Mizengo Pinda Waziri mkuu!

Matokeo.

JUMLA ZILIZOPIGWA 282.

IMEHARIBIKA -1.

HAPANA -2
NDIO -279.

ANatangaza kuwa amepata 99.% hivyo ndio anajiandaa kutoa hotuba nawawekea summary hapa kwa kadri nitakavyoweza,

Hiyo moja iliyoaribika ni ya Mh.Edward Lowassa mbunge wa monduli kwani amechanganyikiwa na hakujua afanye nini.Kwikwi kwi kwi tehe hahahah
 
Wana JF tuwe makini sana. Huyu Pinda hongera zake lakini ukweli ni kwamba wengi wetu humu hatujui utendaji wake zaidi ya hizi sifa za kupakana mgongo za akina Kingunge na fisadi wa AU Mongella. Kama kuna anayejua atupe ACHIEVEMENTS ZAKE KWENYE PUBLIC SERVICE tuone, kama hakuna tumpe mda ila tusiwe over excited!. Swali ni je, is he ready to deal with mafisadi katika serikali? maana naona ndo ngoma bado mbichi kabisaaaa... au ni yale yale "huyu ni mwenzetu?" Nachelea kuwithhold excitement yangu. Hawa viongozi wa nchi yetu mimi sina imani nao siku hizi, especially yanapokuja maswala yanayogusa uhai wa taifa. Au kuna anayejua huyu bwana alichowahi KUSEMA AU KUANDIKA KUKEMEA UFISADI!! Leteni datas, mda wa kudanganywa na peremende na miwani ya viongozi umeshapitwa na wakati!

Hata huu ufisadi tumeujua baada ya DR. SLAA, Zitto na JAMBO FORUM kushika bango! Hawa viongozi wa CCM si walipiga kelele mpaka wakatumia mamilioni ya kodi zetu eti kwenda mikoani kusafisha sumu ya upinzani? Guys lets be more analytical na tusiwape hongera hawa jamaa kwa kitu ambacho wanapaswa kufanya kama viongozi. Kama mnakumbuka watu walikuwa excited 2005 Lowassa alipotangazwa! kumbe it was just our own deathbed...

Lets wait and see how Pinda will adress pressing problems za watanzania.

Yep.Nakubaliana na wewe kwa hili.Ni lazima watu wamuelewe huyu mtu kwanza kabla ya kuanza kumpa misifa kibao.Pili kuwa mtu wa usalama wa taifa haimaanishi kuwa ni mtu safi na mwenye machungu na nchi yake.Tatu kwa chapchap tu ukiangalia hotuba yake bungeni huyu bwana ni YES MAN! sidhani kama anaweza kuwa na msuli wa kuwachukulia hatua watu kama Lowasa,Ben na wengineo waliofuja mali za wananchi.
-Wembe
 
Anaanza kwa kumshukuru rais kwa kumteua , anaahidi kuwa atajitahidi sana kutimiza majuku yake ili aweze kufikia azima ya rais ya kulijenga taifa hili.

Anarudia tena kumshukuru Lowassa na kusema kuwa uamuzi wake wa kujiuzulu ni jambo la mfano mkubwa kwake , na kila mmoja akifikwa na hali kama hiyo lazima naye awe tayari kujiuzulu.

Anasema kuwa ni kweli amevaa kiatu cha Lowassa ila hana hakika kuwa kama kitamtosha kwani lowassa amefanya makubwa sana kwenye elimu na atajitahidi ili aweze kuenea.

Anamshukuru tena Ngwilizi, na makatibu wakuu wote ambao amefanya nao kazi kwa pamoja tangu kipindi chote.

Anashukuru wabunge kwa kumpa kazi ya kufanya ndani ya bunge, anashukuru ushirikiano ambao amekuwa akiupata kutoka kwa spika ,naibu na wenyeviti wa kamati za bunge.

Anasema kuwa alipoingia bungeni kwa mara ya kwanza aliwakuta wabunge wengi wa muda mrefu ila baada ya kukaa kwa muda mfupi alijiona anafanana nao kwani bunge limejenga uwanja wa kuweza kujenga mahusiano mema kati ya wabunge.

Anasema kuwa kamati teule imefanya kazi yake na pengine kazi hiyo ndio imemfanya yeye kuwa hapo alipo, anasema kuwa kwake kubwa ni kukubali kuwa ktk utendaji wa kazi za serikali lazima kila mmoja ahakikishe kuwa anatimiza wajibu wake kwa jinsi inavyopaswa.

Kila waziri lazima ahakikishe kuwa wataalamu wao wanafanya kazi kwa kina na kwa ukweli.

Anasema kuwa ripoti ilionyesha kuwa anapaswa kuhakikisha kuwa anafanya kazi ya kukomesha maovu yote ndani ya serikali na kuyakomesha .

Anasema kuwa yeye kama kiongozi yupo kwa ajili ya kuitumia ripoti hiyo kama dira ya kumwongoza.
Kwake TAKUKURU,POLISI NA USALAMA kazi yao kubwa ni kuweza kuisaidia serikali ili kuweza kufanya kazi zao kwa kina zaidi.

Anaamini kuwa yapo mabadiliko muhimu ili kuhakikisha kuwa majukumu yao yanafanyiwa kazi ipasavyo ,na anaahidi mabadiliko ili kuweza kuhudumia wananchi inavyotakiwa.

Anawataka mawaziri watakaoteuliwa lazima wawe tayari kufanya kazi za wananchi kwa kadri walivyodhamiria.

Anasema kuwa bunge linakidhi mahitaji ya mfumo wa vyama vingi na kuna kipindi wasipokuwa makini kuna tatizo, anasisistiza kuwa jambo kuwa sio vyama ila ni bunge na hoja itakuwa ni kujenga bunge na sio vyama ili kuweza kujenga nchi .

Anawashukuru wote aliokuwa nao ndani ya bunge kwa muda wake wa vipindi viwili.

Katika kutekeleza ilani ya CCM anasema wote tushirikiane na kufuchua maovu yote ili kuijenga nchi na kazi hiyo sio ya mtu mmoja-maovu yafichuliwe kwenye ngazi za serikali za mitaa na serikali kuu.

Anawashukuru sana vyombo vya habari ktk kutoa habari kwa watanzania na atajitahidi kufanya nao kazi,ila taarifa zao watakazozitoa ziwe za kweli na zenye kukidhi haja ya watanzania.

Anawashukuru sana wazazi wake baba 81 yuko mama 79 na wapo hai,anawashukuru kwa sababu anaamini walijitahidi kumlea vizuri na kwa makuzi ya maisha ya kijijini huenda taifa limempata mtu ambaye linamhitaji.

Angependa kuwa na wazazi wake kwenye siku ya kuapishwa, anamshukuru mkwewe wanawe Janneth, fotunata,Henuiq na anaamini kuwa watamsaidia kwenye maisha yake .

Anawashukuru wabunge kutoka mkoa wa Rukwa na anaamini kuwa hawatamtupa kwenye wakati huu mzito.

Anawashukuru wana Rukwa wote kama mjumbe wa halimashauri kuu ya CCM ,na anawaomba wamsaidie kuifanya kazi yake.

Anawaomba wabunge washikamane,waheshimiane, na ana hakika kuwa wakienda kwa mtazamo huo bunge litaweza kutimiza matarajio ya watanzania.

Anawashukuru viongozi wote wa Tanzania bara na visiwani,na hata wale wa CCM ,pande zote.

Anawashukuru sana viongozi wa upinzani na wabunge wote wa upinzani kwa kazi waliyompa ngumu, na anaamini kuwa kwa jinsi anavyoona ni kuwa a=wataweza kushirikiana kujenga nchi kwa pamoja.

Anawashukuru waliompa kura na waliomnyima.

Anarudia kuwa yeye sio mwanasiasa ila ataendelea kujifunza na hapo wataweza kuleta maisha bora .

Anasema kuwa huenda pakawa na hisia juu ya ripoti ya richmond,anaamini kuwa hakuna hisia za nia mbaya ila ni njia ya kuweza kujenga nchi,anawapongeza wote waliojiuzilu na lowassa na anaamini kuwa hiyo ndio njia ya kujenga taifa na CCM .

anaomba kuambia ukweli juu ya yale yote watu wakiona kuwa hayajengi na yeye yupo tayari kuyaacha mara moja.

Anamalizia kwa kushukuriu
 
Pinda ataapishwa kesho saa tano kamili asubuhi ikulu ya Chamwino Dododoma .

Baraza la mawaziri litatajwa jumatatu na kuapishwa ikulu ya Chamwino Dodoma siku ya jumatano wiki ijayo..

Anaitisha kamati ya uongozi ili kuweza kukutana kesho na kuongeza muda wa wabunge kukaa ili kuweza kujadili kwa kina mambo yote Bungeni.

Sherehe za waziri mkuu huwa anapaswa agharimie yeye .

Bunge limeahirishwa hadi siku ya alhamisi ya wiki ijayo ....

My take, je?ni kwenda kuweka mambo sawa juu ya ripoti na kupunguza makali ama siku za kuleta ripoti ya EPA ?KWANI ILIKUWA ILETWE JUMANNE BUNGENI.
 
Pinda, naomba kwa uteuzi wako huo hawa mafisadi uwashughulikie , warudishe mali zetu, Asante.
 
Ni mfano mzuri. Ni bakora nzito, kwa kweli, watu wasifanye ofisi za uma kama vijiwe.
Long live JM Kikwete
 
Jamani katika hiyo Htuba yake je Mmesikia pale aliposema, Tusameehane sasa, na tusahau ya nyuma. Nanukuu " Yaliyopita Si ndwele tugange yajayo, sisi wote ni watanzania na tuna mapungufu yetu, lazima tukubali kusaheeana na kumove one" Sasa ina maana kutokana na hiyo kauli, je hoja muhimu ya Richmond ni kwamba imekufa au?? Au ndiyo yale yale ya kusameehana. Pia hao makatibu wakuu mbona bado wapo?? Ina maana hakuna mwingine wa kuwajibika?
 
Karamagi hakuwepo bungeni kuona waziri mkuu akiwa anaapishwa .

Pinda kaondoka na Msafara , na huku Lowassa akiondoka na walizni wawili, kweli ufisadi ni mbaya sana kwani kama alikuja na vimulimuli na hapa anaondoka kwa gari mbili na walinzi wawili.
 
Masanja....mwanawane!!,

Huyu mama Mongella anachofanya hivi sasa ni kujipendekeza.............ili kujenga future yake na mwanae.........sasa yeye asubiri tu jinsi watu watavyomkoma giladi........hakuna cha kujikomba hapa.......

MP = Mizengo Pinda....hii ndio itakuwa ID yako hapa JF Waziri Mkuu Mizengo!!!....tunakutakia kila kheri na usisahau kupitia pitia JF...........
 
Pinda, naomba kwa uteuzi wako huo hawa mafisadi uwashughulikie , warudishe mali zetu, Asante.

Nimeamini watanzania sisi ni wagumu kuelewa na wepesi kusahau.Huyu Pinda anayeshangiliwa na kuwekewa matumaini kibao emekuwa akiongoza Wizara ya TAMISEMI kwa muda mrefu sasa na kila mwaka Ripoti ya CAG inaonyesha Halmashauri zilikuwa zinaongoza kwa ubadhirifu ni nini ambacho nyie kwenye kumbukumbu zenu zinaonyesha alishughulikia ubadhirifu huu?.Ikiwa hakuna leo hii unategemea ghafla abadilike?.
Mimi ninampongeza Bwana Pinda lakini naona ni mapema mno kuweka matumaini yoyote kwake.Kwa kuwa ndo kwanza amepewa ofisi nitamtendea haki kwa kumpa miezi 3 nione jinsi atakavyoshughulikia huu ufisadi baada ya hapo nitakuwa na tathmini kamili
 
Jamani katika hiyo Htuba yake je Mmesikia pale aliposema, Tusameehane sasa, na tusahau ya nyuma. Nanukuu " Yaliyopita Si ndwele tugange yajayo, sisi wote ni watanzania na tuna mapungufu yetu, lazima tukubali kusaheeana na kumove one" Sasa ina maana kutokana na hiyo kauli, je hoja muhimu ya Richmond ni kwamba imekufa au?? Au ndiyo yale yale ya kusameehana. Pia hao makatibu wakuu mbona bado wapo?? Ina maana hakuna mwingine wa kuwajibika?

Hiki ndicho wana usalama wanataka ili kufunika mambo yao waliyofanya BoT na kwenye migodi ya madini. Kitakachofuata sasa hivi ni kuwa kila atakayeuliza yaliyopita atakumbushwa kuwa Lowasa na Balali hawana kazi na mengine yote ni ya usalama wa taifa! wananchi wawasamehe kina Karamagi na wenzake kisha life ya kulipia umeme kwa bei ghali iendelee kama kawaida huku watanzania wakifuata ushauri wa Mramba wa kula nyasi.....
 
Ni mfano mzuri. Ni bakora nzito, kwa kweli, watu wasifanye ofisi za uma kama vijiwe.
Long live JM Kikwete

Week end Nzuri kweli hii tunasheherekea PM mpya Mizengo Peter Kayanza Pinda, Pia kusheherea kuanguka kwa tawala za kifisadi za Edward Ngoyai Lowasa (MB Monduli) na wale akina Karamagi na Msabaha....it is partying time tukisubiria baraza jipya la mawaziri
Nategemea raisi JK atatufurahisha watanzania kwa kuwapumzisha akina Kingunge, Mramba, Meghji, Msolla, Nchimbi, Kamala, Matayo,Kapuya,na Chenge

Mungu Ibariki Tanzania
 
This guy mimi nimependa jina lake- ni la Kiafrika,

Mizengo Kayanza Pinda (hili la Peter ni la Kizungu tuachane nalo!)

Huyu ni Mwafrika Kweli kweli! Je wale wanaotoka Ufipa- nini maana ya haya Majina?

JF- Je mko hapo?
 
Masanja....mwanawane!!,

Huyu mama Mongella anachofanya hivi sasa ni kujipendekeza.............ili kujenga future yake na mwanae.........sasa yeye asubiri tu jinsi watu watavyomkoma giladi........hakuna cha kujikomba hapa.......

MP = Mizengo Pinda....hii ndio itakuwa ID yako hapa JF Waziri Mkuu Mizengo!!!....tunakutakia kila kheri na usisahau kupitia pitia JF...........

Haya mkuu,

Naona tumpe ID kabisa ya MP

Akifanya kazi vizuri ataenjoy life na watanzania watafaidika na uteuzi wake, ila akipeleka nchi kwenye vitisho basi PM yake nitaibadilisha hapa JF.........

Pata ijumaa njema waziri mkuu mpya MP
 
Jamani katika hiyo Htuba yake je Mmesikia pale aliposema, Tusameehane sasa, na tusahau ya nyuma. Nanukuu " Yaliyopita Si ndwele tugange yajayo, sisi wote ni watanzania na tuna mapungufu yetu, lazima tukubali kusaheeana na kumove one" Sasa ina maana kutokana na hiyo kauli, je hoja muhimu ya Richmond ni kwamba imekufa au?? Au ndiyo yale yale ya kusameehana. Pia hao makatibu wakuu mbona bado wapo?? Ina maana hakuna mwingine wa kuwajibika?

HAKUNA ISSUE SENSITIVE ALIYOGUSA...TUENDELEE KULALA..HAO WABUNGE wanakwenda kucheza kamari nani atapewa uwazir gani..kipindi cha bunge next week kisha kwisha, na wakirudi alhamisi itakuwa kuwapongeza mawazir na usiku kutakuwa na Vilevi vya kupongezana. Maana kila wazir atafanya kijipart chake na kuwalipia Madiwani wake kwenda dodoma kula nao keki. na Hapo Juma limekwisha.

Hapo unazungumza week ileee ambayo wabunge pombe zitakuwa zimekwisha vichwani mwao...na kwakuwa mawazir wageni...mtaambiwa subiri...wapitie upya mafaili...tuwape muda...kushtukizia ishaingia March..08...Hapo kutakuwa na Mvua na mafuriko ya hapa na pale...wazir Mkuu atakuwa busy na Timu kushughulikia mafuriko etc...April..sikukuu zimejaa....Hadi MAY...ndio waanze kujadili..sitabiri ila ukijua nature ya mawazir wetu, wabunge wetu , tarehe za sikukuu, week end..etc..
 
-----------------------------------------------------------------

Mimi ni Mtanzania mwenye haki zote za kuandika hapa, kama wewe.....and to correct you, "Sikuamulia watu cha kuongea hapa", nimesema watu wachangie hoja zenye msingi.

By asking me that question quoted above...aren't you also limiting my freedom of expression???? Tafadhali, tustaarabike kidogo.

Kamanda, shukrani kwa maelezo murua..
 
Anaanza kwa kumshukuru rais kwa kumteua , anaahidi kuwa atajitahidi sana kutimiza majuku yake ili aweze kufikia azima ya rais ya kulijenga taifa hili.

Anarudia tena kumshukuru Lowassa na kusema kuwa uamuzi wake wa kujiuzulu ni jambo la mfano mkubwa kwake , na kila mmoja akifikwa na hali kama hiyo lazima naye awe tayari kujiuzulu.

Anasema kuwa ni kweli amevaa kiatu cha Lowassa ila hana hakika kuwa kama kitamtosha kwani lowassa amefanya makubwa sana kwenye elimu na atajitahidi ili aweze kuenea.

Anamshukuru tena Ngwilizi, na makatibu wakuu wote ambao amefanya nao kazi kwa pamoja tangu kipindi chote.

Anashukuru wabunge kwa kumpa kazi ya kufanya ndani ya bunge, anashukuru ushirikiano ambao amekuwa akiupata kutoka kwa spika ,naibu na wenyeviti wa kamati za bunge.

Anasema kuwa alipoingia bungeni kwa mara ya kwanza aliwakuta wabunge wengi wa muda mrefu ila baada ya kukaa kwa muda mfupi alijiona anafanana nao kwani bunge limejenga uwanja wa kuweza kujenga mahusiano mema kati ya wabunge.

Anasema kuwa kamati teule imefanya kazi yake na pengine kazi hiyo ndio imemfanya yeye kuwa hapo alipo, anasema kuwa kwake kubwa ni kukubali kuwa ktk utendaji wa kazi za serikali lazima kila mmoja ahakikishe kuwa anatimiza wajibu wake kwa jinsi inavyopaswa.

Kila waziri lazima ahakikishe kuwa wataalamu wao wanafanya kazi kwa kina na kwa ukweli.

Anasema kuwa ripoti ilionyesha kuwa anapaswa kuhakikisha kuwa anafanya kazi ya kukomesha maovu yote ndani ya serikali na kuyakomesha .

Anasema kuwa yeye kama kiongozi yupo kwa ajili ya kuitumia ripoti hiyo kama dira ya kumwongoza.
Kwake TAKUKURU,POLISI NA USALAMA kazi yao kubwa ni kuweza kuisaidia serikali ili kuweza kufanya kazi zao kwa kina zaidi.

Anaamini kuwa yapo mabadiliko muhimu ili kuhakikisha kuwa majukumu yao yanafanyiwa kazi ipasavyo ,na anaahidi mabadiliko ili kuweza kuhudumia wananchi inavyotakiwa.

Anawataka mawaziri watakaoteuliwa lazima wawe tayari kufanya kazi za wananchi kwa kadri walivyodhamiria.

Anasema kuwa bunge linakidhi mahitaji ya mfumo wa vyama vingi na kuna kipindi wasipokuwa makini kuna tatizo, anasisistiza kuwa jambo kuwa sio vyama ila ni bunge na hoja itakuwa ni kujenga bunge na sio vyama ili kuweza kujenga nchi .

Anawashukuru wote aliokuwa nao ndani ya bunge kwa muda wake wa vipindi viwili.

Katika kutekeleza ilani ya CCM anasema wote tushirikiane na kufuchua maovu yote ili kuijenga nchi na kazi hiyo sio ya mtu mmoja-maovu yafichuliwe kwenye ngazi za serikali za mitaa na serikali kuu.

Anawashukuru sana vyombo vya habari ktk kutoa habari kwa watanzania na atajitahidi kufanya nao kazi,ila taarifa zao watakazozitoa ziwe za kweli na zenye kukidhi haja ya watanzania.

Anawashukuru sana wazazi wake baba 81 yuko mama 79 na wapo hai,anawashukuru kwa sababu anaamini walijitahidi kumlea vizuri na kwa makuzi ya maisha ya kijijini huenda taifa limempata mtu ambaye linamhitaji.

Angependa kuwa na wazazi wake kwenye siku ya kuapishwa, anamshukuru mkwewe wanawe Janneth, fotunata,Henuiq na anaamini kuwa watamsaidia kwenye maisha yake .

Anawashukuru wabunge kutoka mkoa wa Rukwa na anaamini kuwa hawatamtupa kwenye wakati huu mzito.

Anawashukuru wana Rukwa wote kama mjumbe wa halimashauri kuu ya CCM ,na anawaomba wamsaidie kuifanya kazi yake.

Anawaomba wabunge washikamane,waheshimiane, na ana hakika kuwa wakienda kwa mtazamo huo bunge litaweza kutimiza matarajio ya watanzania.

Anawashukuru viongozi wote wa Tanzania bara na visiwani,na hata wale wa CCM ,pande zote.

Anawashukuru sana viongozi wa upinzani na wabunge wote wa upinzani kwa kazi waliyompa ngumu, na anaamini kuwa kwa jinsi anavyoona ni kuwa a=wataweza kushirikiana kujenga nchi kwa pamoja.

Anawashukuru waliompa kura na waliomnyima.

Anarudia kuwa yeye sio mwanasiasa ila ataendelea kujifunza na hapo wataweza kuleta maisha bora .

Anasema kuwa huenda pakawa na hisia juu ya ripoti ya richmond,anaamini kuwa hakuna hisia za nia mbaya ila ni njia ya kuweza kujenga nchi,anawapongeza wote waliojiuzilu na lowassa na anaamini kuwa hiyo ndio njia ya kujenga taifa na CCM .

anaomba kuambia ukweli juu ya yale yote watu wakiona kuwa hayajengi na yeye yupo tayari kuyaacha mara moja.

Anamalizia kwa kushukuriu

Sijaona anamshukuru mke wake lakini nimeona watoto tu,,,,, hawa watoto hawana mama?????????
 
Back
Top Bottom