Mjadala wa Mafuta na Suala la Muungano

Hakuna Ukristo Zanzibar. na hao unaowasikia Wote wametoka bara na hawafiki hata 1%

Aliekuambia hakuna Ukristo Zinzi-bar ni nani, Hayo Makanisa yaliyoko huko ina maana hawasali binadamu? Au ndo maana Mnayachoma?
 
Source: HabariLeo

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauta kufa kwa sababu ya Wazanzibari kupendekeza suala la mafuta na gesi asilia liondolewe kwenye orodha ya mambo ya Muungano.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa Maji Ujenzi Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid alisema kuwepo kwa mijadala ya wazi kuhusu mafuta na gesi asilia hakumaanishi kutetereka kwa Muungano na badala yake ni kuujengea ukuta imara zaidi.

"Hakuna aliyetaka na anayetaka kujitenga, lililojitokeza ni kuibuka kwa mjadala wa kutaka mafuta na gesi asilia viondolewe katika orodha ya mambo ya Muungano si kujitenga, leo ni miaka 46 kamwe Muungano hautakufa kwa sababu ya mafuta, bendera ile pale inapepea katika ardhi ya Tanzania na sisi tutabaki kama Taifa moja," alisema.

Waziri Mansoor alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya baadhi ya waandishi wa habari kuhoji sababu za Zanzibar kuendelea kung’ang’ania mafuta kuondolewa kwenye Muungano na kuongeza kuwa uamuzi huo ni ishara ya kuyumba kwa Muungano.

“Nilitarajia muniulize Zanzibar inanufaika vipi na mapato ya gesi asilia ambayo hata senti moja haijawahi kupewa… sasa kuna dhambi gani Wazanzibari wakitaka kuondolewa kwa suala hilo?” Alisema Mansoor.

Alisema Zanzibar hainufaiki kabisa na faida ya gesi asilia licha ya kuwa suala hilo ni limo kwenye orodha ya mambo ya Muungano.

Waziri Mansoor alisisitiza kwamba SMZ itaendelea kuheshimu uamuzi wa wananchi kupitia Baraza lao la Wawakilishi lililotaka mafuta na gesi asilia kusimamiwa na SMZ badala ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano.

Alisema bado mafuta hayajagundulika, lakini kuna kila dalili za kuwepo kwa nishati hiyo katika Visiwa vya Unguja na Pemba na sasa tayari mchakato wa kutayarisha Sera ya Nishati Zanzibar unaendelea.

Akizungumza katika mkutano huo, Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Abubakar Khamis Bakar ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni (CUF), alisema uamuzi wa mafuta na gesi kubakia ya Zanzibar si wa mtu mmoja au chama fulani ni wa Wazanzibari wote.

“Wazanzibari tunasema kwa sauti moja mafuta na gesi asilia yasiwe ya Muungano na hilo lipo wazi kabisa…sasa nashangaa hapa kusemwa kwamba Zanzibar ina uchoyo au kutaka kudhoofisha Muungano, hilo si kweli,” alisema Bakar.

Mawazo yangu:

Huu mjadala huwaga najiuliza maswali mengi majibu nakosa!!!
H1: Kwanini wazanzibari huwaga wanasema kuwa rasilimali yao ni ya wazanzibari na ya kwetu iwe yetu sote

H2: Muungano wetu ulianzishwa kivipi makubaliano ya majukumu na mapato ilikuwaje.

H3: Tanzania bila ya zanzibar tutakosa kitu gani?

H4: Je wazanzibar wanafahamu mafuta ni mkosi!!! wakianza kuchinjana humo sisi tuwaache maana walitunyima mafuta yao!!.Maana wakitoka Tanganyika na Zanzibar yataanza mafuta ya wapemba na waunguja!!! Au mafuta ya Waarabu wa hizbul-Tahrir na Watumbatu au wanyamwezi!!!

H5: Je mafuta ya zanzibar yako kwa kiwango gani??? Yatakapopungua au kuisha reserve yake wanajua repurcusion yake au ndio watalamba matapishi yao!!!

Mradi maswali haya nakosaga majibu kabisa hebu nisaidieni waungwana
 
Wazanzibari tunasema kwa sauti moja mafuta na gesi asilia yasiwe ya Muungano na hilo lipo wazi kabisa…sasa nashangaa hapa kusemwa kwamba Zanzibar ina uchoyo au kutaka kudhoofisha Muungano, hilo si kweli

Sawa kabisa. hakuna kuteteleka kwa hilo
 
natumaini serikali ya muungano imeangalia experience
ya trinidad na tobago katika suala la mafuta.

kama bado basi huenda mkulu alipokuwa mitaa ya
huko hivi karibuni alipata wasaa wa kunong'onezana
na wakulu wa huko kuhusu hili
 
What our fellow brothers and sisters in Zanzibar are doing can be compared to a person who is counting his / her chickens before they hatch. It seems like these people are living under the umbrella of wishful thinking. Who told them there is oil and gas in Zanzibar? This is what I know, please someone should correct me if I am wrong, Geologists have told them that Zanzibar doesn't have substantial amount of oil that can be feasibly explored in large scale. My take, Zanzibarians should be careful with what they are wishing for; otherwise, they might end up shooting themselves in the foot.
 
Hii ni kweli kaka but unajua hawa jamaa mie hukaa nikasema ok tuassume mafuta yapo zanzibar. Je uchimbaji wa mafuta utakuwaje na mgawanyiko wa mafuta ukoje. Unajua Znz haipo stable kama Tanganyika na simple kuna siasa za ugozi visiwani humo ukienda utaambiwa huyu mbongo (a.k.a Mtanganyika) au yule mwenzetu, mara utasikia yule hizbu mara huyu mnyamwezi (a.k.a watu wa asili ya Tanzania bara walioenda znz zamani) sasa siasa hizi zinatawala sana hadi katika serikali utakuta mtu anachaguliwa sio kwa merits zake bali ametokea znz sehemu gani either kusini anakotoka Dk.Salmin Amour or Kaskazini kwa Karume.

Siasa za matabaka haya na muunganiko wa ghafla unanipa wasiwasi hata wakija kupata mafuta wataanza tena kugawanyika wenyewe kwa wenyewe mwisho wa siku vurugu tupu!!!

Tuje katika mafuta ni kweli kuwa mafuta hayana uhakika kwamba yapo znz au la. Geological survey reports zinasema inawezekana meaning it is probability condition!! je yakiwa hayapo zanzibar watalamba matapishi yao wenyewe? Tukija katika muungano kuna wapemba na wazanzibari wengi wameekeza Tanzania Bar pita Kariakoo, Ilala Kinondoni utakuta katika kila maduka 10 5 ya watu wa kutoka znz je Tanzania bara wakianza kuweka vizuizi nchi itaenda?? Kwa maana kama wakenya tunawanyima ardhi Tanzania Bara je wazanzibar nao???

Umeme tunawapatia, Security tunawapatia? Je na hivyo vinakuwaje??? Kimsingi tunarudi katika suala la muungano linasemaje???
 
What our fellow brothers and sisters in Zanzibar are doing can be compared to a person who is counting his / her chickens before they hatch. It seems like these people are living under the umbrella of wishful thinking. Who told them there is oil and gas in Zanzibar? This is what I know, please someone should correct me if I am wrong, Geologists have told them that Zanzibar doesn't have substantial amount of oil that can be feasibly explored in large scale. My take, Zanzibarians should be careful with what they are wishing for; otherwise, they might end up shooting themselves in the foot.

Hivi umejiuliza kilichoifanya serekali kutafuta mtalamu wa kufanya mgao wa mafuta ?wakati hayo mafuta yenyeywe hayajagundulikana ?pili umewahi kujiuliza kwanini serekali ya Tanganyika haikuleta mtalamu wa kufanya mgao walipovumbuwa Gas ,madini ya dhahabu na mengineno ?,iwe hili la mafuta tu ?Kambarage aliweza kuwa ngonga visogo wazanzibari kwa miaka mingi na kwa sababu tu ya ule ukarimu wao walionao , sasa wakati umefika wa kuelezana yale ya ukweli huwezi kuwa full watu siku zote ipo siku watakubaini.
 
Ni kwanini hebu tufafanulie!!!
 
ni jambo la kushangaza mtoto hajazaliwa na wala mimba haijawa mnaleta wataalamu wa kugawana faida kwa hiyo inaonyesha mimba iko tayari na ndio maana mnanunua nguo a mtoto kwahiyo mafuta inawezekana yapo zenji kwani wao sio wajinga kusema kuwa mafuta ni yao ukiangalia sana wazenji wengi wapo kwenye hayo makampuni ya uchimbaji wa mafuta lazima data watakuwa wamepata za uhakika na ndio maana bara wanataka yawe yao lakini naona hili wameshachelewa kwa hilo tuwaachie wenyewe wachimbe watatugaia japo kidogo unadhani wazenjiwakiwa na mafuta watataka tena umeme wa bara hilo tusahau
 
Mdondoaji,Barubaru,Kafara,Spear,

..hivi kuna anayefahamu mapato ya UVUVI tunagawana vipi ktk huu MUUNGANO?

..nimewahi kusoma mahali kwamba kuna eneo la mkondo wa bahari kati ya Zenj na Tanganyika ambalo kwa sheria za kimataifa hakuna upande unaoweza kudai mamlaka kamili bila kumuingilia mwenzake. sijui mafuta yakipatikana ktk eneo hilo itakuwaje.
 
Good point but nadhani linaelekea ndani ya swala la muungano wetu ukoje are we a union? a state? Federation? au muungano wa chini ya mwembe?
 
Habari zenu wana JF,

Nilikuwa naipitia hii article ya zamani ya dailynews, na hapo naona huyo mwanasheria mstaafu anavyosema kuwa hili suala halikuwemo kwenye masuala ya muungano...limeingizwa kwenye muungano kinyemela, hivyo mafuta hayamo katika masuala ya muungano.Jee ni kweli hii?

Mr Bakari (Mgogoni-CUF), a former Isles Attorney General, argued that oil was included in the Union constitution as a Union matter but without getting the consent of Zanzibar as a partner in the union established on April 26, 1964.
The chief minister's statement has come a couple of months after a section of the press quoted him as saying oil was a non-Union matter.
 
Jamani naomba nifahamishwe kuhusu mantiki ya haya mambo ya kusema mafuta ya Zanzibar ni ya kwa ajili ya Wazanzibari pekee. Je hayo madini na mafuta ya Tanganyika ni ya nani wakati serikali ya Tanganyika haipo? Au ndio shamba la bibi? Angalia gesi inatumika kuzalisha umeme ambao unatumika Unguja, Tanganyika na sasa Pemba. Fedha zinazopatika kwenye madini ya Tanganyika zinatumiwa na Hazina ya Tanzania kuhumia taasisi za Mungano kama vile Jeshi, Polisi, Usalama wa Taifa, wabunge etc. Mbona Tanganyika aidai madini na mafuta yake yahudumie shughuli zake pekee?
 
Hayo masuali yako yanatoka nje ya maada.Tunachojadili hapa ni katiba na makubaliano ya muungano.Jee mafuta yalikuwemo kwenye masuala ya muungano?Na vipi yalivyoingiziwa yakawa ya muungano, sheria na taratibu zilifuatwa?

P:S
**Aidha kwa masuali yako ya umeme na kwanini madini yanakwenda hazina, hili ni kosa la Mwalimu Nyerere kuifuta Tanganyika.Vyovyote iwanvyo, nafikiria Zanzibar itakuwa inachangia gharama za muungano kama polisi na ulinzi.
**Kumbuka Zanzibar ni ndogo, na mahitaji yake ya ulinzi ni madogo.Hivyo, watakuwa wanachangia sehemu ndogo tuu.Kuna gharama kubwa ya kodi kama za Benk ambazo zinafanya kazi Zanzibar, lakini mapato yanakwenda hazina ya Tanzania.
**Umeme Zanzibar ni mteja tuu wa Tanesco, tumeshashuhudia mara nyingi SMZ ikapiga na chini wawekezaji wengine kulinda soko la Tanesco.Kwa hiyo umeme sioni kama ni hoja yenye mshiko.

Turudi kwenye maada, mafuta yaliingizwa kinyemela kwenye muungano?
 
Mie nilishasema suala lolote la wazanzibar linantia kichefuchefu mno,these pepole will never be satsfied anymore till the end of this planet!
 
Mie nilishasema suala lolote la wazanzibar linantia kichefuchefu mno,these pepole will never be satsfied anymore till the end of this planet!
Hili ni tatizo nalo. Kwa nini jamani mnakimbilia kusema ni wakorofi na hawaridhiki tu!!!. Hili la katika mada hii mi mi naona ni la msingi. Na tuangalie . kama yalingizwa kinyemela-sawa ilikuwa ni kosa. sasa tusikilize matakwa ya Wenzetu, (Wazanzibari) wao wanataka kulitoa hilo katika Muungano lakini si kinyemela bali kwa kufuata sheria na taratibu. Si umemsikia Karume juzi kagusia hilo. sasa kasoro ipo wapi hapo???
 
Jamani naomba nifahamishwe kuhusu mantiki ya haya mambo ya kusema mafuta ya Zanzibar ni ya kwa ajili ya Wazanzibari pekee. Je hayo madini na mafuta ya Tanganyika ni ya nani wakati serikali ya Tanganyika haipo? Au ndio shamba la bibi? Angalia gesi inatumika kuzalisha umeme ambao unatumika Unguja, Tanganyika na sasa Pemba. Fedha zinazopatika kwenye madini ya Tanganyika zinatumiwa na Hazina ya Tanzania kuhumia taasisi za Mungano kama vile Jeshi, Polisi, Usalama wa Taifa, wabunge etc. Mbona Tanganyika aidai madini na mafuta yake yahudumie shughuli zake pekee?

Unajuwa masuwala yako unatakiwa kuuliza viongozi kwa mambo yafuatayo:
!. Kwanini wanasema kuwa madini si suwala la Muungano na mali asili za bahari ni za Muungano?
2. Kwa nini masuwala ya Tanganyika (sio Zanzibar) huwa yanaamuliwa na Bunge na yale ya Zanzibar yanaamuliwa na Zanzibar?
3. Kwa nini Zanzibar ina sheria zake na Tanganyika ina zake?
4. Kwanini tume ya utumishi inayoshughulikia ajira na utumishi wa Tanganyika ndiyo inayotumika kwa Idara za Muungano?
5. Kwanini kuna Marais wawili kwenye Muungano?

Hayo ni baadhi tu ya maswali ambayo inabidi mtu ajiulize katika kuona hichi kitum kinachoitwa Muungano si Muungano bali ni mizungu tu.
 
Ni kweli suala hilo liliingizwa kwenye muungano kinyemela, na sio hilo tuu, yako mengine kibao. Tulipo ungano, mambo ya muungano yalikuwa 11, sasa yanakaribia 30. La mwisho kabisa ni la kuifanya Zanzibar mkoa.......................................................................................................................Jamani muungano wa dhati ni kama ndoa. Mkishaungana, mnakuwa kitu kimoja. Hi kwenye ndoa, ili upate kila kitu, lazima uombe?. Vile ambayo ni stahili yako, unaweza kuomba, ama ukachukua, ili mradi usende kusiko.............................................................................................................Dini ya Kiislamu inaruhusu wake mwisho wanne. Inasema kabla hujaoa tena, omba ridhaa ya mke/wake waliopo, unaweza omba ridhaa na ukakataliwa, ukioa kwa nguvu bila hiyo ridhaa bado ndoa ni halali.................................................................................................................Japo ndoa ni muungano wa hiyari, haiwezi kufika mahali mke aliyeolewa akajiamkia tuu na kusema leo sikutaki, naomba talaka yangu. Talaka atoaye ni muoaji sio muolewaji..........................................................................................................Hizi kelele za muungano ni kama ndoa, hapo kuna muoaji na aliyeolewa, inaonekena kuna kelele za kutaka talaka. Kama kweli umetendewa visivyo, talaka itatolewa, lakini kama umetendewa ndivyo, wataka talaka tuu ili uwe huru kufanya mambo yako, unajisumbua bure, talaka hakuna.............................................................................................Kwa mara ya kwanza Juzi, Karume kaomba gesi na mafuta. Hivi hamjifunzi tuu kwa makosa ya Jumbe kutaka kuipigania Zanzibar uhuru wake UN, yalimkuta yapi?.Komandoo kataka badili katiba ili kuondoa ukomo wa miaka 10, yepi yalimkuta?.........................................................................................................Leo Karume anayaomba mafuta yawe yenu, hivi ni mafuta gani hayo?. Mbona hayajapatikana bado?, au hayo mafuta ya kwenye kinibu yataka watoa roho. Hivi kweli ni mafuta ama kuna mengine?. Mesej ya Karume sent...subirini majibu ila msije kulia!
 
Mie nilishasema suala lolote la wazanzibar linantia kichefuchefu mno,these pepole will never be satsfied anymore till the end of this planet!

Mbona Wazanzibar tayari wanatapika kwa mambo ya Watanganyika. Aisee watu nyie ni wa ajabu kungangania kisicho chenu na huku mkijidai kuwa hakina faida nanyi. Hivyo hujakaa ukafikiri kati ya Wazanzibari na wewe yupi wa ajabu?
 
Back
Top Bottom