Mjadala kuhusu live messenger

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Miaka kadhaa iliyopita wengi wetu haswa vijana tulikuwa tunapenda kuwasiliana na ndugu jamaa au rafiki zetu moja kwa moja kwa njia ya chat ilikuwa ni kawaida sana kukuta watu wengi wamejikusanya katika internet café makazini na mashuleni kwa ajili ya kuchat na rafiki zao , wakati huo wengi walikuwa wanatumia huduma ya messenger toka yahoo , hotmail ambayo yake ilikuwa inaitwa zaidi msn , icq ambayo ilikuwa inauwezo wa kumwezesha mtu kutumia account zaidi ya moja kwa wakati mmoja wakati anachat mfano ukiwa na msn pamoja na yahoo basi unaweza kutumia ICQ kwa account zote hizo

Muda ukaenda haswa wakati kampuni ya google ilivyoshika kasi katika masuala haya ya mitandao kwanza google walikuwa na google talk messenger halafu ikaja messenger ambayo iko ndani ya sanduku lako la barua pepe moja kwa moja kwa sababu huduma hii ilikuwa rahisi sana na watu wengi waliipenda kwa sasa kampuni nyingi zinazotoa huduma za mawasiliano ya moja kwa moja ya chat wamehamia huko kuanzia na kampuni ya yahoo .

Hatukupata muda wa kujadili suala hili haswa kwa lugha ya Kiswahili , nimeona huduma hii na nimekuwa nikiitumia kwa miezi kadhaa toka zilipoanza ingawa kwa siku hizi ninakazi nyingi sio mpenzi wa kuchat kama zamani , kama unavyojua ujio wa huduma hii wengi wamefurahia kwa sababu umerahisisha mambo mengi lakini tuangalie yale machache .

Pindi unapoingia katika inbox yako huduma hii nayo huwa inaanza hapo moja kwa moja mpaka pale utakapoamua uisitishe tofauti na ile messenger ya kwanza ambayo ilikuwa mpaka uchague vitu kadhaa ili iweze kusign in moja kwa moja , moja ya taifa zake moja ni suala la password ambazo huwa zinasahauliwe kwenye computer

Siku hizi kumeibuka wimbi kubwa la programu ambazo zinaweza kutafuta password katika computer ambazo mtu aliwahi kutumia login katika account haswa messenger , programu hizi haziwezi kurecover password ambayo inatumika kuingilia katika sanduku la barua pepe ya mtu haswa katika mihahawa ya internet labda huko mbeleni ila sio kwa sasa .

Pia kwa siku za karibuni kumetokea wimbi kubwa la virus kadhaa kushambulia programu za kuchat , au kubandika matangazo ambayo mtumiaji hapendi yawe hapo yaani kilazima , pindi unapologin na kutumia aina mpya ya chat hiyo wale virus hawataweza kushambulia tena .
Kitu ambacho kinaweze kutokea huko mbeleni ni kwa wahalifu ambao wanatengeneza kurasa bandia za tovuti mbali mbali , wanaweza kutengeneza chat bandia za tovuti hizo hizo ili mtu aweze kujiingiza mwenyewe na kuweka baadhi ya siri zake bila ya yeye mwenyewe kujua .

Kama unavyojua antivirus nyingi zenye huduma ya kuangalia kama kurasa unayoangalia ni bandia au la zenyewe huwa zinafanya kazi zaidi unapotumia search engine kutafuta kitu ndio hapo inaweza kukuambia lakini linapokuja suala la kuingiliwa kama hivi ninavyotabiri inawezekana wengi wakaingia mtegoni kama watakuwa wanategemea antivirus kwa ajili ya kutambua kama kurasa ni yenyewe au la .

Kinachoweza kufanyika huko mbeleni ni wataalamu wa antivirus pamoja na waendelezaji wa tovuti kuwa na tekinologia zinazoweza kutambua kwa urahisi uhalifu wa aina hii ili kuingiza katika programu zao zingine kama inavyofanyika kwa sasa suala hili linahitaji mjadala wa ndani zaidi haswa kwa wadau wa ulinzi na usalama wa mitandao .

Kitu kingine ambacho nimeona ni suala ya kuweza kufuatilia mtu unayeongea nae yuko wapi haswa , anapotumia huduma hii ya chat , ni ngumu kuanzia kutrace baadhi ya anuani za mtu unayewasiliana nae papo kwa hapo , tofauti na zamani ambapo ilikuwa unaweza fanya hivyo katika messenger .

Kampuni nyingi sana zinazohusiana na matangazo katika mitandao inabidi sasa zibadili mbinu za kutangaza bidhaa zao kwa njia ya messenger ,pindi mtindo huu ukizoeleka na ukaweza kufanya kazi tu , inawezekana kampuni za matangazo kwenye messenger zikakosa soko au kulazimika kubadilisha baadhi ya mikataba yao ya matangazo ambayo itaendana na kile ambacho mtumiaji anataka .
 
Back
Top Bottom