Mjadala wa DOWANS ITV waibua mapya!

Anafagilia sana hapa ,halafu kumbe yeye na Kibanda walienda Uswisi kupinga mkataba wa City Water,hawa ni mashujaa wa ukweli na wanakamua kizalendo kweli kweli
 
Kumbe Sitta ana hoja kubwa katika suala la Dowans.ITV walimweka hapa atoe maoni yake.kweli serikali ya jk ina hitajika kuflash out kabisa.Kumbe kina Rostam ndio wanaolipwa?
 
Wandugu,
Kama kawaida yake, Bw. Mkinga ametamka waziwazi bila woga kwenye Kipindi cha Kipima Joto ITV kuwa wamiliki wa Dowans watakaofaidi mabilioni ni Rostam, Karamagi, Msabaha Chenge.

Namimi nipo naangalia kweli nchi hii imekamatwa na viwaji jeshi, nafikiri hata ngeleja yuko ndani maana yeye ni kijana wa Rostam Aziz asilimia 100%.

JK avunje baraza la mawaziri, ama sivyo sina uhakika kama ataweza kutawala nchi, yaani karibu machoni yanitoke
 
watanzania tunaibiwa. tuamkeni, nchi imeishauzwa--wake up Tanzania and fight for your country
 
Wangewaalika wafuatao:

1. Sitta
2. Rostam
3. Werema
4. Mwakyembe
5. Ngeleja
6. Mwanasheria wa Tanesco
7. Karamagi
Sita na mwakiembe wana wanukuu katika vyombo mbalimbali. Duh mjadala ni mkali sana na nimeupenda. Jaman JK na Ngeleja wanauona na wanajisikiaje?!!!
 
mie nimezima tv ctak kusikia huo usenge inauma tunaonekana wote ni vichaa na wajinga sitta ameongea ukweli
 
Ni rais asiye na hekima ndiye anayeweza kuendelea na baraza la mawaziri lenye misimamo tofauti kuhusu suala zito kama la Dowans.
 
Hawa Wote Ni wafadhili wa CCM ndiyo maana wanataka kujilipa zile fedha walizokodisha helikopa za kupigia kampeni ingawa baada ya kushindwa walichakachua matokeo.
 
Wameruhusu kutoa maoni, haya MMJJ ulitaka nafasi ya kutoa maoni, hiyo hapo. Wape taarifa za viinzi vyako mana ile ni noma.
 
sita na mwakiembe wana wanukuu katika vyombo mbalimbali. Duh mjadala ni mkali sana na nimeupenda. Jaman jk na ngeleja wanauona na wanajisikiaje?!!!


ngeleja allialikwa ila sekretary wake amesema yuko china
 
Kikwete ajiuzulu uitishwe Uchaguzi mpya. Mbona Tunisia wamachinga wamemwondoa rais madarakani kwa kumnyanyasa muuza genge. Matatizo yote haya hayatoshi kumuondoa JK madarakani
 
Jamani kwa wale wenye uwezo wakurecord huu mdahalo wafanye hivyo tafadhali... Hii itatusaidia uko mbeleni.
 
Uwiiiii Lowassa katajwa .......huu mjadala babu kubwa...........Moven Peak imegeuka Paris!!!!
 
Jamaa wa ITV anaogopa mafisadi wakitajwa majina anasema hawana evidence!! Mafisadi wanatishae?
 
Haaaa wadau ,majaji wote wa ICC waliotoa TUZO kwa DOWANS walikaa MOVEN PICK NA kutoa Tuzo HII JAMANI TUNALIWA


ANGALIA ITV UPATE UKWELI
 
kumbe kesi ya DOWANS ilifanyika movenpick dar!mwanasheria mkuu kasema-duu hapo nimechoka kabisa huu ni wizi wa mchana wa unyanganyi kwa kutumia silaha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom