Mjadala wa katiba: Prof. Shivji katika Star tv

aisee prof kanitia hasira mnoooo maana kafumbua janja zote za CCM. katiba ni ya wananchi na si ccm niko tayari sasa kufa kwa risasi za ccm ili mapinduzi yafanyike watoto wangu waishi kwenye katiba mpya!
 
mbatia mwenyekiti,microphone yake imezungushiwa kidude cha kijani. mwakilishi wa tadea amwagia sifa jk,asema katiba haiwezi kuandikwa na watu milioni 40
 
aisee prof kanitia hasira mnoooo maana kafumbua janja zote za CCM. katiba ni ya wananchi na si ccm niko tayari sasa kufa kwa risasi za ccm ili mapinduzi yafanyike watoto wangu waishi kwenye katiba mpya!
Tuwekeeni dondoo humu wengine tupo mbali na TV.
 
Hivi Dar ina chuo kimoja tu cha Dar na matawi yake ama ni wanafunzi hao tu ndo wenye uchungu na nchi hii ama ni tatizo la kimantiki linalovikumba vyuo vingine na wanafunzi wake?...

niseme kweli nasikitika kuona mijadala mbalimbali inayokuwa inaendeshwa katika mambo mbalimbali na sehemu mbalimbali wanaoonekana kuguswa,kuhudhuria na kutoa michango ni wanafunzi kutoka chuo kimoja tu cha Dsm,wanafunzi vyuo vingine mfano Ustawi,Kampala,Kairuki,Muhimbili n.k mnashughurika na nini hasa hata mnakosa uwepo wenu juu ya masuala mbalimbali juu ya nchi yetu?ama ndo kusoma sana?ndugu zetu kusoma ni zaidi ya hapo...kwa vile nanyi ni wasomi na kweli ni wasomi basi tunahitaji michango yenu katika mambo ili tupate changamoto vinginevyo Ud itaonekana na itazidi kuonekana na daima itaeleweka ndo kitovu cha kila kitu kwenye jamii...come on,get up guys!!

Yangu ni hayo tu kwa leo.
 
Msikkilize Prof. Shivji Star Tv. anauchambua mswada wa katiba mpya

Prof. Shivji amechambua vizuri sana mswaada ule na amekosoa na kutoa mwongozo wake. hao wengine waliofuatia walikuwa ni walalamishi tu ambavyo inakuwa hakuna tija.
kuhusu tume ya katiba amependekeza vyuo vikuu pamoja na vyama vya kitaaluma ndiyo vichague majina mengi ndiyo yapelekwe kwa Rais naye ateue tume ndani ya majina hayo.
kuhusu Bunge la katiba amesema Bunge lililopo ambalo 70% CCM na wa Zanzibar wachache halitafaa kwa katiba bali ufanywe utaratibu liundwe Bunge lingine lenye uwakilishi mzuri na ambalo lina watu wachache.

lingine ni kuhusu ushiriki wa Wazili katika katiba pamoja na kulipa posho na marupurupu kwa tume. amependekeza posho na marupurupu yatowekwe kwenye mwongozo na yajadiliwe katika bunge na pia uwasiliswaji wa katiba Bungeni ufanywe na members wa tume ie mwenyekiti wa tume ambaye ameshiriki kwenye mchakato badala ya Waziri wa sheria
na mengine mengi aliyasema
 
Hivi Dar ina chuo kimoja tu cha Dar na matawi yake ama ni wanafunzi hao tu ndo wenye uchungu na nchi hii ama ni tatizo la kimantiki linalovikumba vyuo vingine na wanafunzi wake?...

niseme kweli nasikitika kuona mijadala mbalimbali inayokuwa inaendeshwa katika mambo mbalimbali na sehemu mbalimbali wanaoonekana kuguswa,kuhudhuria na kutoa michango ni wanafunzi kutoka chuo kimoja tu cha Dsm,wanafunzi vyuo vingine mfano Ustawi,Kampala,Kairuki,Muhimbili n.k mnashughurika na nini hasa hata mnakosa uwepo wenu juu ya masuala mbalimbali juu ya nchi yetu?ama ndo kusoma sana?ndugu zetu kusoma ni zaidi ya hapo...kwa vile nanyi ni wasomi na kweli ni wasomi basi tunahitaji michango yenu katika mambo ili tupate changamoto vinginevyo Ud itaonekana na itazidi kuonekana na daima itaeleweka ndo kitovu cha kila kitu kwenye jamii...come on,get up guys!!
Hata huyo mwalimu wao Shivji, kila kitu Shivji, Shivji, Shivji, nchi nzima constitutional thinker mmoja!?

Back
Top Bottom