Mjadala wa Pili wa Wizara ya Nishati na Madini: Ngeleja kujiokoa?

Kabakabana

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
5,551
1,158
nimemsikiliza naibu waziri wa nishati na madini,adam malima akianza hotuba yake.kamshukuru mama yake ambae amechelewa lakini atakuja baadaye,mke wake barafu wa moyo wake kipozeo cha roho yake,watoto wake kwa majina zaidi ya kumi,mpaka mashemeji zake na wakwe,jamani was it all necessary?
 
Mh. Ngeleja yupo anatoa hotuba yake ya Makadirio ya Bajeti ya 2011/2012 Stay Tuned
 
Bajeti ya wizara ya Nishati na Madini inasomwa sasa bungeni ambapo inavyoelekea itapita kwa kishindo baada ya kupangiwa Tshs 1.2 trillion . Hapo awali wizara hii iliomba Tshs 600 bn , kwa maana hiyo imeongezwa kwa 100%. Hongereni serikali sikivu kwa kusikiliza maoni ya wananchi na wabunge
 
Jamani huu utamaduni wa kutajana majina mbona naona unapoteza muda tu, kama ni waheshimiwa wote tunawafahamu. waziri anasimama na kuanza kuwashukuru wabunge wachangiaji anatumia dk 20,
Mbunge kuchangia ni moja ya utekelezaji wa majukumu yake aliyotumwa na wananchi, unamshukuru kwa lipi????
Mbona wanaolala au kuwa mabubu hamuwashukuru kwa kuuchapa usingizi.
Swala jingine pamoja na kuwa lishajadiliwa humu, ni la mtu kuanza kumshukuru mara mkewe.. mara housegirl wake...mara mbwa wake nini sasa wananiboa.
Aya ngoja nimsikilize NGEREJA kashaanza michakato.
 
Naona wabunge mbalimbali leo bungeni wako bize wakipeana vimemo na wengine wengi wanaonekana wakijadiliana wakati huu ambapo ngereja anasoma majumuisho ya bajeti yake. Nimemuona Makamba na lukuvi, Wenje na Olesendeka, Zitto na Lissu, sitta na pinda, Mbowe na wenje, machali na mnyika na wengine wengi. Sijui ni mkakati gani wanaoufanya. Zitto pia anonekana kuwa bize kama vile anapiga mahesabu kwenye simu yake.
 
Wapendwa mana JF wizara ya nishati na madini inajadiliwa bungeni!Tuangalie na tuone kama ina jipya ili tuamue kwa busara na sio kusubiri kuhadithiwa,nafahamu kuwa wenye axcess na tv sio wengi lakini kwa wale walionayo wajitahidi sana,Tupo pamoja kwenye maendeleo ya nchi yetu!
 
Naona Mh. Ngeleja leo anawasilisha hotuba yake kwa mara ya pili na naona anashangiliwa sana na wabunge hasa wale wa CCM, na ameongelea miradi mipya kadha huku akisema kuna gharama kubwa itahusika na kwa mtazamo wake hadi mwezi wa 12 mgao utakuwa historia Tanzania.
Hoja je cc watanzania tunaonaje maboreshao haya?
 
Leo ngereja atachomoka maana naona wabunge wa ccm wanalipuka kwa makofi mazito kwa kila point anayoizungumza, nadhani wamejipanga vilivyo kumuokoa leo.
 
Naona wabunge mbalimbali leo bungeni wako bize wakipeana vimemo na wengine wengi wanaonekana wakijadiliana wakati huu ambapo ngereja anasoma majumuisho ya bajeti yake. Nimemuona Makamba na lukuvi, Wenje na Olesendeka, Zitto na Lissu, sitta na pinda, Mbowe na wenje, machali na mnyika na wengine wengi. Sijui ni mkakati gani wanaoufanya. Zitto pia anonekana kuwa bize kama vile anapiga mahesabu kwenye simu yake.
&amp;lt;br /&amp;gt;&lt;br /&gt;<br />
&amp;lt;br /&amp;gt;&lt;br /&gt;<br />
Zito apigi mahesabu kwny simu, ana tweet mkuu.
 
Itabidi Waziri mtoa hoja awe anawashukuru pia "House Girl", na "House Boy" - Maana Malima kawashukuru mpaka MASHEMEJI!
 
Amemaliza kuwasilisha hoja, Spika anatambulisha wageni, yaonekana bajeti ya Ngeleja itapita kwa kishindo maana hata wabunge wa CDM wanaonekana kuikubali kwa kumpigia makofi mtoa hoja
 
Jamani huu utamaduni wa kutajana majina mbona naona unapoteza muda tu, kama ni waheshimiwa wote tunawafahamu. waziri anasimama na kuanza kuwashukuru wabunge wachangiaji anatumia dk 20,
Mbunge kuchangia ni moja ya utekelezaji wa majukumu yake aliyotumwa na wananchi, unamshukuru kwa lipi????
Mbona wanaolala au kuwa mabubu hamuwashukuru kwa kuuchapa usingizi.
Swala jingine pamoja na kuwa lishajadiliwa humu, ni la mtu kuanza kumshukuru mara mkewe.. mara housegirl wake...mara mbwa wake nini sasa wananiboa.
Aya ngoja nimsikilize NGEREJA kashaanza michakato.

Nadhani huwa ni strategy ya makusudi ili kujipunguzi muda wa kujieleza.
 
ngeleja naona anasisitiza kuwa sisi kwetu tanzania tunatoza kiasi kidogo sana kwenye umeme kulinganisha na wenzetu wa kenya na uganda..anataka tanesco wajitegemee kwa kutoza kiasi cha juu.hapa vp wakuu ghalama zitapanda nini? na sijui itakuwa ni lini!
 
Back
Top Bottom