Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?

Ndege ya Uchumi:

Kwani nani amekwambia kuwa kumiliki gazeti ina maana kila habari iliyoandikwa kwenye gazeti husika imeandikwa na mmiliki wa gazeti? Uhuru linamilikiwa na CCM, ina maana kila habari katika uhuru imeandikwa na Mwenyekiti wa Chama hicho? Na Freeman Mbowe anamiliki gazeti la Tanzania Daima. Ina maana Freeman Mbowe ndiye anayeandika habari kwenye gazeti hilo? Gazeti lilikuwa na mhariri na habari hiyo haikuandikwa na mimi. Kama mtu ni mjinga, lakini hajui kama ni mjinga, unafanyaje?


Mkuu kwa Tanzania wamiliki wa Magazeti wana Influence kubwa katika habari zinazoandikwa na Magazeti, na Wahariri wowote Makini wanapogundua kama gazeti lake limeandika habari ya Uongo kwa bahati Mbaya huwa linatoka na Kuomba Radhi kwa Uzito ule ule lilivyoripoti habari ya Uongo, tumeshuhudia magazeti makini yakifanya hivyo. Sasa wewe ukiwa mmiliki wa Gazet baada ya kugundua kwamba hazeti lako lilimchafua Dr. Slaa Uliomba Radhi? Kama Hukuomba maana yake Aidha wewe ndiye uliyetunga ile habari au Ulifurahia huo uongo

Kimsingi hii habari nimeiweka hapa ili ku question credibility yako
 
Mkuu kwa Tanzania wamiliki wa Magazeti wana Influence kubwa katika habari zinazoandikwa na Magazeti, na Wahariri wowote Makini wanapogundua kama gazeti lake limeandika habari ya Uongo kwa bahati Mbaya huwa linatoka na Kuomba Radhi kwa Uzito ule ule lilivyoripoti habari ya Uongo, tumeshuhudia magazeti makini yakifanya hivyo. Sasa wewe ukiwa mmiliki wa Gazet baada ya kugundua kwamba hazeti lako lilimchafua Dr. Slaa Uliomba Radhi? Kama Hukuomba maana yake Aidha wewe ndiye uliyetunga ile habari au Ulifurahia huo uongo

Kimsingi hii habari nimeiweka hapa ili ku question credibility yako

Ndege Uchumi,

Ni nani aliyesema kuwa habari husika ilikuwa ni ya uongo?
 
Mkuu Maggid

Ndege Uchumi,

Ni nani aliyesema kuwa habari husika ilikuwa ni ya uongo?

Kanusha hili

Habari ya gazeti la kwanza jamii yaweza kwa njia moja ama nyingine kupotosha kwa kuonesha kuwa Dkt. Slaa aliruhusu Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kutoa posho kwa wajumbe wa kamati yake na hivyo kupata posho mara mbili.

Napenda kueleza kuwa mwaka 2007, Kamati ya LAAC ilikuwa chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Mgana Msindai. Kamati hizi za 'oversight' - ile ya LAAC na ile ya POAC zimeanza kuongozwa na wabunge wa upinzani kuanzia mwezi machi mwaka 2008. Kama kamati hii ililamba posho kutoka Halmashauri masikini kama ya Sumbawanga, jamii ijue kuwa haikuwa kamati ya Dkt. Slaa, ilikuwa kamati ya Msindai na dkt. Slaa hakuwa sio tu mwenyekiti, wala hakuwa mjumbe.

Hivyo, habari hii ya kwanza Jamii inaposomwa izingatie ufafanuzi huu.
 
Mkuu Maggid



Kanusha hili

Sasa chanzo cha habari hiyo ni kipi? Ni KWANZA JAMII au ripoti ya CAG? Kama ni Ripoti ya CAG, aliyepotosha ni mwandishi wa habari hiyo au CAG? Vinginevyo kama CAG hawakueleza kitu kama hicho katika ripoti yao. Tuwakane sawa hapa, maana kilichoripotiwa na KWANZA JAMII hakikupata kulalamikiwa na CAG iliyotoa ripoti hiyo, kwamba wamenukuliwa kwa makosa. To the best of my knowledge.
 
Sasa chanzo cha habari hiyo ni kipi? Ni KWANZA JAMII au ripoti ya CAG? Kama ni Ripoti ya CAG, aliyepotosha ni mwandishi wa habari hiyo au CAG? Vinginevyo kama CAG hawakueleza kitu kama hicho katika ripoti yao. Tuwakane sawa hapa, maana kilichoripotiwa na KWANZA JAMII hakikupata kulalamikiwa na CAG iliyotoa ripoti hiyo, kwamba wamenukuliwa kwa makosa. To the best of my knowledge.

Ha ha ha Maggid bana, naona unaruka ruka, Report ya CAG hamna sehemu imetaja jina la Slaa kulamba Posho Mbili
 
Kwanza Jamii la Maggid Linasema hivi

Maelezo yaliyotolewa kwa CAG kuhusu malipo hayo yanasema; "Posho kwa ajili ya vikao vya kamati ya Bunge ya hesabu za serikali za mitaa Agosti 7 hadi 16 mwaka 2007 yalikuwa Sh 1,050,000.

Kutokana na kubainika kwa hali hiyo huenda hadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Dk. Wilbroad Slaa, Mbunge wa Karatu, ikaingia doa mbele ya umma wa Watanzania.
Zitto anasema hivi

Napenda kueleza kuwa mwaka 2007, Kamati ya LAAC ilikuwa chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Mgana Msindai. Kamati hizi za 'oversight' - ile ya LAAC na ile ya POAC zimeanza kuongozwa na wabunge wa upinzani kuanzia mwezi machi mwaka 2008. Kama kamati hii ililamba posho kutoka Halmashauri masikini kama ya Sumbawanga, jamii ijue kuwa haikuwa kamati ya Dkt. Slaa, ilikuwa kamati ya Msindai na dkt. Slaa hakuwa sio tu mwenyekiti, wala hakuwa mjumbe.
Nani alikuwa Kiongozi wa LAAC na POAC 2007?
 
Mkuu Pasco Pole sana maana naona na wewe umeingia kichwa kichwa katika kumtetea na Kumpongeza Mjengwa kwa hiyo makala yake. Waandishi kama Mjengwa wanafaa kukemewa na si kupongezwa hata kidogo

Mkuu Ndege ya Uchumi, sijaingia kichwa kichwa kwa sababu namfahamu Mjengwa, huyu jamaa ni mjamaa kwa ile sense ya Nyerere, nimekuwa naye Sweden akiwa na chanel nzuri tuu ya life, ghafla akayaacha yote na kurejea nyumbani nikitegemea angebaki Dar kwenye ma deal kibao, jamaa akaniambia anaenda kijijini huko Iringa. Ni anglab sana mtu wa maisha ya ulaya kurejea nyumbani na kwenda kuishi kijijini maisha ya kijijini.

Naomba pia utofautishe ninatetea nini kwenye makala ya Mjengwa, sitetei context, yaani kilichoandikwa mle, natetea his fundamental right ya expression, hii ni moja kati ya haki kuu zilizoainishwa kwenye lile tamko la haki za binaadam, Universal Declaration of Human Rights, na haki hizi zikikiukwa, ndio pale unasikia hata rais wa nchi huru anatolewa hati ya korokoroni kusubiri kupandishwa kizimba cha mahakama ya dunia.

Mimi, wewe, yeye, yule na sote tuna uhuru wa kutoa maoni ambao hauwezi kuingiliwa na mamlaka yoyote. Mipaka ya uhuru huo wa maoni ni kutoingilia uhuru wa mtu mwingine, kwa mfano naweza kutoa maoni kuwa kwa maoni yangu, namuona jeikei (not a real person) ana I.Q ndogo kuliko ya Dr. Slaa kutokana na uwezo wake wa kufikiri, maneno mbofu mbofu na matendo machafu machafu. Haya ni maoni yangu tuu, lakini kama yameelekezwa kwa realy living person, maoni hayo yanakuwa yameingilia uhuru wa jeikei. Nikiyatoa maoni kama hayo in public, ni jeikei tuu mwenyewe kama ataona nimeingilia uhuru wake, atakuwa na uhuru wa kunishitaki mbele ya vyombo vya sheria kwa kumvunjia heshima.

Hakuna ubishi kuhusu Dr. Slaa ndio tumaini jipya la Watanzania na no matter tunampanda kiasi gani na tunamuombea kwa nguvu zetu zote achukue nchi siku 27 zijazo, lakini hii hainyimi uhuru mtu yoyote mwenye maoni kuwa siku hivyo ikifika, sio tuu kwamba hatachukua nchi, bali atakuwa ni wa tatu!.

Katika mjadala wenye afya, watu hawamchambui mleta hoja, bali wanaichambua hija husika na kuipangua, nikimaanisha heshima ya mleta hoja inabaki pale pale hata awe ameleta hoja ya utumbo vipi.
 
