Mjadala wa katiba na BBC leo

Mbunge Jason Rweikiza wa CCM (Wakili wa Kujitegemea) amethibitisha dhahiri nini CCM wamepanga kutufanya watanzania. Yaani amesema uongo wa dhahiri kuwa kila mbunge alipata huo muswada wa Kiswahili na kujadiliana na wananchi waliomchagua kILA KIJIJI. Wakati anatoa kauli hiyo alisahau kuwa alimuunga mkono Mhe TUndu Lissu kuwa muswada huo ulifikishwa katika Kamati ya Katiba na Sheria tar 24 Oktoba 2011 na kwa maneno yake mwenyewe "leo ni tar 16 Nov ni kama mwezi hivi". Hivi kweli siku 23 tokea tar 24 Okot 2011 zinatosha kwa Kamati hiyo kuwa imeupitia na kuufanyia kazi na kisha kuupeleka kwa wabunge ambao walijadilina na wananchi wao katika kali kijiji? Huu kama sio uongo wenye nia ya kuwakosesha watanzania haki yao kutoa maoni kuhusu mchakato wa kuundwa kwa katiba mpya ni nini? Kwa hakika amewadhalilisha wanasheria na mawakili wote hapa nchini kwa kusema uongo wa kitoto namna ile hadharani. Tokea sasa siwaamini mawakili wa Tanzania tena. Historia ya uundwaji na mabadiliko yote ya Katiba za Tanzania zilizopita ikiwemo hii tuliyonayo vimekuwa vikiwasilishwa bungeni kwa hati ya dharura kama ilivyokuwa miefanyika katika ule muswada wa awali, lengo ni kuwakosesha wabunge na wananchi fursa ya kushiriki mjadal huu muhimu. Kwa kuwa wabunge wa upinzani walifanikiwa kuwashawishi hata wabunge wa ccm kuukata muswada wa awali. Bado lengo la kuwakosesha watanzania haki yao ya kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni yao/ na kuzingatiwa kwa amoni yao katika machakato wa uundwaji wa katiba bado lipo pale pale ndio maana ya wabunge wa ccm walakaa kama kamati ya chama kula njama hii. Ni muhimu watanzania wote wakaelimishwa kwa lugha rahisi nini maana ya muswada wa sheria kusomwa bungeni kwa mara ya kwanza- Ni kwamba baada ya muswada kusomwa kwa mara ya kwanza bungeni wananchi hupatiwa fursaa ya siku zaidi 90 kutoa maoni yao kuhus huo muswada. Hivyo niwajibu wa serikali kuhakikiha yakuwa wananchi nchi nzima wanapata nakala za muswada husika ili waweze kutoa maoni kikamilifu. Pia waelimishwe kuwa muswada kusomwa kwa mara ya pili maana yake ni wabunge kuanza kuujadili na hatimaye kuupitisha kuwa sheria. Hapa ndipo ulipo mgogoro wa wabunge wa CCM na CHADEMA. Wabunge wa CDM wantaka muswada usomwe tena kwa mara ya kwanza halafu wananchi wapatiwe nakala za kiswahili za huo muswada ili waweze kutoa maoni yao; ndipo uje kusomwa kwa mara ya pili na hatimaye ujadiliwe na kuwa sheria. Lakini CCM inawatumia wabunge wake na wale CUF kuwanyima wananchi haki yao ya kupatiwa nakala za muswada huu ili waweze kutoa maoni yao na badala yake wanaharakisha kuupitisha kuwa sheria. Mantiki ya kuharakisha kuupitisha kuwa sheria ni ili kuweza kutumia visingizio vya adhabu ziilizo katika muswada huu yaani kifungo jela cha miaka 30 kwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kuupotosha au kuzuia usitekelezwe. Utaratibu huu wa wananchi kupatiwa haki ya kutoa maoni katika miswada ya sheria inayofikishwa bungeni ili kuwa sheria unastahili kutumika katika sheria zote zinzotungwa na bunge. Ni kwa sababu wabunge wetu hususan kutoka CCM wamekuwa hawako makini kuibana serikali kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kikamilifu katika mchakato wa utungwaji wa sheia mbali mbali ndio maana Tanzania ina sheria mbovu ikiwemo zile za madini, manunuzi n.k HONGERA WABUNGE WA CHADEMA NA NCCR KWA KUWAAMSHA WATANZANIA KUTOKA KATIKA USINGIZI TULIOKUWA TUMELAZWA AMBAPO SASA TUNAWEZA KUWATAMBUA WAZIWAZI MASPIKA WETU WANAVYOTUMIKA KUWANYIMA HAKI WANANCHI. Yeyote anaytaka kusikiliza mjadala huo aingieBBC Video Player
Mjomba umeeleza vizuri sana. Sasa wale vichwa ngumu kama tena watashindwa kuelewa hapa basi wajue vichwa vyao vimejaa makamasi.
 
bi kiroboto alisema kamati haiwezi zunguka mikoani kwa kuwa yeye yupo india!pumbafu kafanya bunge ni kampuni yake binafsi
 
kina Anna Kilango wapo wengi eti wabunge walizunguka mpaka vijijini kupata maoni.
 
Back
Top Bottom