MJUE Lowasa

Mbona mazuri yake hujayaweka hapa. Ni waziri mkuu pekee aliyewahi kufanya maamuzi yanayoonekana kufanywa na kiongozi wa nchi. Big up EL!!!

Haujanyinwa kuyaweka mkuu, we yamwage tu watu wayajue kisha wapime na mabaya yake.
 
ni mwanasiasa pekee aliyesimamia maamuzi yake bila kujali nini kitamtokea baadaye. Baadhi ni haya:-
1. Utoaji wa maji ziwa victoria kupeleka shinyanga bila kujali vitisho vya mataifa wapinzani.
2. Uanzishaji wa hamasa ya shule za kata ingawa baada ya kuondoka waendelezaji wakashindwa kupeleka vifaa
3. Kunusuru taifa kuingia gizani kwa kuagiza richmond ipewe kazi ya kuleta mitambo ya umeme ingawa washindani wa kibiashara na siasa walifanya hujma hadi richmond ikashindwa ku-perform
4. Kueleza wazi wazi tatizo la ajira kwa vijana bila kuogopa kitakachomtokea ndani ya chama
5. Kupinga wazi wazi hoja ya kilimo kwanza. Shughuli ambayo inafanyika bila kuwapo na soko la mazao husika
6. Kuzuiya ujenzi katika eneo la wazi bila kujali aliyetoa ruhusa ya ujenzi huo ni rais wa nchi
.
.
.
.
.
.
.
Huo ni ushahidi wa wazi kuwa hajatokea kiongozi mwenye karisma kama lowassa.

umesahau kuleta mvua ya kutengeneza kukabiliana na ukame!
 
SIFA ZA LOWASA

Katika histori ya tanzania,
hajatokea mwanasiasa mtoa rushwa kama lowasa.


Hajawahi kutokea mwanasiasa Aliyeonyesha tamaa kubwa ya urais kama lowasa.


Ametengeneza mtandao mpana wa wapambe ndani na nje ya chama chake kama lowasa.


Anatuhumiwa kugawa rushwa ndani ya chama chake lakini hatasikumoja hajasimama kuikemea rushwa au kukana hizo shutuma.


Anakashfa ya ufisadi wa mabilioni na alijiuzulu lakini mwenyewe hajawai kuuthibitishia umma kwamba hakuhusika.


Anatumia nguvu kubwa kujisafisha wakati angeweza kuanika ukweli hadharani kwa ushahidi kuwa hausiki then watanzania tukamuelewa.


Mwenye kujua sifa nyingine aongezee.
sifa nyingine kubwa ni kwamba pamoja na porojo ulizotoa hapo juu, ndiye anayefaa kuwa rais Tanzania mwaka 2015, na hakika ndiye atakuwa!
 
Hebu nisaidie Ikulu kwako unaielewaje?.Maana naona mawazo yako yote yako IKULU.

Ngoja nikusaidie ndugu yangu. Issue ya Richmond sio wazi kama ulivyoaminishwa na Mwakyembe na ukakubali. Lowassa alishaizungumzia kwenye kikao cha NEC.

Nyie kwa kutimiza maono ya Mkapa ya mbilikimo wa mawazo na uvivu wa kufikiri bado mnaamini Lowassa ni mchafu.

Wapiga kura hawapo hapa JF. kwanza walio wengi JF tupo nje ya nchi. Wewe fikiria Chadema ilivyokua inaamini inakubalika kati ya kata 29 udiwani imeambulia 5 tu.

What message are you getting?

Ikulu ni makazi na ofisi ya Rais au kiongozi wa mwisho kimadaraka wa nchi.
 
Sio mdini.

lowasa_monduli_na_waislamu_p1_560_416_c1.jpg

Ni Sheikh aliyepata ushehe wake hivi karibuni na kuanza kugawa tende misikitini
 
Muhimu kujiuliza, mtu anayekusanya fedha toka anakojua, na kuwanunua watu wa chama chake mithiri ya mchuuzi wa mifugo afanyavyo kwa kununua mifugo wengi kwa bei nafuu ili badae akawauze kwa faida, anafaa kuaminiwa na watu maskini kama sisi tunaohitaji uadilifu wa serikali ili tuzidi kudumu?
 
Kila jaamii huongozwa na yule ambae yuko best kwa yale ambayo jamii husika huyafanya...

jamii ya waadilifu huongozwa na muadilifu kuliko wote

jamii ya wezi huongozwa na mwizi kuliko wote

jamaa ya majambazi na watoa rushwa..huongozwa na the best among them.....
jamii ya watu dhaifu huongozwa na aliye dhaifu kuliko wote
 
Mbali na utajiri wa kurithi kwa taarifa yako pesa nyingi kaipata kwenye uuzaji wa tanzanite,hizo za kuhusishwa na ufisadi ni kidogo sana,hamna kama yeye ndani ya c.c.m nzima

Hizo Tanzanite zililipiwa kodi kiasi gani? Kama kidi haikulipwa au alilipwa na rafiki zake kwa kuwapa access ya Tanzanite bado huo nao ni uhalifu tu.
 
Kwa nini mtuletee hapa habari za EL hapa? Kwani nani kasema anataka Rais atoke CCM hata kama ni msafi na mweupe kama theruji? Hakuna kizuri ndani ya CCM system nzima imeoza. Hata kama akija msafi na mchapa kazi haifanyia wapi ndani ya uoza wa system ya CCM? Muulize EL alipata wapi utajiri wakati anajulikana akiwa AICC kama mkurugezi alikuwa anatembelea Ki-beatle maskini hoehae? Alipokwenda Wizara chini ya Waziri mkuu inayohusika na maafa pesa nyingi zikachangwa kusaidia maafa ya mafuriko kusini utajiri wake ukaanzia hapo. Ni mtu mwenye tamaa ya kunyakua kila kitu hata kama una kidogo atakitaka kukichukua. Ni mchapa kazi ili kutafuta sifa lakini kwa tamaa zake yuko tayari kuuza nchi mradi hapate hela.
Hongerea jamani ni mikakati gani kuingiza CDM madarakani siyo kutuleta mambo ya Lowasa mwizi mkubwa huyo
 
Ngoja nikusaidie ndugu yangu. Issue ya Richmond sio wazi kama ulivyoaminishwa na Mwakyembe na ukakubali. Lowassa alishaizungumzia kwenye kikao cha NEC.

Nyie kwa kutimiza maono ya Mkapa ya mbilikimo wa mawazo na uvivu wa kufikiri bado mnaamini Lowassa ni mchafu.

Wapiga kura hawapo hapa JF. kwanza walio wengi JF tupo nje ya nchi. Wewe fikiria Chadema ilivyokua inaamini inakubalika kati ya kata 29 udiwani imeambulia 5 tu.

What message are you getting?

Ikulu ni makazi na ofisi ya Rais au kiongozi wa mwisho kimadaraka wa nchi.
Wewe ndiye unahitaji msaada. Lowasa alishiriki kwenye hujuma ya Richmond na akinufaika nao. Hizo ndizo taarifa za kiuchunguzi zilizopo. Na zina ukweli wote zinaaminika kwa wananchi wazalendo na wapiga kura wa nchi hii.
Huwezi kusema eti mwenye issue alikuwa JK. Unajuaje kama walikuwa wote wawili?
Pili ikiwa Lowasa alijua huo ni ufisadi na uwizi kwa taifa na akashiriki kwenye ussue mpaka mwisho kuna haja tena ya kumuengua kuwa alikuwa hahusiki? Hakujua kinachoendekea? Kama ni msafi kana mnavyotaka kutuaminisha uongo huu kwanini alikaa kimya? Kama alikuwa kiongozi waziri mkuu akakaa kimya wakati taifa linaibiwa huyo kweli ndiye anafaa kupewa uongozi wa nchi? Akipewa urais atauza nchi kiasi gani akionyeshwa pesa? He is nothing but plain damn thief. period.
 
Naona Magamba ya Lowassa yako kazini kumsafishi. Watanzania amka usingizini uzi huu hautufai na naona uvivu kuusoma hasa hasa unapomhusu Loawasa na mtu wa CCM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom