Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

hii dawa nami naiamini kwa kiasi fulani lakini hili suala la ushahidi linaleta utata. Ofisini kwetu kuna mtu ana sukari/hiv lakini tangia arejee kutoka Loliondo ni zaidi ya majuma mawili lakini hatwambii lolote!

hilo ndo tatizo. Tunahitaji ushahidi pleeees!
 
mzee wa upako nae nimemsoma kwenye gazeti la jioni hii Dar Leo nae kaanzisha yake,anasema ni kiboko kuliko ya babu.
Swali: walikuwa wapi siku zote?
 
Mbona waathirika wengi wa HIV,na kisukari wameshashuhudia ktk media,ikiwemo njia panda ya radio clouds.Mnatakani nyie tena
 
Dawa zisizo za kimagharibi ( za viwandani) nyingi siyo 'holistic' ndiyo maana hawaielewi dawa ya Babu wa Loliondo. Maana ya dawa 'holistic' ni kwamba inamlenga mnywaji wa kikombe cha Babu kuwa anapona mvumo mzima wa mwili wake kukabiliana na magonjwa sugu ikiwemo na akili yake.

Au kwa maneno mengine dawa ya Babu wa Loliondo ni ya kuustua mfumo wa mwili wa mhitaji wa kikombe kuweza kukabiliana na kutokomeza magonjwa mwilini mwake kwa msaada wa mizizi iliyobarikiwa na Mungu.

Wakati dawa za 'kizungu-kimagharibi' hulenga kuponyesha gonjwa moja mfano dawa ya malaria ni kwa ajili ya 'kutokomeza vimelea vya malaria' tu na siyo kuusaidia mfumo wa mwili wa 'mgonjwa' kutokomeza gonjwa au magonjwa yanayomnyemelea mgonjwa. Dawa za Kichina, Kihindi, Kiarabu na Kiafrika ni 'holistic' tofauti na dawa za 'kisomi-sayansi' za Kizungu.
 
Pole sana kiongozi kwa tukio hili.

Aidha may your beloved relative RIP!

Dawa ya babu imethibitishwa na serikali(KWA TAARIFA ZA LEO) kuwa haina madhara yoyote kwa binmadamu!

Hivyo naomba muwe na amani kabisa, na kuamini kuwa ndugu yenu alikuwa amefikwa na siku yake ya umauti.

Zaidi sana kuna factor ya uchovu wa aina yake hasa kutokana na Jiografia ya mahala kule, pamoja na umbali, ambavyo vinaweza kusababisha mtu akadeteriorate, hasa kama tayari ana afya mbaya!

Zaidi sana huenda Mungu ameamua kumpumzisha kwa namna hiyo kutokaNA NA MATESO MAKALI YA bREAST cANCER ALIYOKUWA NAYO!;

Nawapa pole tena broda!
 
Kwa wanajamii wote, naomba kutoa ushuhuda kuwa nilimpeleka mgonjwa wangu mke wa rafiki yangu mpenzi kwa Babu wiki mbili zilizopita ili kupata dawa kutokana na maradhi ya Breast cancer ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Kama sote tunavyojua hakuna dawa ya kutibu kansa, lakini baada ya kusikia habari za Babu tulijenga imani kuwa huenda akapona. Tulimpeleka huko, na baada ya kukaa siku mbili kwenye foleni alibahatika kupata dawa na kuinywa. Lakini toka anywe hiyo dawa hali yake imekuwa sio nzuri na kudhoofu siku hadi siku hadi hii leo saa nne asubuhi amefariki dunia. Ninatoa ushuhuda huu si kwa kuwakatisha tamaa watu la hasha bali ni kutaka kuweka vitu hadharani ili watu wajue kuwa pamoja na kuwa huenda dawa hiyo ikawatibu baadhi ya watu lakini watu tujue pia hakuna dawa ya kuponya kifo. Huenda kweli babu anatibu kwa imani, lakini sidhani kama wale wote wanaoenda huko hawana imani. Namalizia kwa kuzidi kuwaomba waliotibiwa na kupona kweli wajitokeze watuthibitishie kwa ushahidi wa kitabibu.


Pole sana Kaka... Sisi tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi;
Back to the Topic:
Wapo waliokwenda na Matatizo kama hayo ya cancer, Baada ya Kunywa wamepona na hai zao zinaendelea Vizuri.
Yupo mama aliyekuwa na Cancer ya mapafu anaendelea vizuri alikuwa hatembei lakini Last Saturday Tarehe 26/03 majira ya saa 12 jioni aliweza kutoka nje hadi nyumba ya Jirani ni umbali wa mita 18.

Ninachoamini kuhusu huyo Shemeji yako kama ilivyo kwa wengine waliotutoka wakiwa huko Loliondo kwenye kikombe ni kuwa siku zilifika na hakukuwa na jinsi, tuamini wakati mwingine death can occur in very different ways and reason!!

Pole sana kaka..... Shemeji ametutangulia Mbele za haki.
 
Kwa wanajamii wote, naomba kutoa ushuhuda kuwa nilimpeleka mgonjwa wangu mke wa rafiki yangu mpenzi kwa Babu wiki mbili zilizopita ili kupata dawa kutokana na maradhi ya Breast cancer ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Kama sote tunavyojua hakuna dawa ya kutibu kansa, lakini baada ya kusikia habari za Babu tulijenga imani kuwa huenda akapona. Tulimpeleka huko, na baada ya kukaa siku mbili kwenye foleni alibahatika kupata dawa na kuinywa. Lakini toka anywe hiyo dawa hali yake imekuwa sio nzuri na kudhoofu siku hadi siku hadi hii leo saa nne asubuhi amefariki dunia. Ninatoa ushuhuda huu si kwa kuwakatisha tamaa watu la hasha bali ni kutaka kuweka vitu hadharani ili watu wajue kuwa pamoja na kuwa huenda dawa hiyo ikawatibu baadhi ya watu lakini watu tujue pia hakuna dawa ya kuponya kifo. Huenda kweli babu anatibu kwa imani, lakini sidhani kama wale wote wanaoenda huko hawana imani. Namalizia kwa kuzidi kuwaomba waliotibiwa na kupona kweli wajitokeze watuthibitishie kwa ushahidi wa kitabibu.

Poleni kwa msiba. Kwanza nisahishe kuwa si kweli kuwa hakuna dawa ya cancer. Pili kwa kukusaidia wewe kama mtoa mada kwqa ufahamu zaidi ni kuwa mchungaji Mwasapile huko loliondo atoi dawa za kuzuia kifo bali dawa ya maradhi. Pili maji anayotoa mchungaji ni kitendo cha imani. Kwa hivyo kwa wale wote wanokwenda pale huku mioyoni mwao wana mashaka kibao kuwa haitafanya kazi basi watarajie kuwa hitafanya kazi kwao.

Shuhuda kuwa watu wanapona au la ni nyingi tu fanya homework yako vizuri utafahamu. Labda nisisitize kuwa kwa mchungaji Mwasapile si hospitali hivyo mijadala ya kisayansi dhidi ya kazi zake si mahali pake (kama hufahamu ni kwamba science haina majibu ya kila kitu hususani uhai wa mwanadamu). Kuna wengine wanazungumzia side effects na kusahau kuwa wako pale kutoka na side effects za lifestyle zao!
 
...Kwenye ugonjwa wowote sugu, hasa amabo hauna tiba kukata tamaa ni sehemu ya mchakato wa ugonjwa wenyewe kuelekea kifo. Sioni ajabu watu kwenda kwa babu; kwasababu elimu na maarifa yaliyopo yanatufundisha hivyo. Ninacho sikitika ni kuwa serikali yetu imejivika upofu na kuacha wananchi wakiteseka na kuungana na huyu Babu (ambaye naamini anaumwa pia! NDIYO; afya ya akili ya Babu inahitaji kuangaliwa). Tunadangaya watu kuwa tiba yenyewe ni ya bei nafuu shs mia tano (a.k.a kikombe) wakati tunaona kila siku kuwa nauli ya kufika huko inaanzia shs 30,000 Fuso, 85000 - 150, 000/= Land cruiser na USD 1000 - 3000USD Helikopta. Hivi hatuoni kuwa wananchi wanaibiwa kwa jina la huyu BABU? Serikali ieleze ukweli, Hakuna mtu aliyekuwa treated & cured UKIMWI,CANCER, KISUKARI N.K Kinyume wako wengi wanaokufa am kurudishwa mahospitalini wakiwa na hali mbaya, Hasa wa Kisukari(hasa hasa waliokuwa wanachoma sindano za Insulin).

Najua baadhi yetu tumepeleka ndugu zenu, jamaa na pengine mmeenda wenyewe, najua kuna watu wameteseka na magonjwa na habari za babu ziliwarejeshea matumaini, Poleni sana. Lakini naumia pia kuona UKWELI unabanwa na kunyimwa nafasi hasa na watu wanaopata faida za kibiashara na wengine tunashabikia bila kutaka kuangalia madhara ya hili jambo.
 
Mti aina ya carissa ambao babu anautumia kama dawa aliyooteshwa na Mungu kutibu magonjwa sugu imethibitika kuwa imetumika miaka mingi kama tiba ya magonjwa sugu kama cacer, vidonda vya tumbo, magonjwa ya zinaa, shinikizo la damu na moyo. Suali kuwa babu hata darasa moja hajapitia nani amemwonyesha dawa hiyo kama si Mungu? Tuache kejeli na dharau kwa sababu tu ya uvivu wa kufikiri na kujifunza ama kutafuta ukweli. Angalia attachment ama mtu yeyote achapishe carissa tree and medication kwenye search engine yeyote aone.
 

Attachments

  • Carissa edulis-2.pdf
    48.9 KB · Views: 158
  • Carissa edulis-3.pdf
    45.7 KB · Views: 166
Source : Michuzi Blog : Hii atiko nimeinyaka huko kwa misupu, imenigusa kidogo, hebu tujadilini loliondo​


LOLIONDO; PROGRESS OR A CONFUSED, DESPARATE & HOPELESS SOCIETY? …DEBATE..By John Mashaka

I read with lot of interest Mr. Maggid Mujengwa's article entitled "Ya Loliondo Na Umma Ulio gizani", a philosophical description of a confused society. Mr. Mujengwa depicted Tanzania as a nation that is using a flashlight in a broad day light with a notion that, perhaps, it could aid her see better. Figuratively or philosophically speaking, Socrates the philosopher used this metaphor to describe a hopeless and a confused society. One question Mr. Mujengwa failed to address was the root cause of this confusion. How could Tanzanians be convinced that, flashlight is brighter than the sun? Is it because of ignorance, confusion or desperation?

Plato, one of the greatest philosophers to have ever lived, strongly advocated in favor of an examined life; An examination of one's life addresses fundamental questions such as: who am I, what do I want to do with my life, how will I know whether I have achieved my goals, what matters to me; wisdom; a feeling of accomplishment; wealth, power; social change or pleasure and how will I balance them. If you haven't asked yourself these questions, then life becomes meaningless. You become more like a boat in turbulent high seas without compass direction, going along with the tides and currents of the ocean. A boat that is destined for a clear tragic end of capsizing, Tanzania that is.

Tanzanians are not in control of their lives. Instead, they are controlled by the events of the day, and ignorantly perceiving flashlight to be more powerful than the sun, based on Socrates account on ignorance. As a nation, Tanzania has not asked itself these basic questions, because social-economic, hopelessness and despair amongst her people speak for itself. A sea of humanity flooding Loliondo, is a confirmation of the broken system. Her sick hopping from their hospital beds, carried in stretchers, just to have a sip of the wonder concoction is very troubling. This signifies the dying or non-existing healthcare system in Tanzania. Tanzania does not know where it is headed; it is a lost vessel sailing in the turbulent high seas without a direction, and only waiting to capsize

I must slightly differ with Mr. Mujengwa, based on my strong conviction, that, Babu Mwasapile's patients are not uninformed, but rather hopeless, desperate, CONFUSED and poverty burdened men and women from all walks of life. Loliondo list of visitors is made up of the mighty and the powerful, the rich, the poor, scientists and herdsmen; famous and the little known peasants. Babu has received people who have made their way by selling their few worldly possessions, as well as the flamboyant tycoons arriving in style; in their private aircrafts, all with one goal; drinking the magical mixture, with hope ridding themselves of their excruciating illnesses. This is a national embarrassment, and depiction of Tanzania as a primitive and backward country in the eyes of the world

We are not talking about dumb, stupid, or simple-minded people; we are talking of brilliant and well educated individuals serving in the government, International, private and public agencies. We are talking of people who have been humbled by illnesses, and like anybody else, must heed the need to find treatment by standing in a long queue in the middle of nowhere; away from their posh homes, and comfort of their beds to find cure from the miraculous drink. We are talking of a hopeless and a desperate society on edge.

Desperation has no class, it has no social status or identity, it has no color or creed. It affects PhD holders and the illiterate alike. We must remember that, desperate and hopeless men do not value life; they have no shame or fear. Tell a man, who has exhausted all options to get rid of cancer, that his urine is the only cure to his excruciating illness. Even a King who desperately wants to live will heed the advice. These are the people flanking Babu of Loliondo's compound trying to get rid themselves of terminal illnesses, endless pain, and misery.

Babu of Loliondo could not have emerged at a perfect time for the hopeless, when divine intervention is direly needed to save their souls. Babu has exposed our desperation, vulnerability and weakness as a society. He has exposed how useless education can be in the face of human despair. He has exposed how far we are lost in the turbulent high seas, and only going with the tide and flow. We are lost. Just like DECI which was a product of greed, ignorance and despair, Babu Liliondo's purported magic cup is nothing but a tragic health and social a time bomb yet to explode!

MUNGU IBARIKI TANZANIA

John Mashaka
mashaka.john@yahoo.com
 
Mti aina ya carissa ambao babu anautumia kama dawa aliyooteshwa na Mungu kutibu magonjwa sugu imethibitika kuwa imetumika miaka mingi kama tiba ya magonjwa sugu kama cacer, vidonda vya tumbo, magonjwa ya zinaa, shinikizo la damu na moyo. Suali kuwa babu hata darasa moja hajapitia nani amemwonyesha dawa hiyo kama si Mungu? Tuache kejeli na dharau kwa sababu tu ya uvivu wa kufikiri na kujifunza ama kutafuta ukweli. Angalia attachment ama mtu yeyote achapishe carissa tree and medication kwenye search engine yeyote aone.

Unajichanganya wewe....hapo penye red maelezo yako yanaonyesha kuwa hiyo dawa ni ya muda mrefu..sasa kwanini babu anasema ukiitumia mwenyewe kama ajakupa yeye huponi......?
 
Babu asiusishwe na maelezo hapo juu, kwa sababu dawa ya kikombe cha BABU alishasema wakipima hawataona hizo ingredient zilizotajwa! Mbona tusingekuwa na foleni Loliondo tena, manake akina Mama yoyo wengekuwa na hiyo mizizi pale Kariakoo.

Lakini ngoja tuendelee kusubiri Mganga mkuu wa serikali akitoka abroad wizara itatutangazia wamekuta nini katika hiyo dawa ya Babu!
 
Mti aina ya carissa ambao babu anautumia kama dawa aliyooteshwa na Mungu kutibu magonjwa sugu imethibitika kuwa imetumika miaka mingi kama tiba ya magonjwa sugu kama cacer, vidonda vya tumbo, magonjwa ya zinaa, shinikizo la damu na moyo. Suali kuwa babu hata darasa moja hajapitia nani amemwonyesha dawa hiyo kama si Mungu? Tuache kejeli na dharau kwa sababu tu ya uvivu wa kufikiri na kujifunza ama kutafuta ukweli. Angalia attachment ama mtu yeyote achapishe carissa tree and medication kwenye search engine yeyote aone.

Hivi hapo pekundu ni kweli?
 
Hivi hapo pekundu ni kweli?

Huyu mleta hoja ni mpotoshaji Mkubwa sana Huyu mzee alikuwa mchungaji anasema hajaenda hata darasa moja? Mi ninavyojua wachungaji na mapadri huwezi kuwa bila shule, labda kajisahau kadhani huku kwetu Mskitini hawaitaji elimu Imamu unakuta hata kusoma na kuandika hajui.
 
Hata Kinjeketile Ngwale, alidai kaoteshwa na Mungu, awape wapiganaji wake maji yaliyo changanywa na Mbegu za Mbarika na Mtama Kuzuiya risasi za mjerumani... Kilicho tokea kila mtu anakijuwa.
 
Watu walitajirika sana hasa wenye biashara za magari ! nini kilisababisha hadi watu wakawa wanasema wamepona ? binafsi mtu ninaemjua alienda kwa babu wa loliondo alivyorudi hakuchukua mwaka alikata kamba...Imani hii jamani!
 
Back
Top Bottom