Mjengwa atangaza rasmi gazeti jipya

magoma

New Member
Mar 2, 2009
4
0
( ni kupitia mjengwablog

Pichani ni jina la gazeti jipya la ' Kwanza Jamii' linalotarajiwa kuonekana nchini kote kuanzia Machi 31, 2009. Ni jarida la uchambuzi wa masuala yanayohusu na kuigusa jamii. Haya ni pamoja na siasa, uchumi, elimu, michezo na utamaduni. Kuna masuala mtambuka pia kama vile mazingira,jinsia na UKIMWI/VVU.
Jarida hilo litakuwa likitoka kila Jumanne ya wiki.

Katika muda si mrefu kutoka sasa nitawaletea, kupitia blogu hii, majina ya baadhi ya wachambuzi watakaoandikia gazeti hilo. Kwa sasa naandaa bango la ' Kwanza Jamii' nitakalolitundika hapo juu.

/Maggid

Ikwiriri, Rufiji, Pwani.
Jumapili, Machi 15, 2009.
 
Safi sana Maggid. Kila la heri na natumai utafanikiwa, ili mradi ukae mbali na genge la mafisadi.
 
Mi nina swali tu la kizusshi, ni nini atakuwa anaandika tofauti na magazeti mengine yaliyopo kwa sasa?
 
Kaka Hongera sana, tupo pamoja nawe

Tupo pamoja nae kivipi?unalazimika kueleza uma .tusiwe tunarukia tu na kusema tupo pamoja nawe wakati hatujaona msimamo wake unaeleke wapi na kina nani wapo nyuma yake tumeshaona matokeo mengi kama haya hatma yake tunakuja lalamika
 
Hala hala mti na macho,
Tafadhali waandishi msije mkaanza mambo yenu yaleeeeeee ya mwaka 2005
 
Naomba pia wasiogope kuandika ufisadi wakina RA na EL kwani wakiwaogopa basi hamtakuwa wapiganaji kwa maslahi ya Taifa na Watanzania kwa ujumla.
 
Last edited:
Huyu anaganga njaa tu. Ninafahamu ana uswahiba na baadhi ya vibosile wa serikali walio na utata.

Tutakusoma hata hivyo.
 
Jihadhari sana -- utahakikisha vipi wahariri wakao hawatanaswa na mahela ya wizi ya RA?
 
Mjengwa, inaonekana umejikitita vizuri kwenye fani ya Jamii, hasa kwenye mlengo wa kuimarisha vyuo vyetu vya maendeleo ya wananchi vijulikanavyo kwa kimombo "Folk Develpment Colleges - FDCs." Nadhani pia huko ndipo ilipo ajira yako kwa miaka kadhaa sasa. Kwa kuwa jarida lako ni "Kwanza Jamii", napata mwelekeo wa mawazo kuwa unataka kuwa sauti ya FDCs ambazo kwa kweli jamii haiambiwi sasa juu ya vyuo hivi, japo vimekuwepo nchini kwa muda mrefu. Tunatarajia utatupasha habari zitakazoifanya jamii itupilie macho FDCs pia. Ikiwa ni hivyo, tunatarajia mengi, makubwa na yenye kujenga kwani tumekushuhudia ukizunguka nchini kutembelea vyuo hivi. Tafadhali usianze kwa kutuboa. Weka mambo hadharani taifa lijue. Kama kuna ufisadi huko FDCs, pia tumwagie.
 
Yeah, namkumbuka Majjid yule wa Tambaza sekondari miaka ile.. alikuwa mwandishi mzuri wa michezo wakati akiwa bado mwanafunzi. Habari mojapo ninayoikumbuka hadi leo ni ile yenye kichwa cha habari "Tambaza out for half a basket". Pale Tambaza ilipotolewa kwa nusu kikapu Na Pugu sekondari... UMISETA miaka ya mwisho wa 80.

Sasa hivi nikiangalia majengo ya Tambaza Sekondari, mhn! hayatamaniki kabisa... Toka miaka ile hadi leo hakuna aliyepaka rangi majengo yale...(Mwanzoni ilijulikana kama HH Aghakan Sec. School) Nakumbuka geography room na vyumba vingine.. Wakati sekondari ilikuwa Sekondari kweli.

Nimesikia kuna harambee ya kuchangia shule ile ili ifanye ukarabati wa majengo yake... Wanafunzi miliosoma Tambaza kama kuna mwenye taarifa atupashe humu, ili tujumuike sote.

Majjid ukiwa ni zao la Tambaza tafadhali tuletee maendeleo ya harambee ile kama bado ipo...

Hongera kwa kijarida chako kipya kaka!!! Lakini ungeendelea na habari za michezo, nchi ingefika mbali sana.
 
Huyu anaganga njaa tu. Ninafahamu ana uswahiba na baadhi ya vibosile wa serikali walio na utata.

Tutakusoma hata hivyo.


Kama una ushahidi umwage hapa, we dare to talk openly! Otherwise usianze kumchafua kijana.
 
Tupo pamoja nae kivipi?unalazimika kueleza uma .tusiwe tunarukia tu na kusema tupo pamoja nawe wakati hatujaona msimamo wake unaeleke wapi na kina nani wapo nyuma yake tumeshaona matokeo mengi kama haya hatma yake tunakuja lalamika

Hii imekaa vizuri kabisa. Hapo tumepata jina tu, nakala hata moja mtaani bado, hatuwezi kujua sera na mwelekeo wa gazeti hilo mpaka tuone yaliyomo. Huu ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi 2010, tulishaumwa na nyoka, tunaogopa hata unyasi sasa tunauogopa!!! Hongera kwa lengo jema, weka sera wazi!!
 
Back
Top Bottom