Mizengo pinda kuonana na madaktari ili kumaliza matatizo yao...

hili siyo suala la waziri mkuu asiye na nguvu; hili ni suala la rais na ccm kama chama tawala; madaktari wasikubali kugereshwa kwa maneno ni lazima rais ndiye akutane nao na ccm ibadilishe sera zake kwenye hili suala.

kwa pinda hakuna matumaini kutaneni na rais kikwete
 
Hivi Pinda ana rekodi gani ya kujivunia tangu awe PM?

Ni PM wa kwanza kuangua kilio bungeni baada ya kukumbushwa na wabunge wachokonozi vifo vya kinyama vya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi. Hiki ni kiwango kikubwa cha upendo wa kiongozi kwa wananchi bila kujali rangi, dini, kabila au jinsia.
 
The way nilivyokuwa namchukulia pinda hapo awali ni tofauti kabisa na ninvyomchukulia kwa sasa. Wakati anateuliwa kuwa PM kwa mara ya kwanza niliamini kuwa amepatikana PM makini, mwenye maamuzi magumu yenye maslahi kwa umma. Kumbe sio kabisa, yani hakuna la maana alofanya la maana analoweza kujivunia tangu apewe mamlaka hayo muhimu. Labda afe ndo aanze kusifiwa kama ilivyo kawa, hasifiwi mtu akiwa hai hadi afe!

Usimwonee bure mzee wa watu. Kwa tulipofika usitarajie kiongozi wa ngazi ya waziri mkuu au waziri anaweza kufanya maamuzi ya kutatua matatizo sugu ya nchi hii. Haya ndio madhara ya kukubali kuwa makuwadi wa soko huria. Wao kimsingi ni washauri tu wa mkuu wa nchi ambaye kwa mujibu wa katiba ni Alfa na Omega wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom