Mjini uwanja wa fujo, kila mtu anacheza ngoma anayotaka kivyake!!wenye nyumba mpo???

The King

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
357
1


MJINI UWANJA WA FUJO,KILA MTU ANACHEZA NGOMA ANAYOTAKA!!WENYE NYUMBA MPO???



Huyu dada pichani ni mkazi wa hapa jijini Dar alikuwa kapanga huko Magomeni kwa mwaka mzima nyumba ya dada mmoja hivi.Ila kwa kipindi kirefu anasema mama mwenye nyumba amekuwa akimnyanyasa yeye na wapangaji wenzake.Sasa kodi yake imeisha jumamosi ya juzi 27 na ikawa ndio siku yake ya kuhama.Akaamua kabla ya kuhama kabisa afanye sherehe ya kuhama nyumba hiyo na kumshukuru mungu kumuepusha na balaa la kuendelea kuishi nyumba hiyo.Na pia kumpa mama mwenye nyumba vipande vyake.



Nyumba ndio hiyo hapo inavyoonekana kwa nje getini.

Watu kibao walikuwepo walialikwa katika shughuli hiyo ambayo haijawahi kutokea kihistoria ya maswala ya wapangaji na wapangishaji.

Tena kulikuwa na kitambaa cha sare kwa rangi tofauti

Matarumbeta yalikuwepo na wamelipwa yaleyale kama ya msuto wa magomeni hahahahaha

Teeeeeeeenaaaaaaaaa wapangaji wote wa nyumba hiyo walijumuika na mwenzao kusherehekea kuhama katika nyumba hiyo kwa mauno ya kufa mtu.Hawakuogopa notice hata kidogo hahahaha

Shughuli ni watu..............

GetInline.aspx

Muda wa kula ukafika sasa biriani likapakuliwa saa saba mchana hiyo,watu wakalaaaaaaaaaaa kwa raha zao.



Mwenye shughuli akihudumia waalikwa chakula cha mchana,biriani la nyama.


Mnuso unaendelea hahahahahaha jamani,mmmh.


GetInline.aspx



Kibao kata pia kilikuwepo kwa wale mnaokijua kibao kata yaaani balaaaaaaa



Hapo ni nyimbo za vijembe kwa kwenda mbele ujumbe kwa mama mwenye nyumba


GetInline.aspx




Mizigo ilikuwa imefungwa tayari jioni gari ikifika ni kupakia na kuondoka,kwenda makazi mapya ambayo si mbali kutoka nyumba aliyohama.

Wakati haya yanaendelea mama mwenye nyumba alikimbia na mpaka leo tumeulizia hajarudi.Hii ndio Bongo wapendwa hahahahahah
 
ZE KING: UMETUMWA kuitanga blog ya D Marios kwa wana jf?. Ume höngwa sh ngapi?. Nitakuitia vijana wa Sophia Simba sasa hivi. Ila, big up kwa photo hizi japo ni ngumu kujua kama zinawakilisha stori yenyewe
 
Back
Top Bottom