Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjikumbushe Mzumbe High School

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Bubu Msemaovyo, Nov 26, 2008.

 1. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,489
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 38
  Bila shaka Wana Mzumbe mpo hapa JF, nimetumwa kuwakumbuka wafuatao John Mongela, James Bwana, Michael Thomas Sebastian Sarota, Hassan Rajab Hassan, Patrick Maleva, Anderson Segereti, David Black, Obed Mwakitalika, Clement Mwashambwa, Kwela Mgaya, Theophil Alexander, Njaule Mdendu, Johnson Jasson, Sollomon Shati, Obed Msenga, Charles Nakembetwa, Gideon Mandesi, Isaac Kassanga, Dereck Kassanga, Deus Changala, Timilai Sheshangali, Shemaghembe Ntulwe, Sainet Katulunga, na wengine wengi sana. Waliosoma pale mmeombwa kuongezea majina ya wale mnaowakumbuka.
   
 2. Y

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 3,795
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 38

  Duh, hivi Shema yupo wapi? nilikaa nae pale Mkwawa namba mbili hahaha loooooooooooooooooongtime, jamaa alimaliza form six mie nikiwa form one first term (1991)...was a very nice guy, mgosi wa kaya mwenzangu na alinipa michongo ya ku-survive pale Uzumbeni.
   
 3. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,194
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Nje kiduchu kwa mchomeko, wale wa Sengerema,Bwiru,Nsumba,Ihungo,Kahororo,Tabora Boys,Kantalamba,Moshi Tech,Old moshi,Tosa boys,kasino Mkwawa,SHYCom,Kibohehe, na kule abroad Zenji mpo?
   
 4. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2008
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 558
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh, mnanikumbusha *PIECE* + *GOGO*
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,480
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 63
  Ndio kusema ulikuwa darasa moja na kina Khamis Mwisongo??? Long time, hivi Tabu Samike yuko wapi siku hizi?
   
 6. Y

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 3,795
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 38
  Yap, darasa moja form 1-4!! Tabu mara ya mwisho nilimuona Mwanza mtaa wa Uhuru na rafiki yake Seba wapo njwiiiiii (hiyo ilikuwa mitaa ya 1997)......zaidi ya hapo sina ze dataz!!
   
 7. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2008
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,034
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 36
  Babu, na mimi nipo ktk hilo kundi Mtweve, MD. wanaomkumbuka MOHAMED KISERA, naomba unipe kontakti zake plse. Nimepanga vakesheni ya kwenda kutembea MZUMBE wiki ya pili ya Decemba, na nitatembelea pia sehemu niliyokuwa nazamia msosi pale IDM.
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,480
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 63
  Duh si mchezo, Lile darasa lenu nilikuwa naliadmire sana.
   
 9. Y

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2008
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 3,795
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 38

  wewe ulikuwa form gani wakati ule? ulikuwa unaishi kijiji gani? chances nakujua...hahahahaha:D! Unamkumbuka "Shangazi" na "Physical"? Kuna mtu juzi juzi hapa alinikumbusha Mama Kilwai or so (alikuwa anafundisha geography), alikuwa na wowowo si polepole...Unakumbuka "Chang"/Changarawe na kule tulipokuwa tunaendaga picnic kama "kijiji" kikishida usafi!??

  Song la shule:

  Shule yetu Mzumbe Sekondari, yasifika kote Tanzania.
  Malezi ya Mzumbe, Elimu yake, nikamilifuuuuuu yaki-Tanzania,
  Daima mbele, nyuma mwiko.

  Vijijini pia na mijini, matunda yake yaonekana..
  Malezi ya Mzumbe, elimu yake, nikamilifu ya ki-Tanzania
  Daima mbele nyuma mwiko.


  ...Idd Mkombozi hahaha alikuwa na tafsiri yake ya kifisadi ya "daima mbele, nyuma mwiko." Uzumbeni ilikuwa pouwa, ukiondoa ile typhoid...
   
 10. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2008
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 558
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ee bwana uko wapi siku hizi wewe?
   
 11. H

  HuXiang Senior Member

  #11
  Nov 27, 2008
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Munaboa,ili mrabi mimi ni member mzuri wa mzumbe lakini siwaungi mkono kwa maana hakuna cha maana munachotukumbusha,hata Afande sele alisema mwimbo gani munatajataja majina munachoongea hakina maana,kama munataka mambo ya maana fanyeni mavituzi ili ije siku watu wakisikia then waseme hawa ndio wazumbe.
  Tatizo elimu ya Tanzania ilikaa kwa kubebabeba mno ndio maana hao watu waliotokea huko Mzumbe,Ilboru,kibaa na kwingineko huku sioni cha maana wanachokifanya.
  Jamani elimu sio kufaulu au kuwa TO bali ni nini unakifanya,Nimekaa mzumbe na ninawajua wazumbe ambao walikuwa vipanga ila sasa sioni wanachokifanya especialy wale walioenda nje sehemu ambazo watu wanapima kipaji sio ukaliliji wa pepa za Mungai ambazo wibo tayari kashalikisha 80%.
  Nakumbuka kipindi tunamaliza kuna ile kumi bora yetu ya kitaifa,hao watu waliochukua kumi bora,jamani...Elimu ya Tanzania bado ni tete na imekaa kubeba mno.
  Naomba watupe kamuda kadoogo mno tuje tuprove kuwa sio wote walioko special ni vichwa bali ni idadi ndogo mno kati yao.
  Kumbuka tunaposema Special student tunahitaji ubunifu na si kiwango cha kubeba na kuja kushusha kwenye mtihani.
   
 12. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2008
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 558
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sawa, watu wanajaribu ku-socialize, huwezi kuanza from nowhere thread imeanzishwa hapo hapo mmeanza kuongelea proteonomics! Una point kidogo lakini chuki binafsi imekuzidi- kama 'ulifeli' shauri zako na makarai au ma-D yako.
   
 13. H

  HuXiang Senior Member

  #13
  Nov 27, 2008
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu kama mimi ningepata hayo ma D basi nadhani Tanzania nzima ni wachache mno ambao wangepata hata F kama si -F,mimi ni mwana mzumbe mmojawapo na mkeleketwa mmoja,ila huwa napenda kusema ukweli pale kwenye ukweli,sasa kama kila shule italeta tujikumbushe si JF yote itajaa Tujikumbushe??(Nadhani umeshaona kazi iliyoanza)
  Sisi wazumbe ni wasomi na tunajiita ni vichwa,je tumeshidwa kutafuta njia ambayo itatuweka pamoja na kuitangaza shule yetu zaidi ya mithread ya hapa ambayo punde tu admin ataiban?? Nilikuwa natoa changamoto kwa wanamzumbe,ila pia sipendi hii ya kutajataja majina ya watu eti mutumie hapa kujifagilia,si bora mungeniletea story ya Virei au nyuji ya shangazi au hata mambo ya mongwe ningewaelewa? mungetaja majina ya watu muhimu ambao wanawahusu wote kama Kinunda,Mzee Mwasha,Baba Wibo nk bila kusahau mambo ya Planet,Jidi au Fede hapo tungekuwa wote.
  Ushauri.Tujaribu kutafuta njia ambayo itatuweka pamoja bila ya kubughudhi au kuwakera wengine,stay tuned nipo njiani kudesign kitu ambacho kweli kitafanya kazi na watu mutakiappreciate,ndani ya wiki mutayaona matunda ila sitaki mambo ya kutajataja majina kwani misifa mingi ilikuwa kutokana na Elimu dume.
  Nawakilisha toka Duolojie.
   
 14. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,194
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Well well man wangu.......ma TO nawaona ovyoo sana kazi hawajui material hamna kichwani i could say that walikuwa wanakariri as Wibonele(nimem miss Wibo) alivyowalikishia pepa......Nani asiyejua mzumbe wanapewa pepa(maswali) kabla ya mtihani.Kuna To mmoja nilienda nae sehemu fulani alikimbia akarudi Bongo kwenye elimu ya kukariri.
   
 15. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 461
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 18
  watu kukumbuka good old days sio vibayaa. mimi sikusoma Mzumbe ila kuna washkaji zangu wa karibu niliokutana nao high school waliotokea Mzumbe walikuwa good people na wanasimulia kwamba wali-have fun sana huko, sasa kama wewe hayo yalikuwa yanakupita acha ku-hate. Kusimuliana yaliyopita sii mbaya na kila mtu anapambana na future kivyake, whether ka-make it or not yote maisha.
  [​IMG]
   
 16. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #16
  Nov 28, 2008
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,034
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 36
  mi nipo kusini karibu na MOZAMBIQUE nahudumia wapiga kura
   
 17. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,480
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 63
  Wewe una utani na baba nanihii wa Houston,TX. Anzisha thread ya Mkwawa tuwachane.
   
 18. K

  Koba JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 5,878
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 48
  ...Mzumbe was a good school na memory kubwa ni manyapu wa kilakala na basketball viwanja vya IDM mzumbe,ila lile dongo jekundu na ngama la mama masikio kwenye ndabuli nalo is somethin to remember...nakumbuka kuna teacher mmoja matekele alinipa adhabu ya kuchunga ile ming'ombe basi ilikuwa balaa tupu siku hiyo,niliwachapa wale ng'ombe wakapata kichaa katika kukimbizana nao wakaingia ofisi ya walimu,ilikuwa balaa tupu siku hiyo maana Chiduo na matekele kwa misifa walinishindilia mabakola yasiyo na idadi na kuniongezea mituta ya michicha ...hawa madikteta wangekuwa unyamwezini lazima ningetambaa nao,btw nilikua pale early 90's (Karume village).....tuendelee...
   
 19. Mgoyangi

  Mgoyangi JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka Jaji Makaramba alisoma pale na alikuwa kiongozi wa Mahanga ya Shaaban Robert na nakumbuka akiwa kidato cha sita niliwahi kumpa Shikamoo kwa sababu enzi hizo fashion zilikuwa ni Bugaluu, na Tinaboo zilikuwa ni kwa ajili ya Wazee na walimu, baada ya kuona amevaa hivyo nikajua ni mwalimu. Pia alikuwa mtunzi mzuri wa michezo ya kuigiza kama vile Mafupa - The revenge of the skeleton. lakini hii ni longi ago.
   
 20. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2009
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 466
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 18
  Mzumbe sekondari ilikuwa poa sana. Mimi nilikuwa hapo 1990-92, Mkwawa.
  Listi ni ndefu sana ya walipitia hapo miaka hiyo..hii ni kabla haijawa special school!!
   

Share This Page