Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Hii imekaa sawa kweli? ina maana kwa nyumba ya vyumba 5 alioulizia mkuu inaweza kuwa around Tzsh 25 - 30 Million?.

Hii ukikadiria kwamba kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 10 square meters. ((10 x 5) x 500,000) = 25,000,000.

Kwa utaratibu huu mbona gharama zitakuwa ni ndogo ukilinganisha na gharama tunazozisikia kila siku?
+Bathrooms
+Kitchen
+Sitting Room
etc
 
Average in DSM TZS Million 100/=

With Kigae, Tiles, Fence, paint, plumbing, electricity etc.

...kwa kuchangia tu, gharama huongezeka au kupungua kutokana na Eneo, i.e tambarare au lina muinuko, udongo tifutifu au ufinyanzi, pia upatikanaji wa Maji, mchanga na Cement.

Mfano; hiyo Mil 100 inaweza sana kutosheleza ujenzi maeneo ya kibada-kigamboni, lakini isitoshe kwa ramani hiyo hiyo kujengea maeneo ya vilima vya wazo.
 
Hii imekaa sawa kweli? ina maana kwa nyumba ya vyumba 5 alioulizia mkuu inaweza kuwa around Tzsh 25 - 30 Million?.

Hii ukikadiria kwamba kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 10 square meters. ((10 x 5) x 500,000) = 25,000,000.

Kwa utaratibu huu mbona gharama zitakuwa ni ndogo ukilinganisha na gharama tunazozisikia kila siku?

Umesahau sebule ambalo mara nyingi ni kubwa sana, chumba cha wazazi ambacho nacho ni kikubwa na kina kuwa self-container, chumba cha kulia chakula,vyoo , bafu, jiko, stoo, korido, sehemu inayochukuliwa na kuta, gereji n.k.! Nyumba ya vyumba vitano VYA KULALA kwa matashi ya kitanzania haitapungua mita za mraba 200!

Ukizidisha hiyo na hizo namba zinazotajwa utajikuta uko kwenye milioni 500! Dawa ni kuwa realistic kitu ambacho kinatushinda wengi. Mfano ni kuita nyumba yenye vyumba vya kulala vitano kuwa ya kawaida! Itakuwa ya kawaida tu kama utaijenga mithali ya nyumba zetu za kiasili za kiswahili. Vyumba bila kutofautisha, korido katikati, ua na jiko, bafu na choo nje!

Amandla.......
 
nimefaidika thread lakini naona gharama zinazidi hadi 500M, mkubwa hapo alivosema
 
NINASHUKURU KWA HESABU, NINAHAKIKA NEXT EASTER I WILL BE IN MY HOUSE AT MASAKI AREA SQUARE YA NYUMBA KATIKA RAMANI NI 455m SQUARE. KWELI BONGO LAINI
 
Nakubaliana na SMU huo mjumba balaa, yaani mkubwa kweli kweli. Ukijenga mjumba wa size hiyo jee watoto wako wakishaondoka wamemaliza shule utaufanya nini? Vile vile ni kujihakikishia idadi kubwa ya wageni kwa muda wote kwani kuna nafasi ya kutosha. Maintenance costs ndio hazisemeki, unaweza kufaidi for the first four to five years, baadae ndio harakati za maintenance zinapoanza hapo.

Halafu TRA watakapokupiga hiyo property tax ndio utakoma ubishi.

Majumba ya aina hiyo yalikuwa yanajengwa mnamo miaka ya tisini sio sasa hivi.

Bitimkongwe, inawezekana huyu ni Hamad mwenye wake watatu. Kila mke na chumba chake, kimoja cha watoto na kiume na kimoja cha watoto wa kike.
 
Sasa hivo vya wanaume na wanawake viwe na size ya living rooms, maana wake watatu wanaweza kuamua kukuzalia watoto watatu kwa mwaka.

Hiyo itakuwa ni shule Mzee na sio nyumba.
 
Mkuu hiyo nyumba yenye 50m2 mbona ni vyumba viwili tu, hesabu haipigwi hivyo mkuu kama nyumba ina vyumba vitano havitakuwa mahali pamoja vyote vitakuwa na urefu na upana, umeshawahi kuona ramani lakini?

Unaweza weka vyumba viwili upande huu na vitatu upande mwingine weka urefu wa choo, bafu, jiko, sitting dining room na mengineyo,let say one side is 20m and the second 15m you take 15x20x500,000=150,000,000 upo hapo?

Jikumbushe hesabu mkuu.
 
Hii estimate ni sahihi??!

Stucture yangu ni 10x11=110sqm. X500,000=55,000,000. This isn't realistic in a Tz context. Mimi nimejenga kwa 15mil tu. Kama hizo ndo estimate mnazofanya kwenye miradi ya serikali ndo maana hatuendelei.
 
Hii imekaa sawa kweli? ina maana kwa nyumba ya vyumba 5 alioulizia mkuu inaweza kuwa around Tzsh 25 - 30 Million?.

Hii ukikadiria kwamba kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 10 square meters. ((10 x 5) x 500,000) = 25,000,000.

Kwa utaratibu huu mbona gharama zitakuwa ni ndogo ukilinganisha na gharama tunazozisikia kila siku?

Mkuu, ukichanganya vikorokoro vyote vya nyumba ya kisasa, kama dining, sitting room, jiko, stoo, public toilet, master room toilet, varanda, corido ya kiaina, hapo unakaribia 160sq m. (160 x 500000 = 80,000,000)
 
Hii estimate ni sahihi??!

Stucture yangu ni 10x11=110sqm. X500,000=55,000,000. This isn't realistic in a Tz context. Mimi nimejenga kwa 15mil tu. Kama hizo ndo estimate mnazofanya kwenye miradi ya serikali ndo maana hatuendelei.
Dah mkuu umejenga hadi hatua gani??? Umefanya finishing zote???

Finishings na fittings zinatofautisha sana gharama za ujenzi....nyumba mbili za aina moja na zikijengwa eneo moja zaweza kugharimu bei tofauti sana.......ila million 15 kwa mita za mraba 110 sio realistic kwa sasa....
 
Manyusi katika pekuapekua kwenye mitandao nimekutana na nyumba hii hapa chini nikaipenda. Jamaa hawajasema ina ukubwa kiasi gani (square meter). Ila ina vyumba 4 na bath room 2. Kwa uzoefu wako unaweza kadiria kuwa na mita ngapi za mraba? Hiyo gharama ya laki 5 kwa mita ya mraba inajumlisha na gharama za wajenzi (mafundi)?

2246-resampled.jpg
 
View attachment 14330

kwa kuangalia picha kama hiyo sio rahisi kukadiria sqm kama hapo ulipoona wameweka plan yake iweke hapa nitakupa estimate ya sqm na garama yake,hiyo laki tano per sqm ni kwa kutumia mkandarasi wala sio fundi wa mtaani,hapo unamkabidhi mkandarasi kazi anakukabidhi nyumba wewe unaingia na furniture zako tu.
 
Nashukuru mkuu kwa response yako. Hawa jamaa hawajaweka plan ya hiyo nyumba. Ni kwenye matangazo ya nyumba zinazouzwa TZ hiyo iko Mbezi beach, hawawezi kuiweka kwa kuhofia kuwapa mwanya watu wengine kuchukua na kwenda kuitumia.
 
Hii estimate ni sahihi??!

Stucture yangu ni 10x11=110sqm. X500,000=55,000,000. This isn't realistic in a Tz context. Mimi nimejenga kwa 15mil tu. Kama hizo ndo estimate mnazofanya kwenye miradi ya serikali ndo maana hatuendelei.
Kwenye hiyo 15 mil. uliweka bei ya muda wako ulioutumia kusimamia nyumba hiyo ( muda wako lazima uwe na gharama)? Kama si wako, wa huyo aliyekusaidia kusimamia ujenzi! Umeunganisha gharama ya kufika na kurudi kutoka kwenye sait yako? Gharama ya kuhifadhi vifaa , ingawa uliviweka kwa jirani.

Kumbuka gharama si matofali na pesa ya fundi peke yake! Na hapo bado haujazungumzia ni vitu gani vilikuwepo kwenye nyumba hiyo na umeimaliza vipi. Wengi tunajenga bila msingi, matofali ya nchi nne na kwenye madirisha tunaweka frame tu, mlango wa mbele na nyuma tosha, n.k. n.k.! Kwenye miradi ya serikali yote haya mtu hauwezi kufanya ndiyo maana gharamma zake zinakuwa juu.

Amandla.....
 
Hii estimate ni sahihi??!

Stucture yangu ni 10x11=110sqm. X500,000=55,000,000. This isn't realistic in a Tz context. Mimi nimejenga kwa 15mil tu. Kama hizo ndo estimate mnazofanya kwenye miradi ya serikali ndo maana hatuendelei.
Mkuu be careful!

Utafiti umeonyesha kuwa nyumba nyingi zilizojengwa na "wenyewe" hapa mjini DSM hazina ubora na umadhubuti unao kidhi matumizi ya binaadam.

Watu wengi wanapenda kujenga kwa bei ya chini wakiamini kuwa mradi paa lipo basi usingizi hawakosi.

Matofali karibu yote yanayouzwa mitaani, ukiyakemea yanalala mbele!

Zege linalochanganywa katika nyumba nyingi ni hafifu kabisa, sementi finyu, mchanga mchafu, kokoto ubuyu/chafu, mwishowe zege ukilipiga nyundo moja linasambaratika.

Katika nyumba zilizodondoka hapa mjini DAR , ZOTE NI ZA WATU BINAFSI,hata ile ya ghorofa 10!

Na wote hawa hawakuwatumia wataalam.

Bahati mbaya sana watu wanaidharau sana hii fani ya ujenzi, na baadaye kuishia majuto mjukuu.

Mkuu kama umejenga kwa 15mil nyumba ya 3/4/5 bedroom basi hongera, katika miaka 10-15 ijayo jitayarishe na hela hizo hizo kwa matengenezo na ukarabati(kama El Nino haijakupitia).
 
Ndugu wanaforum. Naomba Ushauri wenu juu ya ujenzi wa nyumba Dar. kutokana na uwezo mdogo, nimeshauliwa nitumie system inyoitwa interlocking blocks, amabyo inatumia tofari zinazotokana na mchanganyiko waudongo wa kisuguu na cement. swali je, hii technolojia ipo Dar? Je inasaidia kupunguza gharama za ujenzi na kwa % ngapi ukilinganisha na nyumba ya tofari za Cement za kawaida? Je nyumba hiyo inaweza kudumu mda mrefu kama ya cement? Nipeni ushauri ndugu zangu.
Embu tembelea pale Mwenge karibu na oil com kuna kituo cha utafiti wa ujenzi
 
Back
Top Bottom