Mjadala wa Umoja wa Upinzani StarTV Dec 5, 2010

Mtatiro anaumiza masikio. Anadhani kusikilizwa ni kufoka? Kafulila nae hajui kama ccm ni mabeberu #1? Bora chadema wamejifafanua kuwa wao ni chotara kuliko ccm inayosema kuwa wao ni mzungu kumbe tunamwona ni mbantu
 
Chadema itaweza tu! Hawawezi kuungana nusu serilali na nusu upinzani yan CUF. Haiwezekani! Star tv,acheni tupate utawala wa watz na si wakoloni weusi ccm!
 
...Nimeangalia kidogo. Huo mjadala hauna maana hata kidogo, ukilinganisha na issues za msingi zinazohitaji kujadiliwa kwa mustakabali wa taifa kwa sasa.

...Yanayosemwa ni yale yale yaliyokwishasemwa kwenye mahojiano na magazeti na kwenye tv nyingine. Kwani, ni lazima star tv i-copy yaliyofanywa na tv nyingine? What a waste of time.

...Nani hafahamu kwamba muungano wa vyama hauna tija, hautakuwapo na utaleta mtafaaruku kama utakuwapo. Its a non issue tayari!

...TV itakoyoleta/host mjadala wa katiba mpya ndio itakuwa imefanya jambo la maana na bora zaidi.
 
mi nafikiri vyama vya upinzani vipo kimaslahi zaidi,kwa mfano ndani tu ya chadema hakuna muungano ona mtu kama zitto madudu anayoyafanya ndani ya chama chake,angalia cuf hamad rashid anajua utamu wa kuwa kwenye uongozi wa kambi ya upinzani ndio maana analeta mashinikizo yasiyoeleweka,nccr ndo basi kabisi kiongozi wao wa chama tena kitaifa anaangushwa hata ubunge tu tena na wapinzani wenzake kwa hali kama hii hawawezi kuungana kila chama kina matatizo na majeraha yake.
 
Dhana nzima ya vyama vya upinzani kuungana HAINA MAANA!
Ni kweli lengo la wapinzani wote ni kushika hatamu kwa kukiondoa chama tawala katika dola, lakn si kweli kuwa shabaha ya wapinzani ni moja pale watakapofanikiwa kushika dola, kila chama kina ilani yake na mwelekeo unique, wazalendo wa kweli ni wale wanaoamua kuanzisha chama kipya cha siasa pale tu wanapoona vilivyopo haviendani na mtizamo wao, hivyo kuwaunganisha watu walio na mitizamo tofauti nijambo la hatari! Lengo lazima liwe pana na lenye ukombozi ndani yake, si kuking'oa chama tawala tu bila dira (uchu wa madaraka)-wananchi wataumia zaidi! Mimi naona heri kila chama kisimame kivyake, kwani kila chama kina wafuasi ambao watakosewa haki kama watauzwa kwa mtu wa chama tofauti (Mfano Zenji). Chama cha kwli kitajulikana tu, na kitasimama pekee hata kikipingwa na wengi!
 
Samahani natoka kidogo nje ya mada lakini nadhani ujumbe wangu utafika! Angalieni jamani kama kuna uwezekano wa StarTv au radio yenu iwe inapatikana kwenye mtandao! Tafadhali lifikishe hili kwa wahusika
 
tumeshasikia porojo na mawazo mgando yawote hao jaribuni kuwaleta wengine kabisa kama wenje mdee magdalena sakaya .

sijaona alie na la kumsaidia mtanzania wote ni kwa matumbo yao tu

kizaz cha mabadiliko kimeanza kujitokeza kitachipua vema 2015
 
Mtatiro anaumiza masikio. Anadhani kusikilizwa ni kufoka? Kafulila nae hajui kama ccm ni mabeberu #1? Bora chadema wamejifafanua kuwa wao ni chotara kuliko ccm inayosema kuwa wao ni mzungu kumbe tunamwona ni mbantu
TV yako haikuwa na kipunguzio?

Hapana najua MTATIRO KASEMA AMBACHO MASIKIO YA WENGI HAYAKUTAKA KUKISIKIA! Mtatiro anawatahadharisha watanzania kuwa wangali uchi wanastahili kuvaa; sasa kama mlitaka awaambie MMEVAA na HALI anawaona MLIVYO... Iko siku MTAINGIA SOKONI mmevaa WA-MNYAMA!:frown:

Mara zote ukweli unaumiza si MASIKIO tu bali hata MOYO! :angry:
 
...Nimeangalia kidogo. Huo mjadala hauna maana hata kidogo, ukilinganisha na issues za msingi zinazohitaji kujadiliwa kwa mustakabali wa taifa kwa sasa.

...Yanayosemwa ni yale yale yaliyokwishasemwa kwenye mahojiano na magazeti na kwenye tv nyingine. Kwani, ni lazima star tv i-copy yaliyofanywa na tv nyingine? What a waste of time.

...Nani hafahamu kwamba muungano wa vyama hauna tija, hautakuwapo na utaleta mtafaaruku kama utakuwapo. Its a non issue tayari!

...TV itakoyoleta/host mjadala wa katiba mpya ndio itakuwa imefanya jambo la maana na bora zaidi.
upo next week kasema Yahya M. hapohapo StarTV stay tuned! (tuna tatizo moja tukishasikia tusiyotaka basi tunaachana na TV!) twawezaje kujufunza kwa taarifa za upande tuupendao pekee? :embarrassed:
 
mi nafikiri vyama vya upinzani vipo kimaslahi zaidi,kwa mfano ndani tu ya chadema hakuna muungano ona mtu kama zitto madudu anayoyafanya ndani ya chama chake,angalia cuf hamad rashid anajua utamu wa kuwa kwenye uongozi wa kambi ya upinzani ndio maana analeta mashinikizo yasiyoeleweka,nccr ndo basi kabisi kiongozi wao wa chama tena kitaifa anaangushwa hata ubunge tu tena na wapinzani wenzake kwa hali kama hii hawawezi kuungana kila chama kina matatizo na majeraha yake.
sijakuelewa vema hapo bold! kwa maana ingelikuwa Mbowe hautaki utamu huo, angelimwachia mtu mwingine ndani ya Chadema awe kiongozi wa upinzani. yani napotaka kukuelewa nimejikuta sikuelewi... maana kuna maana ndefu sana hapo. wanasema wapwani rangi rangile
 
Yahya,
Samahani sana. Shida ya kuunganisha vyama bungeni inatokea wapi? Hapa ndipo inabidi tutafakali na kujiuliza.Huu ni mkakati wa CCm kutupotezea muda wa kuongelea mambo ya muhimu kuliko hili. Katiba ndio issue kubwa sasa yenye haja ya kujadiliwa na si muungano wa vyama bungeni.

Nakupa tano kwani hapo umenena. Tuache kushupalia na kupotezea muda mikakati ya Tambwe Hiza na Makamba. Kuna vyama vilivyojipanga na kuna vyama vinavyoganga njaa. Tusubiri bunge litakapoanza ndipo tutaweza kuchanganua kati ya pumba na mchele.
 
Gurudumu
Kama mada inavyosomeka nilitegemea uaanze kuonyesha njia sasa kwa kujenga hoja ambazo zitasaidia kutoa dira na si kupuuza mawazo mema ya waliotangulia hapo juu.
Lete hoja sasa ya msingi...kama mada inavyosomeka.
Thanks

Wananchi wanachohitaji ni kuwakilishwa vema na chama chochote mahali popote, tutazidi kuipotezea cuf kwa sababu walishindwa kuelewa kuwa watanzania hawaihitaji ccm hata kuitamka, wao wakaipigia kura kwenye baadhi ya chaguzi ndani ya bunge wakidhani wameikomoa chadema, kumbe wametuambia ukitokea hata uchaguzi wowote ni chama gani kinaweza kuwawakilisha wananchi katika mambo ya msingi.
Ibrahim lipumba alijisifia uprof kwenye mdahalo uliodhaminiwa na itv. ina maana tungempa ridhaa kuiongoza nchi hii ili uweze angalau kuongea ungepaswa kuwa prof.
tunahitaji chama kinachoweza kuwatetea wananchi bila kufikiria kuungwa mkono na chama kingine cha upinzani,
nadhani mijadala ya kuunganisha vyama ife, kila chama kitavuna kitakayopanda.
nazingatia:
hata wabunge wote wa upinzani wakiungana hawawezi kuwazidi kwa idadi wabunge wa ccm.
kwa hiyo chama kitacho watetea wananchi iwe kwa kupeleka hoja binafsi bungeni au kupinga fedha za uma kuibwa na ccm, bila kujali hoja itapita mbele ya wezi ccm au itakwama.
 
...Nimeangalia kidogo. Huo mjadala hauna maana hata kidogo, ukilinganisha na issues za msingi zinazohitaji kujadiliwa kwa mustakabali wa taifa kwa sasa.

...Yanayosemwa ni yale yale yaliyokwishasemwa kwenye mahojiano na magazeti na kwenye tv nyingine. Kwani, ni lazima star tv i-copy yaliyofanywa na tv nyingine? What a waste of time.

...Nani hafahamu kwamba muungano wa vyama hauna tija, hautakuwapo na utaleta mtafaaruku kama utakuwapo. Its a non issue tayari!

...TV itakoyoleta/host mjadala wa katiba mpya ndio itakuwa imefanya jambo la maana na bora zaidi.

Tatizo una ushabiki, hatuko hapa kuwasilisha mawazo ya mtu au kumfurahisha mtu. masilahi ya watanzania mbele hata ikiwa kurudia mara 50 tupo tayari hadi somo lieleweke. Unadhani wangapi wameshatambua umuhimu wa huo muungano. kama huna hoja remain silent. ACHA JAZBA
 
upo next week kasema Yahya M. hapohapo StarTV stay tuned! (tuna tatizo moja tukishasikia tusiyotaka basi tunaachana na TV!) twawezaje kujufunza kwa taarifa za upande tuupendao pekee? :embarrassed:

Shukrani Mwanamageuko
Tusaidiane kuondoa hizi fikara za upande mmoja, raha ya siasa uyajue mambo na uwe objective utashinda kwa urahisi sana. Dunia imebadilika
 
Bwana Yahya,

Naomba kama huu mjadala utafanyika J2 ijayo kama ulivyoahidi basi kwa upande wa uccr na cuf tafuta watu wanaoweza kuongea kwa mantiki kidogo kuliko kufoka na kushambulia personality ya wanayeongea naye. asilimia 50 walikuwa wanamshambulia mchangiaji wa chadema binafsi. kisha wakaonesha wanashambulia sera za chadema bila kujua kwamba mapungufu waliyoyataja kwa chadema yako kwao na kwa ccm.

la msingi hawafanyi mjadala ukanoga, tafadhali tafuta wengine.
 
Kuungana kunawezekana tu kama kuna muoano wa itikadi, kuungana ili kushinda chaguzi ni umalaya wa kisiasa tu.

Ni kama habari ya ndoa, ndoa ya kweli ni ile inayotokana na mapenzi ya moyo (kukubaliana kiitikadi) ukioa/ kuolewa ili kupata kitu kama mali (ushindi wa uchaguzi) unatumia ndoa kwa umalaya ili kupata unachotaka.
 
Bwana Yahya,

Naomba kama huu mjadala utafanyika J2 ijayo kama ulivyoahidi basi kwa upande wa uccr na cuf tafuta watu wanaoweza kuongea kwa mantiki kidogo kuliko kufoka na kushambulia personality ya wanayeongea naye. asilimia 50 walikuwa wanamshambulia mchangiaji wa chadema binafsi. kisha wakaonesha wanashambulia sera za chadema bila kujua kwamba mapungufu waliyoyataja kwa chadema yako kwao na kwa ccm.

la msingi hawafanyi mjadala ukanoga, tafadhali tafuta wengine.

Thanks kwa angalizo Gurudumu
Kwa kuwa tushawaalika publicly haitakuwa busara kufanya mabadiliko ghafla. Suala la Katiba litakuwa na version nyingi pia. so spear hayo mapendekezo ama nitumie katika private message kisha tutayafanyia kazi katika episode zijazo ikiwezekana hata jumapili ijayo.
Shukran
 
Shukrani Mwanamageuko
Tusaidiane kuondoa hizi fikara za upande mmoja, raha ya siasa uyajue mambo na uwe objective utashinda kwa urahisi sana. Dunia imebadilika
Yahya, hujaliona tatizo hapa? Ninaposema hapa kuna vipofu wengi huwa wanadhani nazungumzia vipofu wa macho. huwa nawasemea vipofu wa fikra. Hawa hata kama mtu wasiemtaka akiwaambia chakula hiki kina sumu watakila kwa sababu yule wamtakae hajasema. Tatizo wengi wetu tunataka ku-base kwenye yale tuyatakayo na si yale yaliyo kinyume na mapenzi yetu. Je tutaitengenezaje Tanzania tuitakayo kwa kutokuwa na fikra pevu?
Bwana Yahya,

Naomba kama huu mjadala utafanyika J2 ijayo kama ulivyoahidi basi kwa upande wa uccr na cuf tafuta watu wanaoweza kuongea kwa mantiki kidogo kuliko kufoka na kushambulia personality ya wanayeongea naye. asilimia 50 walikuwa wanamshambulia mchangiaji wa chadema binafsi. kisha wakaonesha wanashambulia sera za chadema bila kujua kwamba mapungufu waliyoyataja kwa chadema yako kwao na kwa ccm.

la msingi hawafanyi mjadala ukanoga, tafadhali tafuta wengine.
Tatizo bado ni lile lile... Mara ngapi katika mjadala ule alitajwa HR? au yeye ni haki ashambuliwe? wacheni siasa za kinazi tuwe wakweli. NDIO MAANA NAWAAMBIA HAPA KILA SIKU NA SITOCHOKA KWA HILI:

WANASIASA WENGI TANZANIA HAWAIJUI SIASA NI WAGANGA NJAA. NA NDIO MAANA WANABADILI VYAMA KAMA NGUO ZAO! NA WAFUASI WAO WALIO WENGI NI VIPOFU WANAFUATA MKUMBO, BILA KUTAFAKARI WANAPELEKWA WAPI? (Samahanini kama nimewakwaza ila ndio ukweli msioutaka)
 
sijakuelewa vema hapo bold! kwa maana ingelikuwa Mbowe hautaki utamu huo, angelimwachia mtu mwingine ndani ya Chadema awe kiongozi wa upinzani. yani napotaka kukuelewa nimejikuta sikuelewi... maana kuna maana ndefu sana hapo. wanasema wapwani rangi rangile

Mbowe ni chairman wa cdm. huyo mtu mwingine tena awe kiongozi wake huko mjengoni. hii iko sawasawa?
 
Back
Top Bottom