Mizengo Pinda Waziri mkuu!

Ni poa Amekumbuka Kigoma kwani Mkoa huu ni kama umesahauliwa kama vile sii sehemu ya Tanzania

CV ya Pinda

Mizengo Kayanza Peter

Mpanda Mashariki Constituency

Born 12 Aug 1948- 60 Years of Age

EDUCATION
University of Dar es Salaam LLB 1971 1974 GRADUATE

EMPLOYMENT HISTORY


Prime Minister's Office - Regional Admin.& Local Governments. Minister 2006
Prime Minister's Office - Regional Admin.& Local Governments. Deputy Minister 2000 2005
State House Clerk to the Cabinet 1996 2000
State House Assistant Private Secretary to the President 1982 1992
State House Security Officer 1978 1982
Ministry of Justice State Attorney 1974 1978

[ Retrieved on 6/7/2006 - www.parliament.go.tz ]
 
Name Mizengo Pinda Mizengo Pinda
Surname Pinda
First Names Mizengo Kayanza Peter
Alternate Name
Title
Country of Birth Tanzania
Positions
From To Organisation Position
2006 Prime Minister's Office Minister of State for Regional Administration & Local Government
2005 Mpanda Mashariki Constituency MP for Mpanda Mashariki
Date of Birth 12 Aug 1948
Political Affiliation CCM
eMail
Telephone
Address
Notes EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
University of Dar es Salaam LLB 1971 1974 GRADUATE
CERTIFICATIONS
Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
No items on list
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Prime Minister’s Office - Regional Admin.& Local Governments. Minister 2006
Prime Minister’s Office - Regional Admin.& Local Governments. Deputy Minister 2000 2005
State House Clerk to the Cabinet 1996 2000
State House Assistant Private Secretary to the President 1982 1992
State House Security Officer 1978 1982
Ministry of Justice State Attorney 1974 1978
[ Retrieved on 6/7/2006 - www.parliament.go.tz ]



thanx mkuu.
 
wabunge kwa kupamba utafikiri madalali wa richimod,kama amepinda basi akae akijua kuwa kuna JF kazi yao kunyoosha wale wote waliopinda.
Sasa ndio tunafungua ukurasa wa pili,ajue kabisa kuwa sura ya kwanza bado haijaisha
 
Kama ataweza kusimamia kwa bidii na kuhakikisha LOWASSA anarudisha pesa yetu aliyokwiba basi mimi nitampa CREDIT
 
Kapewa nafasi Zitto kuzungumzia uteuzi huo kwa niaba ya wabunge vijana, naye analisemea jambo la kumchagua meya wa manispaa ya kigoma na jinsi CCM walivyoweza kutaka kumtorosha diwani wa CHADEMA ili CCM washinde.

Pinda ndio alikubaliana kuunda manispaa ya pamoja ya kigoma ,na alikubaliana na pendekezo la kuleta sheria za kuweza kulifanya jambo hilo rasmi.
 
na mie nnatoa pongezi zangu kwake,

karibu ila jitahidi kutokuwa msanii na jitahidi kulitumikia taifa vyema
 
Inabidi Lowassa amtafute Sumaye amwachie vile vitabu alivyokuwa anatumia kule darasani HArvard. Akapige darasa kidogo.
 
wabunge kwa kupamba utafikiri madalali wa richimod,kama amepinda basi akae akijua kuwa kuna JF kazi yao kunyoosha wale wote waliopinda.
Sasa ndio tunafungua ukurasa wa pili,ajue kabisa kuwa sura ya kwanza bado haijaisha

Wabunge wengi ni wanasiasa kwa hiyo wataongea kama wanasiasa leo ili mambo yaendelee. Kumbuka pia kuna issue ya BoT, buzwagi, kiwira, na mengine mengi yanakuja!

JF inangoja kuona Mizengo kama atakuwa huru au atafanya kazi ya wale wabovu huko usalama wa taifa wanaonufaisha matumbo yao na kutisha wanaowakosoa!
 
Pinda sio mtu wa kigoma ila ni mtu wa mkoa wa Rukwa na anatokea Jimbo la Mpanda mashariki.

Kaenda kwa babu nini wakuu,


Mzee Malecela ndio anapongeza busara za spika ambazo zilitumika jana na kumaliza mambo ambayo yalikuwa magumu.

Anampongeza Lowassa kwa kumwita ndugu yake na kijana wake , hapa anaendelea kusema kifalsafa kuhusu historia ya Tanzania .

Anaonyesha historia ya ulaya na jinsi demokrasia ilivyoanzia kule Athens,.
 
Have you noticed?

Kutokana na mengi yaliyosemwa hapa JF dhidi ya EL na mama Mongela, na ukiyasikiliza waliyoyaongea hawa, utagundua ni kwa kiasi gani wanasiasa wengi walivyo wazandiki.

Spika anaonekana kuongea kwa upole ikitokea mbunge wa CCM akienda nje ya hoja, lkn anaongea kwa ukali mbunge mpinzani akifanya hivyo. Mmh!
 
Tunao usemi wetu wa Kiswahili. KAMBARE MPINDE KABLA NI MBICHI.Kwani akishakuwa mkavu na ukajaribu kumpinda atakatika vipande vipande.
Yaelekea huyi Pinda bado ni mbichi kwa hiyo tuanze kumnyoosha kabla hajakauka.
Lakini twampa hongera kwa kuchaguliwa kuwa Waziri Mkuu mpya.hili ni jukumu kubwa sana.Twamuombea wema tu mpaka hapo atakapochafua.
 
Kila la kheri Mhe Pinda.
Ila angalia na wewe usijiingize katika biashara, kwani hiyo ofisi haihitaji wafanyabiashara, ila watumishi wa umma.
 
Kwani usalama wa Taifa nao Mafisadi???????

Fuatilia pesa za wizi BoT na kashfa za madini Tanzania uone zinaishia wapi..... kumbuka pia kuwa sijasema kuwa Mizengo ni fisadi katika hili so far! but fuatilia kashfa Tanzania uone uchunguzi utakomea wapi!
 
Naona huyu jamaa anajieleza vizuri..na anapigiwa kaofi sana..anyaway..huyu bwana mbona kama askari fulani!!.katualia sana kma mchuguzi chuguzi...na madadisi kama anamambo ya kujificha... tumuone..
 
Du!

mwafrika wa kike na mpaka kieleweke,,,

Kama vile hawajafurahia vile?

Poleni... lakini wale tunaopenda taifa letu tunadhani Rais ameteua mtu mzuri...


Mtu akiwa usalama wa taifa ana tatizo gani???
 
Pinda anazungumza na anaanza kwa kusema kuwa yeye ni mtoto wa mkulima na kwenye familia yao yeye ni wa kwanza .

Anasema kuwa anajua hata nyumbani kwake wazazi wake wakisikia amepewa wadhifa mkubwa kiasi hicho watakuwa wamepata taabu sana .

Alifanya kazi na Chenge 1974-76 , kama mwanasheria , na baada ya hapo aliitwa ikulu kufanya kazi chini ya uongozi wa Butiku akiwa katibu wa rais msaidizi, akawa na mwinyi kwa miaka kumi kama katibu wake , na pia alifanya kazi na mkapa .

Anasema kuwa alijifunza kufanya kazi kwa nidhamu ya Ikulu, na pia anakiri kuwa yeye sio mwanasiasa ila ndio anajifunza siasa kwa kuwa karibu na viongozi wa kisiasa haswa ikulu.

Anasema kuwa alijaribu kuingia kwenye siasa ila Mkapa akamwambia ataweza kwenda kufanya kazi ya siasa na haswa ubunge?

Anasema kufanya kazi kama mwanasiasa amefanya kwa kipindi cha miaka saba tuu.

Ila anasema kuwa ukifanya kazi TAMISEMI hata ukiwa nani lazima utakomaa tuu, anawashukuru viongozi waliomsaidia kumkomaza akianza na mkapa ,Ngwilizi na Lowassa na kusema kuwa viongozi hao ndio ambao walimlea.

Anamshukuru sana Lowassa kwani ndani ya kipindi kifupi amemkomaza sana , anasema kuwa Lowassa ni kiongozi mzuri sana kwa maana ya utendaji wa kazi za kila siku.

Anamshukuru Lowassa kwa kumsaidia sana kumjenga kisiasa na kiutendaji, na pia anaomba kura kwa kusema kuwa maelezo aliyotoa ndio.

Anasema kitu kipya ni kuwa ni madaraka tuu ila kwa maana ya Pinda kamam mbunge ,na kama walivyomzoea ataendelea kubakia yuleyule , na atafanya kazi na wabunge na haswa kujenga mahusiano baina yao.

Atajitahidi sana kujenga bunge moja litakalokuwa linasimamia masilahi ya taifa hili, na anatamani sana kufanana na mabunge ya uingereza, marekani na israeli kwani wao kwenye kusimamia masilahi ya taifa huwa wanasimama pamoja hakuna tofauti za vyama ,na hicho ndicho ambachoa anakitamani sana sana kukijenga.
 
Du!

mwafrika wa kike na mpaka kieleweke,,,

Kama vile hawajafurahia vile?

Poleni... lakini wale tunaopenda taifa letu tunadhani Rais ameteua mtu mzuri...


Mtu akiwa usalama wa taifa ana tatizo gani???

hizi bangi sasa mkuu!

kupenda taifa lako kunathibitishwa na kushangilia uteuzi wa waziri mkuu! inaonekana neno kupenda taifa lina maana nyingi sana hapa duniani.
 
Huko kazi mnayo, mpeni basi the benefit of the doubt. Msianze kurusha madongo wakati mtu mwenyewe hamjuhi.
 
Back
Top Bottom