Mitihani darasa la 7 leo, mbona haisimamiwi na walimu wa sekondari kama mlivyoahidi?

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
Serikali imepata woga gani tena, mbona mlitutangazia kuwa katika mkakati wa kuhakikisha hatupati tena wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika kujiunga na shule za sekondari za kata kama ilivyokuwa mwaka jana, serikali ingetumia walimu wa sekondari kusimamia mitihani hiyo.

Sasa nini kimewasibu tena kuna ukweli kuwa ni woga wa kuhofia sekondari za kata kukosa wanafunzi kwani watoto wangefeli sana?.
 
Serikali imepata woga gani tena, mbona mlitutangazia kuwa katika mkakati wa kuhakikisha hatupati tena wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika kujiunga na shule za sekondari za kata kama ilivyokuwa mwaka jana, serikali ingetumia walimu wa sekondari kusimamia mitihani hiyo. Sasa nini kimewasibu tena kuna ukweli kuwa ni woga wa kuhofia sekondari za kata kukosa wanafunzi kwani watoto wangefeli sana?.
Hayo si mawazo ya kitaalam.
 
Darasa la saba hakuna kufaulu wala kufeli,kuna kuchaguliwa.Kama nafasi zipo hata walioshindwa kuandika namba zao na hawajui kuandika huwa wanachaguliwa na kama nafasi hakuna hata waliopata alama za juu huwa wanakosa nafasi.USHAURI,SERIKALI IANZISHE UTARATIBU WA KUFAULU KWA WANAFUNZI NA SIO KUWACHAGUA KAMA WANAVYOFANYA SASA...
ANGALIZO...
Kwa jinsi serikali ilivyo jitahidi kujenga shule nyingi za Kata za Sekondari,wakianzisha utaratibu wa kufaulu,kuna shule zitakosa kabisa wanafunzi.....
 
Back
Top Bottom