Mizengo Pinda for Pres 2015?

Status
Not open for further replies.
usitake nipate ugonjwa wa moyo! yaani Pinda awe rais?? ntakunywa sumu ya panya nife kabisa...leave alone urais hata huo U PM alio nao hajakidhi standards...
 
Amini usiamini habari za kiintelijensia zimetonya kuwa tayari Mheshimiwa Mizengo Pinda ndie Raisi mtarajiwa baada ya Mheshimiwa Kikwete kumaliza nngwe yake.
Habari za ndani ya kasha zimesema kuwa Mheshimiwa Pinda ameshapewa baraka zote za wakuu na kinachoendelea sasa ni mikakati ya kumpa kipau mbele katika harakati nyingi zinazohusisha jamii.
Kwa ufupi hana mpinzani wa kweli zaidi ya vivuli ambavyo vitajiengua katika hatua za mwisho.
Labda awe rais wa chawa, papasi na mende! Pinda ni debe tupu kuanzia kichwani hadi miguuni.
 
Unazungumzia Pinda kuwa Rais wa jamhuri ipi? Tanzania au? kama CCm wanataka kupoteza wamteue Pinda 1. Hakubaliki Zanzibar kutokana na kauli zake za ZNZ ni nchi au sio Nchi 2. Si Kiongozi shupavu mwenye msimamo wa kiuongozi(hana maamuzi) toka aingie madarakani hakuna "Landmark" yake bora hata Lowassa alituletea Shule za Kata ambazo japo zinalalamikiwa lakini zimepunguza wanaokosa nafasi kwenda Form one (secondary) 3. Amejitia Doa kwa kutowawajaibisha Mawaziri wake 8 mpaka akapata shinikizo toka kwa Wapinzani na Filikunjombe baada ya kusaini kutokuwa na imani nae. 4. kuwa partner katika SUMRY EXPRESS soon baada ya kupewa U-PM unatia mashaka kama akipewa nchi ndo atachota balaa 5. CCM tafuteni mtu atakayepambana na CHADEMA 2015. Vinginevyo mnauza Nchi kwa CHADEMA..................vp Dr. Salim Ahmed Salim, Dr.Mwinyi(maana sasa ni zamu ya Zanzibar). Sitta, Membe tulieni mtapewa wizara.
 
Tulikuwa na Rais
1: Mwalimu - Mwenye vision na alikuwa serious kiutendaji.
2: Alhaji Mwinyi - Aliacha mambo yajiendee yenyewe, akatoa ruksa kwa kila jambo.
3: Mkapa-Alie kuwa hana mchezo na ukusanyaji kodi, aliwadharau watu wake na kuwababaikia weupe.
4: Kikwete - Alianza kwa nguvu ya Lowassa, alivyotoswa best yake akaanza kutembelea dunia. Kucheka ni moja ya sifa
yake, kwa matukio yote kwake ni upepo.
5: If Pinda - atakuwa analia upepo ukivuma!
 
Zaidi, Nachelea kwa Pinda kuwa Prez 2015 maana si chaguo la JK hata kuteuliwa kwake ni shinikizo la Mzee Mkapa na ukristo wake (pinda) maana ilikuwa lazima maana President and Vice-President wote ni waislam so katika kuchekecha mtu wa kumrithi EL ambae pia ni mkristo,mbunge wa kuchaguliwa jimboni, mzoefu wa serikalini(Tawala za Mikoa&Serikali za mitaa), CIA,pinda ikabidi abebwe tu. Sita isingewezekana maana alikuwa Spika tayari(mhimili mwingine wa dola)
 
CCM tupeni raha Watanzania ni ama Dr. Salim au Dr. Mwinyi wakati mgombea mwenza Samwel Sitta ama Dr. Magufuli wakati waziri mkuu Dr. Mwakyembe
 
Jamani hama kwelI CCM imeisha.wanataka kuachia madaraka kwa hiari yao wenye kwani Mh.Pinda awezi kusimama na CDM.

Ila sina imani ya kuwa CCM ipo mbioni kuachia ngazi ktk nchi kwa kuwa Mzee wengi ambao wanaipenda CCM ndio wapiga kura wakati vijana uishia kupinga lakini awapigi kura.

NB:Tz tubadilike tuache ushabiki kwenye mitandaoni.
 
guys, this might be true

Hii ni kweli labda litokee la kutokea ambalo lipo nje ya uwezo wa binadamu ,kama utaangalia sana Uraisi wa Tz hauhitaji uwe na nyota nyingi ,na mgombea kwa tiketi ya CCM anakuwa ndie Raisi ,na Raisi ni mtu wa mwisho kwa maana anakuwa na washauri kibao ,na kwa Pinda itakuwa rahisi kwani kubwa ni kusimamia sera ,hivyo kwa wenyewe maana CCM inawenyewe ,wamekwishaona kuwa Pinda ndie aliekuwa hana sumile na anaweza kuamuru lolote likafuatwa within a short time.
Kwa ufupi kama unavyowaona CCM wana utawala wa kicowboy ,Pinda ana uweza wa kuendesha serikali kinguvu kimabavu kushinda hata Mkapa ,kumbuka tu atakuwa anamipaka ambayo haitakuwa rahisi kuona mabavu yake.Umeona namna mawaziri hivi sasa wanavyokwenda mbio ,habari za ndani zinazema msimamizi ni Pinda na hakuna mchezo.
Kama mtachunguza mtaona kuna msukumo fulani ambao umefuta kuogopana au kulindana.
 
Daah naona JF imegeuka kuwa sehemu ya kutema povu tu. toa uthibitisho wa utendaji wa Pinda sio kutoa dhahania tu
 
Nani kasema Serikalini hakuna kulindana? Hosea anafanya nini pale mpaka sasa? Wakurugenz wa Wilaya wabadhirifu wanaendelea kutanua tu.
 
Vipi? Wewe ni 1 kati ya wale waliokosa mgao wa pesa pale jangwani nin? Pole sana mkuu usikumwema.
 
Pinda kuliko awe rais bora nchi ipigwe mnada kila m2 apewe ela atambae zake..mimi ntaenda uhamishoni Moroni.
 
pinda atakua rais wako 2!alishindwa kutoa maamuz kwa mawazr alaf 2mpe urais!kwanza nchi ishachukuliwa na magwanda!
 
we acha ndoto za mchana hivi Pinda yupi unamzungumzia wewe,huyo legelege au amebadilishwa na nini?hebu niambieni ni nini alichofanya cha kukumbukwa?
 
rais ajaye?uyu ambaye anatembea na vote of no confidence moyon au yule aliyesema anastaaf 2015? Tangu mh zitto ampige mkwara wa kumfukuza u Pm haonekan tena! Jana makyembe kasema - siwezi kusema mimi ni waziri ila sina mamlaka,mamlaka yote ninayo na ntawafukuza wengi pale wizarani- hiki ni kijembe na kejeli kwa pm aliyeshindwa kumnasa jairo!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom