MJUE Lowasa

Amevikamata vyombo vyote vya ulinzi na usalama kama JWTZ, TISS na POLICE. Pia viongozi wote wa dini wanamkubali na wanataka awe rais wa Tanzania 2015.
 
Alienda kununua mvua Tailand

alafu akaziuza njiani kabla hazijafika Tanzania.
Chezea lowasa wewe, lol.
Halafu nashangaa kuna watu wanamtetea, kweli fedha mwana haramu.
 
Amevikamata vyombo vyote vya ulinzi na usalama kama JWTZ, TISS na POLICE. Pia viongozi wote wa dini wanamkubali na wanataka awe rais wa Tanzania 2015.

Huyo kiongozi wa dini anaetaka Fisadi awe rais atakuwa hafikirii vizuri.
Kwakifupi hastahili kuitwa kiongozi wa dini bali kiongozi wa mafisadi.
 
Kila jaamii huongozwa na yule ambae yuko best kwa yale ambayo jamii husika huyafanya...

jamii ya waadilifu huongozwa na muadilifu kuliko wote

jamii ya wezi huongozwa na mwizi kuliko wote

jamaa ya majambazi na watoa rushwa..huongozwa na the best among them.....

couldn't be put better... ican only add in a slightly different angle; Nyerere aliingia nchi ikiwa haina wezi wezi na wajanja janja wengi na yeye akaongoza kwa uadilifu mkubwa, Mwinyi alianzisha ujanja ujanja na mission town kwa sera mbovu za uliberali uchwara, Mkapa akaja kukuza na kusimika hawa mission town na sasa JK ni mjanja mission town aliyepikwa na kuwekwa kama chambo ya kutengenza njia ya mnufaika mkubwa wa miaka 25 hii ya ujanja ujanja na umission town; Don Lowassa.

Hii system hadi ife yenyewe au iondolewe kwa nguvu otherwise hamna mtu msafi, muadilifu na mzalendo wa kweli atapenya CCM kuja kutuongoza na hata upinzani kwenyewe wako wachache wale waadilifu wa kweli moyoni (kwa sababu hatujawapa cheo kuwajua, waswahili wanasema kumjua mtu mpe madaraka au pesa hapo utamjua yukoje kiundani).


Mungu ibariki Tanganyika
 
Lowasa ni mwanamume wa shoka,nijembe la kikwelikweli. Naomba mwenye kuratibu mtandao wake ani PM ili nami niwe kwenye mtandao wa kuhakikisha mwanamume huyu akitinga Magogoni 2015.
 
Hana ushawishi wa kutosha kuwaunganisha watanzania wanaoelekea kugawanyika kidini na kikanda.
 
Yeye ndiye mhariri mkuu wa gazeti la Mwananchi kwa sasa.
Hii ni kwa sababu yeye ndiye aliyempa kazi Tido Mhando pale TBC. Na pamoja walifuja mabilioni ya shirika hilo la utangazaji.
Lowassa bado ameishika TBC Kupitia Susan Mongi ila siyo kwa nguvu sana kama wakati wa Tido.
 
Kwa jinsi nchi hii ilivyo shagalabagala, tunahitaji kiongozi anayeweza kuburuza watu angalau kwa kipindi kimoja cha urais. Wapo candidates kadhaa kutoka vyama vya siasa wanaoweza kushika barabara jukumu hilo. Kwa upande wa ccm hakuna mwingine zaidi ya Edward Lowassa. Huo ndiyo ukweli na utabaki kuwa hivyo.
 
images


Majungu sio mtaji; mwenye ushahidi 100% kuhusiana na tuhuma zote mnazosema za mzee huyo hapo juu wekeni wazi hapa jukwaani.
 
Angekuwa na uwezo huo unaodai basi angezuia ufisadi mwingi uliotokea wakati akiwa ndani ya Serikali kama EPA, RADA, mikataba ya uchimbaji madini, Kigoda, Meremeta, Uuzwaji wa nyumba za Serikali na Richmond ambao alihusika kwa karibu na kuliingiza Taifa katika hasara ya zaidi ya $100 million.

Umemsikia hadi hii leo anashindwa kutoa hata kauli moja kuhusiana na ufisadi uliokithiri ndani ya Serikali kwa sababu anajua fika kwamba yeye mwenyewe ni fisadi wa miaka mingi.

Ni mwizi tu huyu na hafai kabisa kupata ridhaa ya Watanzania kuongoza nchi na tutafanya kampeni za hali ya juu kuhakikisha haingii Ikulu 2015. Wakati wa kukaa pembeni na kuangalia nchi yetu ikizidi kuangamizwa na mafisadi ndani ya magamba umefikia tamati.


Kwa jinsi nchi hii ilivyo shagalabagala, tunahitaji kiongozi anayeweza kuburuza watu angalau kwa kipindi kimoja cha urais. Wapo candidates kadhaa kutoka vyama vya siasa wanaoweza kushika barabara jukumu hilo. Kwa upande wa ccm hakuna mwingine zaidi ya Edward Lowassa. Huo ndiyo ukweli na utabaki kuwa hivyo.
 
mnyukano wa siasa za maji taka..! no buddy ever kicks a dead dog!!!! cc bhana.. arghhhhhhhh
 
Hata kama ni kweli, akiwa rais atakuwa wa wote. Na yakupasa kujua kuwa, hakuna mtu atakayeweza kuwa rais kwa kupata kura za waislamu tu au wakristo tu. Ni wote ndo tutakaomchagua rais wetu. Kwahiyo mimi sioni kama EL anafanya vibaya

hakuna Raisi mdini , tuzungumzia usafi wa kulitumikia Taifa letu.
 
masuala magumu tunayatolea majibu mepesi sana,watanzania ni waoga sana kutoa ushaidi mbele ya mahakama kama kweli lowassa ni fisadi peleka ushaidi wako mahakamani.yale yalikuwa ni masuala ya kibunge yaliamuliwa kibunge na yeye mwenyewe kujiuzulu wadhifa wake sasa hii habari kila siku ya fisadi inatoka wapi? Ni vema tukawaambia wale waliomtuhumu wapeleke vielelezo hiyvo mahakamani,kitu ambacho ni kinyume taratibu kwa mujibu wa katiba juu ya mihimili hii.sioni sababu yoyote ya sisi ambao hatuna ushaidi wowote kulizungumzia suala hili kwani ni hatari sana.kingine ni kuwa kama haumfahamu mtu vizuri si vema kumzumgumzia maana utajaa sumu bure na kuzeeka mapema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom