Mjadala wa Dowans ITV wasitishwa

Watulete e kwanza picha halisi ya mmiliki wa dowans, ili tujue ni nani tunamwongelea, hatutaki kufanya umbea!
 
Kwenye viambatisho vya hukumu ya ICC, kama ilivyosajiliwa Mahakama Kuu ya Tanzania, zipo nyaraka
zinazoonyesha kwamba mwanasheria aliyeishauri TANESCO kuvunja mkataba na Dowans – kwa kusema
kwamba sio mkataba halali na kwamba hakuna madhara ya kisheria kuuvunja – ndiye huyo huyo pia aliyeishauri
Benki ya STANBIC kutoa mkopo wa dola za Kimarekani milioni 20 kwa Dowans – kwa kusema
kwamba ni kampuni halali, inakopesheka na ina mkataba halali na TANESCO. Na ndiye huyo huyo aliyeiwakilisha
TANESCO kwenye kesi iliyofunguliwa na Dowans, kesi ambayo imetokana na ushauri wake, na,
baada ya hukumu, ndiye huyo huyo, kwa mujibu wa maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati ya terehe 6 Januari
2011, aliyetoa ushauri kwamba hakuna njia nyingine zaidi ya kuilipa Dowans.

Nimeipata hii hivi punde...Kuna anayeweza kuthibitisha haya!?
 
MM alituhabarisha jana kwamba leo j4 atatujuza baadhi ya sehemu ya mahojiano yake na Brigadier Al Adawi anayesadikika ndiye mmiliki wa DOWANS .. Mwanakijiji je utatuwekea hapa jamvini au ndiyo utaweka wazi kwenye ITV...?
 
Endapo umeme utakatwa kwa sababu yeyote ile kweli itakuwa ni mchezo mchafu unachezwa. Lets wait and see
Mungu ibariki Tanzania
basi nadhan warushe mpaka radio one...ili wakikata umeme tutumie hata redio kwenye simu zetu.
 
Mkuu Mkjj, miye nakuomba usisubiri hao mafisadi walipwe, kama unaweza kuyaweka mahojiano hayo hadharani kabla ya malipo hayo kufanywa basi unaweza kabisa kwa namna moja au nyingine kuinusuru nchi yetu kulipa malipo ya kifisadi ya mabilioni ya shilingi.



Hapana; kwa miaka mitano tumewalilia kuhusu watu hawa hawa na sasa wamekuja na kututhubutisha; sasa watawala wetu wawalipe ili tuwaoneshe jinsi gani utawala wao ulivyo mbovu na Watanzani waliowachagua wajue wametuchagulia madudu gani. Walipeni tu. Nitawekeza dokezo la interview hiyo Jumanne.

MM .... kumekucha na makucha yake... tujuze ahadi yako mkuu
 
Hivi kwanini hawa watu tusiwaue:Rostam na Lowassa.Hawa watu hatari sana.Saa yoyote watatuua sisi.Tuwawahi jamani.Mi namtafuta Al-Aldawi nimuue....:angry:
 
Kama umeme utakatwa kabla ya kipindi maalum litakuwa jambo la kheri kwani ndio nafasi ya kipekee katika kuelekea Tahrir, sio kuipinga DOWAns bali kushinikiza umeme urudi, na ukirudi haturudi nyuma, mpaka DOWANS ajulikane na waliowaleta pia.
 
Kwenye viambatisho vya hukumu ya ICC, kama ilivyosajiliwa Mahakama Kuu ya Tanzania, zipo nyaraka
zinazoonyesha kwamba mwanasheria aliyeishauri TANESCO kuvunja mkataba na Dowans – kwa kusema
kwamba sio mkataba halali na kwamba hakuna madhara ya kisheria kuuvunja – ndiye huyo huyo pia aliyeishauri
Benki ya STANBIC kutoa mkopo wa dola za Kimarekani milioni 20 kwa Dowans – kwa kusema
kwamba ni kampuni halali, inakopesheka na ina mkataba halali na TANESCO. Na ndiye huyo huyo aliyeiwakilisha
TANESCO kwenye kesi iliyofunguliwa na Dowans, kesi ambayo imetokana na ushauri wake, na,
baada ya hukumu, ndiye huyo huyo, kwa mujibu wa maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati ya terehe 6 Januari
2011, aliyetoa ushauri kwamba hakuna njia nyingine zaidi ya kuilipa Dowans.

Nimeipata hii hivi punde...Kuna anayeweza kuthibitisha haya!?

Hao REX attorneys ni mafisadi wanaopata maelekezo yote toka kwa Rostam na kutekeleza
 
Kama umeme utakuwepo kwangu Nitawaleta 'Live Text'

Stay tuned,

Thanx
 
Mmiliki Dowans utata



*Achanganya wananchi, wahoji maswali lukuki
*Mbunge ataka akamatwe apigwe picha kwa nguvu
*CTI wataka mitambo yake itaifishwe haraka


Na John Daniel
Majira

MBUNGE wa Ubungo Bw. John Mnyika ameitaka serikali kutumia vyombo vyake
vya dola kumtia mbaroni Bw. Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, aliyejitaja kuwa ndiye mmiliki wa Kampuni ya Dowans Holdings SA na kampuni tanzu ya Dowans Tanzania Limited.

Mbunge huyo amesema serikali inapaswa kuchukua hatua hiyo kwa madai kuwa mtu huyo alishakana kuhusika na kampuni hiyo wakati alipohojiwa kuhusu uhusiano wake na Dowans.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bw. Mnyika kwa vyombo vya habari jana, Bw. Al Adawi anapaswa kutiwa mbaroni kwa kuwa ametii kile alichosema katika tamko lake la Februari 16, mwaka huu la kutaka mmiliki wa mtambo huo ajitokeze.

Alisema katika tamko hilo aliitaka serikali itaifishe mitambo ya Dowans na kuiwasha kama sehemu ya kupunguza makali ya mgawo wa umeme na kuwataka wamiliki wake popote walipo duniani kujitokeza hadharani iwapo wana sababu za kuepusha mitambo yao isitaifishwe.

"Nilitarajia mmiliki wa Dowans ambaye angejitokeza angekiri hadharani kama wamedanganywa na kampuni ya Richmond na vyombo vingine katika kuhamishiwa mkataba ili kuweka msingi muhimu wa majadiliano, lakini imekuwa tofauti.

"Kutokana na hilo naomba kutoa rai kwa vyombo vya dola vimkamate vimpige picha na kumuhoji Al Adawi kwa mujibu wa sheria ya uhujumu uchumi na sheria nyinginezo kutokana na maelezo tata yaliyotolewa mpaka sasa kuhusiana na kampuni ya Dowans," alisema Bw. Mnyika katika taarifa yake.

Alidai kuwa kilichomshangaza ni kuwa siku chache baada ya tamko lake Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja, alinukuliwa na gazeti moja Februari 18 mwaka huu kuwa serikali haitataifisha mitambo hiyo kwa kuwa hiyo siyo sera ya CCM.

"Ikumbukwe kwamba katika gazeti la Mwanahalisi toleo namba 128 la Machi 2009 Al Adawi alikanusha kuwa yeye sio mmiliki wa Dowans kama alivyonukuliwa katika Mahojiano na KLHN.

Kama amekuwa akikanusha kuwa si mmiliki lakini sasa amejitokeza kuwa ndiye mmiliki kuna kila sababu ya vyombo vya dola kumuhoji zaidi," alisisitiza Bw. Mnyika

Alitaka vyombo vya dola vimuhoji Bw. Al Adawi kuhusu utata wa kampuni ya Dowans Holdings SA ambayo kumbukumbu zake kamili hazipo Costa Rica inapoelezwa kusajiliwa na kuwa na ofisi zake.

"Kwa kuwa sasa wanaotajwa kuwa wamiliki wa Dowans wameanza kujitokeza ni muhimu pia wamiliki wa kampuni ya Portek Systems and Equipment PTE Ltd ambayo inatajwa kumiliki hisa takribani 40% kwenye Dowans wakatajwa na wakajitokeza," alisisitiza.

Alirejea ushauri wake wa kuitaka serikali kuitaifisha mitambo ya Dowans na kuchukua hatua stahiki dhidi ya ukiukwaji wa sheria uliyojitokeza ili kuepusha kasoro zingine kujitokeza katika hatua za dharura zinazokusudiwa kuchukuliwa hivi sasa.

"Kutaifisha mitambo ya Dowans sio kutekeleza sera ya chama chochote, ni kuzingatia maslahi ya taifa na kusimamia utawala wa sheria ikiwemo sheria ya uhujumu uchumi,"alisisitiza Bw.Mnyika katika taarifa yake.

Mbali na Bw. Mnyika, baadhi ya wasomaji wa gazeti walikerwa na kitendo cha mfanyabiashara huyo kukataa kupigwa picha ili Watanzania waweze kumuona, isijekuwa aliyejitokeza ni mtu mwingine asiyehusika.

"Biashara ni matangazo kama ilivyo siasa. Wafanyabiashara na wanasiasa ni watu wanaopenda kupigwa picha na kujitangaza Watanzania, Huyu Al Adawi ni mfanyabiashara wa namna gani asiyependa kupigwa picha na kuonekana? Sisi tuna walakini na biashara yake," alisema Bw. Jerome John, mkazi wa Kigilagila.

Mkazi mwingine wa Ilala ambaye hakutaka kutaja jina lake, alionesha hasira kwa wanahabari kwa kushindwa kumlazimisha Bw. Al Adawi kumpiga picha au kutunmia mbinu za kipaparazi kunasa picha yake ili iweze kuonekana.

Katika hatua nyingine, suala la Kampuni ya Dowans limezidi kuwachanganya wabunge baada ya watumiaji wakubwa wa umeme kuhoji Kamati ya Nishati na Madini, sababu za kushindwa kuishauri serikali kutaifisha mitambo ya kampuni hiyo haraka kunusuru taifa.

Pia kamati hiyo ya bunge imetakiwa kujibu iwapo nchi haikufanya makosa kuingia katika mkataba na Dowans wakati bunge liliazimia kusitishwa kwa mkataba wa Richmond baada ya kubaini mapungufu kadhaa.

Katika kikao kilichofanyika Ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam jana kati ya Kamati hiyo ya Bunge na viongozi wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Baraza la Biashara la Taifa (TNB) na Mfuko wa Sekta Binafsi (TPSF) wadau hao walitaka kamati hiyo kuchukua hatua za haraka kunusuru uchumi wa nchi.

Vyanzo vyetu ndani ya kikao hicho vilieleza kuwa viongozi waandamizi wa taasisi hizo walionyesha wazi kukerwa na mjadala wa Dowans wakati nchi ikiwa katika hali ngumu ya umeme na kuitaka kamati hiyo kutoa majibu ya uhakika na kuweka siasa pembeni.

"Viongozi wa CTI, Bi. Esta Mkwizu, Bw. Arnold Kilewo na wale wa TPSF walituhoji ni kwa nini tunakazania tu kuzungumzia mitambo ya Dowans badala ya kuitaka serikali kununua mitambo yake.

Lakini kubwa zaidi walitaka mitambo ya Dowans itaifishwe haraka ili itumike kuzalisha umeme wa dharura kama mali ya nchi, walishangaa kwa nini nchi inapoteza mabilioni ya fedha bila sababu," kilisema chanzo chetu ndani ya kikao hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho viongozi hao wa wafanbiashara wakubwa ambao ndio watumiaji wakubwa wa umeme kwa asilimia 8,0 waliitaka kamati hiyo kueleza iwapo si kosa kwa nchi kuingia mkataba na Dowans wakati bunge iliazimia kuwa mkataba wa Richmond haukuwa halali.

Awali akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo yaliyojiri katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Januari Makamba alisema wadau hao walilalamikia ukosefu wa umeme na kwamba hali hiyo imelisababishia taifa hasara ya mabilioni ya fedha.

"Tatizo la umeme ni kubwa kiuchumi, kwa mfano Twiga Cement pekee licha ya kutumia jenereta bado wanapoteza karibu milioni 20 kwa siku.

Kama taifa tunapoteza karibu dola za Marekani 200,000 kwa siku kutokana na ukosefu wa umeme, hii ni hali mbaya sana, ndio maana tumelazimika kuzungumza kwanza na wadau kujua ukubwa wa tatizo kiuchumi," alisema Bw. Makamba.

Alisema katika kikao hicho ambacho kilikuwa bado haijafikia mwisho CTI waliweka wazi kuwa kati ya viwanda 280 vinavyomilikiwa na wanachama wake 50 wameshindwa kuendelea na uzalishaji na kusitisha kazi kwa muda kwa ukosefu wa umeme.

"Kama mnavyojua tunatakiwa kuanza vikao vyetu wiki mbili kabla ya bunge lakini tuliomba kibali maalumu kwa Spika kufanya vikao kutokana na ukubwa wa tatizo hili, leo (jana) tumekutana na wadau, kesho (leo) tutakutana na Wizara ya Nishati na Madini na kesho kutwa TANESCO.

"Pia Jumamosi tutaitisha public hearing (mdahalo wa wazi) pale Karimjee, tutaandaa vizuri ili tupate mawazo ya wadau kwa utaratibu mzuri," alisema Bw. Makamba.

Alisema Kamati hiyo itakutana na wadau wote wanaohusika na umeme wa gesi ili kutoa mapendekezo yatakayokidhi haja ya taifa kuondokana na adha ya sasa.

Alisema Kamati yake haijatoa mapendekezo yoyote kuhusu mitambo ya Dowans na kwamba kilichonukuliwa na vyombo vya habari yalikuwa maoni yake binafsi kabla ya kikao cha kamati hiyo.

"Kamati itatoa mapendezo yake kwa serikali Jumanne ijayo baada ya kumaliza kazi yake, kwa sasa tunaendelea na vikao ili kujua nini kinachotakiwa hasa kuokoa taifa letu na ukosefu wa umeme," alisema.

Alipoulizwa iwapo Kamati yake itamwita mtu aliyejitangaza kuwa mmiliki wa Dowans anayedaiwa kutua nchini juzi na kuzungumza na wahariri wa vyombo vya habari kwa sharti la kutopigwa picha alisema hawana sababu ya kufanya hivyo.

Hata hivyo alisema uamuzi wa serikali kutumia au kutotumia mtambo wa Dowans kuzalisha umeme wa dharura kwa sasa ni uamuzi tu na kwamba si jambo gumu na kufafanua kuwa kamati yake haiwezi kuishinikiza kufanya hivyo au kutofanya.

Alisema kabla ya kutoa mapendekezo yake kamati yake itafanya ziara kujionea hali halisi ya nishati hiyo katika vituo vyote vinavyozalisha umeme isipokuwa Mtera ambapo tayari wametembela.
 
Hili suala la Dowans linachanganya kadili muda unavyozidi kwenda. Mwanzoni issue ilikuwa ni uhalali wa mkataba wa Tanesco na Richmund uliopelekea assignment kwenda Dowans. Ni kweli palikuwa na matatizo mengi katika kutoa tenda kwa Richmund na assignment ya mkataba kwenda Dowans. Lakini kitu cha kujiuliza ni tatizo gani lililopelekea Serikali kutangaza tenda ya muwekezaji katika uzalishaji wa umeme? Ni kwa kiasi gani tatizo hilo liliondolewa au halikuondolewa kutokana na ufungaji wa mkataba na Richmund na hatimaye Dowans? Ni kwa kiasi gani Dowans hawakutekeleza au walitekeleza majukumu yao ya mkataba?

Ukiangalia kwa haraka ni kwamba dalili ya ukimeo wa Richmund kuweza kutekeleza majukumu ya kimkataba zilionekana toka mwanzo walivyoshindwa kuleta mitambo. Bahati mbaya Serikali walistuka mapema na kukataa kulipa hata senti hadi Richmund watakapofunga mitambo yao Tanzania na kuzalisha umeme. Richmund walipoona maji mazito na kabla mkataba wao haujavunjwa wakaassign mkataba wao kwa Dowans na Serikali ikaridhia. Ni ukweli ulio uchi kwamba taratibu za msingi za Sheria ya Ugavi hazikuzingatiwa kwa upande wa Serikali. Baada ya mkatba kurithiwa na Dowans na kabla Dowans hawajalipwa hata senti walifunga mitambo yao na kuzalisha umeme kwa mujibu wa mkataba. Tulitumia umeme wao kwa takribani miezi kumi na tatizo la kata umeme likamalizika. Baada ya tatizo la umeme kupungua na hali ya maji kuongezeka issue ya uhalali wa mkataba likajitokeza. Wataalamu na wanasiasa wakabaini utata juu ya uwepo wa Richmund na ukiukwaji wa taratibu za sheria, kwa upande wa Serikali, katika kukubali ufaulishaji wa mkataba kwa Dowans.
Fedha za Serikali zikatengwa watu wakaenda kuchunguza sio kama umeme haukuzalishwa au ulikuwa haukidhi matakwa ya mkataba bali ni kama Richmund ipo katika jalada la makampuni ya nchi husika. Wakati haya yanafanyika Richmund hawakuwa na mkatba wowote na Serikali NA uzalishaji wa umeme ulikuwa unaendelea. Nchi haikuwa gizani na viwanda vilikuwa vinaendelea kuzalishaji. Kwa upeo wangu mdogo wa kuelewa uwepo au kutokuwepo kwa Richmund kungetusaidia katika kuwachukulia hatua waliohusika na kuhakikisha tatizo kama hilo halirudiwi tena. Ni hivyo hivyo kwa matatizo katika mkataba wa Dowans.

Sasa baadae tukaamua kuvunja mkataba wa Dowans bila kutathimini faida na hasara zake. Matokeo yake tumeishia kutakiwa kulipa fidia ya mabilioni ya fedha. Hatimaye issue sasa inakuwa ni makosa tuliyofanya katika kuvunja mkataba. Bahati nzuri kuna wananchi kwa mapenzi yao na uchungu wao na nchi wameamua kulipinga suala hili mahakamani. Uamuzi bado haujatolewa. Kama ikitokea tukashindwa na kutakiwa kulipa kuna uwezekano matashi ya kisiasa yakatutaka tusilipe. Tusipolipa tukapata matatizo makubwa zaidi huko mbele ya safari issue itakuwa kwa nini Serikali haikufikiria vizuri na kuona umhimu wa kulipa?

Kwa hali hiyo mimi naona kuna umhimu sana wa kuweka mipaka kati ya siasa na utendaji, siasa na utaalamu na mambo mengine. Vinginevyo huko mbele hata masuala ya kitaalamu kama kitabibu yataamuliwa kisiasa. Sijui matokeo yake yatakuwa nini?
 
Back
Top Bottom