini kwamba sio tatizo...then we gotta change ourself first.
 
Wewe linakuhusu nini? kwani hana uwezo hao waliosoma wanakwiba pesa zetu si kheri tu badilishe uelekeo??????????? kumbuka Enzi za mwalimu mambo yalikwenda sawa :fencing:
 
Elimu ya bure hadi ulaya waliopata Chenge. Lowassa, Karamagi, Mramba, Yona na wengine kama wao zimetusaidia nini? Niwewahi kushuhudia watu wenye masters na Phd wakitetemeshwa na watumishi wadogo wa Wizara ya Ardhi kwa kuwataka kuhama kutoka ardhi na makazi yao ndani ya siku 30 tu na wote walitetemeka na kuanza kungoa mabati na vigae wakiwemo makatibu wakuu wa Serikali hii hii.

Basi alijitokeza mtu mmoja wa O level ambayo haikuwa ya kuiba mitihani aliwashushia vifungu vya Natural Justice, Human Rights na akamalizia na Sheria za Ardhi na fidia. Ilibidi mawaziri waili wa ardhi wakiri kwamba mradi huo ulikuwa wakitapeli na Serikali akalipa fidia mara ya pili na kuwapa wananchi wakiwemo wenye Master na Phd muda wa miezi tisa kutafuta viwanja na makzi mbadala.

Kichekesho kilikuwa pale mmoja wa makatibu wakuu wa serikali hii ambaye kwa kutojua haki zake alitii amri ya wahuni wa Wizara ya Ardhi na akabomoa nyumba yake nzuri kweli. Siku bush lawyer huyu alipomfanya waziri wa wizara wa ardhi akubaliane na hoja zake na kusitisha mradi huo, alikuwa amebakiza fence tu, nyumba yote ilikuwa chini. Ile tangazo la waziri kutoka akasimamisha ubomaji wa fence ibalki na vifusi vya nyumba vikatumika kama ushahidi na akapata Milioni 60 kama fidia ya nyongeza

Kuelimika ni kujua where to get precise information na namna ya kuzitumia sio makaratasi waliyobeba watu wanayaita kuwa ni vyeti huku vichwani hamana kitu hata kujisaidia mwenyewe kwakati wa shida hawawezi
 
Dr Kikwete akiongea??? na Obama........... "Aiseee, sijui niliishia wapi kuongea....."

Obama-kikwete.jpg
Jamaa alikuwa kashika desa lake mkononi,nadhani Obama anajiwazia atamaliza saa ngapi kusoma risala yake huyu?
 
duh jamani hizi kampeni zinachanganya watu akili,so huyo wa darsa la saba si aende shule kuna elimu ya watu wazima,chadema rudini mkajipange upya
 
Bill Gates aliondoka chuoni akiwa Mwaka wa Pili (College Sophomore), leo ni MULTI-BILLIONAIRE!

Sometimes, suala la elimu halina msingi wala halihusiki na uwezo wa mtu kuwa kiongozi. Unaweza kuwa na PhD lakini usiwe na sifa ya kuwa kiongozi. Uongozi ni kipaji na si elimu! Kama una uwezo wa kuchambua masuala nyeti, kwa kuweza kusoma miswada ya sheria - inayoandikwa kwa Kiingereza - si lazima uwe na Bachelors, Masters au PhD degree.

Binafsi, simuoni Profesa Lipumba (ambaye ana PhD) kuwa PRESIDENTIAL MATERIAL. Ni mchumi, tena mchumi mzuri, lakini HAWEZI KUWA KIONGOZI!

Jamani, jifunzeni kwanza SIFA za UONGOZI. Si elimu peke yake. Mbona Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa hajahitimu Chuo Kikuu alipoanza uongozi wa Tanganyika? Mmesahau hili?

Tuongee mambo muhimu zaidi, si hizi trivial pursuits! Hazijengi!

Mkuu nakuheshimu, lakini huu mtizamo wako kuwa suala ya elimu halina msingi ni upotoshaji mkubwa
 
Nyamizi,

Mfinanga ahhhhh Mziray hata alipokuwa akiongea na Dr. Slaa, bado aliendelea kusoma kama kawaida yake. Muungwana na Desa ni kama chanda na pete. Tanzania mambo swaaafi na kibaya zaidi ni kuona wasomi ambao hadi Ulaya/USA/Asia wamekaa, bado wanamtetea.
Kweli njaa na ufupi wa akili za kufikiri ni shida sana. Watu waoga saana kuanza upya kisa tu hawataweza kuishi bila CCM hata kama maisha na kazi zitakuwa kibao. Wamezoa vya kunyonga, vya kuchinja hawaviwezi.

Rais Slaa anafurahiaaaaa kuona Dr Mwenzake akidesa.......

8E9U0063.jpg

Jamaa alikuwa kashika desa lake mkononi,nadhani Obama anajiwazia atamaliza saa ngapi kusoma risala yake huyu?
 
Tatizo ni katiba walio tuwekea chama twawala ni vigumu kwa wapinzani kupata watu mahiri in both part of muungano, ni sawa na cuf kupata mtu makini bara, na vivyo hivyo kwa chadema kupata mtu kama huyo visiwani.
sasa kukosekana kwa hali hiyo chadema na cuf walitakiwa wafanye kama siasa za kenya zilivyo, kwamba unaweza fanya ndoa na mtu msieelewa ki-mantiki, ili kupunguza nguvu za chama twawala.
lakini hapo hapo tunatakiwa tuelewe ingawa elimu ni kitu kizuri na silaha bora kwa maendeleo ya sasa, pia tunatakiwa tujikumbushe kuwa kumekuwepo kwa watu wengi wasio kuwa na proper formal education, lakini waliendeshwa na nia yao wakafanya vizuri, Karume the 1st, lakini alikuwa na vision ya mafleti ya michenzani, hospital ya mao tse tung, uwanja wa Amani etc
Nasikia Raisi wa Brazili Silva de Lula? sio kasoma saana lakini anachofanya wananchi wake wana mpenda, zaidi ya hapo nini population ya zanzibar? itupe taabu saana watu wa Bara? CCM wameifanya katiba ya muungano iwe hivyo ili kula ya wazanzibar iwe yao.
Dr Slaa ameahidi kubadili huo mfumo, kwa faida ya pande zote, maana kwa sasa wabara ndio huchagua kiongozi wa zanzibar.
 
Mbowe alitetea sana uteuzi huu siku ya uzinduzi wa kampeni za chadema. Mimi nina mashaka CHADEMA kuifanyia majaribio nafasi ya Makamu wa Rais. Wana JF hebu nisadieni kuniondoa mashaka ya Makamu wa Rais huyu endapo haya hapo chini yatatokea.

Sina nia ya kubeza elimu ya mtu lakini naweza kuamini kwamba chadema walikuwa hawajiandaa kwenda kushika dola.

1. Ikitokea Rais akienda safari makamu wa Rais darasa la saba ndiye atakaimu nafasi yake

2. Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu au kupoteza sifa za uchaguzi basi makamu wa rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano.

3. Makamu wa Rais huyu ndiye atakutana na viongozi na wageni wa kimataifa katika majukumu yake na kujadili masula mbalimbali yanayohitaji tafakari ya kina.

4. Endapo itaonekana kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili na akili basi itahesabika kwamba kiti ya Rais ki wazi, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na makamu wa rais.

Je, Dr Slaa kamkubali darasa la saba ili kushika hatamu za uongozi peke yake au anahitaji mtu wa ndio mzee.

Je, jambo hili haliwezi kuathiri uchumi wetu?

Je Makamu darasa la saba ana sifa zote za kumudu changamoto za dunia ya utandawazi?
 
Back
Top Bottom