Mizengo Pinda akunjua makucha

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
Jumatatu, Septemba 17, 2012 05:56 Na Mwandishi Wetu, Misungwi [Waziri Mkuu, Mizengo Pinda] Waziri Mkuu, Mizengo Pinda *Asema imejaa mchwa wanaotafuna fedha za umma *Aagiza watendaji wake wapelekwe mahakamani *Asisitiza itakosa madiwani hadi mwaka 2015 *Wananchi wamzomea mwenyekiti hadharani WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, ametangaza kusudio la kuivunja Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, kutokana na halmashauri hiyo kukabiliwa na kashfa za ufisadi. Uchafu wa halmashauri hiyo umeanzia kwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Benard Polcyarp na baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo wanaokabiliwa na tuhuma za kufuja fedha za miradi ya maendeleo. Mbali na Pinda kutangaza kuifuta halmashauri hiyo kwa kukosa sifa, pia aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), mkoani Mwanza kuchukua hatua. Pinda aliitaka TAKUKURU kuanza mara moja kuandaa mashitaka, kisha kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi katika halmashauri hiyo yenye madiwani 36 wote kutoka CCM. Pinda alifikia uamuzi huo baada ya kubanwa maswali mengi na wananchi katika mkutano wa hadhara, uliofanyika juzi mjini Misungwi. Katika mkutano huo wananchi hao walimtaka Pinda awaeleze kuhusu hatima ya halmashauri hiyo na tuhuma nzito za ufisadi zinazomkabili mwenyekiti wa halmashauri hiyo. Wananchi hao pia walitaka kujua hatua zinazochukuliwa dhidi ya baadhi ya vigogo, wanaotuhumiwa kutafuna mabilioni ya fedha za miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo. Kabla ya Pinda kutangaza kusudio hilo la kuivunja halmashauri hiyo, wananchi waliokuwa wamefurika katika mkutano huo wakimzomea mwenyekiti wa halmashauri hiyo, baada ya kuitwa jukwaani na Pinda kwa lengo la kuwasalimia wananchi. Mara baada ya Pinda kumtaja mwenyekiti huyo, umati karibu wote ulianza kumzomea Polcarp huku baadhi yao wakipiga miluzi na kumwita fisadi mkubwa anayeitafuna halmashauri hiyo ya Misungwi. Wananchi wengine walisikika wakimtaka waziri mkuu aondoke naye, kwani amewachosha kwa vitendo vyake walivyodai vya kuhujumu fedha za miradi ya maendeleo. Pinda alianza kwa kusema. “Kabla sijazungumza lolote, kuna mtu muhimu sana hapa amesahaulika kutambulishwa. Namuomba mwenyekiti wa halmashauri ya hapa Misungwi aje jukwaani japo awasalimie wananchi,” alisema. Kutokana na kauli hiyo, wananchi walianza kuzomea mwanzo hadi mwisho wa kupanda na kushuka jukwaani kwa mwenyekiti huyo. Akiwa jukwaani huku akizomewa na umati huo wa wananchi, mwenyekiti huyo, alianza kwa kusema: "Misungwi oyeee!", akazomewa. Kisha akasema kwa lugha ya kisukuma: "Nalibona mwasayaga gete, lakini unene naliho duhu, (yaani naona mmekasirika sana, lakini mimi nipo tu). Akazomewa tena na kushindwa kuendelea, huku baadhi ya watu wakisikika wakimwita fisadi, aondoke, Edipo Pinda alipomtaka ashuke chini. Baada ya zomea zomea hiyo kuonekana kushika kasi zaidi, waziri mkuu alilazimika kubadili utaratibu wa hotuba yake, ambapo aliomba wananchi wanaochukizwa na vitendo vya mwenyekiti huyo wanyooshe mikono juu ili awaone. Hapo wananchi wengi walinyoosha mikono yao, kisha Pinda akaomba wananchi watano wapite mbele waulize maswali, ambapo watu sita waliuliza maswali yakiwemo ya tuhuma za ufisadi katika halmashauri hiyo. Miongoni mwa vigogo wanaotuhumiwa na ufisadi huo mkubwa ni Polcarp mwenyewe na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Exavieri Tilweselekwa, ambaye baadaye waziri mkuu aliagiza mkurugenzi huyo ashushwe cheo na ashitakiwe mahakamani kwa tuhuma hizo nzito. Akizungumzia tuhuma hizo, Pinda aliyeonekana kukasirishwa na tuhuma hizo, alisema halmashauri hiyo imeelemewa na mchwa mkali unaotafuna fedha za maendeleo, kwani mwaka 2009/2010 ilipata hati yenye shaka. Pinda alisema, mwaka wa fedha 2010/2011 halmashauri hiyo chini ya mwenyekiti wake, Polcarp ilipata tena hati chafu, jambo linalothibitisha kuwepo kwa ulaji mkubwa wa fedha unaofanywa na baadhi ya vigogo wa halmashauri hiyo. Alisema ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeonesha wazi kuwepo kwa upotevu mkubwa wa fedha za maendeleo wilayani humo. Pinda alisema madai ya mwenyekiti huyo kuwa Mbunge wa Misungwi Charles Kitwanga kuingilia ukaguzi huo, hayana ukweli wowote, kwani vyombo hivyo ni vikubwa na vina heshima kubwa ndani na nje ya nchi. "Ripoti ya CAG na ile ya tume maalumu zinatueleza ukweli wa tatizo hapa Misungwi lipo wapi. Mwenyekiti wenu huyu amekuwa akifanya biashara na halmashauri yake kupitia kampuni yake ya ujenzi. Kimaadili, kiuongozi na kisiasa ni jambo lisilokubalika hata kidogo. "Kiongozi mzuri na makini huwezi kufanya hivyo, maana lazima italeta mgongano tu wa kimaslahi. Ni dhahiri hapa Misungwi hakuna kinachofanyika katika kusimamia maendeleo ya wananchi. Nataka TAKUKURU ifanye kazi yake tena kwa haraka sana. Na wahusika wote wa ufisadi huu wapelekwe mahakamani". "Swali la kujiuliza hapa. Kwa nini mwenyekiti ufanyebiashara na halmashauri? Kama una kampuni yako kwa nini usingetafuta mtu ukamuweka akawa ndiye mwenye kampuni badala ya wewe mwenyewe?. “Je ukijipatia tenda ya ujenzi utajisimamiaje, na nani atakuwajibisha?", alihoji kwa jazba Waziri Mkuu Pinda, wakati akijibu swali la Victor Thomas, aliyesema mwenyekiti huyo hahitajiki tena kuiongoza halmashauri hiyo. Alisema, kulingana na uwepo wa tuhuma hizo dhidi ya mwenyekiti huyo, alimshauri zaidi ya mara mbili juzi katika kikao cha ndani na madiwani wote wa halmashauri hiyo. Katika mazungumzo hayo, Pinda alimshauri Polcarp ajiuzulu nafasi hiyo, lakini alikataa ushauri wake ambaye ndiye mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa nchini (TAMISEMI). “Juzi (majuzi), Polcarp alinifuata kuja kuongea na mimi. Lakini nilimshauri ajiuzulu nafasi yake akakataa. Aliniambia Misungwi hakuna tatizo (wananchi wakazomea). “Akaniambia kwamba anayesababisha yeye achukiwe na wananchi ni mbunge (Kitwanga)...lakini mimi (Polcarp), nakubalika sana". Wananchi wakazomea tena. "Mwenyekiti huyu amekataa ushauri wangu wa kumtaka ajiuzulu. Mimi ndiye Bosi wake na ndiye mwenye kauli ya mwisho. Ngoja nirejee Dar es Salaam na ndani ya muda mfupi kisheria nitaivunja halmashauri hii ya Misungwi. "Itakuwa kama ile ya Dar es Salaam ilipovunjwa miaka ile ya nyuma. Maamuzi haya ni mazito maana hapa Misungwi hamtakuwa na madiwani hadi mwaka 2015, na hatua kali za kisheria lazima zichukuliwe kwa wahusika wote", alisema Pinda huku wananchi wengi wakishangilia na kumtaka aivunje halmashauri hiyo papo hapo, kwa madai wamechoshwa na ufisadi. Miaka ya nyuma Serikali iliwahi pia kuivunja halmashauri ya Dar es Salaam, baada ya kuwepo kwa tuhuma zinazofanana na zile za halmashauri ya wilaya ya Misungwi, ambapo italazimika kuundwa tume maalumu ya kwenda kusimamia shughuli zote za madiwani. Baadhi ya wakazi wa wilaya Misungwi, walieleza kufurahiswa na maamuzi ya Pinda kuivunja halmashauri hiyo ndani ya siku chache zijazo, na kwamba wamechoshwa na baadhi ya vigogo wa halmashauri hiyo kutafuna fedha za miradi ya maendeleo.
 
