Mizengo Pinda Waziri mkuu!

MpakaKieleweke:
Umefanya kazi nzuri sana. Tunashukuru kutuletea yote haya. Tunakuomba uendelee na moyo huu wa kulisukuma mbele Taifa letu.
 
Karamagi hakuwepo bungeni kuona waziri mkuu akiwa anaapishwa .

Pinda kaondoka na Msafara , na huku Lowassa akiondoka na walizni wawili, kweli ufisadi ni mbaya sana kwani kama alikuja na vimulimuli na hapa anaondoka kwa gari mbili na walinzi wawili.

Nafikiri LOwassa hastahili kupewa walinzi kwani alichotufanyia watz mungu ndo anajua. ANyway siku zijazo akipita mtaani watu watakuwa wanazomea tu hata kama ameondoka na pesa zetu kibao lakini hakuna heshima yoyote unapozomewa na kudharaulika kama Kibaki.
 
Matokeo.

JUMLA ZILIZOPIGWA 282.

IMEHARIBIKA -1.

HAPANA -2
NDIO -279.

ANatangaza kuwa amepata 99.% hivyo ndio anajiandaa kutoa hotuba nawawekea summary hapa kwa kadri nitakavyoweza,

nahisi kura iliyoharibika ni ya mheshimiwa Getrude Rwakatare maana hajui bado bungeni maana yake nini ...kwi kwi kwi kwi
 
nahisi kura iliyoharibika ni ya mheshimiwa Getrude Rwakatare maana hajui bado bungeni maana yake nini ...kwi kwi kwi kwi

Naona unataka kuanzisha ugomvi na watu fulani hapa .... au ndio ijumaa imeanza hivyo na waziri mkuu kutoka "usalama wa taifa"?
 
MP,

Inabidi tuanze na wewe mchana kweupe!!!!!..............

Hiyo statement yako ya "tusameheane na tugange yajayo"............inatupa mashaka mengi wananchi.............please sameheaneni huko huko CCM.........lakini mbele ya wananchi tunataka kusikia

1.yaliyopendekezwa na tume ya Mwakyembe yanatekelezwa
2.kashfa/kero zote zinashughulikiwa na wahusika wanashughulikiwa kisheria
 
Nami nimpongeze Waziri mkuu mpya Mizengo Kayanza Pinda Lakini ni mapema sana kujua atafanya nini kwa sasa, tumpatie probation period ya six months.

Wasiwasi wangu ni pale Lowasa aliposema Pinda anafanana naye, isije ikawa tumefungwa goli lile lile ingawa sasa la kisigino. nijuavyo mimi Pinda alikuwa mtoto mpendwa wa Mkapa hata iliwahi kutabiriwa angepewa U PM kwenye awamu ya pili ya Mkapa. tusitarajie Pinda kugusa maeneo ya Mafisadi kina Mkapa, Chenge, Lowassa na wengineo. Nilitaraji PM asiyekuwa na mahusiano ya moja kwa moja na system iliyopo madarakani muda mrefu. Vinginevyo sijasikia kashfa juu yake na tumpe nafasi ya ku prove uwezo wake.
 
kama nilivyotabiri mwanzo kuwa Mkuu anampa Pinda kazi...huyu jamaa ni SS..strict and serious na kazi yake.

Tumpe muda tuangalie atafanya nini...yeye hana uwezo wa kuwafungulia mashtaka jina Mkapa Lowassa na mafisadi weengineo bali vyote vyetu vya sheria.

Ninachotegemea kuwa them MMMC hawatarudi kwenye cabinet GOD willingly (Meghji,Mramba,Mgonja na Chenge)
 
Naona unataka kuanzisha ugomvi na watu fulani hapa .... au ndio ijumaa imeanza hivyo na waziri mkuu kutoka "usalama wa taifa"?

mwafrika wa kike!! Spare my ribs....hahahah sidhani kama kutakuwa na ugomvi jamani nimejiuliza tu nani atakuwa ameharibu kura? kuna mwingine alihisi mbunge wa Monduli maana bado yuko kwenye shock....

Bon week end
 
Matokeo.

JUMLA ZILIZOPIGWA 282.

IMEHARIBIKA -1.

HAPANA -2
NDIO -279.

ANatangaza kuwa amepata 99.% hivyo ndio anajiandaa kutoa hotuba nawawekea summary hapa kwa kadri nitakavyoweza,

Kura ilo haribika ni ya Lowassa. Hiii Hii Hii
Kati ya kura 2 za hapana moja ni ya Membe hii nyingine sina uhakika ni nani.
 
Na Mimi Pia Ninampongeza Mh. Mizengo Pinda Kuchaguliwa Kuwa Waziri Mkuu

Mungu Ibariki Afrika!

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Karamagi tunaambiwa na Mpaka kieleweke hakuwa bungeni leo...

Hahahahah,Mzee wa buzwagi ameenda kwa wazeee nini, then what will happen when zito et.al conclude their report, will it be discussed in the parliament?, and as i know, Karamangi will not be in any ministerial post, then what will be his fate, or the report will be a white wash?
 
Hahahahah,Mzee wa buzwagi ameenda kwa wazeee nini, then what will happen when zito et.al conclude their report, will it be discussed in the parliament?, and as i know, Karamangi will not be in any ministerial post, then what will be his fate, or the report will be a white wash?

Bangusilo una undungu na Dr Msabaha, am curious.....!!
 
Ooh really? R.I.P

Anaweza kuangalia namna ya kuoa tena

Du huyu mke wake alifariki mda mrefu?

Je hana mke sasa hivi?

Je ni poa kuwa na Waziri Mkuu asiyekuwa na Mke kimaadili?

Akina dada/mama JF kama kuna mdada mrembo mnamjua basi -mnaweza kumuunganishia Pinda -ila awe na jiko na hulinda heshima ya Serikali!

NakuliliaTanzania- je uko hapo?
 
Sidhani kama tumefungwa goli la kisigino.

Pia sidhani kitendo cha MH Pinda kulelewa na Kundi la watu walioko kwenye list ya Mafisadi ni tatizo kubwa.
MH Pinda hajachagauliwa kuwa PM kwa sababu ya kufanya kazi na hawa waheshimiwa, ziko sababu zilizo wezesha yeye kuchaguliwa kushika wadhifa huo.
Hotuba za waheshimiwa hawa ni za kujikomba tu. wnajikomba kama ilvyo kawaida yao.

Kwamba MH Pinda ni mtu wa usalama wa Taifa na hivyo tuanze kumtilia mashaka!
Sipuuzii hoja hiyo hata kidogo lakini hiyo haina maana kwamba yeye binafsi hana uchungu na nchi yake.
Hii haina maana kwamba ataingia na kuburuzwa na wazembe walomlea.


Hebu fikiria, siku 7 tu zilizo pita hakuna mtu alikuwa na wazo kwamba MH Pinda siku moja angeweza kuwa PM.Hii inaonyesha kwamba uchaguzi wa PM haujafuata majina yalojikita kwenye siasa.
hatuwezi sema mengi sana kwani wengine Pinda hatumjui sana zaidi ya kujua kwamba ni mbunge.

Binafsi sitegemei mabadiliko makubwa sana katika serikali ya Kikwete kwa sababu watu ni wale wale.
Nijuacho ni kimoja tu kwamba ulaji unaweza kuwa umehama kutoka kundi moja la watu kwenda kundi jingine.

Kundi la akina Lowassa lilikuwa ni jamii ya Tumbili sasa pengine ni zamu ya ngedere au kima,sijui.

Wote ni jamii tu ya nyani wanajipao zamu na uhalali wa kuvamia shamba letu la mahindi.
Kwa hilo,Wana JF ni lazima tujue kwamba kazi ya kuhamia nyani bado tunayo tu. Itabidi tubadili mtindo wa kupiga mayowe na mabango tunayo beba. Tusipoteze dira.

Kwamba sisi JF tutaogopa kuandika kwa sababu MH Pinda ni kutoka Usalama wa taifa, hilo ni wazo la kizembe.
Tutahakikisha kwamba PM mpya hapati kabisa wasaa wa kuota ndoto ya kuzuia harakati zetu kwa kutumia hila yeyote..
Tutasema na kukweka wazi kila kitu tunachojua kwa sababu hatumwogopi mtu yeyote awe Shushushi mzoefu au mwanajeshi ngangari.

Karibu MH Pinda macho namasikio yetu wana JF ni kwako tu Mkuu.
 
Back
Top Bottom