Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,315
- 33,111
Hivi gazeti lake alilolianzisha limeishia wapi, lilikuwa linaitwa something ..Jamii>
Hakuna ubaya kutoa analysis kama hii. Tatizo ni pale inapokosa basis, analysis imekaa kitabiri wakati tunajua mtabiri tunaye mmoja tu nchi hii. Angetuambia amewahoji watu kadhaa sehemu kadhaa au angetumia matokeo fulani, lakini sasa unalala leo unapata hisia kwamba CUF itakuwa ya kwanza, kesho unapata hisia zingine kwamba CHADEMA itakuwa ya nne, then unaandika makala, ebo!! Mbona wanaoota wapo wengi tu, lakini hawawezi kuandika kwa sababu ndoto haziwezi kuwa basis ya makala!!
Unaota!!! Vijijini watu wamebadilika sana juzi nilikuwa naongea na rafiki yaku kutoka kyela anasema kabisa wanavijiji wanamwambia Mwakyembe ubunge tunakupa lakini swala la Urais kikwete si chaguo letu safari hii. Geita vijijini wananchi wanasema kabisa safari hii ni Dr. Slaa. Musoma vijijini walimu wanasema waziwazi kuwa tunampa Dr. Slaa. Sasa wewe unatoa tu maelezo bila data.
MAGGID ni kimada wa CCM.
Maggid mark my words, matokeo ya ucahaguzi huu yatakushangaza sana kama tathmini yako ndiyo hiyo!!!!!!!! Kwa uhuru huo huo unaouzungumzia, this is my prediction
Wa kwanza Dr. Slaa, wa pili JK na wa tatu Lipumba.......... haha ahaha ahahah
Kijana yuko kazini!
Magid Mjengwa,
Pole kaka na kazi.
Makala yako ni nzuri kutegemea ni nani anasoma, wala huna sababu ya kusema utaudhi wengi, hii ni jamiiforums.
Mimi nashindwa kukuelewa baada ya kusoma na kuona ni makala zile zile za siku zote. Nilitegemea wewe kama mwandishi wa habari kama sijakosea, ungekuja na tathimini yakinifu ya uchaguzi wa 2010 badala ya kutumia takwimu za zamani ambazo zinaweza zisifanyekazi mwaka huu. Dr Slaa alishinda ubunge Karatu 1995 bila ya kuwa na madiwani kama sio mmoja vilevile Dr walid amani kaburu, Lyatonga mrema Temeke, Makongoro nyerere Arusha nk.
Nilitegemea kwa kuwa wewe unabahati ya kukutana na wapiga kura katika pita pita zako ungeleta takwimu hata kama sio rasmi. Mfano ungewauliza wapiga kura kila unapopita usingekosa kumi au ishirini kwa jimbo moja na kuweka viswali virahisi angalau mmbunge na raisi ukaweka vyama, ungeweza kuja na picha ambayo tusingeweza kuweka walakini na kazi yako ya uandishi.
Nikijaribu kufuatilia makala zako, naona kama vile unaogopa kitu fulani kwahiyo huna jinsi ila kuna wakati unakuwa wewe kuna wakati inabidi uridhishe upande. Inaniwia vigumu kama Synavote wameminya matokeo ya utafiti ulioonyesha Dr.Slaa anashinda. Vilevile matokeao ya maoni kwenye majimbo mbali mbali yanaonyesha jinsi wapinzani wanavyokubalika sio Chadema pekee kuna baadhi Chadema, CUF. Kizazi hiki tunatakiwa kuwa tofauti kidogo badala ya kuandika ukiwa chumbani twendeni kwenye maeneo ya tukio na tuandike habari inayotokea.
Sina chanzo za habari zako, ila nanona umetumia uchaguzi wa mwaka 2005. Mapinduzi ya demokrasia duniani huwa yanashangaza wengi, watawala wengi wanashtukizwa ndio maana wengi wanaishia kuleta vita, kama Mugabe, nk. Wamarekani waliamini Obama hawezi kuwa Raisi kwani ni mweusi na kazaliwa na baba mwafrika. Walishangaa sana walipomkuta Ikulu, mpaka hivi leo wapo amabao hawaamini.
Sikulazimishi uandike habari ambayo unaona si ya kweli, lakini habari yako haina mshiko wowote. Tukiangalia mwamko wa wananchi mwaka huu tunaona uko juu, elimu ya uraia na uchaguzi na watu kujua haki zao imepanda, watu wa kada mbali mbali wameanza kuamini kuwa wapinzani nao wanaweza kuleta mabadiliko. Majimbo mengi wamesimama wagombea ambao wanaeleweka na wananchi tofauti na miaka mingi, wachangiaji wamaeongezeka wanakisaidia chama hii ikiwa ishara ya kukubalika.
Ni wabunge wangapi Chadema inaweza kupata, Tendwa alisema 80-100, wewe mjengwa unasema wachache kuliko wa CUF, Chadema wanasema zaidi ya 100. Na sisi tunasema tutawapata wengi kwani mori upo juu. Sisi tuliopo kwenye uhamasishaji kuanzia ngazi za matawi tunapata matumaini makubwa, tunaona tofauti yawananchi wa leo na 1995.
Ndugu Mjengwa Duniani hakuna kampuni ya poll ya chumbani, zote zinakwenda kufanya kazi na kuuliza wapiga kura waliojindikisha, na sayansi hiyo inafanya kampuni hizo zisitofautiane kwenye majibu yao kwa asilimia nyingi. Mara nyingi wanasema ukweli kutokana na hali halisi. Sasa wewe kuja na takwimu za chumbani sio za kisayansi kwenye dunia ya leo ukiwa mwandishi unakuwa umeshindwa kazi yako. Takwimu za ukweli hakuna wa kuziogopa wala kuchukia labda mwehu kama wananchi watasema tunamchagua Mjengwa huwezi kataa. Ila kutumia kalamu kuwa mtabiri kama shekhe Yahaya ni usaliti wa elimu ya uandishi wa habari. Kazi kubwa ya waandishi ni kuelimisha umma kwa kutumia vyanzo vya ukweli na habri zilizotafitiwa.
Unapima mwendo wa uchaguzi kwa kuuliza wapiga kura kwa wakati huo. Siasa za Tanzania zinabadilishwa na nani anagombea wakati huo, bado hatuna siasa za kichama sana, watu wanaswing na mgombea na rushwa wakati mwingine inahamisha wapiga kura. Sasa badala ya kutuletea matokeo ya maruhani anza kujadili jimbo kwa jimbo au mgombea kwa mgombea.[/QUOTE]
Hapo Kwenye red, umemwambia ukweli. How much money amepokea mpaka awe blind kiasi hiki? Sijui kama nitasoma tena makala zake kwenye gazeti nilipendalo la Raia Mwema.
Yafaa watu wajue kwamba pesa si kila kitu duniani, lazima uheshimu utu wako!
Mjengwa? NO!!!!!!
Mjengwa bwana anajulikana huyu katika mambo makuu mawili (kwa mtazamo wangu); ukichunguza sana kwa makini machapisho yake, ninashawishika kuamini ama ni kada wa kile chama kikongwe (japo hataki kuweka bayana); ama pia ni mfurukutwa wa zile siasa zinazoleta shida kati ya watu (za kiimani). Anyway, huu ni mtazamo wangu lakini nina uhakika siku moja nitakuja kuwa proved right. Ni sawa na usanii niliuona 2005 na kutokutoa kura yangu kwa "tumaini jipya". Madudu yalivyoanza moyoni nilipata amani maana nilijua kuwa nilikuwa sahihi kwa wakti ule (japo kwa hisia tu). Kuhusu Mjengwa.... tusubiri tuone... ndio wakuu wa wilaya wateule hawa wanaokuja...time will tell
Lengo ni kututayarisha kisaikolojia kwa mchezo mchafu wenye baraka za dola na hivyo kupunguza hasira za wananchi dhidi ya kitendo kama hicho. Mfano moja mzuri ni kufichwa kwa matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na Synovate yaliyompa Dr. Slaa ushindi. Hatudanganyiki !