Mkuu ama hujamsoma Maggid kwani kisha kuwa na gazeti, blog na huandika makala nyingi tu pengine wewe ndio hujamsoma. Kisha unapokuwa na blog yako tayari inakuweka ktk nafasi ya wanahabari kwani kama kuna mashtaka yeyote yale dhidi ya chombo au bandiko ktk blog yako unakuwa responsible.. Hii ni sawa na kazi ya mtu hivyo wasivamie vitu tu ili mradi wana own blog kwani nayo pia ina majukumu yake..Mtandao ndio gazeti la karne hii mkuu wangu...
Mkuu Mkandara, kama tafsiri yako ya mwandishi wa habari inajumuisha social media, then nakubaliana na wewe kwa hilo, sasa every Tom, Dick and Harry ni wanahabari, then every body is na Mjengwa ndani.
 
Pasco,
Pamoja na kuwa unamfahamu huyu bwana mdogo, Mimi pia namfahamu toka Tosa lakini naona hapa alichemsha big time!
 
Pasco,
Una maana ya kuniambia kuwa wote wale walioikataa CCM Tarime ni wasomi wa mitandao? Tuna tendency ya ku-underestimate understanding ya
watu wa vijijini kana kwamba wao hawana macho ya kuona. Nilikuwa Mugumu mwaka juzi na kitu nilichogundua ni kwamba raia wa kawaida wanatambua kuwa viongozi wa CCM ni matajiri, wengi wao wakiwa na biashara za mahoteli, malori, vituo vya petroli, na magendo ya kupeleka madawa ya kulevya Kenya. Hawa ni raia wa kawaida tu wasiotoa maoni yao kwenye mtandao. Tusiwa under estimate, for lack of a better Swahili phrase.
Jasusi, nakubaliana na wewe, awareness level ya Watanzania inapanda siku hadi siku, ila Tarime ni issue nyingine, watu wa kule wana msimamo usioyumbishwa kwa fulana, kofia na shibe ya siku moja. Nilishuhudia gharama za umasikini uliotopea kwenye uchaguzi mdogo wa Busanda na Biharamulo, nusu kilo tuu ya sukari na Shilingi elfu 1,000 ya kitafunio kwa kila kaya siku ya kuamkia kupiga kura, iliweza kubadili matokeo. Several 40 ft containers za campain materials za CCM zinasubiri port clearance (kama kawaida ili kupata msamaha wa ushuru), this time sio tena fulana tuu na kofia, bali kanga, raba mpaka opener watakazo sambaza baa zote, ukifungua tuu kinywaji, zinapiga kawimbo ka CCM.

Mikoa yenye neema kiuchumi, wanaweza kufanya kweli, ila kule umasikini uliotopea, aliyetoa shibe ya mwisho, ndiye atakayelamba kura!
 
Pasco,
Pamoja na kuwa unamfahamu huyu bwana mdogo, Mimi pia namfahamu toka Tosa lakini naona hapa alichemsha big time!
chibhitoke, kama nikweli umemfahamu toka Tosa, jee sasa amebadilika mpaka kuchemsha big time?. isije ikawa ni emotions zako kwa Dr. Slaa?.
Wapenda mageuzi wote wanataka Dr. Slaa ashinde, ila tusihamanike na ushindi tuu, werevu wote huwa they hope for the best and prepare for the worst, mtu anayekupa matayarisho ya kujiandaa kwa habari mbaya ndio unamuita amechemsha big time?.
 
Nimekupota Mjomba kwahiyo unataka kuniambia hao redet nao kura zao za maonI wanazifanyia wapi? au nao wanatumia hii system ya online polls? na kama sio hivyo na kama hawatadanganya matokea mambo yatakuwa ni yaleyale I MEAN DR SRAHA
Redet wametuma watu vijijini, mahali kusiko na umeme wala mtandao, huko redio inayowafikia ni RTD tuu, yaani TBC Taifa. Subiri matokeo yao watayatangaza hivi karibuni. Ila kama hawatayatangaza, basi nitajiandaa kusheherekea ushindi maana nao watayaminya kama yale ya Synovate na hili litakuwa ndile anguko kuu la CCM!, na Mjengwa atatoa makala kurekebisha kwanini alikosea.
 
kwa hiyo wewe, mjengwa na redet ndio msimamo wenu/opinion yenu? kama ni hivyo kwanini ccm watumie nguvu namna hiyo, mpaka wawatumie watu wenye shida binfsi ku-drive the point, nimeona husna akitumika, kitanda cha teremka tukaze, mwalimu wa zamani, tendwa kuachimpeni kuendelea baada ya saa 12 jioni, mabasi kukodishwa kupeleka watu wahudhurie fiesta, vyombo vya serikali kutumika kwenye propaganda au kuwa biased? vyombo vya serikali iwe jeshi nk ? je hivi vitu vyote vinaelekeza picha hii? je walio mfukuza uday iringa ni mtandao/internet, zomea zomea bukombe napo ni internet? kumtumia mshauri wa uganga mnajimu sheikh yahya? nk nafikiri hapa uhitaji nuklia formula ili uapate jibu?
halafu na wewe mwanzo umeaqinisha vizuri mwandishi na mtoa makala, lakini hitimisho lako ni la mtoa makala?
.
August, nilisema kule nyuma na sasa narudia tena, mwandishi wa habari, akiandika habari, haruhusiwi kuweka opinion yake, mtu ambaye sio mwandishi wa habari, haruhusiwi kuandika habari for public consuption kama ilivyo mtu ambaye sio daktari haruhusiwi kutibu public.

Kwenye vyombo vya habari kuna habari na makala, kwenye habari, opinion hairuhusiwi, kwenye makala, opinion inaruhusiwa.

Kwenye social media, blogs, online forums, fb etc, kila mtu anaruhusiwa kuandika chochote na kupost chochote awe ni mwandishi au si na anaweza kuweka opinion yake atakavyo.

Hitimisho langu sio kuunga mkono alichoandika Mjengwa, bali ni kutetea uhuru wake wa kutoa maoni yake freely kama mtu mwingine yoyote.
 
Kwanza Jamii la Maggid Linasema hivi

Zitto anasema hivi

Nani alikuwa Kiongozi wa LAAC na POAC 2007?

Ndege ya uchumi

Sasa kinachoonekana hapo ripoti ya CAG ilizungumzia hicho, lakini mwandishi amemtaja mwenyekiti wa kamati kama Slaa badala ya Msindai kwa vile inahusu 2007 na 2008. Basi, mwandishi wa habari hiyo alikosea katika kipengele hicho. Na mimi sikuwa mwandishi wa habari hiyo katika KWANZA JAMII na leo siwezi kumhukumu kama alikuwa na dhamira mbaya. Yawezekana ni kosa la kibinamu.
Nikushukuru kwa mazungumzo haya.
 
tatizo lako wewe vs mjengwa mtoa makala ni lileli , yaani hitimisho hata hapa nilipo ku-quote nikiangalia hitimisho unamuelewa huyu mtu yupo poje objective au sio objective? sasa kama ungependa kujitofautisha na sisi tusio wajuvi wa uwandishi wa habari rekebisha hitimisho zako toa habari tu? mfano slaa alikuwa njombe jana/leo kasema dash dash na watu walizome/walishangilia basi sio kuweka hitimisho.
maanake wewe umekuwa prosecutor jaji na mtuhumiwa vyote at ze same time
August, hapa ni online, hii ni social media, hivyo opinion ni ruksa.
 
Pasco,
Pamoja na kuwa unamfahamu huyu bwana mdogo, Mimi pia namfahamu toka Tosa lakini naona hapa alichemsha big time!

Chibhitoke,

Hunifahamu, maana sijawahi kusoma wala kuishi Tosa. Au labda kama umekunywa kidogo!
 
Kumbe wewe na Mjengwa lenu moja!Haya,umejuaje matokeo ya utafiti wa REDET kabla wenyewe hawajayaweka hadharani?Na umejuaje kuwa matokeo haya yatatushangaza?Jibu jepesi ni kwamba wewe na Mjengwa mmegeuka kuwa wasaidizi wa Sheikh Yahya,yani mmejipachika unajimu.
Mlalahoi, mimi ni mimi na Mjengwa ni Mjengwa, the only thing wen have in common wote ni wapiganaji ila kila mtu kwenye anga zake. Mimi ni mpigania haki na demokrasia ya kweli nikisupport mageuzi kwa asilimia 100%, yeye siwezi kumsemea.
Huhitaji kuwa Sheikh Yahya kuyajua matokeo ya utafiti wa Redet, trend inatosha kupredict outcome. Uliyoyasema kuhusu Redet ni kweli na hayo ndio matokeo, ila tusiandikie mate, wino upo, opinion poll ya Mjengwa imetoka kaiandika tumeijadili, tuisubiri na hiyo ya Redet ndipo yuyadajili.
 
Mwalimu Nyerere, Ndugu Benjamin Mkapa, na Dr Peter Onu katika Mkutano wa 17 wa OAU (sasa AU) Addis Ababa, Ethiopia

CDmD3IfWAAAYuMa.jpg
 
Back
Top Bottom