Mitihani ni kigezo kimojawapo kitumikacho katika kupima uelewa wa mwanafunzi. Mitihani imekuwa ikifanyika toka mwanafunzi toka mwanafunzi yuko ngazi za awali(std one) hadi anafika chuo kikuu. Mitihani imekuwa ikiwasaidia sana wazazi na walimu kujua uwezo wa watoto/wanafunzi wao kupitia ufaulu wao japo si kweli kuwa mwanafunzi akifeli basi hajui au akifaulu anajua sana. Hivi sasa maarifa kwa wanafunzi walio wengi yanapungua kwa kuwa wamekua wakisoma kwa ajili ya kufaulu mitihani tu(cramming). Chukulia mfano wa chuo kikuu kwa nini wasibuni njia mbadala ya kupima uuelewa wa wanavyuo wao na kuachana na dhana ya kutumia mitihani? Ni njia zipi mbadala ungeshauri zitumike hasa katika ngazi ya chuo kikuu katika kupima uelewa wa wanaosoma huko?