Duh! Yaani PM anashauri ukiwa na kampuni umuweke wife kuendesha afu umpe dili za ofisi kama alivyofanya mkurugenzi wa tanesco! Hajawahi kusikia kuhusu conflict of interest? Zile semina telekezi hawa viongozi wanafundishwa maadili gani, ya kuvaa nguo ndefu?
 
mimi sina la kusema!
waziri mkuu anambembeleza mtu ajiuzuru!
itakuwa ngumu kufikia tanzania tuitakayo!
 
Pindamgongo yeye mwenyewe ndio tatizo, labda ofisi ya Waziri Mkuu ndio inatakiwa ivunjwe. Watu wanafanya madudu utadhani hakuna serikali? Huyo Mwenyekiti wa Halmashauri wanamuonea tu tatizo ni "Udhaifu" wa Dhaifu pamoja Pinda Mgongo
 
Mkumbusheni mabilioni ya Swiss! Waziri mkuu alikuwa Sokoine, hawa wengine ni wanafukuzana na waiba kuku wakati nchi inatafunwa.
 
Safi mh Pinda kuna watu wanafkr serikali ni kama kuendesha toroli!!
 
Sidhani kama kuna maamuzi ambayo yatatolewa kwa huyu PM tuliyenae kwa sababu tangu awe PM sijawahi kuona wala kusikia kafanya maamuzi ambayo yameliokoa taifa lisipate hasara na hususani tumeona ubadhirifu katika wizara mbali mbali lakini hakuna uwajibishwaji uliotolewa ambao umesaidia kurudisha mali au fedha zilizopotea kilicho baki ni kuhamishana au kumwachisha muhusika pasipo hatua yeyote ya kisheria kuchukuliwa.
 
Bora umetupa ukweli kwani humu JF kuna mtoa hoja katueleza Mh. Pinda kazomewa huko Mwanza leo hii.
Hii Wilaya ya Misungwi ina matatizo ni bora waipige chini hata taarifa ya CAG inaonyesha wanachota fedha kushirikiana na Benki mojawapo.
 
Kama huyo mwenyekiti angekuwa katoka CDM, Pinda angemwomba na kumwangukia mara mbili ili ajiuzuru? Hapo ndipo naona UDHAIFU wa CCM na PINDA.
 
Hao ndio saizi ya PINDA! Mchwa wakubwa katika baraza lake la Mawaziri amewaacha waendelee. Hebu fikiria Prof. wa Nishati anavyowaumbua Ngeleja na TANESCO sasa huyu PINDA ni muoga kwa mawaziri. Hafai UWAZIRI MKUU SHAME!!
 
Back
Top Bottom