Mjengwablog Na Hoja Ya Kugomea Habari Za Kipolisi...

mjengwa ndo mdudu gani jamani? au ndo yule mtu wanamwita mwanakijiji? ye ni nani,

ni mwandishi wa habari na makala ktk gazeti la raiamwema ambaye mwaka2010 alinunuliwa na ccm kumpigia debe jk na sasa amenunuliwa na jeshi la polis kulipigia debe ktk kampen ya jeshi hilo ya kuua wandishi wa habari na raia wasio na hatia
 
tatizo wa tz tunakurupuka,
nani anaweza kutuambia faida ambayo raia wa kawaida ataipata kutokana na huo mgomo?
Kuigomea polisi ni kuadhibu raia na sio polisi.
Kwahili waandishi wamekurupuka na huo mgomo wao utayeyuka wenyewe kwani hauna faida na mwisho wa siku kila mtu analinda ajira yake, atafanya kile muajiri atakacho muagiza.
Tuache kudanganyana na kushawishiana ktk mambo yasiyo na tija.

wanahitaji taarifa sahihi na si upotoshaji wa mambo kwa mfano polisi wanatoa matamko kuwa daudi alifungwa bom na wafuasi wa cdm ili akalipue polisi, mara cdm ndo walilusha bom lililomwua daud. Upotoshaji ni mkubwa toka jeshi la polisi pia polisi wamekuwa wakilazimisha waandishi kuandika habari nzuri zinazowahusu na kuwatisha zinapoandikwa habari mbaya
 
Mjengwa unaonyesha wazi mahaba yako na magamba! lakini bora umeonyesha kuwa wewe ni mwandishi kanjanja hadharani!
 
Weka ukada pembeni onesha umoja na wanahabari wenzako wa Iringa. Umoja kwanza ukada baadae
 
Tujadili hoja, tusijadili watu. Akili ndogo ndio zenye kujadili watu.
Mkuu, kumuelewa mtu inasadia sana kujadili hoja yake, mfano kama nisingeelewa kuwa yeye anaandika habari lakini si mwandishi wa habari imetosha kwangu kutomjadili kabisa, maana imetosha.
 
Hii itakuwa VIGUMU I mean haitawezekana WAANDISHI WETU ni CCM in LOVE; Yaani kweli UTAMWAMBIA MICHUZI na

NDUGU ZAKE WAIGOMEE KUANDIKA HABARI ZA POLISI WA SERIKALI YA KIKWETE? Na Unajua Vitrip anapata Vya

kutosha Nje ya Nchi? Kweli Utasema MENGI na TV na RADIO yake Isiandike ya POLISI WA KIKWETE wakati anaalikwa PARTY

ZOTE KUBWA IKULU Wengine Wamepata VIBALI VYA TV na RADIO kwa MSAADA na NGUVU ZA CCM

CLOUDS, CHANNEL 10, Diallo TV... Hii ya kugomea haita shinda - LABDA uwe na Mamilioni ya Dola za kuwalipa hawa

waandishi... CCM Inazo...

Noted with thanks!
 
sionagi habari yoyote ya maana inayotokea polisi kwa hiyo hata wasiporeport habari zao itakua afadhali zaidi
 
Huyo Mjengwa hana hata cheti cha uchochoroni cha uandishi. Ameingia kwenye hiyo fani kwasababu anajua kupiga picha na hakuna kingine. Hastahili hata kujadiliwa kilaza.

PIA NAOMBA TUWEKE LIST YA HAO WASALITI KWA MATUMIZI YA BAADA YA UKOMBOZI WA TAIFA :-
1. maggid
2. michuzi.
3
4.
5.
6.
........................1000
 
Ndugu zangu,

Kufuatia mauaji ya kutisha na ya kusikitisha ya mwandishi Daudi Mwangosi ambapo askari wa Jeshi la polisi wanatuhumiwa kuhusika, kumekuwa na mitazamo na mikakati tofauti miongoni mwa wanahabari ikiwamo kugomea kuripoti habari zinazotoka kwenye jeshi la polisi.

Mjengwablog, kama chombo cha habari na mawasiliano ya kijamii, ina mtazamo wa kuendelea kuripoti habari za kipolisi, za kutoka ndani na nje ya jeshi hilo ikiwamo taarifa za kichambuzi.

Tunafanya hivyo tukiamini, kuwa habari za kipolisi kwa kiasi kikubwa ni habari zenye kuihusu jamii.

Maggid Mjengwa.

My Take: Naona usaliti umeanza rasmi.
 
ma mods inabid waweke na sehemu ya ku dislike... maana msimamo wa vibaraka kama hawa unaboa aiseee
 
Ndugu zangu wana jamii, kwanza heshima mbele,
Kuna hii habari ambayo nimeikuta kwenye blog ya mjengwa. Mi nafikiri kama anaamua kuwasaliti wenzake kwa ujinga wake mwenhyewe, na yeye asusiwe na blog yake aisome mwenyewe. Leo Mwangosi, kesho atauliwa yeye

Kufuatia mauaji ya kutisha na ya kusikitisha ya mwandishi Daudi Mwangosi ambapo askari wa Jeshi la polisi wanatuhumiwa kuhusika, kumekuwa na mitazamo na mikakati tofauti miongoni mwa wanahabari ikiwamo kugomea kuripoti habari zinazotoka kwenye jeshi la polisi.

Mjengwablog, kama chombo cha habari na mawasiliano ya kijamii, ina mtazamo wa kuendelea kuripoti habari za kipolisi, za kutoka ndani na nje ya jeshi hilo ikiwamo taarifa za kichambuzi.

Tunafanya hivyo tukiamini, kuwa habari za kipolisi kwa kiasi kikubwa ni habari zenye kuihusu jamii.

Maggid Mjengwa,
Mwenyekiti Mtendaji,
Mjengwablog.
Iringa
0788 111 765
 
wanahitaji taarifa sahihi na si upotoshaji wa mambo kwa mfano polisi wanatoa matamko kuwa daudi alifungwa bom na wafuasi wa cdm ili akalipue polisi, mara cdm ndo walilusha bom lililomwua daud. Upotoshaji ni mkubwa toka jeshi la polisi pia polisi wamekuwa wakilazimisha waandishi kuandika habari nzuri zinazowahusu na kuwatisha zinapoandikwa habari mbaya

ndiomaana wanatakiwa wasisuse ili wafichue uovu unaofanya na jeshi la polisi.
Waandike kila baya lao hata watakapo tishiwa wandike wametishiwa ili hao wanaotoa vitisho wajulikane na wachukuliwe hatua stahili. Media ni sehemu nzuri sana ya kufichua uovu wowote ule, mafisadi wengi wameumbuliwa na media na hata ambao hawajashtakiwa bado lakin jamii imewajua kuwa ni mafisadi. Mf Mzee wa vijisenti
 
Kama maggid Mjengwa angetoa taarifa ya kuungana na wanahabri wenzake kususia shughuli za jeshi la polisi ndiyo ingekuwa habari kwangu. Lakini hili la kuendelea kuwapa coverage si habari, na kama ni habari si habari mpya ama yenye mashiko, kwani anafahamika wazi kwamba yeye ni muumini wa chama twawala na madudu ya serikali yake.

Bila shaka anadhani huu ndio wakati muafaka wa kupata upenyo wa kujitanua kwa wasomaji wengi wa mitandao ya kijamii na wakuu wa serikali, ccm na jeshi la polisi lenyewe wakati huu ambapo waandishi wa habari wengine wamesusa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom