Mjadala wa Katiba Mpya

Manyi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
3,253
604
Nimefuatllia kwa karibu sana vipindi vya midahalo ya upatikanaji wa katiba mpya TBC kutoka sehemu mbalimbali nchini, kwa sasa, na kwa kweli wananchi wanaonyesha ukomavu na ujasiri wa hali ya juu wa kudadavua na kupembua mambo.

My Take
Kwa hali jinsi ilivyo, kuna wapambanaji wa ukweli sana mikoani, wanahitaji kuwezeshwa ili wawe wapiganaji kamili. Magamba mna hali mbaya sana katika ulimwengu huu wa sasa, kumbukeni hii si 1961 na saa ya ukombozi ni sasa.
Makamanda tukaze buti, ukombozi uko karibu sana.
 
Mkuu tuelekeze tujadili nini; Katiba mpya au hali mbaya ya magamba au saa ya ukombozi?
 
kwenye katiba mpya nataka sheria za kazi zibainishwe wazi haki ya mfanyakazi hasa wakati huu kuna makampuni mengi ya kigeni yana exploits wabongo sana tu, km hawa Erolink. Kuna kampuni moja ya simu watu waliokuwa customer care waliugua masikio baada ya kupokea simu kwa miaka takriban mitano, lkn wakaachishwa kazi kishenzi sana. Bado mioyo yetu inauma ndugu zetu kuachishwa kazi namna ile. hawakulipwa kabisa. So napitia sheria zote za kazi halafu ntakuja na draft kamili ya mapendekezo. Najua kuna akina Mnyika, Lissu, Zitto wapo humu watafanikisha tuu.
 
kuna na ss wengine wa migodini tuna tatizo kama hilo unapo pata matatizo ya kiafya yanayotokana na kazi unayo fanya unatibiwa kidogo tu ikishindikana kupona ndani ya miezi 6 basi kazi ndo hakuna na unaendelea kujitibisha mwenyewe sasa ebu chukulia labda mtu umeufua mgongo na matibabu ya mgongo ni gali mtu kazi ndo hauna vipi utayamudu? mi nahisi hawa wawekezaji wa nje wapo juu ya sheria za nchi maana wanafanya mambo kinyemela na hakuna anaye wauliza
 
Back
Top Bottom