Mjomba wangu amemtongoza mke wangu

Nakushauri usimuulize huyo mjomba , maana mtafaruku utakaoibuka utakuwa mkubwa sana. mshukuru Mungu mkeo kakwambia kwa hiyo
hakuna baya lolote litakalotokea
Shantel!

Kama huyu kaka ana ushahidi na atamuapproach mjomba kistaarabu sidhani kama kutakuwa na mtafaruku na hata kama ukitokea basi utakuwa ni for the better! Pia hii itatoa mwanya ili na upande wa pili wa mashtaka usikike, unajua so far ameskilikana mwanamke tu! na usishangae pengine hili swaga lote mwanzilishi ni huyo mwanamke. Wanawake tunaambiwa ni mazaifu lakini kwenye mpango wa kutubambikia kesi wako strong kweli aisee!
 
Loh humu duniani mbona kuna mambo mazito na magumu yaani hata ndugu bado anatamani kushea mke wa anko wake, inaonekana ana tabia chafu na ndio tabia zake hizo siku zote.
Pole sana hii ndio mitihani ya maisha.
 
yeye si kamwaga ugali wewe mwaga MBOGA kabisa, heri ya shari kamiri kuliko shari nusu.
 
kama vp mpotezee tu sema akija kwako ndo hvyo utafnyaje ndo ndugu wa mama yako mchekeee tu ongea nae ukishndwa mwambie aache tabia yake ili uache salama hata ukiondoka akija aogope kufanya uovu
 
Mwanamke akitongozwa hasemi, akishatoa mchezo ndio anasema katongozwa. Na siku Mjomba wako akimuuliza mbona umenisaliti, atasema siku ile fulani alikuona na ili kuuwa soo ndio ikabidi nikutose ki aina. Take it from me. Mjomba kishakula mali yako. Na nnakuhakikishia hilo kwani "Mjomba" hatongozi kwa maseji, awache ushahidi akikataliwa? Huyo mkeo anakuzuga na kisha liwa, na ukimuuliza hizo meseji, atakuambia alizifuta.
 
Naombeni ushauri wadau,nilikuwa miangaikoni nje ya mkoa ninaoishi takribani miezi miwili,nikiwa safarini siku moja mjomba(mdogo wake mama yangu tumbo moja) alikwenda arusha kikazi na huko ndo nilipomwacha mke wangu,mjomba alikwenda kuisabai familia yangu mchana ilipofika usiku akaanza kumwandikia mke wangu sms za mapenzi akamtongoza na kumwaidi kuwa endapo atampa penzi angemwambia kitu cha muhimu kuhusu mimi,wife alimkatalia na kumwambia hawazi nisaliti coz ananipenda sana,kesho yake mjomba alirudi nyumbani kwangu akaendelea kumlazimisha wife amkubalie ila alikataa katakata na kumwambia amemchukia milele na nikirudi lazima amshitaki kwangu,mjomba alipoona karata yake imegonga mwamba akabadili mada na kusema alikuwa anamtega ajue msimamo wake kama nimwaminifu kwangu! Na kumsisitiza asinieleze na afute zile sms alizomtumia. Nimerudi arusha wife amenieleza story nzima na zile sms kanionyesha ila amenisii nisimfanye chochote uncle coz ndugu zangu watamuona mchonganishi. Hivyo wadau naombeni ushauri nifanyaje?

Ndugu nini? huyo mjomba kwanza unamfungia safari kisha unampa kibado mbaya sana, kisha unampigia marufuku kufika kwako, alafu kama kuna ndugu yeyeto akijitia kiherehere naye una mburn.
 
Mkeo yukoje? jiulize pia mjomba kawezaje mtongoza, maana tunalalamika tukitongozwa na sie wakati mwingine tunaalika mitongozo
usijenge bifu nakushauri unaweza mwambia tu mjomba najua ulichofanya ukamwacha anahangaika, ila usimnunie wala kumtenga mpaka ndugu wengine waingilie kati
 
Mkeo yukoje? jiulize pia mjomba kawezaje mtongoza, maana tunalalamika tukitongozwa na sie wakati mwingine tunaalika mitongozo
usijenge bifu nakushauri unaweza mwambia tu mjomba najua ulichofanya ukamwacha anahangaika, ila usimnunie wala kumtenga mpaka ndugu wengine waingilie kati

Mjomba kama ana akili atajistukia mwenyewe tu. Hakuna haja ya kumuambia. Lakini kama ni zuzu basi kuna haja.
 
Kwa vile kwa mila zetu huyo ni mzazi wako si busara kum-confront na kumweleza alichofanya wewe peke yako. Ni Busara zaidi kumshirikisha mama yako ambaye ni dada'ke ukamwonyesha vielelezo vyote na kumsihi amkanye mdogo wake kindugu na kwa siri ili asirudie tena.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kuna mzee mmoja wa makamo kidog aliwahi kunieleza wafuatayo; Mke akikueleza mambo ya kutokewa na mwanaume, be careful kwa sababu haina uhusiano wa moja kwa moja na uaminifu; kuna uwezekano mkubwa kuwa hakumpenda jamaa na kama ni mwaminifu sana basi akwambiye pia na wale ambao huwajui wamewahi kutoka na out au anawazimia but hajapata nafasi ya ku interact nao. Sjui kauli hii ina ukweli kiasi gani?????? Wana JF mwaweza nisaidia.
 
.......kazi kweli kweli, kuna dada yeye alitongozwa na mkwe wake yaani baba ya mume wake.
 
Kuna magonjwa sio ya kulea hata kidogo...mjomba inabidi awekwe chini na akanywe mara moja.
 
Mtongoze na wewe huyo mjomba wako bila kumuogopa tena mwambie unamzimia sana mgongo wake na kiuno chake! Mbembeleze kuwa hata suna tu, kiingie kichwa tu we utaridhika!!
<br />
<br />
duh! Hii hatari, kwani! Hii ki2 ina kichwa sawa, lakini haina mabega! Siitaenda yote!
 
Kuna mzee mmoja wa makamo kidog aliwahi kunieleza wafuatayo; Mke akikueleza mambo ya kutokewa na mwanaume, be careful kwa sababu haina uhusiano wa moja kwa moja na uaminifu; kuna uwezekano mkubwa kuwa hakumpenda jamaa na kama ni mwaminifu sana basi akwambiye pia na wale ambao huwajui wamewahi kutoka na out au anawazimia but hajapata nafasi ya ku interact nao. Sjui kauli hii ina ukweli kiasi gani?????? Wana JF mwaweza nisaidia.
<br />
<br />
uyo mzee kama yupo mtumie vizuri, nimependa aiseeh...
 
niliwahi kuulia swali hapa zamani na sikujibiwa

je mke akisema fulani kanitongoza ina maana kashaliwa?

na kama sio lazima awe ameshaliwa,why jamii ina amini hivyo?

nakumbuka ya shyrose banji na sugu ilikuwa hivyo hivyo....

na sasa nimemsoma faizafoxy hapo juu

naanza kuamini hivyo...
 
Kaka una mke wa maana sana! Katika mazingira mengi najua wanawake wengi wangekataa ila wasingewaambia waume zao, ( Hii tabia inaniudhi!) Kama mtu umekataa kweli kwanini usiseme? Eti utasikia 'niliogopa kuwagombanisha' Bull shit!...................
Sokwe wa Town nimekuelewa ila nafikiri mii ni mmoja wa wanawake hao wanakuudhi! NISINGESEMA katu ila ungenisoma kwenye matendo au kama ange'endelea' kuni'omba' ndo ningempasulia mwenyewe nimpe maneno yake akashiba kisha aamue mwenyewe kunisemea kwako kama mkosa adabu ndo ningefunguka lakini nimemweleza mwenyewe kuwa sipendi, kaonekana kunielewa sasa naja shtaki ili iweje?? Unione mwaminifu kwako? je nakwelezaga hata hao wanaoni'finyia' mijicho yao huko barabarani??

Rafiki yako sawa nitampaka na kisha nije nikupe live but ndugu yako?? hapana ntakuonyesha tu kwa vitendo kuwa mtu huyu mie simpendi ukitaka kujua zaidi utachunguza but sio mie out of nowhere naanza tu......Mume wangu unajua mkwe wangu (wengine sie wajomba wa waume zetu ni sawa na baba mkwe!) kanitongoza (sasa hapa sijui ndo ntasema na hayo maneno alotumia kunitongozea??).

Hapa mkeo kama ndo ningekuwa mimi kwa vile nlishampa Mjomba black and white na mjomba akaonyesha kunielewa basi kifuatacho ITV ni kukeep distance kiaina na huyo mjomba na kutomuintatain kabisa labda kama atarudia kunsumbua na mitongozo yake. Hii itanisaidia kwani kama mume wangu wewe ni mchunguaji ni wazi utayaona mabadiliko yangu dhidi ya huyo mjombako na hata ikitokea umesikia kuwa alishanitokea itakuwa rahisi kuelewa why ninamvalia miwani ya mbao!! lakini nianze tu kukwambia ?!! Siku ukinigeuka nakunitimua kwako si nyie mwashikana mikono na mjombako?!! Damu nzito bana.
 
Back
Top Bottom