Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

kwanza kwa wote mliochangia hii post nawaomba niwagongee senksi,kwa sababu ile kitufe cha kubofya senksi hakionekani kwangu.
Pili kuna nyumba (flat) ni mpya vya vyumba vitatu inauzwa kwa milioni 53 hapa Tanga.Naomba wadau mniambie ni deal nzuri kununua au ni vizuri kujenga mwenyewe kwa hapa Tanga?asanteni.

Kama hizo nyumba mpya ni mgogoro hapo Tanga nikuunganishe ununua ya zamani Kisosora ufanye marekebisho kisha tandika jamvi na wazee mnywe kahawa.
 
Mkuu Amoeba ramani nzuri sana na inavutia, lakini kujenga nyumba hiyo inabidi uajiriwe BOT au TRA na ufanye kamchezo ka EPA, na kujitayarisha kwenda Kisutu kwa miaka 2 mfululizo.

Si kweli mkuu, maisha mazuri ni mipango mizuri, bidii na kujinyima tu. Halafu vilevile usitishwe na hesabu za wadau humu ndani, unaweza kuwa na altenative ukajenga kwa gharama nafuu tu.

Kuna kajengo ambako nimefanya kama kijihotel flani uchwara mkuu, ramani yake ni balaa haswa, nikiweka hapa nitakuwa naexspose ID, lakn nilichofanya ni kuchukua ramani yangu, nikatafuta constructor wa kkusuka foundation, kkunyanyua beams na kazi zote za zege, mkataba wake ukaishia hapo. Nikanunua tofali za kuchoma,Nikatafuta mason mzuri akapandisha kuta kwa bei nafuu sana, nikatafuta vijana wengine wa roofing kwa robo tu ya bei ya constructor, Jengo likawa limesimama, Nikatafuta interior designer kwa ajili ya ushauri tu lakini kazi halisi nikachukkua vijana wa wanaofanya kazi kwenye makampuni ya ujenzi wakafanya kazi zote zilizobaki.

Mpaka nafungua sehem hiyo nimeweka mpaka vitanda na gadgets zingine daftari linasoma chini ya M650! (10 executive rooms+a descent restaurant, bar & kitchen !).

Ninachotaka kusema ni kwamba, kazi ukiizoea kiasi unaweza kujua fundi mzuri nampata wapi na kwa bei gani, pia unapunguza kuibiwa na mafundi ukkiwa karibu nao wakati wote wa ujenzi.

Ukigawa project yako katika smaller projects unapunguza gharama hapa kwetu bongo.
 
Wow! Hii ndo nyumba haasaa. Wabeja wang'wa baba. Manyusi hii nyumba ya kwenye post ya 44 ya Amobea naweza kuijenga kwa 110M? Nimeipenda kwelikweli maana inawakawaka hasaaaaaaaaaa.

Wabheja chene ngalu, bhaghishage gukaya.
 
Si kweli mkuu, maisha mazuri ni mipango mizuri, bidii na kujinyima tu. Halafu vilevile usitishwe na hesabu za wadau humu ndani, unaweza kuwa na altenative ukajenga kwa gharama nafuu tu. Kuna kajengo ambako nimefanya kama kijihotel flani uchwara mkuu, ramani yake ni balaa haswa, nikiweka hapa nitakuwa naexspose ID, lakn nilichofanya ni kuchukua ramani yangu, nikatafuta constructor wa kkusuka foundation, kkunyanyua beams na kazi zote za zege, mkataba wake ukaishia hapo. Nikanunua tofali za kuchoma,Nikatafuta mason mzuri akapandisha kuta kwa bei nafuu sana, nikatafuta vijana wengine wa roofing kwa robo tu ya bei ya constructor, Jengo likawa limesimama, Nikatafuta interior designer kwa ajili ya ushauri tu lakini kazi halisi nikachukkua vijana wa wanaofanya kazi kwenye makampuni ya ujenzi wakafanya kazi zote zilizobaki. Mpaka nafungua sehem hiyo nimeweka mpaka vitanda na gadgets zingine daftari linasoma chini ya M650! (10 executive rooms+a descent restaurant, bar & kitchen !). Nachotaka kusema ni kwamba, kazi ukiizoea kiasi unaweza kujua fundi mzuri nampata wapi na kwa bei gani, pia unapunguza kuibiwa na mafundi ukkiwa karibu nao wakati wote wa ujenzi. Ukigawa project yako katika smaller projects unapunguza gharama hapa kwetu bongo.

Safi sana Mkuu, ningeomba unipatie anwani ya hawa Interior designers.
 
Wow! Hii ndo nyumba haasaa. Wabeja wang'wa baba. Manyusi hii nyumba ya kwenye post ya 44 ya Amobea naweza kuijenga kwa 110M? Nimeipenda kwelikweli maana inawakawaka hasaaaaaaaaaa.
Mkuu, hako kajumba mbona hakana mvuto kabisa mkuu? Hebu angalia hiiView attachment 14386 kwa gharama hiyo hiyo
View attachment 14384View attachment 14385View attachment 14386

...khaaa! Amoeba kajumba kazuri sana haka. Mpaka ufikie kujenga kajumba haka lazima nawe EPA iwe imekukalia vizuri, Mfano; hizo location za Bathroom na gharama za plumbing (incl drainage & sewarage system) lazima kichwa kiingie akili.
Safi sana.
 
Hapo sijakusoma mkuu, au ni msemo mpya?
 
Hii estimate ni sahihi??!. Stucture yangu ni 10x11=110sqm. X500,000=55000000. This isn't realistick in a tz context. Mimi nimejenga kwa 15mil tu. Kama hizo ndo estimate mnazofanya kwenye miradi ya serikali ndo maana hatuendelei.

Tuko pamoja mkubwa ukipata muda na kusimamia mwenyewe au mtu unae muamini Vyumba vitatu vya kulala, sebule na other rooms ka za choo,bafu etc gharama yaweza kuwa ndogo around 20m unahamia kwako ndani ya miezi michache tu. Hao wa 100m, 200m and abovu ni wakinga na wachaga wanaokwepa ushuru kariakoo na mafisadi wa TZ sie watumishi wasafi wa Serikali na vimshahara mbuzi we have to use common sense.
 
Dah mkuu umejenga hadi hatua gani??? Umefanya finishing zote???
Finishings na fittings zinatofautisha sana gharama za ujenzi....nyumba mbili za aina moja na zikijengwa eneo moja zaweza kugharimu bei tofauti sana.......ila million 15 kwa mita za mraba 110 sio realistic kwa sasa....

tuacheni kudanganyana hapa ... mfanyakazi gani wa kawaida (awe wa serikali au binafsi) mwenye uwezo wa kujenga nyumba ya mil 100+?? Labda ni makatibu wakuu na wakuregenzi tena kwa kupata mikopo ya riba nafuu benki!! vinginevyo ni wizi ndo utakufanya upate mil 100+ za kujengea nyumba! tunafurahisha baraza kwa kusema nyumba za m15+ sio realistic wakati wengi humu tumepanga kwenye nyumba za namna hiyo na wengine wazazi wetu walijenga nyumba za namna hiyo na tumekulia humo tukiwa angalau part ya middle-class families. No wonder nchi yetu inaibiwa sana kwa wanaojiita professionals ..... mfano mdogo ... barabara ya 1km inagharimu 2.5 bil - 10 bil?? nyumba ya gavana wa benki ... 1 bil?? Kwa kweli .... ni wizi tu!! Mungu atusamehe!!
 
I hope Guantanamo, you have gotten an answer and thank you for contributing such a open end question. I have learned a lot.
Wakuu asanteni. nimenufaika na discussion yetu.
 
tuacheni kudanganyana hapa ... mfanyakazi gani wa kawaida (awe wa serikali au binafsi) mwenye uwezo wa kujenga nyumba ya mil 100+?? Labda ni makatibu wakuu na wakuregenzi tena kwa kupata mikopo ya riba nafuu benki!! vinginevyo ni wizi ndo utakufanya upate mil 100+ za kujengea nyumba! tunafurahisha baraza kwa kusema nyumba za m15+ sio realistic wakati wengi humu tumepanga kwenye nyumba za namna hiyo na wengine wazazi wetu walijenga nyumba za namna hiyo na tumekulia humo tukiwa angalau part ya middle-class families. No wonder nchi yetu inaibiwa sana kwa wanaojiita professionals ..... mfano mdogo ... barabara ya 1km inagharimu 2.5 bil - 10 bil?? nyumba ya gavana wa benki ... 1 bil?? Kwa kweli .... ni wizi tu!! Mungu atusamehe!!

Hapa nadhani ishu kubwa ni aina na kiwango cha nyumba. Ni kweli unaweza kujenga nyumba kwa mil 15 au chini ya hapo lakini swali ni ya kiwango gani? Actually huko vijijini watu wanajenga 'nyumba' kwa hata laki moja tu (ya miti na udongo, juu nyasi, nk ambavyo almost vyote anavipata bure tu) anachohitaji ni nguvu zake mwenyewe au kwa kushirikiana na ndugu na jamaa (hiyo laki moja ni ya kunuua mabaki ya ya madebe kwa ajili ya milango na madirisha na pombe ya watu kunywa wakati wakifanya kazi!).
 
tuacheni kudanganyana hapa ... mfanyakazi gani wa kawaida (awe wa serikali au binafsi) mwenye uwezo wa kujenga nyumba ya mil 100+?? Labda ni makatibu wakuu na wakuregenzi tena kwa kupata mikopo ya riba nafuu benki!! vinginevyo ni wizi ndo utakufanya upate mil 100+ za kujengea nyumba! tunafurahisha baraza kwa kusema nyumba za m15+ sio realistic wakati wengi humu tumepanga kwenye nyumba za namna hiyo na wengine wazazi wetu walijenga nyumba za namna hiyo na tumekulia humo tukiwa angalau part ya middle-class families. No wonder nchi yetu inaibiwa sana kwa wanaojiita professionals ..... mfano mdogo ... barabara ya 1km inagharimu 2.5 bil - 10 bil?? nyumba ya gavana wa benki ... 1 bil?? Kwa kweli .... ni wizi tu!! Mungu atusamehe!!
Duh inategemeana na ufanyaji kazi wako mheshimiwa. Milioni 100 unapata kabisa kwenye mshahara + consultancy tena bila kuiba. Kwani hawapo watu wanaolipwa 3 mil na si wakurugenzi???
 
Hakuna mtu anayesema kuwa lazima ujenge nyumba ya milioni 100. Makosa ambayo wengi tunafanya ni kwanza kuchagua nyumba halafu kuulizia gharama za kuijenga!

Ni kama vile mtu kuchagua suti ya Armani halafu kulalamika unapoambiwa ulipe maelfu ya dola. Kitu cha busara ni kuangalia kwanza uwezo wako, chagua mtaalamu kwa makini (yule ambaye unadhani atakuelewa na kujitahidi kutimiza mahitaji yako kwa uaminifu), kaa naye halafu muangalie kwa pamoja nini mnachoweza kupata kutokana na fedha ulizonazo.

Ukweli ni kuwa kwa mfanyakazi wa kawaida hata nyumba ya milioni 10 inahitaji kujinyima sana. Lakini ukipata mchoraji creative, anaweza kukubunia kitu ndani ya bajeti hiyo ambacho utaridhika nacho. Kama uwezo wako ni sh. 100,000 kuna mafundi vyerehani kibao wanaoweza kukutengenezea suti isiyo na label ambayo unaweza kuolea bila matatizo. Kama uwezo ni 10,000 basi itabidi ukaazime au ukabahatishe kwenye mitumba. Nyumba ni hivyo hivyo.

Kama uwezo wako ni 10,000 kwa mwezi itabidi ukubali kupanga au ujenge nyumba isiyo na msingi, kuta za nchi 4, bila siling, madirisha, milango na choo na bafu nje. Hauwezi kutaka nyumba yenye self container na jacuzzi, gereji ya magari mawili, maktaba, jiko la nguvu, chumba cha kuoshea nguo n.k. halafu ukagwaya unapoambiwa mamia ya mamilioni! Wengi wetu hatuko realistic yanapokuja maswala ya nyumba.

Amandla......
 
Kwa haraka haraka nitakupa makadirio maana ndizo kazi zangu hizo chukua square meter za ramani yako times 500,000 utapata garama ya morden house with everything you need. Kama hujaelewa nina maana Urefu X Upana X 500,000=Construction cost
Hapo nina maana unatumia mkandarasi. visit our web;Juin Co. Ltd

Manyusi kuna Archtecter mmoja aliwahi kuniletea proposal ya kujenga nyumba kapiga mahesabu kwa dola ambazo ni kama Tsh.520,000 kwa square meter na anasema hiyo ni gharama ya materials tu. Kumbe alitaka kuniibia eeeeh!
 
Yes huyo huenda alitaka kupata faida kubwa zaidi hiyo 500,000 ni material and labor na kwa kuwatumia wataalamu wa ujenzi waliosajiliwa na bodi kabisa.Ila angalizo ukienda kwenye kampuni kubwa kama Holtan,Noremco utakuta the same sqm wanacharge 700,000 overhead cost zao ni kubwa na kampuni kama hizo hazichukui miradi chini ya 1bn
 
Nashukuru sana mkuu kwa ufafanunuzi, huyu jamaa naona alitaka kuniibia. Basi nami mambo yatapaokuwa yameninyookea nitafuata ushauri wako wa kutafuta wataalamu ili niweze kupata kitu chenye ubora.
 
Nyumba ya kawaidda ya vyumba 5,jiko,dinning na sitting ambayo haina tiles,haina ceiling board na ina madirisha ya nondo na mbao tu inagharimu 20,000,000/=milion. hapa kiwanja unacho na maji yapo kalibu.sema tena kamanda!
 
Kwa kukupa picha kidogo:

Mimi nina ongoing project, imefika kwenye linter, (Nyumba ya kawaida): 1 Masterbedroom moja, 1 Guest Room with attached toilet, 2 other Bedrooms, Study room 1, Laundry, Kitchen, Public Toilet & Bath, Dinning Room na Sitting Room...hadi sasa tayari $65,000 zimekatika!

I just received estimates ya kupauwa (Kwa bati pana) ni kama $18,000..hapo ni mbao, mabati na ufundi etc. Sasa nikianza kufikiria finishing nahaisi nitapaswa kuwa na kama $30,000 nyingine (total kuanzia kuezeka)! Hapo sijaweka hesabu ya fence.....

Kwa mantiki hiyo bosi waliosema uwe na kama 100,000,000/= kwa uchache hawajakosea (ingawa mimi nashauri uwe na kama 160,000,000/=
 
Kaka Guantanamo kwa pesa hiyo unaweza kujenga hiyo nyumba garama ya nyumba ni finishing material na roofing material,ukiezeka na DECRA tiles garama ni tofati na ukiezeka na Industrial Trough(IT) au Corrugated Aluminium sheets,pia tiles za spain au italy zinatofautiana sana bei na za china nitakupa mfano tiles ya spain 1sqm ni 35,000-42,000 na tiles ya china 1sqm ni 9,000-25,000 unaweza ukaona tofauti ilivyo kubwa hilo ndilo has linachangia kukuza bei ya nyumba na muonekano wake ni tofauti pia nikipata namna nitaweka hapa moja ya finishing tunazofanya ili uone utofauti na nyumba za watanzania wengi,waatanzania wanapenda vitu vizuri ila wengi hawajui namna ya kuvipata na utakuta wanatumia hela nyingi halafu hawapati quality wanayotaka.Tumia wataalamu wakupe thamani ya pesa yako.Mkuu hiyo nyumba unaweza nunua ni bei nafuu na ukinunua unaweza ibadilisha taratibu to your stardards kama kuweka tiles na vitu vingine ila jiridhishe kwanza na ubora wa nyumba hiyo unaweza tafuta fundi hapo tanga akakupa ushauri baada ya kuiona hiyo nyumba.

Mkuu Manyusi hebu tuwekee hii sample ya finishing zenu tuone zinavyopendeza
 
Back
Top Bottom