Mjadala wa wa bajeti 2011/2012 - ITV

Paul S.S

JF-Expert Member
Aug 27, 2009
6,402
3,242
Wadau mjadala kuchambua bajeti unaendelea itv live msemaji mkuu akiwa James Mbatia, pia namuona pro Lipumba
 
Naona anasisitiza bajeti hii ku address zaidi matatizo yaliyoko vijijini ambako hali ni mbaya sana pamoja na Dar es salaam hasa kutafuta namna ya kuondoa foleni. Anaendelea.....
 
Msemaji mkuu ni Prof Lipumba, James mbatia anatoa ufunguzi inaeonyesha umeandaliwa na nccr mageuzi.
Mbatia nasema ni ajabu walipa kodi ni asilimia 20 hivyo wanalipa kuhudumia asilimia 80 wasiolipa kodi
 
Miondombinu ya reli na barabara kama Kigoma , Rukwa, Katavi ianagliwe kwa umakini. Anasema bado tupo kwenye hali ya kusua sua

Anawakaribisha wachangiaji sasa baada ya maneno ya ufunguzi, Wazo lako laweza kuwa bora kuuliko lingine lolote hivyo usiogope kutoa wazo lako
 
Bajeti ni kioo cha fedha za serikali ili kuona ni mambo gani serikali inataka kuyatekeleza. Bajeti ni muungoza wa kutekeleza sera zilizoibuliwa.
 
Malengo ya uchumi ni pamoja na kukuza pato la taifa. Kukua kwa pato la taifa kunaenda sambamba na ukuaji wa pato la mtu mmoja mmoja.
Bajeti isisababishe gharama za maisha kuongezeka, kwa hiyo lazima kuwa makini na hilo. Lazima uhakikishe unafedha za kigeni za kutosha ili kutoshusha thamini ya sarafu. Yote hayo yanaangaliwa wakati wa kuandaa bajeti.
 
Matumizi ya bajeti yaliza yawe na nidhamu hasa kwenye vipaumbele ulivyovipanga. Atafafanua katika hili. Lazima kuwa na nidhamu wakati wa utekelezaji na si vinginevyo
 
Tusiibue sera kwenye majukwaa ya kisiasa. Mfano unafika chalize unakuta watu wamesimama unasema sasa nitawajengea hiki na hiki kisha unapigiwa makofi na kuondoka, Jiulize fedha ya kufanya hivyo umeitoa wapi? Je jale yaliyopangwa kwenye bajeti yamefikiwa? Je fidha zilizo tengwa zimetumika?
 
Wanaotazama waendelee kumwaga vitu hapa jamvini ili kuwasaidia walio mbali na Tv zao nahata wale walio nje ya nchi.
Ninalazimika kuondoka kwasababu ya majukumu mengi
 
isee prof yupo njema kwenye hii nyanja, naona anaidadafua in deep
 
Serikali hukusanya kiasi kidogo kuliko matumizi ya kawaida, deficit ni zaidi ya shilingi trilioni 1...ni udhaifu wa kibajeti.
Bajeti ya serikali huwa haitabiriki....mfano 2010/11 kiasi cha fedha ya umeme kilichotumika ni 46% ya bajeti iliyotengwa.
Bajeti inayotangazwa siyo inayotolewa kwa ajili ya matumizi.

Vipaumbele vya serikali na matumizi yake ni tofauti kabisa. asilimia 53.6 ya matumizi ya bajeti 2010/11 ilitumika katika maeneo yasiyo ya kisekta.

Mkanganyiko wa kupanda kwa gharama za maisha na mahusiano yake na ongezeko la maisha na inflation rate haviendani na ni upotoshaji
Suala la kuangalia upya tozo za bei za mafuta lina mkanganyiko kwa sababu formula inayopangwa na EWURA iko juu kuliko bei inayotozwa na wafnyabiashara na gharama ya tozo zenye uwezekano wa kuondolewa ni sh.86 tu kwa lita. kuna uwezekano wa kuondoa hizo tozo na bei isipungue na wafanyabiashara wakafaidi.
Misamaha ya kodi ni mianya mikubwa ya kupunguza pato la taifa mfano misamaha ya kodi kwa viongozi wa nchi, kwenye madini.
Lazima kodi iongezwe kwenye dhahabu na siyo kwenye sigara.
tupitie matumizi ya serikali tuweze kujua namna gani fedha zinavyotumika.
 
Back
Top Bottom